Mtanzania aaga dunia huko rwanda

Mtanzania aaga dunia huko rwanda

papa anayevutia

Senior Member
Joined
Sep 5, 2012
Posts
153
Reaction score
52
Ndugu wanajukwaa..naleta habari za masikitiko za kifo cha Mtanzania mwenzetu aliyefariki kwa ajali ya maji hapa Rwanda.Kifo kimemkuta leo mida ya saa nne katika ziwa Kivu- mjini Gisenyi/Rubavu karibu na mpaka wa Goma/Kongo.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina Nasib Athuman(23),Mkazi wa Kinondoni(mchaga);alikuwa katika safari ya masafa marefu kutoka DSM kuelekea Goma-Kongo.Leo asubuhi walifika Gisenyi.Huku taratibu za kuvuka mipaka zikiendelea kijana huyo alikuwa na watanzania wenzake akiwemo kaka yake waliyekuwa pamoja katika roli hilo la mizigo; baada ya kuchezacheza mpira kijana huyo aliamua kwenda kuogelea ziwani(lipo eneo hilo).
Hivyo kijana alielekea eneo moja karibu na hotel ya serena..alijirusha majini(diving)..basi alivyo-dive hakuweza kutokea tena hadi vijana walipoamua kufuatilia na kumkuta chini kabisa akiwa ameshakata roho.Maiti ya kijana huyo imehifadhiwa katika hospitali ya serikali-Gisenyi.Tunasubiri kesho(siku ya kazi) ili kwa kushirikiana na mamlaka husika tutoe taarifa ubalozi wa Tanzania-Kigali kuona taratibu za kusafirisha mwili hapo kesho..Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.Amina
 
Poleni. Tunawaombea Mungu awatie nguvu ktk kipindi hicho kigumu. Mods wataweka uzi panapohusika. Hapa siasa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom