Elections 2010 Mtei amwonya Kikwete

CCM wana mkakati wa kuwa kila mwenye maisha ya kati (middle class) au tajiri ni FISADI. Ili baadae tuamue kutafuta suluhu kuwa mwenye nacho abakie nacho tuanze afresh. Hili linaanza kupikwa hapa hapa.

Take care, huenda hili ndo kundi la majambazi alosema HALISI.
 
William ajajibu swali aliloulizwa tangu mwanzo. Ataje mali na utajiri wa mzee Mtei alioona unamweka katika kundi la mafisadi.
Naona hakujibu badala yake amejaribu kupindisha mjadala na kuelekea kutojibu swali hilo.
Please William. Jibu hili kwanza ua kanusha statement yako.
Mzee mtei alikuwa kiongozi mwaminifu hafananishwi na hizi taka za leo hata kidogo. Maana sikuwahi kusikia vituhuma kama hivi kwake. Lakini kwa miaka ya 90 na kuja mbele tumesikia vituhuma vingi tu kwa viongozi wetu wengi. Shame.
 
anna kilango malecela aliiba fedha za Gulf Airways wakati ameajiriwa kama mhasibu wao. william malecela kabla hujamvamia edwin mtei anaza kumhoji anna ambaye mnaishi nyumba moja.
 
Felister,
Ni life uncertainty gani iliyomsibu Lowassa? He has everything and more and he still wants to grab more.
 
Felister,
Ni life uncertainty gani iliyomsibu Lowassa? He has everything and more and he still wants to grab more.

Baada ya uhuru watanzania wote tulikuwa poor either absolutely or relatively kwa kipimo cha dolar so to me we all started as poor ila society yenyewe ndo iliharibu kwa kuwamistreat watu wote waliojitolea kwa moyo kulitumikia Taifa na ku end up kutupwa na community baada ya kikomo cha utumishi wao. We now call them our heros yes they are but also are the victims of their own decision for it was them who did not creat the sustainable system which could have taken care of them after the retirement. Hata hivyo si kosa kufanya kosa but ni kosa kurudia kosa lile lile kila mara. Ndiyo maana kwa mtu anaeona mbali atajihusisha katika kujenga sustainable system itakayo take care everybody for if its not system which would take care of the individuals then the fact is; the life of an individual is shotter than that of the institutions otherwise kamba uliyoisuka mwenyewe yaweza kugeuka kuwa kitanzi chako and therefore become a victim of your own decision.
 

swali kwani NSSF si wanawakata watu kila mwezi kwani hawalipi watu pension zao au zote ndio manji kashagawana na mkullo, alafu watu wakienda wanazungushwa
embu wenye kujua NSSF ikoje watudokezee ...
 
anna kilango malecela aliiba fedha za Gulf Airways wakati ameajiriwa kama mhasibu wao. william malecela kabla hujamvamia edwin mtei anaza kumhoji anna ambaye mnaishi nyumba moja.

- Labda ungemshauri mjomba wako Mboma kwanza arudishe Kiwira, halafu uje uongelee wizi wa Mama Kilango, au?

Respect.

FMEs!
 

- Mkuu jitahidi kutaja jina langu na hoja nzito, swali langu vipi mbona hujalijibu juu ya mali za wizi za viongozi wa CCM? Kwa maneno yako hapo juu ni clear kwamba humjui Mtei, wanaomjua wamesema alifamnya kazi nje kama Director wa IMF, hawakusema maneno kama yako, next time kabla hujanitaja jina langu jaribu kutumia busara mkuu, na usiniulize majibu wakati unaoneakan unayo maswali.

Ahsante Mkuu.

William.
 
- Labda ungemshauri mjomba wako Mboma kwanza arudishe Kiwira, halafu uje uongelee wizi wa Mama Kilango, au?

Respect.

FMEs!

Kwi kwi kwi!!! hawa mafisadi wameua Kiwira yetu yaani hata mimi nikiwaona naweza kurusha ngumi.

Kule Kyela hakuna ajira nyingi za maana, ndugu zetu walikuwa wanaponea pale Kiwira, sasa imegeuka gofu. Kumbe Mboma naye yumo?

Afadhali mungu alimlaani kule Mbeya vijijini. kwi kwi kwi!!!
 

- Sawa sawa aje ndugu yake akanushe hapa kwamba baba yake mdogo hayumo Kiwira, halafu aeleze pale kwenye Hotel ya karibu na JFK Airport baba yake alienda kukutana na nani ile siku?

- Wewe unafikiri wananchi wa Mbeya ni wajinga kumnyima ubunge Mkuu mzima wa Majeshi? Uliwahi kusikia wapi ex-Chief Defense Force anashindwa kura za maoni tu? Tena Mbeya kule kijijini duh noma sana!

FMES!
 

Felister,
nimefurahi sana kuona post zako mbili kwenye mada hii.......keep it up!

In short......hili lishetani/lijinamizi la UFISADI tumelijenga sisi wenyewe....and the only way out ni kuondoa mizizi yake.....kubadilisha systeme ambazo zitatumia vyema resources tulizonazo kwa faida ya wote........again im impressed the way you put it...
 


huyu mzee mchango wake ni mkubwa
Tungekuwa na wazee kama hawa nchi hii ingeendelea
 

Bubu haya ni maneno uliyosema mwaka 2009, almost mwaka na nusu uliopita lakini ni very valid sasa. Hili swali ingekuwa vizuri tumuulize malaria sugu atujibu. Yanayofanyika sasa ni mipango ya Mkapa na Kigoda, sana sana awamu ya nne imefanya kazi ya kuyavurunda.
 
Huyu mzee asijifanye mtu wa uwiano wakati kama huu. Hiyo risala angeitoa mwaka jana au juzi ningemwelewa. Wakati huu alitakiwa kufanya kazi ya kampeni kwa chama chake ili tuje kumuenzi kama baba wa mageuzi. Inaelekea pia hafaham kuwa kipindi hiki ni cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu. Chadema for change!
 
Kingi,
Acha kukurupuka. Hiyo risala ilitolewa miaka 2 iliyopita. Angalia dateline.
 
Huo ni ushauri kutoka moyoni. Alipomshauri Mwl Nyerere akubaliane na ushauri wa IMF, Nyerere alikakata na kumwambia kama ushauri wake ulikuwa wa dhati ajiuzuru.

PHP:
Ushauri wangu wa kutoka moyoni, Kikwete jitoe kwenye kinyang'anyiro cha urais
 
Hapa angalia tofauti ya hekima na busara anayoitoa Mzee Mtei, isiyokuwa na ushawishi wa kisiasa bali mapenzi ya nchi na utaifa. Je unaweza kufananisha busara zake na zile pumba zilizotolewa na wale wazee waganga njaa wakina Ndejembi?

Namsifia Nyerere, mbona yeye mwenyewe alitolewa baruti alipotoa mapendekezo yake ya kuimarisha shilingi.

Na Nyerere alimtukana na kusema anatumiwa na wamagharibi. Kama ni CV toka kwa nyerere, basi Mtei aasingepewa hata nafasi ya kuzungumza.
 
Baadaye Mwalimu aligundua ushauri wa Mtei ulikuwa sahihi. Ndio maana Mwalimu akamshauri Mwinyi akubaliane na IMF. Kama Mwalimu angeambilika wakati aliposhauriwa na Mtei, hali haingekuwa mbaya kama ilivyokuwa miaka 80 - 85.

Mwalimu hakutaka "kugeuka jiwe" wakati akingali madarakani. Lakini alitambua mapema usahihi wa ushauri wa Mtei. Ndio maana hata akaamua kumteua Mtei awe mteule wake wa kazi ya Alternate Director IMF.

Kuna siku Mwalimu atakutana na Mtei Mbinguni. Mie nadhani Mwalimu ataomba msamaha.

Hayo yote ni tisa. Kumi ni kwamba someni kitabau cha Mtei "From Goatherd to Governor". It is a must read for anyone who has an interest in the contemporary history of Tanzania.
 
hivi JK aliwahi kusoma hii makala?? au hata kumpigia simu huyu mzee,mwanauchumi mwenzake??
 
Kwa muda mrefu sikusoma/sikufungua kompyuta na kusoma yanayosemwa juu yangu binafsi. Leo ndiyo naona hii ripoti ya Asha Abdalla baada ya kuzungumza nami hapa nyumbani kwangu.

Nashukuru wanaJF wengi kwa kukubaliana nami kwamba nilikuwa mnyofu na muwazi ktk kutoa ushauri kwa Rais wangu. Nakubaliana na wale wanaodhani kwamba ni vema wazee walio na uzoefu wakachangia nao ktk mijadala.

Nikiri kwamba nimesikitishwa sana na matamshi ya wanaJF, kama William Malecela, kwamba mimi pia nilifanya mambo ya kifisadi.

Kwanza niseme kwamba mimi si tajiri. Hata katika kitabu nilichoandika na kuchapisha hivi karibuni "From Goatherd to Governor" nimeeleza jinsi nilivyoweza kununua shamba la Ogaden baada ya kujiuzulu Uwaziri wa Fedha mwishoni mwa mwaka1979. Shamba hili lenye ekari 52 tu, lilibadilishwa na nyumba yangu ya Mzinga Way, OysterBay baada ya Mkadiriaji (Valuer) kukadiria thamani ya hiyo nyumba. Hiyo nyumba niliijenga kwa mkopo toka Serikalini.

Nimeeleza pia kwamba kwa miaka minne nilikuwa Executive Director wa IMF kwa kuteuliwa na Mwalimu Nyerere; na kwamba napokea pensheni toka Shirika hilo tangu nilipotimiza miaka 55; pamoja na ya Serikali ya Tanzania kutokana na utumishi wangu kama Permanent Secretary to the Treasury nilikostaafu kutokana na kuteuliwa Gavana wa Benki Kuu Januari 1966. Tunajazia pensheni hizi kwa kulima kahawa na kufuga ng'ombe, nguruwe na kuku.


Najivunia kwamba siishi kwa kujititimua, na mke wangu pia hana makuu. Kwa hiyo tumeweza kusomesha watoto wetu waweze kujitegemea; na sasa sisi wenyewe tunaweza kuendesha maisha bila matatizo ya fedha.


Nieleze pia ni jambo la kusikitisha kwamba Watanzania tumedidimia kimaadili kiasi kwamba vijana wetu wengi, kama William , wana dhana kwamba mtu yeyote mwenye fedha ni lazima awe fisadi. Tunahitaji Mabadiliko ya kweli kuondoa dhana hii. Ni lazima tuwe na watu wanaojituma na kutoa jasho ili tupate kipato cha kuridhisha.

Fursa ya kubadili imejitokeza sasa kutokana na CHADEMA, kumteua Dr. Slaa kugombea u-Rais. Ni excitement hii ya kwamba INAWEZEKANA KULETA MABADIKO YA KWELI ifikapo Oktoba 2010 yamenifanya, kama Muasisi wa hiki chama, nikose kusoma thread hii mapema. WanaJF nawaomba radhi kwa ku-comment so late.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…