Mtanzania kwenda anga za juu; gazeti lasema "mwezini"!

Netanyahu

Senior Member
Oct 2, 2008
147
22
Na Festo Polea
10/16/2009

ASHISH Thakkar anatarajia kuwa Mtanzania wa kwanza kwenda mwezini wakati atakapofanya safari hiyo mwakani.

Mtanzania huyo, ambaye ni chotara wa Kiingereza alienda Ikulu jijini Dar es salaam jana kumueleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu safari yake na kumuaga.

Thakkar, ambaye mama yake ni mzaliwa wa Mwanza na baba Uingereza, alimwambia rais kuwa anajisikia vizuri kuwa mwakilishi wa Afrika, na hasa Tanzania kwenye safari hiyo ya angani.

"Najisikia vizuri kuwa mwakilishi wa Afrika hasa Tanzania ambako mama yangu alizaliwa, na hii itakuwa nafasi muhimu kwetu kujitangaza duniani kote na kuieleza dunia kuwa Afrika tunaweza na tuna maliasili za pekee,"alisema Takkar alipokuwa akizungumza na Rais Kikwete.

Rais alimweleza Mtanzania huyo anatakiwa apige picha nyingi atakapokwenda mwezini kwa ajili ya kujitangaza zaidi na kuinadi sekta ya utalii kwa juhudi zake zote.

Rais Kikwete alimkabidhi mwanaanga huyo bendera ya Tanzania na kusema watu wenye damu ya Tanzania wapo wengi duniani kote, lakini hawajitokezi kuitangaza nchi kama anavyofanya Thakkar.

"Ni nafasi nzuri kujitangaza kwa kuwa hauwezi kufanikiwa katika utalii bila kujitangaza na tunataraji kupitia Thakkar tutatangaza vyema utalii wetu popote atakapokuwa mwanaanga huyu angani na ardhini,"alisema Rais Kikwete.

SOURCE: MWANANCHI NEWSPAPER .

MY COMMENTS

Ingekuwa nchi nyingine habari hii ingekuwa breaking news vyombo vyote vya habari vya nchi husika lakini Tanzania mhhhhhh hatujui kupigia kelele na parapanda tunapofanya vizuri medani za kimataifa kwa vitu kama hivi yaani taarifa hii haikupewa hata robo saa kwenye vipindi vya vyombo vyetu vya habari wako tayari kuweka nusu saa vipindi vya kuigiza vya BONGO DAR ES SALAAM NA VILE VYA ZE COMEDY VYA AKINA MASANJA LAKINI HABARI KAMA HII NZITO HAINA NAFASI.NDIO MAANA WATANZANIA WENGI NI MABWEGE.

Hongera Takkar na hongera Kikwete kumtambua na hongera Gazeti la Mwananchi kuweka habari hii.
 
Anaenda na nani sasa huko mwezini? Au Tanzania na sisi tumetengeneza chombo cha kwenda huko? Waandishi wa bongo bana...wanaboa kwelikweli
 
tusubiri tamko la CHADEMA juu ya hili
yaani hata katika masuala kama haya Mkuu Game, unaingiza game la politiq!
Labda langu liwe swali, Utanzania wa huyu mwanaanga ni kwa sababu ya damu ya mama yake, au ana uraia kwa maana ya kuupata kwa haki yake ya kuzaliwa nchini Tanzania, au ana dual citizenship ambayo Bongo ilikataliwa?
Na je, ni vema role yake iwe kutangaza utalii au kuinua sayansi nchini, hususan utafiti, ugunduzi, n.k
 
Hata vyombo vyote vya habari vingeiweka kuwa iwe breaking news inayorudiwarudiwa kila baada ya dakika moja kwa muda wa mwaka mmoja bado matatizo yetu ya umaskini yako pale pale. Waafrika tumeshindwa kufanya chochote cha maaana mpaka sasa tunataka mafanikio ya "kuchovya". Sio kama napingana na matakwa yako lakini naomba tusije kujisahau na kuanza kusheherekea mafanikio ya wenzatu huku kwetu bado kunazidi kudidimia...
 
yaani hata katika masuala kama haya Mkuu Game, unaingiza game la politiq!
Labda langu liwe swali, Utanzania wa huyu mwanaanga ni kwa sababu ya damu ya mama yake, au ana uraia kwa maana ya kuupata kwa haki yake ya kuzaliwa nchini Tanzania, au ana dual citizenship ambayo Bongo ilikataliwa?
Na je, ni vema role yake iwe kutangaza utalii au kuinua sayansi nchini, hususan utafiti, ugunduzi, n.k

Nitasema neno langu baada ya swali la maana sana la huyu mkulu hapa juu kujibiwa . Kijana huyub haijui TZ leo anarudi Tanzania kwamba ni Mtanzania kwa sababu mama yake alizaliwa Mwanza ? Hili pekee laweza kumfanya awe Mtanzania ? Sasa mwezini anaenda matembezi hadi aje an picha kibao kama JK alivyo muomba au inakuwaje ? Huko mwezini anatakiwa akawaeleze habari za Utalii ama inakuwaje maana nasoma sielewi message za JK kwa huyu jamaa
 
Hii inaonyesha ni jinsi what we can achieve given the opportunity.

ps. am i supposed to care?, or else join their club (what Phd does next) guys just hate, funny i aint spoken to many over a decade
 
Haendi mwezini. Who wrote this rubbish? He's only going about 100km up.. Pre-orbital space on Richard Branson's new Virgin Galactic "space ship" or rather more specifically a plane that reaches the border of space after being launched from a mothership. Tickets cost 200,000 dollars and ata papaa msoffe anaweza kwenda if he ddnt buy a few cars next year. I myself plan to go in the next 15 yrs if all goes well. Its not mwezini, ignorance is some crazy ish.LOL
 
Duh!

JF hamwezekaniki

yaani mjomba ulivyooua mpaka bas mwenyewe nimenyanyua mikoni juu
1
 
Haendi mwezini. Who wrote this rubbish? He's only going about 100km up.. Pre-orbital space on Richard Branson's new Virgin Galactic "space ship" or rather more specifically a plane that reaches the border of space after being launched from a mothership. Tickets cost 200,000 dollars and ata papaa msoffe anaweza kwenda if he ddnt buy a few cars next year. I myself plan to go in the next 15 yrs if all goes well. Its not mwezini, ignorance is some crazy ish.LOL

Pheeeew! afadhali wewe umekuja na kusema anaenda na nani na nini. Miafrika mingine hapa ilikuwa inazidi kuendeleza ujinga na uduni wa IQ zao bila hata kujua anaenda endaje huko 'mwezini'. I'm sick of Miafrika.
 
Huyo mtanzania anaishi wapi, Kariakoo, Lindi au Kahama?
Anasema mama yake ni/alikuwa mtanzania, na baba yake ni Muingereza, sasa ni rais wa wapi, Tanzania kweli? Atakuwaje raia wa Tanzania wakati hajakna uraia wa UK?
This is all about populist politics!

Huu ni udugu wa kujishikiza; tusubiri kidogo tutasikia kamegewa kipande cha wilaya fulani, licha ya kuwa siyo raia wa Tanzania!
Tumeliwa!
Ama kweli wenzetu wanajua namna ya kutumia weakness za viongozi wetu (cheap), style ya mkuu wa kaya wetu.
 
Jamani mbona watu wengine mnataka kukifanya kitu kidogo kama hiki kuwa big deal na ubishi wenu wa asili usio na maana yeyote, huyu hata kama sio raia wa Tanzania lakini kutokana na mama yake kuwa Mtanzania, hiyo pekee inamfanya awe na damu ya kitanzania, yeye kuja Tanzania kuchukua bendera ya nchi ni hisani kubwa sana kwani angeweza kufanya safari yake ya Space/Pre-Orbital Space bila hata kutaja asili yake ya Kitanzania.

Lakini kama kawaida wabongo mmeshaanza kutokwa na mapovu midomoni mwenu na maswali yasiyo na msingi. Ingekuwa nchi nyingine hii habari ingekuwa big deal na wangehakikisha wanatumia nafasi hiyo kutangaza utalii wa nchi yao ili kuvutia wengi kuitembelea.
 
Hmmm, hiyo safari ya kwenda mwezini iko lini au mwandishi anamaanisha kwenda kwenye International Space Station?
 
Wewe acha tu. Yaani habari yenyewe ina mapengo kama ya crackheads wa Bunkhead!

Mjomba anakwenda kama mtalii.

Dubai-based entrepreneur Ashish Thakkar, CEO of Kensington Real Estate, is in training at the NASTAR center near Philadelphia for his flight aboard Virgin Galactic. He’s keeping an online journal:

“Now we are taken to experience G force hands on in the machine! It’s difficult to describe this but is the closest thing to going into space and is seriously amazing…

“While I’ve known for months now that I’m going into space, today I really felt it. Virgin’s organisation, attention to detail and hospitality makes a real difference; and most importantly, the actual training is just out of this world – quite literally! Virgin is genuinely giving us an incredible experience.”
http://www.arabianbusiness.com/537086
 
Anaenda na nani sasa huko mwezini? Au Tanzania na sisi tumetengeneza chombo cha kwenda huko? Waandishi wa bongo bana...wanaboa kwelikweli

Mkuu, tena wanaboa kuliko unavyoweza kufikiri! Huyo bwana wala haendi mwezini bali anakwenda matembezi anga za juu kutokana na mpango uliobuniwa na baadhi ya taasisi za anga za juu huko marekani na russia kwa ajili ya watu wenye pesa zao kama huyo 'mtanzania' mwenzetu! Kwenda kutalii anga za juu na kufika mwezini ni vitu viwili tofauti!! Mwananchi na Wasaidizi wa raisi walipaswa kujua na kufafanua hili ili kuepusha raisi wetu kudanganywa. 'mtanzania wa kwanza kufika mwezini', my a*s!!!
 
Hivi u-Tanzania ni sawasawa na uraia wa Tanzania? Hivi mimi nikichukua uraia wa nchi nyingine basi utanzania wangu ( uasili wangu) unapotea? Kwani kwa kuchukua uraia wa nchi nyingine ni sawa na kukana uasili wangu?

Amandla...........
 
Dubai-based entrepreneur Ashish Thakkar, CEO of Kensington Real Estate, is in training at the NASTAR center near Philadelphia for his flight aboard Virgin Galactic. He’s keeping an online journal:

“Now we are taken to experience G force hands on in the machine! It’s difficult to describe this but is the closest thing to going into space and is seriously amazing…

“While I’ve known for months now that I’m going into space, today I really felt it. Virgin’s organisation, attention to detail and hospitality makes a real difference; and most importantly, the actual training is just out of this world – quite literally! Virgin is genuinely giving us an incredible experience.”

Ahsante sana... sasa nimejua ni kwa nini Game Theory amekuwa anatema povu kwenye hii thread...
 
Back
Top Bottom