Mtendaji: Ulitakiwa uandike "Mgombea Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwembeni" na siyo "Mgombea Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwembeni"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,485
147,246
Mmoja wa wagombea aliyekatwa ameelezwa na Mkuu wa Rufaa kwenye kata yake kuwa wamemuondoa kwa sababu kwenye fomu yake ameandika anagombea nafasi ya “Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwembeni”.

Mtendaji kamwambia alipaswa kuandika anagombea nafasi ya “Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwembeni”

Source: ITV habari

My take:
Nimebaki nacheka tu kwa mshangao!!!!
 
Nasubiria na vyama vingine vyenye ushawishi kama Cuf, Act, Nccr, nk navyo kutangaza kujitoa ili ibakie Ccm yenyewe. Hii ndiyo njia pekee sahihi iliyobakia.
 
Suluhisho ni nini?
Waresist ili mje na hoja ya waleta vurugu?

Walichokifikia mi nadhani ni wapo sahihi tuu ili Wenye mji wao wapite bila kupingwa kiulain zaid.
Ukiwa mwanasiasa ni lazima uwe na ngozi ya chuma!
 
Utetezi wa Polepole ndiyo ujinga zaidi.

Et kuna wagombea wamekosea majina ya vijiji na mitaa wanayogombea!!

Kama baadhi ya vijiji/vitongoji/mitaa vingekosa wagombea wa vyama vyote kwa kujaza form isivyo sahihi inge-make sense.

Yaani CCM nchi nzima akosekana popoma hata mmoja ila wapinzani tu?

Hizo semina za kufundisha wanaCCM kujaza form zilifanyikia wapi,mbona huku nilipo hazikufanyika?

Mambo mengine ni fedheha.
 
Daah kwa hiyo hii ni mojawapo ya sababu za kuondolewa?

Hivi Watendaji wanapomkata mgombea hawapaswi kutoa sababu?
 
Unafanya mazoezi miaka yote, viwanja vyote vya mechi unamiliki wewe, umefanya usajili wa vipaji vyote vikubwa.

Refa, kamisaa, VAR na mashabiki wote ni wa kwako na wanakushangilia wewe, kwanini upige risasi za miguu wachezaji wa timu pinzani siku ya mechi inapokaribia?
 
Back
Top Bottom