Mtanzania Kuongoza Tume Ya Anga Duniani

M

MegaPyne

Guest
MTANZANIA KUONGOZA TUME YA ANGA DUNIANI

Na Saidi Yakubu, London

Baraza la Kimataifa la Usafiri wa anga limemteua mtanzania Omari Nundu ambae ni mtaalam wa masuala ya anga kuwa Rais wa tume yake ya ufundi inayoundwa na magwiji wa fani hiyo duniani. Bwana Nundu ataiongoza tume hiyo kwa mwaka 2008 na anakuwa ni mwafrika wa kwanza kushikilia wadhifa huo mkubwa katika duru za anga duniani.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Baraza hilo la usafiri wa anga, Bwana Nundu alichaguliwa baada ya kumbwaga Carlos Cirilo wa Brazil katika uchaguzi mkali uliofanyika mwishoni mwa wiki.

Tume hiyo ndio chanzo kikuu cha sheria, hatua na viwango vya kufuatwa katika utengenezaji wa ndege, viwanja na vifaa vya kuongozea ndege na pia ndio inayotuinga na kusimamia sheria za usafiri wa anga duniani.


Nundu ni mzaliwa wa Tanga na safari yake ya Urais wa tume hiyo ya magwiji wa anga ilianza mnamo mwaka wa 2005 wakati nafasi ya wajumbe (makamishna) zilipoongezwa kutoka 15 hadi 19 ambapo Tanzania ilimteua Bwana Nundu kugombea nafasi hiyo iliyogombewa na nchi tisa na kuibuka na ushindi mkali dhidi ya mataifa mengine. Alianza kutumikia nafasi hiyo mwaka huo huo na makamishna wenzake wakamchagua kuwa Makamu wa Rais wa tume hiyo mwaka huu.


Bwana Nundu anakuwa pia ni rais wa kwanza kuchaguliwa akitokea katika nafasi ya Umakamu wa Rais.

Tume hiyo inaundwa na wataalam wa hali ya juu duniani katika fani ya usafiri wa anga na kila kamishna huchaguliwa kwa vigezo vya umahiri na mchango wake mkubwa aliowahi kutoa katika fani hiyo duniani na kila kipindi huwa na waombaji wengi kuliko nafasi ambapo makamishna hao huishia kuteuliwa kwa ushindani mkali wa kura.


By Saidi Yakubu, London

The Council of the International Civil Aviation Organisation has appointed a Tanzanian Aeronautical Engineer Omari Rashid Nundu as President of its technical body, the Air Navigation Commission for the year 2008.

The Commission consists of distinguished experts nominated by ICAO Contracting States and appointed on a highly competitive basis by the ICAO Council to serve in the Commission for a period of three years.

The Commission is the technical source of all standards, rules and procedures for the design of aircraft, airports and aeronautical equipment; and for the safe conduct of international air transportation.

Omari Nundu who was born in Tanga 59 years ago triumphed against Carlos Cirilo of Brazil to serve in the top seat of the high profile international body as far as air transport is concerned.

Engineer Nundu’s journey to the Presidency of the Commission started in 2005 when the number of seats on the Commission was increased from 15 to 19 and he was nominated by Tanzanian Government to contest for the additional seat. He began to serve in the Commission in 2006 and in the same year his colleagues in the Commission unanimously elected him to be their First Vice President for 2007.


It is not customary or assurance that the First Vice President becomes the next President and this has never happened before but on 14th December 2007 the Council of ICAO elected Engineer Nundu the President of the Commission for 2008.

The commission is currently served by only 2 Africans amongst its 19 commissioners. Each Commissioner must have excelled outstanding qualifications and experience in the science and practice of aeronautics to be considered for appointment and since there are always more candidates than seats appointment is through serious competition.
 
huyu si alinyimwa kazi na JK kwa kisingizio eti mzomi sana na hatowapa access ya kuiba ndio maana wakaamua kumpa MATAKA

halafu wanatuambia turudi
 
Bravo
Bwana Omary Nundu endelea kupeperusha bendera yetu. walau tunaweza kuanza kuonekana Duniani
 
Hongera bwana Nundu, chapa kazi kwa nguvu zote kwa faida yhako binafsi na jamii yote unayoiwakilisha.
 
Achape kazi ila asituaibishe kama mama Mongela ambaye amekuwa rais wa bunge la Africa na kuanza kuajiri watoto wake na wakwe zake.

Pia anatuhumiwa kwa wizi wa pesa za bunge hilo na hii ni aibu kubwa kwa mtu kama yeye kuanza kuchunguzwa.
 
Bwana Omari Nundu- hongera sana! Tanzania wapo wengi wenye vichwa- sema hawapewi heshima na kutambuliwa home!
 
Baraza la Kimataifa la Usafiri wa anga limemteua mtanzania Omari Nundu ambae ni mtaalam wa masuala ya anga kuwa Rais wa tume yake ya ufundi inayoundwa na magwiji wa fani hiyo duniani. Bwana Nundu ataiongoza tume hiyo kwa mwaka 2008 na anakuwa ni mwafrika wa kwanza kushikilia wadhifa huo mkubwa katika duru za anga duniani.


Saaafi sana mkuu Nundu, this is what I am talking about, kichwa kikiwa kizima wenye vichwa vizima watakupata tu hata uwe bongo,

tatizo ni pale unapokuwa mbabaishaji, sasa Mkuu Kieleweke, huyu mama amefanya nini tena huko?
 
MPAKA KIELEWEKE PLEASE LETE DATA ZA HUYU MAMA....labda tofauti kinachoonekana kwa huyu Mama na Bro Nundu ni utaalam zaidi kuliko sense ya kuteuliwa pasee...Walio karibu na Nundu msisahau kuturushia makombo alau muweke ka-shule kule Pangani...
 
Hongera Bw. Nundu kwa kuonyesha kuwa Tanzania kuna Vichwa ingawa serikali zetu zilizopita na iliyopo kutojali wasomi wetu.
 
Tupeni wasifu wa Nundu. Tutashukuru sana.
MpakaKieleweke, mboa unatulambisha asali halafu unatoweka zako bwana!
 
Mama Mongella mbona hata ubalozi wa Tanzania UN alimchomeka dada yake, anajulikana kwa undugunaization.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom