Mtindo wa kuita miundombinu majina ya watu binafsi pamoja na maraisi ukomeshwe, unaleta kutukuza watu isivyostahili wanapotimiza wajibu wao

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nachukia sana hili suala la kuiita miundombinu kwa majina ya watu binafsi, kama maraisi au watu wengine wanasiasa na wengineo. Kinachoniudhi zaidi ni kwamba mapendekezo ya majina haya mara nyingi hufanywa na watu ambao wana ajenda ya kujipendeke kwa raisi au wengineo.

Sikatai kwamba hawa watu, kwa mfano maraisi, wanakuwa wamesimamia vizuri mambo fulani. Lakini tujiulize, hivi kuna raisi au kiongozi yeyote ambae anasimamia hayo mambo kwa utashi wake, au anayafanya kama wajibu wake kwa kutumia kodi na tozo zinazolipwa na wananchi?

Tuchukue kwa mfano Mfugale Flyover, ambayo ilipewa jina la Mfugale kwa sababu wakati huo alikuwa ndio Mkurugenzi wa TANROADS. Sawa alifanya kazi nzuri, labda ni kweli, maana ndivyo alivyosema Magufuli, lakini nani alikuambia hakuna Mkurugenzi wa TANROADS atakae kuja kufanya kazi nzuri zaidi ya Mfugale? Kwa nini tuiite hii flyover jina la Mfugale kama vile yeye ndio amevunja rekodi ya Tanzania ya wakurugenzi bora wa TANROADS na hakuna atakaetokea kuwa bora zaidi yake?

Hivyo hivyo kwa maraisi. Mwinyi kile sijui, Mkapa hiki sijui, Kikwete hapa, Magufuli pale sijui, na sasa watu wanaanza kupendekeza Samia nini sijui. Kwa nini? Kwani hawa watu wanafanya hizi kazi kwa utashi wao au wajibu wao? Wanatumia fedha zao toka mfukoni au fedha zetu za kodi na tozo? Kwa nini tuwatukuze kwa kutimiza wajibu wao kwa kutumia kodi na tozo zetu?

Hili jambo liwekwe wazi, kwamba majina ya miundombinu ambayo tutayaacha ni ya Nyerere na Karume tu, waasisi wa Tanzania. Na ndio maana tulikubaliana kuwa hakuna picha ya raisi mwingine itawekwa kwenye fedha. Na iwe hivyo kwa miundombinu pia. Tuache hii tabia ya kujipendekeza kwa viongozi.

Tunaondoa majina yenye umaana mkubwa kihistoria kwa sababu tunataka kujipendekeza kwa raisi aliyeko madarakani. Kwa mfano daraja la Wami. Nani anajua historia ya jina Wami hadi tuamue halitufai na labda tuliite daraja la Samia?

Nakusihi Samia usikubali huu ujinga wa kutukuzwa, kama kweli kazi unayofanya kama raisi unaiona kama wajibu wako wa kikatiba na sio favor unayotufanyia Watanzania. Kama Samia unataka tuite kitu kwa jina lako, labda basi jitolee fedha zako kukijenga ili tukuenzi, lakini sio utimize wajibu wako kama raisi, utumie kodi na tozo tunazolipa kwa maumivu makubwa, halafu mwishowe tukiite kitu fulani ulichosimamia kwa jina lako.

Na pia ninapendekeza kwamba majina ya miundo mbinu iliyopewa viongozi zaidi ya Nyerere na Karume yabadilishwe mara moja!

Tuondokane na huku kujipendekeza kwa kuwatukuza watu, wanadamu kama sisi. Kwanza inawakatisha tamaa watu ambao wanachapa kazi zaidi hata ya raisi, the unsung heroes, wao watatukuzwaje?

Na pia Samia, kwa taarifa yako tu, kwenye mradi wa anuani za makazi watu wametoa fedha ili mitaa iitwe kwa majina yao, ujinga mwingine huu.
 
Mko wangapi kwani?
Au wewe ni msemaji wa wananchi millioni 60
Kwa hiyo ili nitoe maoni yangu lazima kwanza nikubaliane na wananchi milioni 60? Kwani wewe kutoa pointi hii ya kuniuliza swali hili la kijinga na kitoto umekubaliana na watu wangapi? Acha kuwa mtumwa wa kuongozwa na watu wengine kifikra. Be an independent thinker enough to provoke thinking by other people.
 
Unapendekeza tuipe majina gani?
Majina ya kihistria au yaliyopo yaendelee

Mkapa stadium - National Stadium
Mfugale Flyover - TAZARA flyover
John Kijazi Interchange - Ubungo Interchange
Bibi Titi Avenue - United Nations Avenue
  • Ocean Road
  • Independence Avenue
Mandela Freeway - Port Access Freeway
Magufuli Terminal - Mbezi Bus Terminal, nk
 
Hata ile fly over ya John Kijazi ibadilishwe, iitwe Mkwawa flyover kutambua mchango wake wa kupambana na Wakoloni
John Kijazi Interchange = Barabara ya Juu ya John Kijazi. Hivi ipi ni sahihi ya kimombo au ya kiswahili?
 
Libaki jina la JPM tu
Yabaki majina ya Nyerere na Karume tu, mengine yote futa rudisha majina ya zamani.

Tusipokomesha huu ujinga kuna siku watu watu wenye kimbelembele cha kujipendekeza watapendekeza Mlima Kilimanjaro uitwe Samia Mountain au raisi mwingine ajaye

Tulia anakuwa raisi labda, utasikia watu wanasema Lake Victoria tuliite Lake Dr. Tulia!
 
Back
Top Bottom