Basi limefeli breki na kushika moto Dar es laam

Basi limefeli breki na kushika moto Dar es laam

carbohydates

Senior Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
125
Reaction score
213
Abiria waliokuwa wakisafiri na basi la Kampuni ya Baraka Classic jijini Dar es Salaam wamepatwa na taharuki baada ya basi hilo kufeli breki na kushika moto.

Basi hilo lililokuwa safarini kutoka Mtwara kuelekea Dodoma, limeshika moto saa 1 asubuhi ya leo Jumatatu Oktoba 19, 2026.

Tukio hilo limetokea jijini Dar es Salaam, Barabara ya Mandela eneo la Tabata Mwananchi na kusababisha taharuki na hofu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Hali hiyo ilibainika baada ya moshi kuonekana chini ya tairi la mbele kushoto, huku juhudi za kuzima moto huo zikiendelea kufanywa na wahudumu wa basi hilo.

Akieleza chanzo cha moto huo, dereva wa basi hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, ameeleza chanzo cha moto huo ni hitilafu ya breki ambayo umesababisha msuguano iliyosababisha moto kutokea.
Chanzo : Eatv

BASI.jpeg
 
Electrical fault ya hizi gari za Yutong , naona kama zina changamoto kubwa sana 🤔 cc Xi Jinping
Kama ni hiyo chuma kwenye picha ni Zhongtong Mega

Kwa maelezo ya dereva inaonekana hapo chanzo ni brake overheating

Sio Mchina tu hata vyuma vya wazungu hupatwa na hizo hitilafu

Mkurugenzi anataka hesabu tu inapigwa tupa geuka bila service ya maana lazima yakukute

New Force ana Zhongtong Mega (Dar-Tunduma) hzijawahi kushika moto, matunzo baba
 
Back
Top Bottom