Adha ya foleni katika makutano ya barabara ya Mwenge

Makamura

JF-Expert Member
May 19, 2022
356
550
Kwa watumiaji wa barabara ya 'Bagamoyo Road' adha hii imekuwa janga kubwa sana hasa wakati wa Asubuhi na Jioni.

Ile sehemu ina Taa za kuongoza magari, lakini muda wa Asubuhi na Jioni wanakaa Trafiki ambao ndio chanzo cha foleni, mfana wasipokwepo huwezi kuta foleni kabisa.

Kama kuna utaratibu ambao sio wazi kuwa kwanini wanakuwa pale kusababisha foleni basi uwe wazi na waangalie namna nzuri ya kuepusha foleni lile eneo magari yanajaa mnoo hasa wanaotoka upande wa tegeta kuelekea mjini, na ile ni HighWay ila inakuwa na mkanda kutoka pale kwenye taa hadi njia panda ya Kawe au Darajani(Bondeni).

Naomba wajali swala la muda wote tunahitaji kuwahi tunaomba hili swala lishughulikiwe na mamlaka husika mana ni keroooooo sanaaaaa, na linakwaza.

images%20(35).jpg
 
Niliwahi kupata ushuhuda mmoja wa ajabu sana hapo kwenye hiyo jam, tena aliyeniambia ni mmoja kati yao kwamba inatengenezwa jam ili wapige hela! HAKUFAFANUA
Huenda.. coz ni kazi yao asubuhi na jioni ndo kunajaa mnoo..
 
Halafu hapo pesa nyingi zimetumika zilizoambatana na usumbufu mkubwa kwa kisingizio cha kupanua hiyo barabara ili kupunguza foleni ila taabu iko pale pale.
 
Hata Kwa wale wanaotokea upande wa barabara ya kutoka Coca-Cola kwanza Ltd kuja mataa ya Mwenge ni mtihani mkubwa sana.

Askari hawakupi kipaombele hasa akiwepo yule Wipiii (woman police),

Haiti magari ya upande huo hadi foleni inafika Coca-Cola karibia ,

Akiona foleni imezidi anaitelekeza na kuondoka kuacha watu wajipitie watakavyo.

Kina askari mmoja Mwanaume pale huwa anajitahidi ku-balance katika kuita pande zote kwa uwiano,

Lakini akiwepo yule wipii ni shida, Mara nyingi imeonekana hivyo,

Na wala hajali wala nini!
 
Back
Top Bottom