Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Mtanzania mwenzetu yupo Dubai anahitaji msaada

Kabisa mku, Bandle za lain za tourist zitamkwangura sana, Drh 50 wanakupa sana sana gb 2, hata wiki humalizi.
Speaking of line, Kuna mawasiliano ya agent nilipewa na member mmoja humu ila jamaa nilivyoitumia Ile Namba ya simu, akanambia eti line yake ni ya kupokea tu simu kupiga hawezi....hiyo nayo inakuaje wakuu?
 
Speaking of line, Kuna mawasiliano ya agent nilipewa na member mmoja humu ila jamaa nilivyoitumia Ile Namba ya simu, akanambia eti line yake ni ya kupokea tu simu kupiga hawezi....hiyo nayo inakuaje wakuu?

Labda iwe hajaitia pesa tu, Ukitua Air port Dubai Lain wanakupa bure kabisa siku hizi. wewe ununue vocha uweke tu. Na kwa kupiga ndani ya UAE gharama sio kubwa, akitia kadi ya Drh 25, kwa kupiga tu ndani ya nchi anaweza kutumia vizuri kwa mawasiliano ila asijiachie sana tu.
 
Kazi bongo zimeisha,, hao waarabu siwaelewi kabisa .. siwezi kwenda nchi yoyote kwa ujira wowote hata kama kuosha gari moja nilipwe dola 20..sikuzaliwa kwa ajili hio thamani yangu ni kubwa sana ..bora nibaki bongo
Au sio
 
Wachangiaji wengi hii hoja ni wanafiki na waongo wakubwa, hapa nchini fursa ni za connections tupu,kuna wengi humu wanalalama kuhusu ajira uchwara za afya na ualimu, welldone mkuu iliyetake risks na kwenda Dubai, maisha bila ya kutake risks, will die trying...asikate tamaa huko Dubai abakie huko huko apambane kiume na mwambie asahau kabisa msaada wa watanzania, akae nao mbali kabisa maana wengi ni washenzi tu.
Mkuu umenena vyema kabisa,wengi naona wanaleta hoja za kichawi tu. Eti "anaendaje sehemu hapajui", apajue ili iweje? Mwanaume hachagui kambi,na kambi ni popote kudadadek!!
 
Hiyo hela ya nauli,passport na gharama nyingine si bora tu angetegesha mahali hapahapa Bongo,angeweza hata kufungua carwash ya maana na angepiga hela ya kutosha,kuliko kuacha fursa hapa halafu unaenda kutafuta vibarua vya kuosha magari Dubai...
Mawazo ya watu waoga waoga haya,kwani unadhani jamaa kaziona fursana kuziacha tu hapa bongo? Kwamba unaamini jamaa ni mjinga sana kiasi kwamba hajawaza kama hiyo pesa anaweza kufanya iwe mtaji?
 
Nimemsikitikia huyo kijana na ninachoweza kusema ni arudi tu nyumbani. Alishafeli mapema sana kuanzia wakati anapanga safari yake. Ilitakiwa ampange mtu wa kufikia kwake tokea akiwa Dar. Pia kitendo cha kuchukua hela za bi mkubwa wake ni udhaifu na inaonekana kwao hawako vibaya kihivyo ila ni kutaka tu sifa kwamba anafanya kazi Dubai. Kikubwa zaidi kwa mpambanaji hupaswi kumlaumu mtu yeyote kwenye nyakati kama hizo.... anatakiwa amwombe Mungu na kukubaliana yuko Dubai yeye kama yeye sio mambo ya kusema "watanzania wenzetu". Na wewe unamfelisha zaidi kwa kuanza kumwombea msaada hapa JF.
 
Ilikuwa mwaka gani mkuu?
2007 mpaka kesho kuingia Hong kong sio rahisi lazima interview na wanarudishwa watu wengi maana wengi walikamatwa na unga kwa hiyo Watanzania lazima wapitie maswali tofauti na mwanzo...mimi nilienda hata kabla ya Corona napita kama naingia Tanzania tu
 
Yani natoka Tz kula ugali na Dagaa,Nazamia nchi ya watu kutegemea nitasaidiwa
 
Wakuu naomba msaada kwa yeyote ambae anaishi Dubai, nina Rafiki yangu huko ana mwezi wa pili Sasa tangu ameenda ila Bado hajapata Kazi

Jamaa ni kama alijitoa muhanga sababu hakuwa na connection yeyote, alijiandalia kuanzia Passport, Visa hadi Ticket ya ndege mwenyewe, Sasa kafika huko anadai mambo magumu.

Kakutana na baadhi ya wabongo wenzake anadai kwamba ni Binafsi sana, wanamchora tu mshkaji, ni kama vile wanaotaka jamaa arudi Bongo. jamaa nimempa moyo aendelee kupambana huenda atatusua

Mimi imeniuma sana kusikia wabongo tunakunjiana hivyo, hivi kweli unamuangalia Mbongo mwenzako anavyotaabika kwenye ma nchi ya watu Wakati chance ya kumsaidia unayo

Wakuu nawaomba msaada kama Kuna yeyote humu yupo Dubai amshike mkono jamaa, at least hata kimiongozo afanyaje ili aingie katika system angalau apate ahueni ya maisha

Haitapendeza kabisa kama jamaa atarudi Bongo, atakuwa ame waste time na fare, ukizingatia nauli yenyewe jamaa kafanya kuchangiwa na Bi mkubwa. Bi mkubwa kajitoa mwanae akapambane halafu ndio arudi bila bila.....Tusaidiane Wakuu

Natanguliza Shukrani[emoji1545]


View attachment 2275923View attachment 2275925View attachment 2275926

Anaitwa nani, mimi nipo hapa Dubai. Na pia alikuja huku kufanya nini, maana anaweza kuwa kibaka!
 
Mkuu umenena vyema kabisa,wengi naona wanaleta hoja za kichawi tu. Eti "anaendaje sehemu hapajui", apajue ili iweje? Mwanaume hachagui kambi,na kambi ni popote kudadadek!!
Sasa kinachomfanya analialia anaomba msaada ni nini😁
 
Muda mzuri kwa ajili ya kuzamia ni mwezi wa 9... Hapa unakata viza ya utalii so atakaa hapo kwa miezi 3. Ndani ya hii miezi ni yeye tu na kutafuta connection.
Na hiyo connection ni mpaka uipate, kama wenyeji wanamtolea macho tu, itapatikana kweli?
 
Aende sharjah ni mji karibu kidogo na dubai hapo pana unafuu wa chakula na kupanga kama hostel mnakua mnashare pia atembe sehem za construction sites zinaitaj watu sana ajaribu kuteka uaminifu wa watu aridhike na akipatacho ausome mji mwishowe atafanya kile kilichompeleka alichodhamiria mwanzo ni mgumu apambane ameshathubutu kimaisha endele kuthibitisha ni mpambanaji
 
Mwambie atafute Mkenya,Mganda, Mcongo,Mrundi na Sio wabongo watampa michongo,kwani Ile website ya job in Dubai aitembelei mbona Wana deiwaka za kutosha
 
Mwambie aende mji wa Sharjah kazi za meli tele akaombe deiwaka.
Anarudije home Sasa kwani yeye bubu.
Hata kazi za Bustani,usafi, ulinzi ajaona tu
 
Acheki Dubai job agency kazi zipo nyingi hata Qatar ajichanganye tu,hasa Kama ni Muislamu waislamu wenzake hawatamtupa kwa asiye chance ya ubaguzi ni kubwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom