Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Mtoto aliyekataliwa na baba yake

kaka yako anaubabe wa kizamani..we fanya jambo jema na kaka yako asikutishe kuhusu kuvunja undugu wenu kwa maana hata huyo mtoto ni ndugu yako.msaidie mtoto na achana na irresponsible father,life is full of suprises watoto kama hao huwa hawatupwi na mungu so jst adopt him

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kama ameshasema mtoto sio wake sasa analalama kitu gani? We cha msingi mwambie huyo si mtoto wake bali ni wa rafiki yako.
 
Hongera sana kwa kuwa na roho nzuri kiasi hicho. Endelea kumlea mtoto huyo na umlee kama vile ni mwanao kabisa. Kaka yako huyo wala usimshirikishe kabisa. Miaka ijayo penye majaliwa huyu mtoto atapakuja kupata mafanikio ya kimaisha ndio huyo kaka yako atataka kujisogeza karibu na mtoto na kujifanya yeye ndio baba halali wa huyo mtoto. Hongera sana WALIMWEUSI wakati mwingine huwa tunadhani hii dunia watenda wema hakuna tena lakini anatokea mwanadamu ambaye matendo yake yanatupa faraja kubwa sana kwamba kumbe wanadamu wema bado wapo duniani.
 
I will give you my story. I was suspecting for many years kwamba baba yangu ana Mtoto nje kila nikiuliza alichomoa. Mungu mwema siku moja tukagundua. Ikawa mgogoro mkubwa sana

Mama mzazi akasema hataki kumsikia yule Mtoto. Mimi nikasema nitamsaidia. Lilimuuma sana mama yangu na bado linamuuma lakini Huyu binti sasa nasomesha chuo na baba angu technical anamkana but it is what it is.

Ushauri acha huyo kaka ako anune some day atacheka it is that simple. Acha anune don't quit kussoport damu yenu
 
Binafsi nikupongeze kwa moyo wako wa ushujaa na huo ndio uwanaume ,sio huyo bwana kaka ambaye anakwepa majukum kwa kujifanya yeye ni mbogo wala usitishike mungu atakubaliki kupitia huyo mtoto songa mbele
 
Kwa kifupi mwambie kaka yako kuwa eti, naye atazaa watoto wakiwemo wa kike. Aangalie sana laana ya kumkataa huyu binti ikamfuata. Kuna baba mmoja alikuwa anazaa sana na mabinti wa watu, watu wakawa wanakasirika maana anawazalisha na hakuna ndoa. Kuna mama mmoja alilaani sana kitendo cha yule baba kuzaa na mtoto wake tena inasemekana was virgin bila kumuoa. Kilio cha yule mama kimepelekea watoto wa yule mzee wa mke wa ndo hakuna hata mmoja aliolewa after that, na waliolewa waliachika au kufa. Hadi leo ile nyumba hata wajukuu wanazaa na waume za watu na hawaolewi kabisa!!! Haya mambo yapo na tusipuuze. Wewe tunza mtoto na Mungu atamtegemeza, wanasema hivi, Jiwe walilolikataa waaashi mara nyingi huwa ndilo jiwe kuu la pembeni!!! Huyu mtoto atakuwa jiwe nililokataliwa ila kaka yake aangalie sana asijea akawa ndiyo jiwe kuu la kumtunza siku za uzee wake!!!! Laana hii inaweza kudhuru watoto wake anoona ni bora kumbe siku moja wasijeuke wala unga, bangi, elimu mbovu na maisha mambovu. Mtoto sitamkataa hata kama nimezaa na mwendawazimu. Hongera shangazi mtu na mungu atakurujeshea kwa kila wema wako. Mpende mtoto hadi basi.
 
Habari zanu wana JF,

Naombeni ushauri wenu katika hili lililonikuta, ni story ndefu ila in short miaka ya nyuma kipindi tukiwa tunasoma, our mom alikuwa anaishi na kabinti fulani, by that time she was 10 yrs na kiliacha shule kutokana na matatizo ya wazazi wake so kikawa home kinamsaidia mom kazi ndogondogo tu na kumpa mom kampani. Tulimchukulia kama mdogo wetu na tulimpenda sana. After two years my sis aliyekuwa anaishi DSM alijifungua so akamchukua kuishi nae ili amsaidie kazi. Kaka yetu mmoja by that time alikuwa anasoma alikuwa akiishi hapo kwa sister.

After two years binti akagundulika kuwa mjamzito na alipoulizwa nani mhusika alisema ni huyo kaka yangu ila yeye alikana kabisaaaaa!!!Binti wa watu akarudishwa kijijini na alijifungua mtoto wa kike akiwa na miaka 15. Mwaka juzi nilienda kijijini na nikabahatika kumuona huyo mtoto, honestly she resembles my brother kabisaaaaa!!! Nilimpigia na kumweleza kuhusu hilo but alisema kuwa yeye hahusiki na kama anafanana na yeye it is not his business. Huyo mtoto alikuwa anaishi maisha magumu sana imagine at the age of 12 hajaanza darasa la kwanza. ilimuomba mama yake nimchukue niishi nae na pia nimsaidie kwa vile yule kweli ni mtoto wa kaka yangu!

Kwa vile bro alishakataa hata nilipomwambia kuwa mtoto kafanana nae, sikumshirikisha uamuzi wangu niliouchukua wa kumlea huyo mtoto ila mom nilimshirikisha na hakuwa na tatizo na yeye toka zamani alishataka kumchukua ila bro alimkataza so ikabidi aheshimu uamuzi wake. Hadi sasa naishi nae na the girl is very inteligent, amini usiamini nilipompeleka shule walimpa mtihani na kugundua kuwa hakustahili kuanza drs la kwanza, wakampeleka la 3 now yupo la 5.

Last week mke wa huyo brother alikuja kwangu kunitembelea na kumuona yule mtoto, akaniuliza mtoto wa nani?Nikamjibu ni mtoto wa shemeji yangu ili kuua soo wasie gombana na mumewe. Sasa jana narudi toka job namkuta brother kwangu kafura vibaya sana na anadai mimi ninadharau kwa nini nimemchukua mtoto ambae sie wake na amedai kuwa mimi na yeye undugu wetu umeisha na akaondoka bila hata kuniaga.

Naombeni ushauri wenu katika hili mana that brother of mine ni mbabe balaa, yani ndugu wanamwogopa balaa isipokuwa mimi tu!!

Nawakilisha.

Achana nae
 
huyu kaka yako anatakiwa aende milembe kwanza hayo yapo ila huwezi jua nini kilitokea kati yao hapo mwanzo wakiwa kwenye ushirikiano. kuna dogo naye alifanya hivyo ila mimi niliporudi nilimwamlu huyo mtoto aletwe home kwa mama hadi leo yupo pale maana hakuna mwanamke kichaa akasema huyu ni mtoto wako hadi kajifungua bila kumpeleka kwa mtu mwingine. Kama amekusingizia kwa nini iwe wewe? dogo hakujibu hata swali mmoja
 
huyo bro asikukatisha tamaa,undugu sio kufanana,anakulisha?!!!mlee mtoto na achana na huyo mwehu kk
 
M/mungu akubaliki kaka na akuzidishie baraka katika maisha yako kwan huyo kaka yako ip siku moja atajutia maamuzi yake keep it up
 
Back
Top Bottom