Mtanzania aliyeko kwenye jeshi la Marekani

Wakuu,

Kuna mtu kanidokeza eti kuna jamaa mmoja ambae ni mtanzania ni askari mwenye cheo cha Luten General yuko kwenye jeshi la Marekani.

Kuna mwenye data za huyu jamaa?
Somebody Mtunguja. Usiniulize nimejuaje
 
Mkuu US ni moja ya nchi duniani ambazo zinaruhusu uraia pacha, hivyo raia wa nchi nyingine ambaye anataka kuchukua Uraia wa US hana ulazima wowote kisheria kuukana uraia wake wa awali.

Ni kweli kuna watanzania ni wanajeshi na police nchini marekani na uwingereza.......

Lakini lazima kwanza kiapo cha mahakama kuukana uraia wako wa zamani....

Hiyo inawezekana kwa sababu vijana wengi wanaozaliwa sasa hasa USA wanakuwa goigoi kuendesha operations za kijeshi hivyo wanakopa wageni kutoka Israel, Nigeria,Mexico na Canada na kwingine kunakoaminika si maadui wa marekani......

Ndio maana unaona trump baada ya kuwashambulia Mexico atakwama na hawezi tena kuwa rais wa marekani....
 
Wakuu,

Kuna mtu kanidokeza eti kuna jamaa mmoja ambae ni mtanzania ni askari mwenye cheo cha Luten General yuko kwenye jeshi la Marekani.

Kuna mwenye data za huyu jamaa?
Hizo data za huyo mtanzania hukumwambia akupe ili uzilete humu.

Nachojua nchi kama USA mwanajeshi lazima awe raia wa kuzaliwa kama ni Mtanzania ina maana hana sifa tayari.
 
Wakuu,

Kuna mtu kanidokeza eti kuna jamaa mmoja ambae ni mtanzania ni askari mwenye cheo cha Luten General yuko kwenye jeshi la Marekani.

Kuna mwenye data za huyu jamaa?
Ni miye, unasemaje?
 
Wako wengi tu hawajitangazi!! Kua katika haya majeshi wala sio issue, wenzenu Ghana na Kenya nafasi za geshi zinatangazwa kwao ili watu wanaaply wanajoin hayo majeshi ya ughaibuni sio big deal mkuu!
bongo kilA kitu ni dili. ndo maanA mpakA passport kuipatA ni zaidi yA kipaji yaani maswali kibao sijui wanadhani unatakA kukimbia nchi yaan shidA.
 
Mkuu US ni moja ya nchi duniani ambazo zinaruhusu uraia pacha, hivyo raia wa nchi nyingine ambaye anataka kuchukua Uraia wa US hana ulazima wowote kisheria kuukana uraia wake wa awali.

Mkuu BAK, kwahio kuna watanzania (kama wapo) ambao wakisafiri wanabeba ile ya TZ na USA BABY

Lakini akifika JNIA si anaweza kuambiwa asalimishe moja ya pasi hizo au hii imekaaje mkuu?

Nimeuliza hivyo kwa sababu jamaa mmoja alipokuwa mpakani sehemu moja anataka kuvuka yule ofisa uhamiaji akaiona pasi ya nchi ingine kwenye beki ( kwa bahati mbaya) na kumpa mkwara jamaa kwamba inabidi aache pasi moja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni kweli kuna watanzania ni wanajeshi na police nchini marekani na uwingereza.......

Lakini lazima kwanza kiapo cha mahakama kuukana uraia wako wa zamani....

Hiyo inawezekana kwa sababu vijana wengi wanaozaliwa sasa hasa USA wanakuwa goigoi kuendesha operations za kijeshi hivyo wanakopa wageni kutoka Israel, Nigeria,Mexico na Canada na kwingine kunakoaminika si maadui wa marekani......

Ndio maana unaona trump baada ya kuwashambulia Mexico atakwama na hawezi tena kuwa rais wa marekani....
Ni kweli wapo watanzania wengi sana huko nakumbuka wakati Bush anakuja hapa walitangulia wadada wawili kuja Dar wao wapo idara ya Usalama kule Marekani walikuja mwezi mmoja hapa na wakawa wanalala resort gest house kimara tena vyumba vya sh.5000 kwa siku ila walikuwa wanahama hama,Bush alivyofika wakaenda Nairobi kwa hiyo hizi habari za kweli marekani wana maafisa kutoka nchi mbali mbali Duniani na wanakuwa wanatoa taarifa za nchi walizotoka,nasema hivyo kwa sababu tulikaa nao tukagonga nao mvinyo mpaka wanaondoka ila hawasemi siku ya kuondoka kwao wanaondoka kimya kimya
 
Mkuu Richard kama tujuavyo kwa Tanzania yetu ukishachukua gamba la nchi nyingine ndiyo ushapoteza Utanzania wako. Ni kitu cha kushangaza sana kwa maoni yangu ni roho mbaya na kutoelewa kwa hawa watawala wetu umuhimu wa kuendelea kuwaruhusu Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine waendelee kuwa Watanzania. Mbona nchi nyingi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Ghana , Nigeria, Cameroun zimeruhusu uraia pacha? Kwanini Tanzania bado tunalipiga vita kwa nguvu zote hili la uraia pacha!?

Mkuu BAK, kwahio kuna watanzania (kama wapo) ambao wakisafiri wanabeba ile ya TZ na USA BABY

Lakini akifika JNIA si anaweza kuambiwa asalimishe moja ya pasi hizo au hii imekaaje mkuu?
 
Ni kweli wapo watanzania wengi sana huko nakumbuka wakati Bush anakuja hapa walitangulia wadada wawili kuja Dar wao wapo idara ya Usalama kule Marekani walikuja mwezi mmoja hapa na wakawa wanalala resort gest house kimara tena vyumba vya sh.5000 kwa siku ila walikuwa wanahama hama,Bush alivyofika wakaenda Nairobi kwa hiyo hizi habari za kweli marekani wana maafisa kutoka nchi mbali mbali Duniani na wanakuwa wanatoa taarifa za nchi walizotoka,nasema hivyo kwa sababu tulikaa nao tukagonga nao mvinyo mpaka wanaondoka ila hawasemi siku ya kuondoka kwao wanaondoka kimya kimya

Kwahiyo hao wadada walivyolala hapo Kimara na ulipa 5,000 dalas ukaona ni lazima watakuwa watu wa usalama.

Inaweza kuwa ilitokea tu waliamua akufanya vekesheni Kimara ila walikuwa raia wa kawaida tu.

😀😀😀
 
Mkuu Richard kama tujuavyo kwa Tanzania yetu ukishachukua gamba la nchi nyingine ndiyo ushapoteza Utanzania wako. Ni kitu cha kushangaza sana kwa maoni yangu ni roho mbaya na kutoelewa kwa hawa watawala wetu umuhimu wa kuendelea kuwaruhusu Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine waendelee kuwa Watanzania. Mbona nchi nyingi za Afrika zikiwemo Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Ghana , Nigeria, Cameroun zimeruhusu uraia pacha? Kwanini Tanzania bado tunalipiga vita kwa nguvu zote hili la uraia pacha!?

Huwa nafikiri labda imeandikwa mahali fulani na waasisi wa taifa hili kwamba "no dual citizenship" kwa mtanzania yoyote yule kutokana na hali ilokuwepo huko nyuma hasa ya wale baadhi ya watanzania ambao waliishi nje ya "system" kwa muda mrefu na kujulikana wapo "exiled" kutokana na uhusiano wao na nafasi zao za kisiasa.

JK na ucheshi wake wote ule na Membe nae na umahiri wake kwenye masuala ya diplomasia walishindwa kugeuza hio "rule".

Na sidhani kama serikali hii itaweza hata kukaribisha hoja hiyo kwa sasa.

Ila hiyo "mentality" ya kutoa sababu mbalimbali ambazo zinaonekana ni za chuki inabidi ifutwe.

Ila uraia pacha ni moja ya njia endelevu kwa maendeleo ya kasi na uboreshaji maisha ya watanzania wote.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
itakuwa tunajuana tu, watoto wa mbax ....mimi nimepiga naye engineering pale mlimani, wakati yeye anaenda usa masters, mimi nikaingia Finland pia kupiga masters
Una masters hata kuandika hujui
 
Back
Top Bottom