Mtoto ajirusha kutoka ghorofani

Mtoto ajirusha kutoka ghorofani

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
MTOTO wa shule ya DYCCC huko Chang'ombe jijini Dar es salaam ambaye jina lake halijafahimika kwa haraka,amejirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini,imesemekana hivyo kama uonavyoona kwenye hii video, chanzo cha kujirusha kwake bado hakijajulikana .

 
Kama taifa tunahitaji washauri wa kifamilia kuliko kipindi chochote kile hasa zama hizi za digital science.....
Huwezi jua... Kuna wazazi vichaa wanalea watoto... Bila kutambuliwa ni hatari sana...
 
Kama taifa tunahitaji washauri wa kifamilia kuliko kipindi chochote kile hasa zama hizi za digital science.....
Huwezi jua... Kuna wazazi vichaa wanalea watoto... Bila kutambuliwa ni hatari sana...
Sheria ya asili inasema kuwa kila binadamu afanyalo ni lazima liwe na matokeo, haijalishi ni matokeo hasi au chanya.
Kwanza tuliambiwa na Mkoloni mwanzoni kuwa kodi ni lazima tukadhani ni unyonyaji, akaja Mwalimu akatushinikiza kufuata maadili na kuichukia rushwa lakini tukamuona anabania raia wake 'fursa'. Hapa katikati tumelazimishwa na mfumo uliopaliliwa na watawala kukumbatia rushwa na vipato visivyo halali ambavyo vimepelekea nyumba ndogo kuwa sehemu ya maisha huku fahari ya watoto sio kukaa nao ukawapigia hadithi na wenyewe wakakusimulia tena bali kuangalia invoices za shule zinataka karo kiasi gani na kusikiliza vingereza wanavyoongea kwa muda kidogo tunaowaona.
Matokeo yake ndio haya. Narespond kwenye hoja ya mkuu mirisho pm maana anataka washauri wa familia, ninalomkumbusha ni kwamba ndio sisi wenyewe na vichwa vyetu havielewi hata tatizo lenyewe! Inasikitisha sana.
 
Mbaya zaidi watu wanapata fursa ya kuchukua hadi video.

Kweli hata wangejaribu kulala chini ili awaangukie juu ya Migongo yao kwani still ni mdogo wangeishia kuumia kidogo tu au majeraha ya kawaida.
 
Sina mb mwana Jf aliyeko karibu na mm badae napita anionyeshe
 
MTOTO wa shule ya DYCCC huko Chang'ombe jijini Dar es salaam ambaye jina lake halijafahimika kwa haraka,amejirusha kutoka ghorofa ya nne mpaka chini,imesemekana hivyo kama uonavyoona kwenye hii video, chanzo cha kujirusha kwake bado hakijajulikana .


Fuatilieni utakuta alikuwa anakimbia kipigo Cha Mama yake au Mama wa kambo...
 
Back
Top Bottom