Mtanzania aliyeko kwenye jeshi la Marekani

Mtanzania aliyeko kwenye jeshi la Marekani

Kama Membe na Kikwete ambao walijitahidi sana kulipigia debe hili na wakashindwa sijui kama litakuja kupitishwa labda nchi zote za Afrika ziruhusu na hawa "watawala" wa Tanzania waone aibu kwa kuwa nchi ya mwisho Afrika ambayo hairuhusu uraia pacha.

Kikwete na Membe nadhani walikusanya hata data za faida za kuruhusu uraia pacha kutoka baadhi ya nchi za Afrika magharibi na Carribeans lakini bado hawakufanikiwa.

Sababu nyingine ni za kipuuzi mno eti hawa wenye uraia pacha watakuja nchini kufanya ufisadi kisha kukimbilia huko waliko na uraia mwingine. Ukweli ni kwamba mafisadi wote nchini hawana uraia wa nchi nyingine na wote wako nchini hawakukimbilia nchi za nje lakini hakuna wa kuwagusa maana wameamua kulindana kwa hali na mali.

Huwa nafikiri labda imeandikwa mahali fulani na waasisi wa taifa hili kwamba "no dual citizenship" kwa mtanzania yoyote yule kutokana na hali ilokuwepo huko nyuma hasa ya wale baadhi ya watanzania ambao waliishi nje ya "system" kwa muda mrefu na kujulikana wapo "exiled" kutokana na uhusiano wao na nafasi zao za kisiasa.

JK na ucheshi wake wote ule na Membe nae na umahiri wake kwenye masuala ya diplomasia walishindwa kugeuza hio "rule".

Na sidhani kama serikali hii itaweza hata kukaribisha hoja hiyo kwa sasa.

Ila hiyo "mentality" ya kutoa sababu mbalimbali ambazo zinaonekana ni za chuki inabidi ifutwe.

Ila uraia pacha ni moja ya njia endelevu kwa maendeleo ya kasi na uboreshaji maisha ya watanzania wote.
 
Kama Membe na Kikwete ambao walijitahidi sana kulipigia hili na wakashindwa sijui kama kitakuja kupitishwa labda nchi zote za Afrika ziruhusu na hawa "watawala" wa Tanzania waone aibu kwa kuwa nchi ya mwisho Afrika ambayo hairuhusu uraia pacha.

Kikwete na Membe nadhani walikusanya hata data za faida za kuruhusu uraia pacha kutoka baadhi ya nchi za Afrika magharibi na Carribeans lakini bado hawakufanikiwa.

Sababu nyingine ni za kipuuzi mno eti hawa wenye uraia pacha watakuja nchini kufanya ufisadi kisha kukimbilia huko waliko na uraia mwingine. Ukweli ni kwamba mafisadi wote nchini hawana uraia wa nchi nyingine na wote wako nchini hawakukimbilia nchi za nje lakini hakuna wa kuwagusa maana wameamua kulindana kwa hali na mali.

Hapana, sababu kubwa ni wivu tu si unafahamu jinsi sisi waafrika tulivyo?

Watanzania wengi walosoma kisawasawa nje na ambao wameishi lets say 10-20 years wanahofiwa wakiingia kwenye mfumo watawanyima wale ambao wapo tayari kwenye system na ambao wengi ni mafisadi.

Lakini ukweli umegundulika kwamba watu wengi waliomo kwenye system wana vyeti vya kughushi na vile vya majina ya watu wengine.

Ni wivu tu.
 
Uko sawa kabisa Mkuu hakuna cha zaidi ni wivu tu na kuogopa exposure kubwa waliyonayo hawa Watanzania wenzetu walio nchi za nje katika mambo mbali mbali.

Sasa ngoja mmoja wa Watanzania hawa wenye uraia wa nchi nyingine wapate wadhifa mkubwa tuseme UK, USA etc uone jinsi atakavyopigiwa debe "Mtanzania mwenzetu" huyu pamoja na kuwa kwa sheria za nchi alishapoteza uraia wake wa Tanzania miaka mingi iliyopita.

Hapana, sababu kubwa ni wivu tu si unafahamu jinsi sisi waafrika tulivyo?

Watanzania wengi walosoma kisawasawa nje na ambao wameishi lets say 10-20 years wanahofiwa wakiingia kwenye mfumo watawanyima wale ambao wapo tayari kwenye system na ambao wengi ni mafisadi.

Lakini ukweli umegundulika kwamba watu wengi waliomo kwenye system wana vyeti vya kughushi na vile vya majina ya watu wengine.

Ni wivu tu.
 
Unachojua sio sahihi
You can serve in the US army as a permanent resident

Army Careers: Ways to Serve in the Army | GoArmy.com

Huu ni uongo wa kuaminika,utakuwa ndani ya hilo jeshi lakin kitengo kingine cha jeshi la ugenini,wajeruman na waingereza wana huo mchezo Maana wana bajeti mpaka za hayo ya majeshi,narudia tena jeshi la marekani hauwez uingia mpaka uwe na uraia aisee,ukiwa Kama permanent resident unaruhusiwa kuingia kitengo cha jeshi la ugenini na ndo huko watu hufanya course za fani mbali mbali
 
Nimekaaa nimewazaaa nikawazua hiyo miaka kumi ya anko alcohol nitakua nimechakaa huu mmoja tu msoto bora nikaombe kujiunga jeshi USA nitarudi baada ya kuisha miaka kumi ya anko mapadrock [emoji16][emoji16]
Pumzi haiuzwi
 
Wakuu,

Kuna mtu kanidokeza eti kuna jamaa mmoja ambae ni mtanzania ni askari mwenye cheo cha Luten General yuko kwenye jeshi la Marekani.

Kuna mwenye data za huyu jamaa?
Kishakua mmarekani huyo,
 
Hahahhaa, Watanzania kwa kujifanya wanajua...hahhaha! Kwahiyo mna maajent wenu kwenye jeshi la US na wenyewe hawajuwi siyo? Duh, hiyo kali! Hao ni waajiriwa tu wameajiriwa na jeshi kwa kazi mbalimbali kulingana na profession zao, hata wewe uliyesoma Kiswahili siku wakihitaji wakalimani wa kiswahili tuma maombi tu huenda ukavaa gwanda za kijivukijivu!
Nilicheka sana baada ya kuona hiyo comment ya mdau kwamba tuta blow cover ya jamaa

Bongo nyoso
 
Huu ni uongo wa kuaminika,utakuwa ndani ya hilo jeshi lakin kitengo kingine cha jeshi la ugenini,wajeruman na waingereza wana huo mchezo Maana wana bajeti mpaka za hayo ya majeshi,narudia tena jeshi la marekani hauwez uingia mpaka uwe na uraia aisee,ukiwa Kama permanent resident unaruhusiwa kuingia kitengo cha jeshi la ugenini na ndo huko watu hufanya course za fani mbali mbali

Kwa taarifa yako I'm ex-marine Na sina passport Ya mnyamwezi
 
Kwa taarifa yako I'm ex-marine Na sina passport Ya mnyamwezi

Lakin wakati unaingia ulikuwa na permanent resident na Ndo hiyo iliyokufanya uingie katika Marine lakin ulikuwa katika kitengo kingine cha wageni angalau mnavaa uniform moja na kushirikiana pia na inawezekana pia uliingia kwa sababu ya kuendelea na course flani au kusomea course flani,au pia inawezekana ulikuwa unasomea kitu hicho Kama scholarship Maana kuna watanzania wengi ambao walikuwa wanaenda USA kitambo kwa scholarship za CIA,so unabaki na uraia wako na ni wao ndo wanalipa kila kitu,lakin haiwezekani kuingia katika jeshi la nchi yoyote ulaya au marekani Kama hauna uraia wao,that's IMPOSSIBLE bro
 
Iwapo wabeba mabox tu na wafanyakazi wa care home wanaonekana tishio hawa waliojifunza kushika bunduki naona.siku wakifika airport Tanzania wanaweza ambiwa rudi huko huko ulipotoka.

Nchi imejaa viongozi waoga
 
Mkuu Richard kama tujuavyo kwa Tanzania yetu ukishachukua gamba la nchi nyingine ndiyo ushapoteza Utanzania wako. Ni kitu cha kushangaza sana kwa maoni yangu ni roho mbaya na kutoelewa kwa hawa watawala wetu umuhimu wa kuendelea kuwaruhusu Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine waendelee kuwa Watanzania. Mbona nchi nyingi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Ghana , Nigeria, Cameroun zimeruhusu uraia pacha? Kwanini Tanzania bado tunalipiga vita kwa nguvu zote hili la uraia pacha!?
Na sijuwi wanaogopa nini hasa?!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom