Mtikila: Kagame amepenyeza Wanyarwanda 35,000 Tanzania, Burigi, katika Wilaya ya Muleba

KING COBRA

JF-Expert Member
Nov 10, 2011
2,782
864
Mtikila amesambaza Waraka unaomtuhumu Kagame Kusambaza Wanyaranda 35,000 katika Tz na ameitaka serikali kuchukua hatua!!!

Ni jambo la Kushangaza Gvt inatumia Nguvu nyingi kulinda mpaka wa Malawi na Tanzania lakini Wamemwacha Kagame na Mseveni wakipenyeza Wanyarwanda 35,000 na wamehesabiwa katika sensa huku wakiendelea kuwatesa Raia!

Ni Ujinga mkubwa kuona kwamba Wanyarwanda wengi wameshaghushi Vyeti vya uraia na wengine wameanzisha makanisa kama alivyo Askofu Mulileghe Mkombo Kutoka DRC lakini Serikali badala ya kushughulika na Watu hao , inageuka na kuwatesa viongozi wa dini wanao pinga ufisadi ndani CCM na kuwakumbatia watu kama Mkombo ati kwa sababu anaombea viongozi wa Kitaifa!!!

Suala la kujiuliza ni Watanzania wangapi wanaweza kwenda Rwanda na kushika madaraka ra Serikali ya Rwanda na kuingiza mifugo huku wakitukana serikali ya Kagame???
Kama Wahutu wenye uraia wa Rwanda wamenyongwa kwa kuanzisha vyama vya upinzani sembuse Watanzania kuishi Rwanda???

Serikali itazame jambo hili kwa makini ikifikia Kagame na Joyce Banda wakaungana tunaweza kupata matatizo Makubwa!!!
Soma Waraka Wake Hapa:

 
Hawa jamaa ni noma,hapa Tz wamo Jeshini,Polisi,Magereza,TRA,TCRA,TANESCO,PCCB,MUHAS,EWURA,DAWASCO,TISS,mpaka Task Force,wanaangalia saa tu siku moja mkuu wa majeshi atakuwa na Tutsi origin,TISS HIVYOHIVYO,PCCB NA SERIKALINI KOTE.Wameingiza watu mpaka wamefikia ngazi za ukurugenzi na ukuu wa idara.
 
Nimetembea Karagwe na baadhi ya sehemu tajwa, ni bayana makundi ya Ng'ombe aina ya Ankole wenye Pembe ndefu wanaharibu mazingira kwa kiasi kikubwa. Wanakotoka na nani anahusika hapo sijui mcjenitoa roho. Serikali ifanye utafiti wa kina kuokoa hali hiyo.
 
Huyu mzee Mtikila serikali huwa inampuuza na kumwona kama hamnazo vile lakini kiukweli mambo ambayo huwa anayatoa ni kweli tupu!

Kagame na Mseveni lao ni moja...kumega ardhi ya Tanzania yaani mkoa wa Kagera uende Uganda na Kigoma uende Rwanda! kila mwaka mseveni anasogeza mpaka wake kuingia ardhi ya Tz. beacons za mpaka zimeng'olewa, waganda wanalima katika ardhi yetu na wanamiliki kuwa ni mali yao! Kagame yeye anaruhusu wafugaji wa nchi yake kuingiza ng'ombe katika misitu ya hifadhi ya nchi yetu. kagame ameruhusu wanawake wa kinyarwanda waolewe na watanzania lakini kamwe wao na watoto wanaozaliwa hawaachi asili yao. Wanasoma katika nchi yetu wanakuwa viongozi tangu ngazi za vitongoji, wanawakaribisha ndugu zao toka Rwanda. Idadi yao inaongezeka na kuwa threat kwa usalama wa TZ, but the giant Tanzania is sleeping!


Mkitaka kujua Kagame na Mseveni lao ni moja na wako against Kikwete tafakari hili. Hivi karibuni baada ya serikali yetu kupitia Waziri Membe kutoa tamko dhidi ya wapiganaji wa M23 kwamba tutapeleka majeshi yetu DRC Kagame na Mseveni waligoma kuhudhuria hafra moja ya E
AC huko Arusha. walituma wawakilishi wao tu!

Our dear President Kikwete and TISS wake up and ACT now
! sisi tunaweza tukafa leo lakini tukawaachia matatizo watoto na wajukuu wetu kesho!
 
Kwa serikali yetu kihiyo utasikia TUNATOA TAMKO huku mali zetu zinaenlea kuharibiwa wao wanakomalia matamko na miito.
 
namuunga mkono Mtikila asilimia 100 mf, cheki Idara za Serikali Police, magereza, Jwtz wakurugenzi kama aliyestaafu sengerema mwaka jana nenda SUA mwanza jiji, jamaa wa juzi aliyekuwa anatetewa na Mh, Kagasheki kule Bukoba Mh, Chagonja na na mkewe ambae kajipenyeza na na kuwaingiza jeshini ndugu wa mkewe ikapelekea kutaka kumfukuzisha jamaa mmoja wa uhamiaji kazi hadi akahamishiwa loliondo sababu alishindwa kumpatia mnyarwanda paspot shemeji ya chagonja. Juzi ng,ombe wa kinyarwanda wamekamatwa huko Ngara wakiharibu mazingira
 
Hii Tanzania na aina ya viongozi tulionao inatia shaka. Inakuwaje mtu ambaye hata jeshi,usalama wa taifa,polisi wala intelijensia ya namna yoyote akapata taarifa muhimu namna hii kuhusu usalama wa taifa letu wakati tuna idara lukuki zihusuzo uslama ziko kimya! Tueleweje? zaidi ya kuamini yasemwayo?

Wenzetu wameshaanza kujipanga kuishi kama ufalme (empire) kwa ajili ya vizazi vyao, sisi tumebaki tunaishi kama kuku kwamba kesho itajiju! hii ni hatari sna ki kweli kwa usalama na uhai wa taifa letu.

Hao wenye mamlaka ni kazi gani wanafanya?
 
Serikali pamoja na TISS wako makini kuidhibiti CDM na upinzani kuliko Kulinda Usalama wa watanzania na Mipaka yake, kwao adui yao mkubwa ni Vyama Vya Upinzani na hasa CDM. Pengine hata Mkulu naye si Mtz!!

Hapa ndipo ambapo wale watanzania wenye "akili" wanapomkumbuka "Baba wa Taifa", JK orijino!!
 

Kikwete ni dhaifu mno, TISS wamekuwa kitendo cha upelelezi chini ya CCM, kupeleleza upinzani. Polisi wanaitumikia CCM kazi yao kubwa ni kudhibiti upinzani. Na msishangae kusikia kuwa kutakujakuwa na nchi inayoitwa CCM baada ya miaka ijao. Who cares about Tanganyika au Tanzania. Wakubwa wa Jeshi wanasubiria kupewa ukuu wa Mikoa na wilaya ndio imekuwa kazi yao siku hizi. Tanzania amekufanayo JK Nyerere
 
Serikali ya CCM itampuuza Mtikila na huu waraka wake kwa vile adui namba moja kwao ni Chadema na Dr Slaa pekee. Nguvu na akili wamezielekeza huko.
Ila ukweli taifa linaangamia kwa ajili ya vionggozi wetu kukosa uzalendo na maarifa
 
MENGINE YANA UKWELI NA MENGINE NI CHUKU TUUU YA WATUTSI, Me naona Kagame na Mseveni wanaiba kivyaoo ila kuhusisha sijui na serukama mara sijui nani hizo ni chuki za ziada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…