Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,036
- 144,401
Kwa mtazamo wangu,mwaliko wa baadhi ya vyama siasa kwenda Ikulu ulikuwa ni mpango mkakati wa kuwagawa wapinzani na hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo lengo likiwa ni kuwafanya wasiaminiane na pia ili waje wagawane kura.
ACT wamealikwa sambamba na vyama vingine ambavyo baada ya kikao cha huko Ikulu, baadhi ya vyama vilivyoshiriki vinaanza kuwashambulia CHADEMA na UKAWA kwa ujumla, hii ni kuleta tafsri kuwa wote walioshiriki hicho kikao hawakuwa wapionzani wa kweli hivyo hata ACT nayo itatazamwa kuwa sio wapinzani hata kama waliitikia wito huo kwa ni njema tu.
Kwa mtazamo wangu,wapinzani(CHADEMA na ACT) walipaswa kukutana kwa dharura na kutafakari mwaliko ule na zaidi wangejiuliza ni kwanini CHADEMA hawakualikwa na nini yangekuwa matokeo ya ACT kushiriki mkutano ule bila wenzao wa CHADEMA.
Kwahiyo, hawa walioshiriki mkutano ule na sasa wanaishambulia CHADEMA, watu hawa wako katika utekelezaji wa mpango wa kuwagawa wapinzani ama kwa kujua au kutokujua.
Combination ya ACT na CHADEMA ni tishio kwa chama cha kijani kwa pande zote za Jamuhuri na wakifanikiwa kuwagawa, basi chama cha kijani kitakuwa kimefanikiwa kuzigawa kura za wapinzani hasa kwa upande wa Zanzibar na katika kura za wagombea uraisi ambazo zinatoka pande zote za Muungano licha ya Zanzibar kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura ila kura zao bado ni muhimu hasa pale ushindani unapokuwa mkali(ikitokea hivyo).
Wadanganyika tungekuwa tunajitambua, CCM ingepata kura chache kuliko vyama vingine vyote vikubwa vya upinzani hata ikitokea wapinzani wamegawanyika ila ndio hivyo wajinga bado wengi nchi hii.
NB:
Katika juhudi za kuendelea kuwagawa wapinzani na kuwafanya wasiaminiane,ACT kuanzia sasa wanaeza kuachwa wafanye siasa bila kubughudhiwa huku CHADEMA wakiendelea kushughulikiwa-Zitto itumie nafasi hiyo kuendelea kurusha makombora.