Ndugu wanajukwaa..naleta habari za masikitiko za kifo cha Mtanzania mwenzetu aliyefariki kwa ajali ya maji hapa Rwanda.Kifo kimemkuta leo mida ya saa nne katika ziwa Kivu- mjini Gisenyi/Rubavu karibu na mpaka wa Goma/Kongo.
Kijana huyo aliyejulikana kwa jina Nasib Athuman(23),Mkazi wa Kinondoni(mchaga);alikuwa katika safari ya masafa marefu kutoka DSM kuelekea Goma-Kongo.Leo asubuhi walifika Gisenyi.Huku taratibu za kuvuka mipaka zikiendelea kijana huyo alikuwa na watanzania wenzake akiwemo kaka yake waliyekuwa pamoja katika roli hilo la mizigo; baada ya kuchezacheza mpira kijana huyo aliamua kwenda kuogelea ziwani(lipo eneo hilo).
Hivyo kijana alielekea eneo moja karibu na hotel ya serena..alijirusha majini(diving)..basi alivyo-dive hakuweza kutokea tena hadi vijana walipoamua kufuatilia na kumkuta chini kabisa akiwa ameshakata roho.Maiti ya kijana huyo imehifadhiwa katika hospitali ya serikali-Gisenyi.Tunasubiri kesho(siku ya kazi) ili kwa kushirikiana na mamlaka husika tutoe taarifa ubalozi wa Tanzania-Kigali kuona taratibu za kusafirisha mwili hapo kesho..Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.Amina
CHANZO CHA HABARI: mimi mwenyewe nipo eneo la tukio