Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Mtoto aliyekataliwa na baba yake

Habari zanu wana JF,

Naombeni ushauri wenu katika hili lililonikuta, ni story ndefu ila in short miaka ya nyuma kipindi tukiwa tunasoma, our mom alikuwa anaishi na kabinti fulani, by that time she was 10 yrs na kiliacha shule kutokana na matatizo ya wazazi wake so kikawa home kinamsaidia mom kazi ndogondogo tu na kumpa mom kampani. Tulimchukulia kama mdogo wetu na tulimpenda sana. After two years my sis aliyekuwa anaishi DSM alijifungua so akamchukua kuishi nae ili amsaidie kazi. Kaka yetu mmoja by that time alikuwa anasoma alikuwa akiishi hapo kwa sister.

After two years binti akagundulika kuwa mjamzito na alipoulizwa nani mhusika alisema ni huyo kaka yangu ila yeye alikana kabisaaaaa!!!Binti wa watu akarudishwa kijijini na alijifungua mtoto wa kike akiwa na miaka 15. Mwaka juzi nilienda kijijini na nikabahatika kumuona huyo mtoto, honestly she resembles my brother kabisaaaaa!!! Nilimpigia na kumweleza kuhusu hilo but alisema kuwa yeye hahusiki na kama anafanana na yeye it is not his business. Huyo mtoto alikuwa anaishi maisha magumu sana imagine at the age of 12 hajaanza darasa la kwanza. ilimuomba mama yake nimchukue niishi nae na pia nimsaidie kwa vile yule kweli ni mtoto wa kaka yangu!

Kwa vile bro alishakataa hata nilipomwambia kuwa mtoto kafanana nae, sikumshirikisha uamuzi wangu niliouchukua wa kumlea huyo mtoto ila mom nilimshirikisha na hakuwa na tatizo na yeye toka zamani alishataka kumchukua ila bro alimkataza so ikabidi aheshimu uamuzi wake. Hadi sasa naishi nae na the girl is very inteligent, amini usiamini nilipompeleka shule walimpa mtihani na kugundua kuwa hakustahili kuanza drs la kwanza, wakampeleka la 3 now yupo la 5.

Last week mke wa huyo brother alikuja kwangu kunitembelea na kumuona yule mtoto, akaniuliza mtoto wa nani?Nikamjibu ni mtoto wa shemeji yangu ili kuua soo wasie gombana na mumewe. Sasa jana narudi toka job namkuta brother kwangu kafura vibaya sana na anadai mimi ninadharau kwa nini nimemchukua mtoto ambae sie wake na amedai kuwa mimi na yeye undugu wetu umeisha na akaondoka bila hata kuniaga.

Naombeni ushauri wenu katika hili mana that brother of mine ni mbabe balaa, yani ndugu wanamwogopa balaa isipokuwa mimi tu!!

Nawakilisha.

Dada hongera sn sn sn kwa uamuzi wa ajabu sn ambao hakika mko wachache sn, ubabe wa kaka yako kwakuwa ni mzima, Biblia inasema watu kama hao wanakiburi cha uzima, uzee waja, kumbuka, Jerry rollings, Rais wazamani wa Ghana, alikataliwa na baba yake, lkn aliposikia mwanae ni Rais akaja, alipofika airport akasema yeye ndo baba wa Rais, walipopiga cm ikulu akasema sina baba, mwambieni aondoke maramoja akikataa mwekeni ndani,
My Beloved sister, wapi watotowananunuliwa? unabahati kubwa sn kumpata waziri wa elimu ajae atakaekusaidia zaidi ww siku hizo zijazo, bro, hata akiwa mbabe, hawezi kuzuia oxygeni yako hata sekunde moja, ubabe ni wake, na wema ni wako, keep it up, achana nae undugu si maji ni damu akiktaka abadili damu ndo utakufa,
siye wakwanza kusema hivyo, alikuwepo Masawe, alipogombana na nduguye, akasema kuanzia leo, undugu na ufe, na mm ni Masawo, si Masawe tena, alipozaa mtoto akagombana nae, mwanae kasema mm si masawo, ni masawi,hata kama undugu ukifa, atakusaidia nn? Neno linasema, mtu hafi wala haishi ila kwa neo litokalo kinywani mwa Mungu pekee. fanya mema ndiyo yenye thawabu.
 
umesema kweli mtupu na...... amhurumiaye masikini humkopesha Mungu naye atamlipa kwa tendo lake jema na dini nzuri ni kuwaona wagonjwa na kusaidia masikini neno linasema.
pia inasemwa utampendaje Mungu usiyemwona ukampa mamilioni kuliko kumpenda yule maskini unaye mwona ,mgonjwa mwenye shida yatima ,wajane nk huwezi sema wampenda Mungu kama humpendi jirani /ndugu yako
 
ni ngumu kukwepa extended families in africa my dia!kwa mfano huyo brother alichaguliwa kusoma azania na sister alikuwa anaishi karibu na shule so ili kuupunguza gharama ikabidi aishi na sister ili iwe rahisi kwake kwenda na kurudi shule.
exactly Nicas Mtei
 
Last edited by a moderator:
Usijali ubabe wake ukisikia ufisadi wa roho za watu ndio huo,yeye kwani huyo mtoto anamzidishia nini akiwa hapo kwako au anampunguzia nini? anajua kosa alofanya na nafsi yake inamsuta ila bado hataki kukubali makosa,cha muhimu mlee huyo bint kwa mapenzi kama mtoto wako na mwenyezi mungu atakupa kheir yako na ipo siku huyo kakako atajuta kwa nini alimkataa...inshallah mungu akupe umri mrefu na akuzidishie kipato na akupe ushujaa wakuweza kuhimili kila mtihani...

Amina!
 
Ulichofanya ni sahihi kabisa. Usimlee tu eti sababu ni wa kaka yako! Ila pia unaweza kufanya kama unamsadia yeye(pia na mama yake sababu hawana uwezo).

Huyo kaka na hizo hasira zake zitamtokea puani siku moja!
 
hatuishi nao ni wale wakupita likizo ya shule nk.binafsi sipendi kabis aila umaskini wa familia zetu ndio unapelekea hayo,hata wewe katika maisha hautaliepuka .huyo kijana alikuwa yuko likizo ya chuo ile ya june akapita home kuchukua ad na matumizi mengine maana ndio tunamsomesha akaacha na mimba hahahaahahahahaah dalaliiiii labda ukaishi mars kwakeli

Na mambo hayo ndo yanaongeza umaskini. Mimi sikubaliani nayo
 
Hvi kwa nini huwa mnapenda kuishi na ndugu wa mume/mke pamoja? Ni tabia gani hyo?

vp kwenu ni ULAYA YA KASKAZIN AU MASHARIKI?
km ni africa specificaly tanzania EXTENDED FAMILY BADO ZIPO

kuna factor nyng sana zinazopelekea kuish nao....so sio suala la KUPENDA KUISH NAO...SOMETMES INABD TUISH NAO....
 
Dada hongera sn sn sn kwa uamuzi wa ajabu sn ambao hakika mko wachache sn, ubabe wa kaka yako kwakuwa ni mzima, Biblia inasema watu kama hao wanakiburi cha uzima, uzee waja, kumbuka, Jerry rollings, Rais wazamani wa Ghana, alikataliwa na baba yake, lkn aliposikia mwanae ni Rais akaja, alipofika airport akasema yeye ndo baba wa Rais, walipopiga cm ikulu akasema sina baba, mwambieni aondoke maramoja akikataa mwekeni ndani,
My Beloved sister, wapi watotowananunuliwa? unabahati kubwa sn kumpata waziri wa elimu ajae atakaekusaidia zaidi ww siku hizo zijazo, bro, hata akiwa mbabe, hawezi kuzuia oxygeni yako hata sekunde moja, ubabe ni wake, na wema ni wako, keep it up, achana nae undugu si maji ni damu akiktaka abadili damu ndo utakufa,
siye wakwanza kusema hivyo, alikuwepo Masawe, alipogombana na nduguye, akasema kuanzia leo, undugu na ufe, na mm ni Masawo, si Masawe tena, alipozaa mtoto akagombana nae, mwanae kasema mm si masawo, ni masawi,hata kama undugu ukifa, atakusaidia nn? Neno linasema, mtu hafi wala haishi ila kwa neo litokalo kinywani mwa Mungu pekee. fanya mema ndiyo yenye thawabu.

Thanks Jalem
 
Achana naye wewe fanya kazi ya mungu!
 
vp kwenu ni ULAYA YA KASKAZIN AU MASHARIKI?
km ni africa specificaly tanzania EXTENDED FAMILY BADO ZIPO

kuna factor nyng sana zinazopelekea kuish nao....so sio suala la KUPENDA KUISH NAO...SOMETMES INABD TUISH NAO....
Rose1980 mzima wewe?
 
Last edited by a moderator:
Ni ngumu kukwepa extended families in Africa my dia!Kwa mfano huyo brother alichaguliwa kusoma Azania na sister alikuwa anaishi karibu na shule so ili kuupunguza gharama ikabidi aishi na sister ili iwe rahisi kwake kwenda na kurudi shule.

Ki ukweli kuna matatizo huwa tunayalea wenyewe. Ni ujinga pia ni uzembe.. Mashemeji, mawifi, wakwe, mara nyingi hao ndo wamekuwa chanzo cha ndoa nyng kuanguka.. Acheni hayo mazoea.
 
mimi niko radhi kuonekana mbaya kuliko kufanya uzembe huo. Bora lawama kuliko fedheha.
kanusha hiyo kauli hapo sio uzembe kabisa hivi kweli anakuja mtoto wa dada yako wa kiume au wa kaka yako kukusalimu anakaa 1week utamfukuza?????????????
 
vp kwenu ni ULAYA YA KASKAZIN AU MASHARIKI?
km ni africa specificaly tanzania EXTENDED FAMILY BADO ZIPO

kuna factor nyng sana zinazopelekea kuish nao....so sio suala la KUPENDA KUISH NAO...SOMETMES INABD TUISH NAO....

Kwetu ni hapa hapa Tanganyika bt hyo hainipi uhalali wa kuish na ndugu zangu au wa mke wangu pamoja ktk ndoa yangu. Kama ni msaada wa aina nyngne ntawapa bt sio kuishi nao pamoja.. Ninao ushahd mkubwa sana wa hao ndugu kuvuruga ndoa nyingi.
 
ki ukweli kuna matatizo huwa tunayalea wenyewe. Ni ujinga pia ni uzembe.. Mashemeji, mawifi, wakwe, mara nyingi hao ndo wamekuwa chanzo cha ndoa nyng kuanguka.. Acheni hayo mazoea.
sasa unataka nikamfukuze yule mama mkwe kaja kwangu juzi kusalimia dalaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
kwetu ni hapa hapa tanganyika bt hyo hainipi uhalali wa kuish na ndugu zangu au wa mke wangu pamoja ktk ndoa yangu. Kama ni msaada wa aina nyngne ntawapa bt sio kuishi nao pamoja.. Ninao ushahd mkubwa sana wa hao ndugu kuvuruga ndoa nyingi.
utamfukuza mama mkwe wako kaja kuwaona wajukuu dalalii
 
Ki ukweli kuna matatizo huwa tunayalea wenyewe. Ni ujinga pia ni uzembe.. Mashemeji, mawifi, wakwe, mara nyingi hao ndo wamekuwa chanzo cha ndoa nyng kuanguka.. Acheni hayo mazoea.

Ni kweli wao watataka care kama unavyo mpa mkeo wakati mke atabaki kuwa mke na care zake ni special tofauti na dada,wifi nk......mtu atawaacha wazazi wake na kuambatana na mkewe.....mawifi wanafuata nini? kama kaka yao asingeoa wangekaa wapi?au akiwa maskini mbona hawasogei....mtu anasema nimekuja kusalimia miaka 2 upo tu unasalimia nini.
 
kanusha hiyo kauli hapo sio uzembe kabisa hivi kweli anakuja mtoto wa dada yako wa kiume au wa kaka yako kukusalimu anakaa 1week utamfukuza?????????????

Dalali sijakataa suala la kukaa week 1. Nakataa wale wanaohamia jumla jumla.
 
sasa unataka nikamfukuze yule mama mkwe kaja kwangu juzi kusalimia dalaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

hahaha. Usimfukuze. Ila asihamie hapo sasa. Ndoa haitakuwa na uhuru na amani dalaliiiíi
 
Hvi kwa nini huwa mnapenda kuishi na ndugu wa mume/mke pamoja? Ni tabia gani hyo?

Yani wewe umenikuna, nimeshasikia matatizo mengi sana ya hawa ndugu mnaorundika kwenye majumba yenu. kama ni misaada kwanini msiwapelekee pale walipo? mimi kuishi na mtu baki kwangu labda awe yatima. tumeshasikia story za ndugu kubaka watoto wa wenye nyumba watu bado hawasikii!!!
 
Back
Top Bottom