MANSA MUSSA
JF-Expert Member
- Feb 11, 2017
- 373
- 1,487
Pole kijana
Asante sana kwa taarifa!!!Huyo mtoto amepona watu walimdaka kwa chini, mzima wa afya na kisa chenyewe alikuwa juu na watoto wenzake na mama ake, watoto wote wakashuka mama ake akamfungia mlango eti kisa aligoma kushuka chin, dogo alipoona hivyo akatokea dirishan akijua eti angeshuka weee! Kilichotokea ndio hicho ulichokiona kwenye video ila dogo mzima hajavunjika hata kiungo na wakat anajirusha walijazana chin kumdaka kwahivyo yupo salama! Ila wanawake we acha tu maana mpaka leo bado namfikiria mama mtu n kwanini alifikiria kumfungia mtoto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo pia.
Joshua Benjamin (14) ambaye alikuwa akisoma darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ukonga, anadaiwa kupigwa usiku kucha na mama yake huyo ambaye baadaye alimfunga kwa kamba kwenye mti, nje ya nyumba yake, hadi saa 11 alfajiri alipogundulika kuwa ameshakufa.
Tukio hilo, mashuhuda walisema jana, lilisababisha taharuki kubwa mtaani hapo kwani baadhi ya wakazi walitaka kumpiga mama huyo kabla ya polisi kufika na kumuokoa.
Mmoja wa majirani wa mama huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa walianza kusikia kelele za mtoto huyo akiomba msaada tagu usiku huku mama huyo akiendelea kumpiga.
"Tulisogea hadi jirani na dirishani kwake," alisema shuhuda huyo na "tukamkataza."
"Tulimwambia adhabu hiyo inatosha kwa mtoto maana hadi mtoto aliishiwa nguvu, (hakutusikiliza) tukaondoka na kumuacha akimpiga tu.
Mtoto huyo amefariki ikiwa ni miaka miwili tangu kifo cha baba yake, jirani huyo alisema zaidi.
"Mume wa huyu mama tumemzika mwaka juzi, tuliumia majirani tukawaza pengine baba yake angekuwepo angemsaidia kumuokoa kijana yule.
MTOTO MWINGINE
Jirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Subira alisema chanzo cha kipigo ni madai ya mama huyo kuibiwa Sh. milioni 1 na mwanawe huyo.
"Cha ajabu ni kwamba ana mtoto mwingine mkubwa, na mle ndani kuna ndugu zake wengine sasa kwa nini asiwafikirie hao?" Alisema Subira.
"Alimpiga vibaya mno, yaani alimpiga utafikiri anapiga kibaka.
"Watu wengi tumeshuhudiia akimpiga na yeye ameokolewa na polisi la sivyo watu wangemmaliza."
Shuhuda mmoja aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo ana watoto wanne akiwamo marehemu ambaye ni wa tatu kuzaliwa. Wa kwanza amemaliza kidato cha nne, wa pili kidato cha pili na wa nne anasoma shule ya awali.
Alisema pia kwenye familia hiyo kuna mtoto wa kufikia wa mama huyo, wa marehemu mume wake.
Imeelezwa kuwa mtoto huyo alifariki saa 4 asubuhi baada ya mwanamke huyo kuona mtoto wake haamki, aliamua kupiga simu kwa watu wake wa karibu kuomba msaada.
Kamanda Hamduni aliiambia Nipashe jana kuwa watu wawili akiwamo mwanamke huyo wanashikiliwa na polisi tangu juzi.
"Ni kweli tukio hilo limetokea huko Kinyerezi na tunawashikilia vijana wawili pamoja na mwanamke huyo kwa ajili ya upelelezi," alisema.
Chanzo: Nipashe
Hawa jamaa kujitoa muhanga hua wanaanzia mbali duh
Hapa tatizo liko kwa shule na wajenzi wake, unatengenezaje darasa la watoto wadogo juu bila kuweka protection?Acha upotoshaji, nlikuwa eneo LA tukio ni ktk mambo ya watoto alipanda ghorofani bahati mbaya akadondoka lakini hakuumia sana na ni mzima was afya , mtoto was miaka minne ajitose toka ghorofani kwa lipi analolifaham kuwa limemkwaza. Acheni uchochezi na kutoa taarifa kwa ushabiki , nyambafu
Acha uongo tizama tena iyo Video ckweli km alianguka kwa bahat mbaya wala hakuteleza alikaa akajininginiza kisha akajiachia ukitaka kujua km alijitayarish hata watu ktk eneo latukio walikua wanamuangalia kabla kujiachia kuonesh huenda alipiga kelele nkAcha upotoshaji, nlikuwa eneo LA tukio ni ktk mambo ya watoto alipanda ghorofani bahati mbaya akadondoka lakini hakuumia sana na ni mzima was afya , mtoto was miaka minne ajitose toka ghorofani kwa lipi analolifaham kuwa limemkwaza. Acheni uchochezi na kutoa taarifa kwa ushabiki , nyambafu
Duh! Maisha yanakaza mpaka kwa watoto!!!! hatari hii.
Acha upumbavu,huyu naye anaanza kujifundisha ufisadi na ujambazi na kujitoa mhanga toka mdogo?Kwa vile ni ndugu yetu,kwa Bwana,hili tunaliona ni tukio la kawaida
Hakuna namna talaka halali ykeYule ni mama ake wa kambo ndo alimfungia mlango
Pengine kagombana na mpenzi wakeBasi ngoja tusubiri mkuu maana tumezoea kuona watu wazima wakifanya hayo.
Sasa kama mpaka watoto nao wameanza hapo kuna tatizo tena kubwa sana
Jiwe nimelirusha kweupe,kawaida haturushi gizani,kama limekuumiza,sikupi pole.Ungegugumia kimya kimya.Ubarikiwe,katika Bwana.Emeeen.Hahahahahaaha jiwe limerushwa gizan, pole mkuu pitia panadol hapa Sinza upunguze maumivu
Huyo mtoto ni mdogo sana mpaka kufikiria ku commit suicide,akili yake haijakomaa kihivyo,
Hujawahi kuona mtoto anaona kitu cha hatari lakini anakisogelea?
Hujawahi kuona mtoto wa 3 to 4 years anakula kitu cha hatari kama vigae,wembe,wadudu,uchafu n.k bila kujua kua hivyo ni vitu vya hatari? Mtoto angekua anakijua kifo unadhani angefanya hivyo?
Hujawahi kuona mtoto wa miaka 4 kafiwa na wazazi wake na siku ya kilio yeye ndio kwanza anacheza tu na wenzake wala hajui kifo ni nini??
Jitafakari kijana acha majibu mepesi.