Mtazamo wangu, mabadiliko yanayohitajika...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Naona haya ni mabadiliko ambayo watanzania wengi wanataka...

1. Kuvunja Muungano..

Huu Muungano na uvunjwe Tu kuliko kutumia Damu za watu kuulinda..

2. Kuifuta CCM..
Hiki chama hakiwezi kabisa kushindana bila kuiba kura wala ubabe na vurugu.
Kwa afya ya Demokrasia yetu kivunjwe na kipigwe marufuku kushiriki siasa, kibaki kwenye history Tu.

3.Katiba Mpya
Kila tukitaka katiba mpya zoezi
linaharibika kwa sababu ya Muungano
Tukishavunja Muungano
Katiba mpya itakuwa rahisi kuifikia..

4 Cheo cha Waziri Mkuu kifutwe.
Hiki cheo kinakuwepo sababu ya Muungano. Bila Muungano makamu wa Rais atafanya shughuli zote za Waziri Mkuu. Hakuna sababu ya kuwepo hiki cheo.

5. Mengineyo ongezea..
 
Katika mambo ambayo ni Magumu kutekelezeka ni haya uliyo ya ainisha hapa Mkuu ,nnaikumbuka kauli aliyowahi kuitoa hadharani na kusema nna mnukuu"atakae jaribu kuuvunja Muungano atavunjika yeye".

Ukijumlisha na Mfumo mzima wa Muundo wa Serikali inayo tokana na Chama Tawala ,Mfumo unao weza kuingiliwa/kutumika na wenye Chama kwa maslahi yao hakika ni ngumu hasa.

Mfano mzuri ni ktk Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 na yaliyo tokea ,wenye kutakiwa kusimamia Sheria waliacha jukumu lao na kuungana na Chama dola kuhakikisha Matakwa ya Chama dola yana timizwa kwa gharama yoyote ile.

Poleni sana wapenda Demokrasia ,poleni Wapinzani kwa Vifo/ vilema / Kesi za kubambikiwa na madhila ya kial namna.

R.I.P... Demokrasia ya kweli.
 
Hapo kwa waziri mkuu nakuunga mkono. Nchi nyingi (ukiacha zinazopenda kupeana vyeo) utakuta wana waziri mkuu au makamu wa rais lakini si wote.
 
Katika mambo ambayo ni Magumu kutekelezeka ni haya uliyo ya ainisha hapa Mkuu ,nnaikumbuka kauli aliyowahi kuitoa hadharani na kusema nna mnukuu"atakae jaribu kuuvunja Muungano atavunjika yeye".

Ukijumlisha na Mfumo mzima wa Muundo wa Serikali inayo tokana na Chama Tawala ,Mfumo unao weza kuingiliwa/kutumika na wenye Chama kwa maslahi yao hakika ni ngumu hasa.

Mfano mzuri ni ktk Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 na yaliyo tokea ,wenye kutakiwa kusimamia Sheria waliacha jukumu lao na kuungana na Chama dola kuhakikisha Matakwa ya Chama dola yana timizwa kwa gharama yoyote ile.

Poleni sana wapenda Demokrasia ,poleni Wapinzani kwa Vifo/ vilema / Kesi za kubambikiwa na madhila ya kial namna.

R.I.P... Demokrasia ya kweli.

Hata huko chama Dola kuna watu wanapenda demokrasia ya kweli pia
IPO siku watapata nafasi
 
Ibakie CCM imara tu na vyama vyote vya upinzani vifutwe na pia watu kama kina Zitto, Maalim Seif, Mbatia, Lissu, wasiruhusiwe kujiunga na chama chochote cha siasa.
 
Kwa mujibu wa Katiba kama Rais anatoka bara Makamu wake anatoka visiwani au vice versa hivyo cheo kinachotakiwa kufutwa ni cha makamu wa Rais isitoshe maswala ya muungano yako chini ya makamu wa Rais.
Muundo wa muungano ubadilike ama tuwe na serikali tatu au tuwe na serikali moja kwa muundo wa sasa hivi kila siku kushugurikia kero za muungano hautatufikisha popote na kila kiongozi anaona aibu muungano kuvunjikia mikononi mwake anahalalisha maovu ili mradi amalize kipindi chake
 
Katika mambo ambayo ni Magumu kutekelezeka ni haya uliyo ya ainisha hapa Mkuu ,nnaikumbuka kauli aliyowahi kuitoa hadharani na kusema nna mnukuu"atakae jaribu kuuvunja Muungano atavunjika yeye".

Ukijumlisha na Mfumo mzima wa Muundo wa Serikali inayo tokana na Chama Tawala ,Mfumo unao weza kuingiliwa/kutumika na wenye Chama kwa maslahi yao hakika ni ngumu hasa.

Mfano mzuri ni ktk Uchaguzi Mkuu huu wa 2020 na yaliyo tokea ,wenye kutakiwa kusimamia Sheria waliacha jukumu lao na kuungana na Chama dola kuhakikisha Matakwa ya Chama dola yana timizwa kwa gharama yoyote ile.

Poleni sana wapenda Demokrasia ,poleni Wapinzani kwa Vifo/ vilema / Kesi za kubambikiwa na madhila ya kial namna.

R.I.P... Demokrasia ya kweli.
Kumbuka na kusema pia,karibu democrasia feki.
 
Rais alipwe mshahara kama wa mbunge (anaolipwa mbunge kwa sasa) na mbunge alipwe msahara kama wa mwalimu.
Posho ya mbunge iwe sawa na posho ya mtendaji wa kata anayopewa anapohudhulia kwenye vikao vya halmashaur (hapa mbali na hiyo posho mbunge tumpe chumba cha kulala na chakula anapo kuwa bungeni )

Hapa ndio watajua ni nn tunaowachaguwa wanakipitia sio kutuletea ujinga
 
Kwa mujibu wa Katiba kama Rais anatoka bara Makamu wake anatoka visiwani au vice versa hivyo cheo kinachotakiwa kufutwa ni cha makamu wa Rais isitoshe maswala ya muungano yako chini ya makamu wa Rais.
Muundo wa muungano ubadilike ama tuwe na serikali tatu au tuwe na serikali moja kwa muundo wa sasa hivi kila siku kushugurikia kero za muungano hautatufikisha popote na kila kiongozi anaona aibu muungano kuvunjikia mikononi mwake anahalalisha maovu ili mradi amalize kipindi chake
Ukishavunja Muungano huitaji makamu wa kutoka Zenji
Makamu atatokea bara na atakuwa msaidizi wa Rais kama alivyo waziri mkuu..
Sio lazima aitwe makamu wala waziri mkuu
Anaweza kuitwa naibu Rais kama South Africa na Kenya
 
Nchi kubwa zinajaribu kuungana wakati nchi maskini zinajaribu kuvunja muungano, kumradhi ila haya ni mawazo ya kijinga na kibinafsi, mnatamani kuwe na serikali ya majimbo au kuvunja muungano ili baadhi ya wanasiasa wa upinzani na wao wajiite marais tu, huu ni ubinafsi, mnaonyesha rangi zenu zilivyojawa na tamaa, ubaguzi uliokithiri na ujinga usiomithilika.
 
Back
Top Bottom