Chilisosi
JF-Expert Member
- Oct 19, 2008
- 3,051
- 747
Ndugu zanguni,
Kama mjuavyo, Le mutuz ameshikilia bango suala la mbongo kuchomwa moto Marekani baada ya kukosekana dola $6,000. Lakini nataka niwaulize mnaotukosoa, JE MNAMFAHAMU MARAEHEMU?, MNAWAFAHAMU NDUGU ZAKE?
Katika pitia pitia kwenye mitandao na baada ya kuongea na wabongo wawili watatu walioko boksi la US nimegundua kuwa jamaa hakuwa karibu na ndugu zake na hajawahi kanyaga Bongo miaka thelasini. Tunaambiwa kuwa hata mke na watoto wake hawajui jamaa alitokea wapi.
Sasa kama hata mke na watoto wake hawajui asili yake kwa nini watu walikuwa wanangangania arudishwe bongo?
Mnapigania maiti irudishwe bngo wakati angekuwa mzima mngemnyima uraia?
Mimi nawaasa tu jamaa zangu wabeba boksi, mkiwa huku nje muwe mnakumbuka nyumbani, msisahau kwenu na mhakikishe hata watoto wenu mliozaa na vishoka wanakwenda home waumwe na mbu kidogo ili wajue wazazi walitokea wapi.
Pia jamaa yangu Le mutuz acha kutulaumu, sisi hata hatujui jamaa katokea wapi ulitaka tuchange hela apelekwe wapi? Unaweza kwenda kuzika mtu Tanga kumbe katokea Angola, huoni kama ni dhambi hapo?
Kama mimi mwongo naomba kama kuna mtu anaemfahamu hata ndugu mmoja tu wa marehemu ajitokeze hapa