source mwananchi
Mtoto aeleza kupigwa risasi
Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na
mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi,
wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu
yake, Fahdi katika eneo la Soweto.
Alisema akiwa njiani, aliona watu
wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa
kupigwa risasi na kuanguka chini.
Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa
amevaa sare za polisi, alisema Adam
mwanafunzi katika Shule ya Msingi
Levolosi huku akitokwa machozi.
Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya
watoto katika Hospitali ya Mount Meru,
Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto
huyo ana vyuma viwili katika mguu wake.
Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari
mashine ya X-ray inaonyesha vyuma
kuwepo katika mguu wa Adam siwezi
kusema ni risasi au la, alisema Semdeli.