Mtazamo: Mwaliko wa vyama vya siasa Kwenda Ikulu ulikuwa ni mkakati wa kuwagawa wapinzani hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,036
144,401
Kwa mtazamo wangu,mwaliko wa baadhi ya vyama siasa kwenda Ikulu ulikuwa ni mpango mkakati wa kuwagawa wapinzani na hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo lengo likiwa ni kuwafanya wasiaminiane na pia ili waje wagawane kura.

ACT wamealikwa sambamba na vyama vingine ambavyo baada ya kikao cha huko Ikulu, baadhi ya vyama vilivyoshiriki vinaanza kuwashambulia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla, hii ni kuleta tafsri kuwa wote walioshiriki hicho kikao hawakuwa wapionzani wa kweli hivyo hata ACT nayo itatazamwa kuwa sio wapinzani hata kama waliitikia wito huo kwa ni njema tu.

Kwa mtazamo wangu,wapinzani(CHADEMA na ACT) walipaswa kukutana kwa dharura na kutafakari mwaliko ule na zaidi wangejiuliza ni kwanini CHADEMA hawakualikwa na nini yangekuwa matokeo ya ACT kushiriki mkutano ule bila wenzao wa CHADEMA.

Kwahiyo, hawa walioshiriki mkutano ule na sasa wanaishambulia CHADEMA, watu hawa wako katika utekelezaji wa mpango wa kuwagawa wapinzani ama kwa kujua au kutokujua.

Combination ya ACT na CHADEMA ni tishio kwa chama cha kijani kwa pande zote za Jamuhuri na wakifanikiwa kuwagawa, basi chama cha kijani kitakuwa kimefanikiwa kuzigawa kura za wapinzani hasa kwa upande wa Zanzibar na katika kura za wagombea uraisi ambazo zinatoka pande zote za Muungano licha ya Zanzibar kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura ila kura zao bado ni muhimu hasa pale ushindani unapokuwa mkali(ikitokea hivyo).

Wadanganyika tungekuwa tunajitambua, CCM ingepata kura chache kuliko vyama vingine vyote vikubwa vya upinzani hata ikitokea wapinzani wamegawanyika ila ndio hivyo wajinga bado wengi nchi hii.

NB:
Katika juhudi za kuendelea kuwagawa wapinzani na kuwafanya wasiaminiane,ACT kuanzia sasa wanaeza kuachwa wafanye siasa bila kubughudhiwa huku CHADEMA wakiendelea kushughulikiwa-Zitto itumie nafasi hiyo kuendelea kurusha makombora.
 
Pona na ccm ni kuhakikisha wapinzani hawaungani. chondechonde wapinzani msiingie kwenye mtego wa ccm.
 
Kabla ya mwaliko wa ikulu wapinzani walikuwa wanapatana ?,,ilikua sio rahisi kukutana kwanza wakati wenyewe kwa wenyewe hawapatani,na hata hao walio alikwa ikulu bado hawaaminiani mpaka sasa!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikunbushia juzi kwenye mada ya kuwanya wapinzani wawe wamoja na wasisikilize wapambe nuksi. Tunafahamu mlengwa ni chadema na ACT. Ndio maana Mara baada ya kutoka ikulu Maalim Seif gwiji was siasa alilazimika kuweka wazi mazungumzo yao na alimtaka Rais kukutana na upinzani kwa Pamoja. Na vile vile alizungimzia mambo ya Zanzibar. Kitaalamu ACT wako shwari. Huo msala wameachiwa lipumba na Mbatia. Lipumba anaeleweka alivyosaliti ukawa na anajulikana anavyoendelea kutumika kuvuruga upinzani. Huyu Mbatia yeye ni ingizo jipya kwa Sasa. Vyama makini vya Chadema na ACT vinahitajiana kila upande. Viongozi wajenge kuaminiana na kuzungumza wenyewe ndani huko. Kama Kuna msaliti atajulikana tu. Lin nasisitiza kuwa making Sana kwenye hoja na kiongozi wasisikilize wapambe nuksi.
 
Tuache utani, chai ya ikulu nani anaweza kuikataa? Ni kuandika historia!
Kwanini kila anaefika pale akitoka huwa ni mwingine kabisa?? Ile chai huwa ina nini?? Ule ukuta wa jengo jeupe kila anaengia ndani na kuitizama kwanini akili zake zinabaki pale pale?? Ref Wale wote waliokuwa na misimamo ya dhati wakishaingia mle ndani wakitoka akili siyo zao tena. Nawaza tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbatia kutaka kushambulia upinzani kwa kutumia hoja za ukawa bi ishara kuwa hip ni entry point katika kazi anayoifanya Sasa. Kwa Nini Sasa? Hapa panaashiria kuwa Kuna Jambo. Siasa ni sayansi. Usikute anejitathmini kwa Sasa Hana nafasi kwenye ukawa na kaamua kujipeleka karibu zaidi na CCM ili aweze kuservive. Mazingira ya Sasa hayampi nafasi kuendelea kutrend Kama ilivyokuwa wakati ule.
 
Lipumba ni old dog aliyebebwa kwa kazi maalumu kumsaidia Magufuli kwa njia mbali mbali. Ukabila ukihusishwa. Huyu Hana nafasi zaidi ya kazi ya usaliti kuelekea 2020. Sio material popote zaidi ya kutoa uzoefu wake kwa dola kuhusu mbinu za upinzani. Yupo pale Kama tester tu, ama kionja mchuzi Cha kuharibu demokrasia. Huyu ataalikwa pasipostahili ilimradi kuzuga na kuharibu.
 
Yup, ACT ni hatari kwa Zanzabar wakati CDM ni hatari kwa upande wa Tanganyika. Wakiacha ubinafsi na uroho wa madaraka wanaweza kuigalagaza CCM, na safari hii mabeberu wako macho, serikali ikiingia tu kingi basi kuna watu tanzania ya 2021 wataisikia kwenye redio tu.
 
Kwa mtazamo wangu,mwaliko wa baadhi ya vyama siasa kwenda Ikulu ulikuwa ni mpango mkakati wa kuwagawa wapinzani na hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo lengo likiwa ni kuwafanya wasiaminiane na pia ili waje wagawane kura.

ACT wamealikwa sambamba na vyama vingine ambavyo baada ya kikao cha huko Ikulu, baadhi ya vyama vilivyoshiriki vinaanza kuwashambulia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla, hii ni kuleta tafsri kuwa wote walioshiriki hicho kikao hawakuwa wapionzani wa kweli hivyo hata ACT nayo itatazamwa kuwa sio wapinzani hata kama waliitikia wito huo kwa ni njema tu.

Kwa mtazamo wangu,wapinzani(CHADEMA na ACT) walipaswa kukutana kwa dharura na kutafakari mwaliko ule na zaidi wangejiuliza ni kwanini CHADEMA hawakualikwa na nini yangekuwa matokeo ya ACT kushiriki mkutano ule bila wenzao wa CHADEMA.

Kwahiyo, hawa walioshiriki mkutano ule na sasa wanaishambulia CHADEMA, watu hawa wako katika utekelezaji wa mpango wa kuwagawa wapinzani ama kwa kujua au kutokujua.

Combination ya ACT na CHADEMA ni tishio kwa chama cha kijani kwa pande zote za Jamuhuri na wakifanikiwa kuwagawa, basi chama cha kijani kitakuwa kimefanikiwa kuzigawa kura za wapinzani hasa kwa upande wa Zanzibar na katika kura za wagombea uraisi ambazo zinatoka pande zote za Muungano licha ya Zanzibar kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura ila kura zao bado ni muhimu hasa pale ushindani unapokuwa mkali(ikitokea hivyo).

Wadanganyika tungekuwa tunajitambua, CCM ingepata kura chache kuliko vyama vingine vyote vikubwa vya upinzani hata ikitokea wapinzani wamegawanyika ila ndio hivyo wajinga bado wengi nchi hii.

NB:
Katika juhudi za kuendelea kuwagawa wapinzani na kuwafanya wasiaminiane,ACT kuanzia sasa wanaeza kuachwa wafanye siasa bila kubughudhiwa huku CHADEMA wakiendelea kushughulikiwa-Zitto itumie nafasi hiyo kuendelea kurusha makombora.
Uhakika ni kwamba alichoongea Magufuli kwa Maalim Seif hakifanani hata chembe na alichoongea na Mbatia na Lipumba , hawa wawili walipewa maagizo tu , Maalim Seif si mtu wa mchezo hata chembe
 
Pona na ccm ni kuhakikisha wapinzani hawaungani. chondechonde wapinzani msiingie kwenye mtego wa ccm.

Kimsingi muungano ni hiari, kama mtu anaona akiwa ndani ya muungano anapoteza anatakiwa atoke haraka sana. Niwe mkweli, muungano wa vyama vya upinzani ni hatari kuliko faida zinazosemwa.
 
Kwa mtazamo wangu,mwaliko wa baadhi ya vyama siasa kwenda Ikulu ulikuwa ni mpango mkakati wa kuwagawa wapinzani na hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo lengo likiwa ni kuwafanya wasiaminiane na pia ili waje wagawane kura.

ACT wamealikwa sambamba na vyama vingine ambavyo baada ya kikao cha huko Ikulu, baadhi ya vyama vilivyoshiriki vinaanza kuwashambulia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla, hii ni kuleta tafsri kuwa wote walioshiriki hicho kikao hawakuwa wapionzani wa kweli hivyo hata ACT nayo itatazamwa kuwa sio wapinzani hata kama waliitikia wito huo kwa ni njema tu.

Kwa mtazamo wangu,wapinzani(CHADEMA na ACT) walipaswa kukutana kwa dharura na kutafakari mwaliko ule na zaidi wangejiuliza ni kwanini CHADEMA hawakualikwa na nini yangekuwa matokeo ya ACT kushiriki mkutano ule bila wenzao wa CHADEMA.

Kwahiyo, hawa walioshiriki mkutano ule na sasa wanaishambulia CHADEMA, watu hawa wako katika utekelezaji wa mpango wa kuwagawa wapinzani ama kwa kujua au kutokujua.

Combination ya ACT na CHADEMA ni tishio kwa chama cha kijani kwa pande zote za Jamuhuri na wakifanikiwa kuwagawa, basi chama cha kijani kitakuwa kimefanikiwa kuzigawa kura za wapinzani hasa kwa upande wa Zanzibar na katika kura za wagombea uraisi ambazo zinatoka pande zote za Muungano licha ya Zanzibar kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura ila kura zao bado ni muhimu hasa pale ushindani unapokuwa mkali(ikitokea hivyo).

Wadanganyika tungekuwa tunajitambua, CCM ingepata kura chache kuliko vyama vingine vyote vikubwa vya upinzani hata ikitokea wapinzani wamegawanyika ila ndio hivyo wajinga bado wengi nchi hii.

NB:
Katika juhudi za kuendelea kuwagawa wapinzani na kuwafanya wasiaminiane,ACT kuanzia sasa wanaeza kuachwa wafanye siasa bila kubughudhiwa huku CHADEMA wakiendelea kushughulikiwa-Zitto itumie nafasi hiyo kuendelea kurusha makombora.

ACT Wazalendo haijaalikwa Ikulu. Muhimu sana hilo lieleweke vizuri.
ACT haitagonganishwa na CHADEMA. Viongozi wetu ni werevu sana
 
Mbatia kutaka kushambulia upinzani kwa kutumia hoja za ukawa bi ishara kuwa hip ni entry point katika kazi anayoifanya Sasa. Kwa Nini Sasa? Hapa panaashiria kuwa Kuna Jambo. Siasa ni sayansi. Usikute anejitathmini kwa Sasa Hana nafasi kwenye ukawa na kaamua kujipeleka karibu zaidi na CCM ili aweze kuservive. Mazingira ya Sasa hayampi nafasi kuendelea kutrend Kama ilivyokuwa wakati ule.
Ninachokiona mimi ni kwamba, Mbatia amekuwa na mazungumzo na baadhi ya wabunge ambao mazingira yalivyo sasa yanawafanya wasiwe na nafasi ya kupitishwa tena na Chadema kugombea ubunge, na kwa kuwa anawahitaji akidhani wataongeza kuaminika kwa chama chake, tayari ameishajua anaenda kuwa adui wa Chadema muda mfupi ujao. Ameanza na madiwani wale wa Mbeya.

Ifahamike uwezo wa Mbatia kisiasa katika kushawishi umma ni mdogo sana, hivyo katika kupambana na Chadema anaona back up yake iwe CCM, ambao pia lazima wataenda au tayari wameishampa fungu. Lakini, ni wapi Mbatia atakishambulia Chadema umma umwelewe? Ni vigumu. haishangazi sasa anaanza kuibuka na mambo ya UKAWA leo.Kote huku ni kutapa tapa, amejichafua na kama atapata jimbo 2020 labda ni kwa mtutu wa bunduki, ametibua nyoyo za wananchi ambao wamekerwa na siasa za CCM za awamu hii, ambao miongoni mwao ndio angeweza kupata kura kutoka kwao!

Asichokifahamu Mbatia ni kwamba, wananchi wana hasira kali, wala hawasumbuliwi tena na hii hama hama, ambayo wanajua ina ghiliba ndani yake!
 
ACT Wazalendo haijaalikwa Ikulu. Muhimu sana hilo lieleweke vizuri.
ACT haitagonganishwa na CHADEMA. Viongozi wetu ni werevu sana
Huu ndio muda wa kuanza kudai TUME HURU YA UCHAGUZI, huonekani kuonesha njia katika hilo. Mnataka kuidai lini?
 
Nilikunbushia juzi kwenye mada ya kuwanya wapinzani wawe wamoja na wasisikilize wapambe nuksi. Tunafahamu mlengwa ni chadema na ACT. Ndio maana Mara baada ya kutoka ikulu Maalim Seif gwiji was siasa alilazimika kuweka wazi mazungumzo yao na alimtaka Rais kukutana na upinzani kwa Pamoja. Na vile vile alizungimzia mambo ya Zanzibar. Kitaalamu ACT wako shwari. Huo msala wameachiwa lipumba na Mbatia. Lipumba anaeleweka alivyosaliti ukawa na anajulikana anavyoendelea kutumika kuvuruga upinzani. Huyu Mbatia yeye ni ingizo jipya kwa Sasa. Vyama makini vya Chadema na ACT vinahitajiana kila upande. Viongozi wajenge kuaminiana na kuzungumza wenyewe ndani huko. Kama Kuna msaliti atajulikana tu. Lin nasisitiza kuwa making Sana kwenye hoja na kiongozi wasisikilize wapambe nuksi.
Unachosema ni sahihi kwa asilimia 100 na wapinzani wakisiliza wapambe,basi wajue wataishia kutoaminiani na hata kugawanyika huku CCM wakifaidika na mgawanyiko huo.

Ni bahati mbaya hata baadhi ya washabiki wa CHADEMA wanaamini propaganda za wana-LUMUMBA kuwa ACT inataka kutumika na CCM kuhujumu upinzani.

Binafsi naamini CHADEMA wana nguvu sana kwa huku Bara, ila kwa Zanzibar bado, hivyo tunawahitaji ACT kwa upande wa Zanzibar na kwa maeneo machache huku Bara hivyo umoja wa hivi vyama ni muhimu sana katika uchaguzi mkuu ujao ingawa kutokuwa na Tume huru ni kikwazo kikubwa zaidi kwa upinzani hata wakiwa wamoja.
 
ACT Wazalendo haijaalikwa Ikulu. Muhimu sana hilo lieleweke vizuri.
ACT haitagonganishwa na CHADEMA. Viongozi wetu ni werevu sana
Asante sana kwa ufafanuzi huu na msimamo wenu kama chama wa kutogombanishwa na CHADEMA ni faraja kubwa kwetu tuliochoshwa na tawala hizi za CCM ambazo ndio chanzo cha umasikini wa Taifa hili na watu wake.

Pia, ni vizuri kama nyie ACT na CHADEMA pamoja na vyama vingine vyenye kujitambua(kama vipo) mkakutana na mkaja na kauli moja ya kuonyesha kuwa mko pamoja na hii itapunguza kama sio kuondoa kabisa hizi propaganda za kudai ACT inatumika na CCM.

Propaganda hizi zijibiwe kila inapobidi na bila kuchelewa.
 
Back
Top Bottom