Simulizi: Kibwe katika safari ya ajabu

bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,261
2,095
IMEANDIKWA NA : SANGO
KIPOZI
*********************************************************************************
Simulizi : Kibwe Katika Safari Ya
Ajabu
Sehemu Ya Kwanza (1)

MWANA MTEULE

Ukimya wa kutisha ulitawala eneo zima, na Kibwe akahisi woga wa ajabu ukimtambaa mwilini na kuzitawala fahamu zake zote. Alikuwa na kila sababu ya kutawaliwa na woga, kwani pamoja na kwamba hapakuwa na hata mtu mmoja pamoja naye, lakini vilevile hakukusikika kwenye msitu ule mlio hata wa ndege wala wadudu kama ilivyo kawaida.

Kimya kizito! Mara, sauti za ajabu zinasikika angani. Bundi na sauti za ndege wengine zisizopendeza masikioni zilivuma ghafla na kuzidi kumuongezea hofu Kibwe. Alipoangaza huku na kule, alishangaa sana kuona majabali na milima iliyotanda kila upande, bila kuwepo dalili ya mimea wala miti! Ardhi ya eneo lile ilikuwa imekauka na katika sehemu nyingi ilikuwa imepasukapasuka.

Kijana yule aliegemea mwambaulioelekea kwenye pango moja kubwa. Hivi naota…au ni kweli niko kwenye sehemu hii isiyoeleweka? Aliwaza huku akitetemeka kama mpapai uliopigwa na kibunga. Licha ya zile sauti za bundi na zisizopendeza masikioni za ndegewa ajabu, kwa muda wote wa saa kadhaa alizokuwa pale mahali, hakusikia sauti nyingine yoyote, hata ya upepo ukivuma, isipokuwa pumzi yake mwenyewe tu!

“Nimekusubiri kwa miaka mingi mno kijana, sikudhani kama siku hii ingefika.” Kibwe alipogeuka na kuangalia pangoni, alihisi ganzi kwenye miguu yake kwahofu! Moyo wake uliacha kudunda kwa sekunde chache, akatoa macho pima kutokana na kile alichokiona! Aka! Ni kitu gani hiki mbele yangu tena? Alijiuliza, huku fahamu zakezikimshauri atimua mbio kuelekea popote pale, alimuradi tu pawe mbali kabisa na mahala pale!

Kwa sekunde kadhaa, kile alichokuwa akikiona kilimfanya ashindwe kabisa hata huko kukimbia kwenyewe. Mbele ya
macho yake, kilisimama kitu kisichoeleweka, kama kijitu kidogo sana mithili ya mbilikimo, lakini udogo wake ulizidi ule wa
mbilikimo! Kilikuwa ni kijitu chenye uso ulioshupaa kama mzee wa miaka zaidi ya tisini.

Uso ule ulipambwa kwa msitu wa ndevu nyingi za mvi tupu zilizofika hadi magotini kwake! Kibwe alianza kukimbia lakini
ghafla, pale mahali alipokanyaga wakati akiruka kwa hofu, palianza kutitia na ardhi ikajiachia na kuporomoka pamoja naye! Wakati akiporomoka, alipoangalia chini kabisa, aliona uwazi usio na mwisho! Kwa hofu kubwa mno, aliachia ukelele wamfululizo, akihangaika kutafuta sehemu ya kukamata.

“Wooooooooooooooo…! Wooooooooooooa…….!” Kwa wepesi wa ajabu, yule mtu mdogo alinyoosha juu mkono wake na kuwahi kukamata mzizi uliokuwa ukining’inia juu yake. Alikunja miguu yake akijiandaa kubembea kwa kutumia mzizi
ule, akiazimia kujirusha kuelekea katika sehemu iliyokuwa imarakidogo. Alipofanya vile, alibembea huku akimchukua Kibwe pamoja naye kwa mkono wake wa pili, na wote wawili wakabembezwa na mzizi ule na kutupwa kwa mweleka mzito kiasi cha mita kumi hivi kutoka pale walipokuwa, wakiwa salama salimini ndani ya lile pango kubwa, lakini Kibwe akiwa ameshituka sana!

“Heeeeh! Ilikuwa kidogo niporomoke shimoni na kupotelea sijui wapi tu kule!” Kibwe aliropoka, akimshukuru Mungu kwa nusura aliyoipata. Alimtazama yule mtu mdogo wa ajabu, na kushangaa kuona jinsi alivyomnyakua kwa wepesi kama
mtu aliyechukua unyoya. Alitaka sana kujua alikuwa ni kiumbe wa aina gani yule!

Wakati wote ule wa pata shika, upepo mkali ulioambatana na dhoruba ulikuwa ukivuma, huku majabali yaliyotanda eneo lile yakiyumba na kutingishika vibaya. Ilikuwa ni hali ya kuogopesha mno kwa Kibwe. Kijana yule na mwenzake yule mwenye umbile dogo kama tumbiri, waliketi kwa muda wa kutosha pale mahali walipoangukia. Kile kijitu kilinyamaza kimya, kumpa nafasi Kibwe apumue kidogo, na Kibwe naye akanyamaza kimya, akijaribu kuelewa yule alikuwa ni nani, na ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea pale, na kwa nini?

Baada ya nusu saa hivi, muda ambao kwa Kibwe ulionekana kama siku nzima, ile hekaheka ya maporomoko ilitoweka, na polepole upepo na dhoruba vikapunguza kasi yake. Alipoangalia nje ya pango lile kubwa, kwenye upeo wa macho
yake, akaona maajabu mengine. Katikati ya majabali makubwa na milima mirefu, aliona maumbile ya watu wakubwa mno! Aliinuka na kujaribu kutoka nje kidogo ya lile pango lililotitia bila kizuizi muda mchache uliopita, akitaka kuhakikisha kuwa ni kweli aliona kile alichokiona?

Ghafla alishikwa mkono na yule mtu mdogo aliyemrudisha nyuma kwa nguvu. “Chunga hatua zako kijana! Eneo lote hili linakabiliwa na uwazi mkubwa katika kila sehemu, na kama ulivyoona, inaweza kutokea hatari kubwa upande wetu. Kwa
sababu ya kuzuia hatari hiyo, ndiyo maana nikakuambia kuwa nimekusubiri wewe Kibwe kwa miaka mia moja!” Khah!

“Imekuwaje ukafahamu jina langu? Kwani wewe ni nani?” “Jina langu ni Bunga, na ni kiumbe pekee niliyebaki katikasehemu hii…” “Kiumbe pekee uliyebaki…??” “Naam. Nilibaki mimi na raia wachache tu, tulionusurika katika
nchi ya Sabaa miaka mia moja
iliyopita.” Kile kijitu kilichojinadi
kwa jina la Bunga kilimjibu, na
Kibwe akazidi kutoelewa.
“Mi..mi…mi sikuelewi we
babau!” Alimwambia.
“Huwezi kuelewa mpaka
ueleweshwe Kibwe. Hebu kaa
chini unisikilize basi…” Bunga
alimjibu, na KIbwe hakuwa na
namna ya kufanya vinginevyo.
Ndipo kibabu/kidudu Bunga
alipomsimulia za madhila
makubwa, akimuelezea habari za
nchi ya Sabaa ambayo ilikuwa ni
moja katika nchi za falme za
Kaskazini Mashariki ya dunia
zilizotawaliwa na wanawake
waliorithi falme za baba zao.
Alimwambia kuwa miaka mingi
nyuma, ikiwa chini utawala wa
Malkia Balika, nchi ya Sabaa na
jamii yake ya ‘Wanahewa’
iliteketezwa vibaya sana na jamii
yenye asili ya ‘Wanamoto’ kutoka
katika falme za majini, kwa
kutumia mioto iliyotokana na
pumzi zao.
“Kutokana na mashambulizi yao,
hakikubaki chochote katika
utajiri mkubwa wa nchi ya
Sabaa!” Alisema, akiongezea
kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku
ambayo ‘Wanahewa’ waliandaa
hafla maalum ya kumtoa kijana
wao mteule na kumkabidhi kwa
mwalimu maalum ambaye ndiye
angemuelekeza kijana huyo jinsi
ya kutumia vipaji vyake vya
kipekee kwa faida ya jamii ya
sayari yao.
Bunga alikumbuka kuwa katika
baraza rasmi la Malkia Balika wa
Sabaa miaka hiyo mia moja
iliyopita, ulifanyika utabiri
kuhusu Mwana Mteule
aliyezaliwa nchini mwao. “
Atakapofikia umri wa miaka
kumi na nne, kijana huyu
mwenye vipaji maalum,
atakabidhiwa kwa mwalimu
ambaye atamwelekeza jinsi ya
kuvitumia vipaji hivyo kwa faida
ya jamii ya sayari hii, kwani yeye
ndiye mwokozi wa jamii zote
duniani...!” Mzee yule wa ajabu
alimwambia Kibwe kuwa tamko
lile lilitolewa na wazee
waheshimiwa, katika lile baraza
maalum la Malkia Balika.
“Walikuwa katika maandalizi ya
kutafuta mustakabala mwema wa
taifa lao.” Alisema.
“Ama! Sasa ikawaje tena?” Kibwe
aliuliza, akionekana kuvutiwa na
maelezo yale.
Bunga alimfafanulia kuwa kitu
kilichowaponza ‘Wanahewa’
miaka mia moja iliyopita ilikuwa
ni neema kubwa na mafanikio
yao ya ajabu yaliyotokana na
rasilimali yao ya kipekee ya vito
na madini, na pia vipaji vyao
adimu walivyojaaliwa.
“Katika miaka hiyo mia moja
iliyopita, nchini Sabaa alizaliwa
mwana wa kipekee mwenye
vipaji vingi vya ajabu na uwezo
mkubwa wa kimazingaombwe.
Kuwepo kwake katika sayari ile
ilikuwa ni kwa ajili ya kuinusuru
jamii yake katika sayari yake
pamoja na kuipa matumaini.
Utabiri wa wanataaluma
ulionesha kuwa kijana yule
angeelekezwa mbinu za
kumwezesha kuvitumia vipaji
vyake kwa ajili ya kuinusuru
jamii yake pindi atakapofikisha
umri wa miaka kumi na nne.
“Lakini looh! Hili halikutimia,
kwani chuki na inda za jamii ya
majini waovu dhidi ya jamii yake
vilitimia, na kijana yule
akateketezwa na moto katika
uvamizi ule wa wanamoto’,
uvamizi uliokusudiwa kumzuia
asitekeleze kazi muhimu
iliyomleta katika sayari ya dunia.
Kazi ya kuinusuru jamii ya
Sabaa!”
“Heh! Kwa nini ilikuwa hivyo
sasa?” Kibwe aliuliza kwa
hamaniko.
Kidudu Bunga alipiga kimya kwa
muda, kisha akamweleza Kibwe
chimbuko la uhasama
ulioiangukia nchi yake ya Sabaa.
Nchi iliyoneemeka. Nchi yenye
hewa safi pasina mfano. Nchi ya
wanahewa…
***
Miaka elfu mbili iliyopita huko
nyuma, nchi ya Sabaa ilineemeka
kwa kila fani – utajiri, maendeleo
makubwa na ustaarabu wa hali
ya juu, chini ya malikia wao
Balika. Sabaa ilitegemea zaidi
madini,vito pamoja na kilimo
kutokana na ardhi yake iliyokuwa
na rutuba, na hali ya hewa yake
mwanana. Baada ya uvamizi wa
Wanamoto ambao ni majini
wachokozi, raia wachache
waliobaki chini ya Malkia mpya
bibi Sultana, mdogo wake Malkia
Balika, walijitahidi kuijenga upya
nchi yao na kuanzisha utawala
mpya. Miongoni mwa mambo
waliyoyafanya ni kuanzisha
kanuni mpya za maendeleo, na
za kuendesha mambo yao kadhaa
wa kadhaa, na kuonesha kwa kila
hali ukomo wa ustaarabu
ulionawiri upya, alioufikisha
malkia wao huyo mpya. Hata
hivyo, kukosekana kwa ile neema
ya Mwana Mteule aliyehusudiwa
awali katika utawala ule tangu
miaka mia moja iliyopita,
kuliwapa Wanahewa majonzi na
masikitiko makubwa mno. Tukio
lile lilichelewesha sana
utekelezaji wa malengo bora ya
nchi ya Sabaa kwa ajili ya jamii
yake kote ulimwenguni kwa
kipindi cha miaka mia moja,
athari ambayo ilitabiriwa kuwa
ingejidhihirisha kwa dalili
mbalimbali katika sehemu nyingi
duniani!
“Kukosekana kwa kijana mteule,
kumeondoa matumaini miongoni
mwa jamii na kuzuia nusura si
kwa raia wa Sabaa pekee, bali pia
duniani kote.” Malkia Sultana
aliyerithi kiti cha Malkia Balika
aliwaambia wazee waheshimiwa
katika baraza lake la mashauri.
Alitoa wazo kwao kwamba ni
vizuri kuitisha mkusanyiko wa
raia wa Sabaa wakiwemo
wanataaluma ya nyota na
wanajimu, ili watabiri
mustakabala wa nchi yao pamoja
na dunia nzima, kuelewa ni
matatizo gani yatakayowakabili
katika sayari yao na jinsi gani
yanaweza kutatuliwa. Wazee
wale waheshimiwa ambao ni
washauri wa Malkia Sultana
katika utawala wake, waliafiki
mawazo yake, na ndipo
ulipoitishwa mkusanyiko wa raia
wote wa Sabaa katika uwanja
maalum. Uwanja ulifurika watu
waliokuwa na hamu ya kufahamu
hatima ya sayari yao. Wakati huo
sayari ya dunia ilikwishafikia
kiwango kikubwa cha nyuzi joto
ambacho haikuwa rahisi
kukipunguza, na kilikuwa
kikiongezeka kwa kasi kubwa.
Hali ile ilitishia mno maisha ya
viumbe wote duniani!
“Kwa hakika ingawa mwana
mteule aliteketezwa na moto kwa
njama za wale viumbe waovu
kwa nia ya kutuondolea
matumaini yetu, lakini hivi
tunavyozungumza umejitokeza
uwezekano mkubwa wa kupata
ufumbuzi utakaorejesha
matumaini kwa wanahewa wote
nchini Sabaa, na jamii nyingine
duniani.” Alitabiri mmoja kati ya
wanajimu waliohudhuria,
ambaye kwa maelezo yake hayo
hakuwatosheleza raia waliokuwa
na shauku ya kupata majawabu
ya maswali waliyokuwa
wakijiuliza. Malkia Sultana
alimwangalia mzee yule kwa
makini na kisha akamuuliza.
“Unaonaje ukitufichulia kuwa ni
matumaini gani hasa
yatakayopatikana, ili kila mmoja
wetu aondokane na wasiwasi
alionao hivi sasa?” Malkia yule
alihisi kuwa mnajimu kwa
makusudi kabisa, hakupenda
kufichua ukweli wa sababu za ule
utabiri, ambazo aliamini kuwa
zilikuwa ni nzuri tu, lakini hata
hivyo bado alitaka ufafanuzi wa
namna fulani, ili kurejesha imani
kwa raia wake, na kuwaweka
katika hali ya utulivu. Raia wote
nao waliafiki hoja za Malkia wao
na wote wakamkodolea macho
mnajimu yule, wakisubiri jibu
lake la kuridhisha, lakini kabla
yule mnajimu hajafungua mdomo
kusema lolote, kishindo kikubwa,
mithili ya kile kitolewacho na
gari moshi likichemka,
kilirindima eneo lote lile.
“Aaaa! Aaach-ch-chuuuuu!
Aaaa---aaaaach-ch-chuuuuu!”
Pale uwanjani vumbi lilitimka
kama kimbunga! CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jamii yote iliyohudhuria
mkusanyiko ule iligutuka na
kuruka kutoka vitini mwao. Vitu
vidogo vidogo vilivyokuwepo
katika eneo la mkusanyiko ule
kama vile mazulia, viti ambavyo
havikukaliwa, makaratasi na
vinginevyo, vilirushwarushwa na
kutawanywa huku na kule.
Hamadi!
Kumbe ilikuwa ni chafya moja ya
nguvu iliyotoka miongoni mwa
raia waliohudhuria mkusanyiko
ule. Kila mmoja alitaharuki na
kugeukia upande kilipotokea
kishindo kile, kushuhudia ni nini
hasa kilichotokea.
“Hayaaa! Hayaaaa! Jamani! hebu
tulieni kidogo! Tulieni jamani!
Bila shaka baadhi yenu
mnafahamu jinsi Mzee wa Busara
anavyokuwa kila anapokuwa na
mawazo mazito, kutokana na
matatizo ya aina hii.” Alisema
mmoja kati ya wazee
waheshimiwa.
“Mara nyingi anapofanya hivi
huwa na wazo muhimu la
kuchangia! Kwa hiyo ni bora
tutulie na tumsikilize kwa makini
ndugu zangu!” Mwingine
aliafikiana na yule mzee
muheshimiwa wa kwanza.
Naam. Mzee wa Busara alikuwa
amejirundika kama kifusi
pembeni kabisa ya ule uwanja!
Kwa haraka haraka mtu
angeweza kudhani kuwa ni
kilima kidogo kilichotokana na
takataka nyingi! Mzee yule wa
ajabu alianza kujigeuzageuza na
kunyoosha nyoosha shingo yake
ambayo awali haikuonekana.
Alikuwa kama mnyama mwenye
miguu minne na mkia mnene
kama wa mamba, na ngozi yake
ilikuwa na magamba kama ya
samaki, lakini zaidi yalionekana
kama ya mamba kwani yalikuwa
mapana mno!
“Aaaa—ch---chu---!” Alianza tena
Mzee wa Busara akiwapa wahaka
mkubwa wote waliokuwa
wakimwangalia. Alichukua nafasi
ile na kuanza kuelezea jambo
lake, wakati ambapo wote
waliohudhuria walikuwa makini
kabisa, wakidhani kuwa litatoka
chafya jingine babu kubwa
liwatimulie vumbi kama awali!
“Sisi---eh! Mhh-khuu! Sisi t-tun-
nafahamu kuw wa y-yapo mat-
tumaini ma-kubwa m-mbele-
yetu! Tusub-iri tu---aaach-ch-
mhhh!” Mzee wa busara
alijitahidi kuzuia chafya yake, ili
asiwavuruge raia waliokuwa
wakimsikiliza.
“Tuv-vute s-subira, maa n-na s-si
muda mr-refu t-tutapata maj-jibu
yatakayo turudishia imani na
matumaini, pamoja na nusura
tuliyoitegge—m-eaaaaaaa----c-h---
u….....!” alisema mzee yule wa
busara huku akizuia chafya zake
kwa taabu sana, akiwa pembeni
mwa uwanja na huku shingo
yake ndefu ikizunguka zunguka
kwa madaha kama shingo ya
twiga mtoto. Alimgeukia mtu
mmoja mdogo sana ambaye kimo
chake kilikuwa mithili ya kimo
cha ngedere. Mtu yule aligubikwa
na ndevu nyeupe tupu zenye
urefu wa kama mita thelathini
hivi, zilizoburuza hadi aridhini.
“Na matumaini hayo
yatadhihirika itakapokamilika
miaka mia moja kamili tangu
nchi hii ilipovamiwa na
kuteketezwa na majini wa
bahari.” Kijitu kile kidogo
kiliongezea taarifa katika maneno
ya Mzee wa Busara. Awali kabla
ya uvamizi wa nchi ya Sabaa,
kijitu kile ndicho kilichotarajiwa
kuwa mwalimu wa yule Mwana
Mteule aliyeteketezwa na moto
wa majini, katika siku ambayo
raia wa Sabaa waliazimia
kumkabidhi kwake.
“Kwa hiyo hakuna yeyote kati
yenu atakayekuwa na ufafanuzi
wa ufuatiliaji wa jambo
litakaloturudishia matumaini
yetu?” Alidadisi Malkia Sultana,
akiwaangalia wazee wake
waheshimiwa na watabiri wake
wa mambo waliohudhuria.
Mmoja kati ya wanajimu
aliyekuwa amejiinamia kwa
muda wote wa mkusanyiko ule
alisema; “Kwa hakika hatuwezi
kufafanua zaidi kwani
tutakapofanya hivyo tutavunja
mwiko, na hivyo kuweka ugumu
zaidi katika upatikanaji wa
ufumbuzi wa mambo
yanayohusika. Ila, tunachoweza
kusema ni kwamba maelekezo ya
dalili za madhara yanayoikabili
sayari yetu na jinsi ya
kukabiliana nayo, yameandikwa
katika moja ya vidani vya fedha
vyenye umbile la kucha za Simba,
kwenye mkufu unaoning’inia
shingoni mwa sanamu la shaba la
kichwa cha Simba, katika nchi ya
milima minne myeusi ya
maangamizi, kwenye uwanda wa
jabali la kisiwa cha Baharia!”
Raia wote waliohudhuria
waliduwaa!
Kwenye milima myeusi ya
maangamizi? Ndio wapi huko?!
Ukimya mkubwa ulitawala
uwanja ule wa mikutano, kila
mmoja akitafakari kuhusu taarifa
ile mpya ambayo kwa hakika
iliwakatisha tamaa zaidi, kwani
walihisi kuwa lile ndilo lililokuwa
jukumu la Mwana mteule,
ambaye walikwisha mpoteza!
***
Naam, Kibwe alimsikiliza Bunga
kwa makini sana, akijaribu
kuhusisha taarifa ile ya kidudu
Bungan a yale na maneno yake ya
awali, kwamba ‘alimsubiri yeye
kwa kipindi cha miaka mia moja’.
Hapo akasikia mikoromo ya
kutisha nje ya lile pango
walilokuwemo. Akakumbuka yale
majitu ya ajabu aliyoyaona kule
nje muda mchache uliopita.
Alizidi kuogopa.
“Yale…ni majitu gani kule nje?”
Kibwe alimuuliza yule mzee wa
ajabu, huku akioneshea na
akichungulia nje ya lile pango
kujaribu kuyaangalia majitu yale
aliyoyaona awali. Kama hapo
awali aliogopa, basi safari hii,
aliogopa maradufu, kwani baada
ya lile giza la vumbi nene
kutoweka, aliweza kuyaona vizuri
sana yale majitu ya ajabu! Miili
yao mikubwa kama milima
ilikuwa na vichwa vyenye
mapembe vilivyofanana na
vichwa vya ng’ombe! Halafu lo!
Mikono na miguu yao ilikuwa na
makucha marefu ya shaba!
Wakati akishangaa kwa kuhofu
namna ile, aliyaona yale majitu
yakipasua majabali na
kuchimbua milima. Huku
yakikenua meno yao makubwa ya
shaba yaliyong’ara mno kwa
mwanga wa jua, Kibwe
aliyashuhudia yale majitu
yakitafuna mawe bila kizuizi
kama kwamba yalikuwa
peremende! Miguu ilimwisha
nguvu, na kumfanya kijana yule
anyong’onyee taratibu na kurudi
chini, akiwa dhofu-l-hali kwa
hofu.
“Ama hakika leo ndio kifo
changu! Hakuna uwezekano wa
kunusurika hata kidogo hapa! Na
kama ninaota, mbona siamki
mpaka sasa? Laaa! Sijui
nitanusurika vipi mimi!” Aliwaza
kijana yule kwa hofu na wahaka.
Alimwangalia Bunga
aliyeonekana kuwa hana hofu
hata chembe, na kwa sauti ya
kutetemeka, akamuuliza kwa
mara nyingine, “Aaa...eeeh…
hivi…eeeh…. wale ni kina nani
babu….? Wametoka wapi…..na
kwa nini….wanafanya vile
wanavyofanya?”
“Wale kijana ndio wala mawe.
Kila mwaka kwa muda wa miaka
mia moja sasa, watu hao wa
ajabu wamekuwa wakitokea,
wakisindikizwa na upepo mkali,
vumbi, dhoruba na matetemeko
ya majabali. Wakifika tu, huanza
kuchimbua milima na mawe na
kupasua majabali, ili kujipatia
chakula chao. Watu hao wala
mawe wataendelea kufanya hivyo
hadi kuimaliza dunia yetu yote,
wakisababisha uwazi wenye kina
kirefu kisichokuwa na mwisho!”
Bunga alimwambia, na Kibwe
akaduwaa akiwa kinywa wazi.
Bunga alizidi kumkatisha tamaa
ya nusra pale alipomweleza kuwa
hata yeye anahofu kwamba
hatimae, hata ile sehemu ya ardhi
kwenye lile pango alikokuwa
anaishi kumsubiri, pia itatoweka
pamoja naye, na kuacha uwazi
kama sehemu nyingine katika
eneo lile, ambao uliwapoteza
viumbe wengine wengi kabla
yake.
“Oooh! Haponi mtu hapa!” Kibwe
alijisemea kwa sauti huku
akijishika kichwa kwa kukata
tamaa.
“Wewe pekee ndiye
utakayesaidia kuzuia hali hii
isiendelee na labda kuirudisha
vile ilivyokuwa awali Kibwe,
kwani wewe bado ni damu
changa, hujaanza kufikia umri wa
kukata tamaa.” Bunga
alimwambia, na Kibwe
akamshangaa. Hakujiona yeye
akimuokoa yeyote kutokana na
maangamizi ya ile mijitu
inayokula mawe, lakini pia
alishangaa kwani hakuona
uhusiano baina ya kuiokoa dunia
na ule uwazi ulioikabili. Vyote
kwa vyote, hakuelewa ni vipi
yeye angeweza kuzuia ile hali ya
hatari isitokee, hasusan
akizingatia kuwa waliohatarisha
hali ile ya dunia walikuwa ni
majitu makubwa mno kwa yeye
kuyadhibiti!
Kama vile aliyekuwa akiyasoma
mawazo yake, Bunga aliendelea
kumwelezea hatua zipi achukue,
ili kuinusuru dunia.
“Wewe ndiye mteule mwenye
jukumu hilo Kibwe, pamoja na
mengine ya kuitahadharisha jamii
na kuiokoa dunia na ukame, na
uwazi ulioikabili. Hiyo ni pamoja
na matatizo ya kiafya na vifo vya
binaadamu na viumbe wengine,
na pia kuinusuru dunia na uovu
na uadui miongoni mwao,
pamoja na kuwajengea imani na
matumaini...”
“Khah! Mimi?”
“Wewe, Kibwe! Kwa hiyo, ili
ufanikishe kazi hiyo, lazima
ufanye safari ndefu na yenye
mitihani mikubwa. Safari hiyo
ndiyo itakupatia ufumbuzi wa
jambo hilo. Kwa vyovyote vile,
usikubali kabisa kukata tamaa
kwa jambo lolote litakalotokea,
kwani utakapokata tamaa, azma
yako haitatimia.” Bunga
alisisitiza, mara kwa mara
akikunja uso wake uliokomaa na
uliopambwa na zile ndevu zake
nyingi za mvi.
“Lakini bado sijaelewa jinsi
nitakavyotimiza azma hiyo babu!
Na hiyo safari nitakayoifanya ni
kuelekea wapi baada ya kutoka
hapa?” Kibwe alihoji, yote yale
yakiwa ni mazito kwake.
Maelekezo ya Bunga kuhusu
safari yake yalizidi kumtia hofu,
kwani yalimdhihirishia kuwa
hakika safari ile ingekuwa ngumu
mno na isiyo ya kawaida.
“Mara baada ya kuondoka wale
wala mawe, takriban nusu saa
kuanzia sasa, utaelekea
magharibi ya dunia hadi ufike
mahali kunakokuchwa jua, katika
makutano ya mbingu na ardhi,
ambapo jua huonekana kama
kwamba linazamia hapo. Kwenye
ufukwe wa bahari utaona
mtumbwi. Tumia mtumbwi ule
kwa safari yako ya kuelekea
kisiwa cha mazimwi, viumbe
ambao nusu;yaani kuanzia
kuanzia tumboni kwenda
miguuni ni wanyama, na kuanzia
tumboni kwenda kichwani ni
wanadamu. Katika kisiwa hicho
utakuta ngome moja imara, na
ndani ya ngome hiyo, huishi hao
mazimwi ambao hulinda upanga
wa radi. Jitahidi uupate upanga
huo ili ukusaidie katika
mapambano ya kuzuia vitendo
vitakavyozidi kueneza uwazi
mkubwa katika dunia hii.
Utakapofanikiwa kuupata upanga
wa radi na kuondoka katika
kisiwa cha mazimwi salama
salimini, utaelekea katika nchi ya
Azarbajan iliyoko kaskazini ya
mbali ya dunia, baina ya milima
miwili mirefu sana. Ili kuupata
upanga wa radi kwenye kisiwa
cha mazimwi, lazima uwe
mwangalifu mno, uhakikishe
kuwa unaingia kwenye ngome
yao wakati ukiwa na hakika
kuwa wote wamelala usingizi
kwani….”
“Sasa, nitahakikisha vipi kwamba
mazimwi hao wamelala ili niweze
kuingia kwenye hiyo ngome?”
Kibwe alimkatisha kwa
mshangao. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Utakapo sikia kelele nyingi na
zogo kutoka ndani ya ngome
kama vile unazomewa na kundi
kubwa la watu, hapo ndio
utaanza kuingia ndani polepole,
na utakapofika ngomeni,
utawakuta mazimwi hao
wamelala sesa; fo-fo-fo! Humo
ngomeni utaona mnara wa
dhahabu, na juu ya mnara huo
wa kipekee, utauona upanga wa
radi uliowekwa nje ya ala yake na
unang’ara kama jua.” Bunga
alitoa maelekezo yale
yaliyomshangaza mno Kibwe,
aliyestaajabu sana kusikia kuwa
eti zinaposikika kelele nyingi za
mazimwi, ndio ishara kuwa
wamelala! Alijiuliza sana moyoni
mwake kama mambo yote yale
aliyokuwa akisikia yalikuwa
katika ndoto, au kweli yalikuwa
alivyokuwa akiyasikia!
Wakati Kibwe anahoji uhakika
wa mambo mengi yaliyomtokea
katika kipindi kifupipale kwenye
ule mji wa wala mawe, alimsikia
tena Bunga akisema; “Ingawa
utafaulu kuwakimbia mazimwi
wa ngomeni, hutaweza kuvuka
mpaka wa nchi hiyo ili kuendelea
na safari yako, kwani njiani
utazuwiliwa na kiongozi wa
mazimwi hao, zimwi ‘Nyalile’
mwenye jicho moja. Kwa bahati
nzuri icho hilo moja la zimwi
‘Nyalile’ halioni vizuri. Na kama
atajaribu kukuzuia usipite, lazima
umuimbie wimbo mzuri
utakaomvutia na kumlaghai, ili
asiweze kujua kama wewe ni
mwanaadamu!” Lo! Hapo Kibwe
akazidi kuhofu, na kuzidi
kumaizi kuwa kazi iliyokuwa
mbele yake, kamwe haikuwa
rahisi! Aliogopa sana kusikia
maelezo ya Bunga, na akakosa
imani kabisa ya kuendelea na
jukumu lile la kuiokoa dunia
isikumbwe na janga la uwazi
ulioikabili, pamoja na majanga
mengine.
Bunga alifahamu wahaka na
taharuki ya Kibwe baada ya
kumpa maelezo ya jinsi safari
yake itakavyokuwa, hivyo akazidi
kumpa moyo akiongea naye kwa
upole, na kumuhakikishia kuwa
hatapata tatizo lolote katika safari
hiyo, kama atatumia busara na
kufuata maelekezo yake.
“Nimekuambia tokea mwanzo
kuwa wewe ndiwe mteule wa
jukumu hilo, kwa hiyo kabla
hujaondoka kuelekea kwenye
safari hii ya aina yake, nitakupa
silaha mbalimbali, ambazo
utazitumia kadiri inavyostahili.”
Baada ya kusema hivyo, Bunga
alijisogeza ndani ya pango lake
na kutoa mfuko mmoja mkubwa
wa gunia na kumkabidhi Kibwe.
“Humu ndani kuna silaha nyingi
utakazozitumia utapozihitaji……”
Bunga alizitoa zile silaha moja
baada ya nyingine, akielezea kazi
zake taratibu na kwa makini,
Kibwe alisikiliza maelezo hayo
kwa umakini mkubwa. Bunga
akamuuliza iwapo ameelewa
maelekezo yote. Kibwe akaafiki
kuwa ameelewa.
“Haya kijana, hebu fumba macho
kidogo….” Hatimaye Bunga
alimuamuru, na Kibwe akafanya
alivyoambiwa. Wakati macho
yake yakiwa yamefumba, alihisi
mtikisiko na akasikia mvumo
ulioambatana na mtikisiko ule
mithili ya mtu aliyekuwa kwenye
gari moshi. Naam, hapo ndipo
ilipoanza safari ndefu na ya ajabu
ya Kibwe. Alipofumbua macho
kuelewa ni jambo gani lililokuwa
likiendelea, alijikuta ufukweni,
na mbele yake ulikuwepo
mtumbwi!!
***
Kibwe aliendelea na safari ile
kama alivyoelekezwa na Bunga.
Kwa muda mrefu mno aliendesha
mtumbwi alioukuta ufukweni,
hadi akachoka sana na kuanza
kusinzia kwa uchovu.
Alipokaribia kile kisiwa cha
mazimwi, Kibwe alianza kusikia
sauti nyororo na nzuri zikiimba
wimbo ulioburudisha kupita
kiasi! Alipotupia macho mbele
kabisa ya kisiwa, akawaona
mabinti saba wazuri, waliovalia
mavazi ya hariri yaliyometameta
juani, na waliovutia kupita kiasi.
Lakini zaidi ya uzuri wao, sauti
zao ndizo zilizomvutia Kibwe
zaidi. Alitega sikio na kusikiliza
kwa makini. Lo! Sauti zilikuwa si
za kawaida! Kibwe akazidi
kusinzia kwa burudani ilepamoja
na uchovu aliokuwa nao. Mara
akakumbuka maneno ya Bunga!
“Karibu na kisiwa cha mazimwi,
kuna mabinti saba laghai wenye
sauti nyororo za
kimazingaombwe. Ukizisikiliza
sauti zao nzuri kwa mfululizo,
lazima utawafuata walipo, na
ukifika kule watakuwekea ulozi
kwenye kinywaji chako na
kukufanya usahau kabisa
kutekeleza malengo yako!
“Kwa hiyo nitafanyaje kujinusuru
na ulaghai wao?” Kibwe aliuliza
“Utachukua hii ‘nta’ na kuziba
masikio yako ili usiweze kuzisikia
sauti zao.”
Haa! Sijui kwa nini Kibwe alitaka
kusahau jambo lile muhimu
kabisa. Haraka akatoa ile ‘nta
aliyowekewa kwenye mfuko wa
gunia na kuyaziba barabara
masikio yake, kisha akaendelea
na safari yake kwa amani hadi
alipofika kisiwa cha mazimwi.
Kibwe alianza kuangalia huku na
huko akitafuta sehemu ya kivuli
aweze kupumzika kabla ya
kuanza kutekeleza ile kazi
iliyompeleka kule. Alipata
sehemu yenye mti wenye matawi
marefu sana yaliyokuwa
yakiburuza hadi chini, na hapo
akaketi na kutumia yale matawi
kwa kujificha, ili asionekane.
Baada ya kunywa maji
aliyowekewa na Bunga kwenye
ule mfuko mkubwa wa gunia,
Kibwe alipata lepe zuri la
usingizi, kutokana na upepo
mwanana uliopuliza sehemu ile.
Alilala kwa muda mrefu
akapumzika vya kutosha, ili
apate nguvu ya kuanza kuelekea
kwenye ngome ya mazimwi,
kuchukua upanga wa radi, kama
alivyoelekezwa na Bunga.
Baada ya mapumziko yake, Kibwe
alianza ufuatiliaji wa kazi
iliyompeleka kule. Alikumbuka
maneno ya Bunga. “Itakubidi
kwanza uende kwenye mlima
ambao chini yake kuna shamba
kubwa la ufuta.” Alifahamishwa
kuwa sehemu ile ilikuwa karibu
na makazi ya wale mazimwi
hatari wafuasi wa Zimwi
mkubwa aliyeitwa ‘Nyalile’ na
ambao kwa pamoja, wakati fulani
waliwateketeza wakazi wa kisiwa
hicho kwa kuwatafuna. “Lazima
upande mlima huo hadi kileleni,
na huko utakuta jumba
wanamoishi mazimwi hao,
lililozungushiwa ngome
madhubuti.” Aliambiwa kuwa
lazima akachukue upanga wa radi
unaotoa cheche za moto kila
unapotumiwa, na kumpa ushindi
yule anaye utumia. Aliambiwa
kuwa ile ndiyo silaha pekee
ambayo ingemsaidia kupambana
na mitihani mikubwa iliyokuwa
mbele yake, akiendelea na safari
yake kuelekea matokeo ya jua,
baina ya mashariki na magharibi.
Kibwe alipita kwenye shamba
kubwa la ufuta na kuanza safari
yake ngumu ya kupanda mlima
akielekea kileleni kwenye jumba
la mazimwi. Katika jitihada zake
hizo, mara kwa mara kijana yule
aliteleza na kuporomoka, lakini
alizidi kuupanda mlima bila
kuchoka wala kukata tamaa.
Mchana kutwa Kibwe aliendelea
na safari ile ya kupanda mlima,
na ilimchukua takriban siku mbili
njiani akila matunda ya porini
kujinusuru na njaa. Kila
alipokutana na wanyama wakali
kama simba, chui , faru, mbogo
na wengine, Kibwe aliwakwepa
kwa kujificha vichakani. Hadi
kufikia saa kumi jioni siku ya tatu
jua lilipoanza kuchwa, kijana yule
aliona ngome ndefu mno,
iliyosimama kwenye upeo wa
macho yake katikati ya msitu!
Taratibu, huku akiangalia huku
na kule, Kibwe alisogea karibu na
ngome ile. Alipokaribia zaidi
alistushwa na kelele na zogo
kutoka ndani ya ngome ile
madhubuti! “Huyooooo! Anakuja
kuchukua upanga wetu! Haraka
mkamateni! Mfuateni mumlete
haraka kabla hajaingia ndani!
Hayaaa! Kamataaa! Chinjaaaa!
Uwaaaa! Nyongaa!” La haulaa!
Kibwe alianza kukimbia kwa hofu
ya kukamatwa na kutafunwa na
mazimwi wale hatari, na kusahau
kabisa usia aliopewa na Bunga!
“Utakapo sikia kelele nyingi na
zogo kutoka ndani ya ngome
kama vile unazomewa na kundi
kubwa la watu, hapo ndipo
utaanza kuingia ndani polepole,
na utakapofika ngomeni
utawakuta mazimwi hao
wamelala sesa, fo-fo-fo !
Kutakapokuwa kimya basi
tahadhari sana, kwani mazimwi
hao watakuwa wako macho!”
Hilo lilikuwa ni onyo la Bunga
kwa Kibwe.
Haa! Ilikuwaje akasahau jambo
jingine muhimu kama lile?
Hamadi! Palepale alipokumbuka
onyo lile na taarifa ya Bunga
kuhusu maajabu ya wale
mazimwi, Kibwe aligeuka na
kupiga mbio kuelekea kule
ngomeni. Alipofika langoni huku
akipumua kwa kasi, Kibwe
alichunguli ndani kwa uangalifu
na umakini mkubwa kuona kama
wale mazimwi walikuwa
wamelala. Hakuona dalili ya mtu
au kitu chochote katika upeo wa
macho yake. Taratibu aliingia
ndani akinyata polepole na
alipoangalia mbele zaidi, akaona
eneo kubwa la wazi lenye bustani
nzuri ya maua. Aliambaa na
ukuta, huku polepole akinyanyua
mguu mmoja mmoja, akishikilia
pumzi yake kwa hofu ya kusikika
na madude yale hatari
aliyoambiwa na Bunga. Mwisho
kabisa wa eneo lile la wazi,
Kibwe aliona lango jingine kubwa
lenye mbao za marembo
marembo. Alinyata taratibu na
alipogundua kuwa lango lile
lilikuwa wazi, alilisukuma na
kuchungulia uwani. Hamadi!
Kibwe hakuamini macho yake
kwa kile alichokiona! CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Macho ya kijana yule yalikutana
na kundi zima la madude
makubwa kupita kiasi yaliyokuwa
nusu ni watu, yaani kutoka
tumboni kwenda kichwani na
nusu, katika sehemu ya tumboni
kwenda miguuni walikuwa kama
sokwe! Kundi lile la madude yale
ya ajabu na ya kutisha, lililala
sesa kwenye nyasi za eneo lile, na
huku kelele zao za kuzomea
zikiendelea! Wakati sauti zao
zikimbabaisha Kibwe, miili yao
ilimtisha sana kwani ilikuwa na
manyoya marefu kupita kiasi
yakiburuza hadi chini kama
ufagio! Viumbe wale walikuwa
na midomo iliyojaa meno yenye
ukubwa mithili ya pembe za
ndovu! “Lo….. ndiyo maana
ilikuwa rahisi sana kwa madude
haya kuwatafuna na
kuwateketeza mara moja watu
wa kisiwa chote hiki, kutokana
na urefu na wingi wa meno yao
makali!” Kibwe aliwaza, akiwa na
woga na wahaka mkubwa usio
mfano.
Haraka Kibwe alifuata yale
maelekezo ya Bunga, akianza
kuwatambuka taratibu wale
mazimwi waliolala huku
wakipiga kelele na kuzomea
kama kwamba walikuwa macho,
hali iliyomfanya Kibwe azidi
kuhofu, kwani muda wote alihisi
kuwa huenda ghafla wakamrukia
na kumshambulia. Hiyo Ilikuwa
ni kazi ngumu mno kwa kijana
yule na muda wote wa zoezi lile,
jasho lilikuwa likimtiririka na
mara nyingine alihofu kuwa
huenda jasho lile likawadondokea
na kuwaamsha wale mazimwi, na
huo ukawa ndio mwisho wake!
MAJANGA YA SAYARI
Wakati Kibwe akiwa katika
jitihada za kutekeleza malengo
yake ya kuinusuru jamii kule
machweo ya jua katika kisiwa cha
mazimwi, katika sehemu
nyingine iliyo baina ya mashariki
na magharibi mbali kabisa
kutoka kisiwa kile cha mazimwi,
katika milki ya Sultani Bashar,
majini yalitawala sehemu kuu
iliyowapatia maji raia wa nchi ya
Shamsi mjini Majabali. Jambo
hilo lilisababisha shida kubwa ya
maji na ukame uliathiri maeneo
mengi ya nchi ile, iliyokosa
chakula cha kutosha kwa watu
wake. Ili kuwanusuru raia wake
na shida ile ya maji, kila mwaka
Sultani Bashar wa nchi ya Shamsi,
alimtoa kafara binti yake kwa
joka moja kubwa ambalo
lilimchukua binti yule na kuzama
naye kwenye mto Sakara ulioko
kati ya majabali mawili na
kumpeleka kwa jini ‘Makattani,’
mfalme wa majini yote. Mpaka
kufikia wakati ule Kibwe
alipokwenda kisiwa cha
mazimwi, tayari Sultani Bashar
wa nchini Shamsi alikwisha
watoa kafara watoto wake sita,
binti mmoja kila mwaka na kila
mara akiwapatia raia wake
mwaka mmoja wa kuchota maji
kutoka mto Sakara. Hatimae
Sultani yule alibaki na binti
mmoja tu, Bhaduri binti sultani
ambaye kwa bahati mbaya
kwake, alitakiwa kumtoa kafara
wiki mbili zilizofuata kwenye mto
uleule Sakara, ili kuwapatia raia
wake mwaka mmoja zaidi wa
kutumia maji yake!
“Ama kweli hali hii ni ya
kusikitisha na kusononesha
mno,” Malkia wa Shamsi
amlalamikia mumewe Mfalme
Bashar, huku akilia bila kizuizi!
“Haya ni maonezi makubwa na
ni unyanyasaji wa aina yake, wa
kuwalazimisha mabinti zetu
wajitowe mhanga, eti kwa ajili ya
kunusuru raia wako! Hili si
jambo la kibinaadamu hata
kidogo.” Malkia yule alisema kwa
masikitiko makubwa. “Sasa mke
wangu unadhani tungefanya nini
kulitatua tatizo hili sugu
linalotukabili kila mwaka?”
Sultani Bashar alimuuliza mkewe
kwa upole.” Hata mimi nina
majonzi makubwa kuhusu
mabinti zetu, lakini hii ndiyo njia
pekee ya suluhu kwa jambo hili.”
Katika mji ule mkuu wa Majabali
nchini Shamsi, baada ya Suitani
kufanya maandalizi ya
kumpeleka kitindamimba wake
Bhaduri kule mtoni Sakara kwa
ajili ya kafara, aliketi kwenye kiti
chake cha enzi na kujiinamia kwa
fikira na majonzi ya kumpoteza
binti yake mwengine! Ama kweli
Sultani yule alikuwa mtawala wa
aina yake! Eti kudiriki kuwatoa
kafara mabinti zake saba! Si
jambo la kawaida asilani!
Kule Azarbajan nako kwa Sultani
Kash Kash kaskazini ya mbali ya
dunia, ingawa chini kabisa ya
bahari, i jini ‘Makatta’na
wenzake walikuwa wakiandaa
vichafuzi vya hewa safi
iliyowasaidia watu kuishi, na
kuigeuza hewa ile kuwa
hatarishi, lakini Mfalme wa nchi
ile hakutambua hivyo. Hakujua
kama hewa ile iliyogeuka kuwa
moshi mnene ilipoanza kuzizima
na kisha kuwazingira watu katika
himaya yake, ndipo walipogeuka
kuwa mawe ya theluji! Kwa kuwa
hawakuelewa chanzo hasa cha
janga lile, watu wote wa kule
waliingia hofu kubwa na Mfalme
wao alikuwa akimtafuta
mkombozi atakaye wanusuru raia
wake kutokana na janga lile!
“La mgambo! La mgamboooo!
Likilia lina jamboo! Asiye mwana
a eleke jiwee!” Kijumbe wa
Mfalme Kash Kash alipita mitaani
akiwatangazia raia wa Azarbajan
kama kawaida wakati inapotokea
dharura ama ya raha, au ya
karaha, akianza kwa kupiga goma
lake kubwa alilolibeba kifuani, na
lililofungwa kwa kamba iliyopita
mabegani na kuzungukia
makwapani.
Kwa kupiga ile ngoma kijumbe
yule aliwavutia watu na
kuwasogeza karibu, ili waende
kumsikiliza. “Jamani eeeh!
Kuhusu janga linalotukabili la
raia wengi kugeuka mawe ya
theluji, mpaka hivi sasa bado
haujapatikana ufumbuzi wa
tatizo hilo, na wala bado
hajapatikana mkombozi atakaye
saidia kunusuru maisha ya raia
wa nchi hii. Hivi sasa wazee wa
baraza la Mfalme, wako mbioni
kutafuta njia ya haraka ya
ufumbuzi wa tatizo hilo. Kwa
hiyo yeyote atakaye kuwa na
mawazo tafadhali asisite
kujitokeza na kuchangia, ili
kulipiga vita janga hili la
kihistoria nchini kwetu…..! La
mgambooooo! La mgambooooo!
Likilia lina jamboooooo!”
Kijumbe yule alihitimisha
tangazo lake na kisha kuendelea
katika maeneo mengine ya mji
wao mkuu. Tangazo lile
lilitangazwa mara kwa mara
katika miji mbalimbali ya
Azarbajan, lakini hakujitokeza
mtu yeyote aliyeweza kutoa
ushauri kuhusu utatuzi wa tatizo
lile.
Katika ngome ya jumba la
mazimwi kwenye kisiwa chao,
Kibwe alitumia muda ule ambao
mazimwi wale walikuwa
wakipiga kelele, kwa kuendelea
kuwatambuka mmoja mmoja,
hadi alipofika kwenye ule mnara
wa dhahabu. Pale alipumua
kidogo kabla ya kuanza kupanda
mnara huo ambao juu yake
ulikuwepo upanga wa radi
alioutaka. Kelele za mazimwi
zilizidi kuliko awali, kama
kwamba walihisi kuwa kuna mtu
karibu ya hazina yao.
“Naomba Mungu majitu haya
yasiamke ama sivyo sitanusurika
asilani!” Kibwe aliwaza.
Alikumbuka kuwa mara tu, kelele
zitakapokoma, ndio utakuwa
wakati wa hatari kubwa kwake!
“Na kutakapokuwa kimya basi
tahadhari kwani watakuwa wako
macho!” Bunga alimwambia.
Ingawa aliogopa sana na kuhofu,
lakini kijana yule shujaa alipanda
juu ya ule mnara mrefu akafika
kileleni, na kwa uangalifu
akauchukua ule upanga na kuutia
kwenye ala yake, na kisha
akaupachika kiunoni kwake na
kuanza kuteremka chini kwa
uangalifu! Alipofika chini,
akarudia lile zoezi la wasiwasi la
kuyatambuka yale mazimwi
yaliyolala! Lo! Kwa bahati mbaya,
alipokuwa akimalizia zoezi hilo,
alilikanyaga zimwi la mwisho
lililolala karibu na lango kuu la
kutoka ngomeni, na hivyo,
lilipokuwa kimya tu, kwa ishara
ya kuamka, na menzake yote
yakawa kimya! Masikini wee!
Mazimwi yote yakawa macho!
Kabla hayajataharuki na
kugundua kuwa alikuwepo mtu
ngomeni mwao na amechomoka
na kupenyeza getini wakati
mmoja wao akiamka, Kibwe
alipiga mbio kama mshale!
Alikimbia kuelekea mpakani
mwa nchi ile kama alivyoambiwa
na Bunga, akiazimia kupita katika
njia kati ya mashariki na
magharibi!
Walipoangalia mnarani na kukuta
upanga wa radi umetoweka,
mazimwi wote walitaharuki na
kuwa na hasira nyingi “Bila shaka
alikuwepo mtu humu ngomeni.
Afuatwe haraka kabla
hajaondoka na upanga wetu!”
Baada ya kusema hivyo, wote
walitimua mbio, huku vumbi
likitanda kwa heka heka hiyo, na
baadhi ya miti ikikatika kwa
vikumbo vyao! Alipoangalia
nyuma, kibwe aliona vumbi
lililotanda hadi mawinguni! “Leo
ndio hatima yangu mimi! Sijui
kwa nini nilifika huku!” Kibwe
alisema kwa majuto. Mazimwi
yalipoanza kumkaribia alihisi
miguu yake ikiwa inalegea mno
na kukosa nguvu kwa hofu! Moyo
wake ulienda kwa kasi mno!
Alikumbuka maneno ya Bunga.
“Wakikaribia kukufikia, watupie
kichupa kimoja kati ya vichupa
hivi vidogo vya mazingaombwe,
ili uwacheleweshe.” Kibwe
haraka alitoa kichupa kimoja na
kukitupia nyuma yake kwa yale
mazimwi. Lo! Mara ukatokea
msitu mnene kupita kiasi.
Mazimwi yalianza kuhangaika
kukata miti ya msitu ule uliozuka!
Kutokana na ukubwa wao, muda
si mrefu yalifaulu kukanyaga
kanyaga miti midogo na kuipiga
vikumbo miti mikubwa, na kisha
kuendelea kumkimbiza Kibwe,
ambaye alipoona hivyo, alirusha
kichupa cha pili, na mara
zikazuka mbigili nyingi mno
nyuma yake! Mazimwi
yaliumiaumia miguu yao, na
wengi wakaachwa nyuma. Kibwe
aliyaona baadhi ya mazimwi
yakizidi kumfuata, huku yeye
akiwa amechoka mno kukimbia.
Alipatwa na wasiwasi mkubwa,
“Sasa nikishindwa kukimbia na
madude hayo yanazidi kunifuata,
itakuwaje?” alijiuliza huku
akipapasa papasa kwenye fuko
lake, kutoa kichupa kingine
miongoni mwa vichupa
alivyopewa na Bunga. CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa kuwa mazimwi hupenda
sana kula ufuta, utakapo watupia
kichupa cha ufuta, wote wataketi
chini na kuanza kula, na hivyo
utapata nafasi ya kuwakimbia.”
Kibwe alikumbuka maneno hayo
ya Bunga! Mara moja akarusha
kichupa cha ufuta, na hapohapo
ukazuka mlima mkubwa wa
ufuta, na kuwafanya mazimwi
wote kuchanganyikiwa kwa
uchu! ”Aaaaa! Ufutaaaa! Ufuta
mtamuuuu! Nakula ufutaaa!”
Wakawa wanajisemesha maneno
hayo, kila mmoja akifurahia
chakula kile akipendacho, na
kumsahau kabisa Kibwe na
upanga wa radi! Waliketi chini na
kuanza kuushambulia ufuta!
Kibwe naye aliongeza kasi ya
mbio zake, akiruka mabonde na
kuangukia kwenye makorongo na
mito, misitu na nyika hadi
kwenye mpaka kuelekea
kaskazini ya mbali, kulikozizima
baridi ya ajabu, iliyowagandisha
watu na kuwageuza mawe! Pale
mpakani alisimama ghafla
akitahamaki na kuona moshi
mwingi uliotanda mbele yake, na
umbile la dude kubwa
lililofichwa na giza la moshi huo,
likiashiria kuwepo kwa jitu
kubwa likishughulika chini ya mti
mkubwa kupita kiasi! Muda wote
aliokuwa akiwakimbia wale
mazimwi, alimsahau kabisa
kiongozi wao, aliyeitwa Nyalile!
Kibwe alitaka kufahamu ule
moshi uliotanda vile ulitokana na
nini. Huku akihofu, lakini kwa
moyo wa kishujaa, taratibu
alisogea kule kulikotoka moshi
ule, akiangalia huku na kule kwa
wasiwasi hadi akafika karibu
kabisa na sehemu ile. Aliona
kuwa ule moshi ulitokea bondeni,
wakati yeye akiwa juu kidogo
kwenye uwanda. Aliposogea na
kukodoa macho yake vizuri ili
aweze kuona kama kwenye ule
utando wa moshi kulikuwa na
nini, alihisi kama vile anaangalia
umbile kubwa sana la jitu la
miraba minne, likishugulika
kufanya kazi fulani. Alipozidi
kutazama kwa makini aliona
kuwa lile halikuwa jitu la miraba
minne tu, bali lilikuwa ni kitu
kama mtu, na vilevile kama
mnyama, likishugulika kuandaa
chakula chake chini ya mti
mkubwa sana! Lo! Kumbe
alikuwa akiliangalia dude moja la
kutisha mno, lililokuwa na
manyoya mwili mzima, meno
marefu kama pembe za tembo
lakini yaliyojaa kinywa tele, na
kuanzia tumboni kwenda
miguuni, Kibwe alikuwa
akiangalia mwili wa binaadamu
mithili ya sokwe, isipokuwa
ulikuwa mkubwa kupita kiasi!
Uso wa dude hilo uliokuwa
kwenye kichwa kilicho fanana na
cha tembo, na katika paji la uso
wake, kulikuwa na jicho moja tu!
Naam, kwenye bonde
lililozungukwa na msitu wenye
miti mirefu kupita kiasi,
alikuwemo zimwi Nyalile, na juu
ya bonde hilo, alikuwepo Kibwe
akimwangalia! Utakisia
mwenyewe hali ya Kibwe
ilivyokuwa, mara alipotahamaki,
akagundua jinsi alivyokuwa
karibu kabisa na kubwa la
mazimwi wote, ambalo sifa zake
alizipata kutoka kwa Bunga!
“Mama yangu weee! Sasa kweli
niko hatarini!” Kibwe aliwaza.
Alijibanza kwenye miti mirefu
kabisa, huku jasho likimtoka, na
hofu iliongezeka kila sekunde,
wakati kijana yule alipoyaona
yale aliyoyaona mle bondeni!
Kwenye mafiga makubwa sana
kupita kiasi, Nyalile alikua
ameinjika jungu kubwa mno.
Wakati likichemka, alimkamata
ng’ombe mzima na kumnyonga
na kisha kumtumbukiza ndani ya
lile jungu. Pamoja na ng’ombe
huyo Nyalile alichukua kama
gunia mbili za mchele na kuutosa
kwenye lile jungu lililokuwa
likichemka kwa mchemko wa
kelele kubwa za ngurumo pale
msituni! Shughuli iliendelea na
muda wote lile zimwi lilikuwa
likichochea mapande ya miti
mikubwa mafigani, kukoleza
moto wake ili chakula kichemke
vizuri. Kitendo kile kilisababisha
moto mkubwa sana kuwaka ,
ulioambatana na moshi mnene,
ikawa kama msitu wote ulikuwa
unawaka moto!
Pale alipokuwa Kibwe,
ukilinganisha ukubwa wa miti
iliyomzunguka, alionekana kama
kidege kidogo mno. Aliwaza na
kukumbuka maneno ya Bunga,
kwamba akitaka kuvuka mpaka
kuelekea kaskazini ya mbali bila
kukamatwa na Nyalile, lazima
amliwaze kwa wimbo mzuri
utakaomburudisha na
kumfurahisha, kwani
atakapofanya hivyo lile zimwi
litadhani kuwa ni kidege
kinachoimba! Vilevile, Bunga
alimwambia kuwa lile jicho moja
la Nyalile halioni vizuri. Habari
yote hiyo ilimpa moyo Kibwe,
akahisi kuwa angeweza
kufanikiwa kulikwepa zimwi lile,
kama akijitahidi kufanya vile
alivyaelekezwa na Bunga. Lakini
imani yake ilipungua wakati lile
zimwi lilipomaliza kupika na
kisha kuketi chini ya mti
mkubwa, na kuanza kufuta jasho
lililotiririka kama mfereji wa
maji! Maajabu yale yalimfanya
Kibwe aduwae kabisa na hofu
yake kuongezeka upya! Hakujua
afanye nini! Je, akimbie?
Akimbilie wapi na njia ni ile
moja tu! au arudi alikotoka
walikokuwa wale mazimwi wala
ufuta? Aliona kuwa hapana budi
afanye alivyoambiwa na Bunga,
kwani hakuona njia nyingine!
Hivyo, kwa sauti iliyojaa
mawimbi kwa wingi wa hofu,
Kibwe alianza kuimba wimbo,
kwa maneno yaliyomjia katika
mawazo yake wakati ule…..!
Nyaalileee! Nyaalileee, Nyaali…
Nyaalileee, Nyaali……
Nyaalileeee! X2
Babu zimwi nipe motooo,
Nyaali Nyaalileee,
Niikapikie waanaanguuu,
Nyaalii Nyalileee,
Niipate viijunguuu namiii,
Nyaali nyaalileee,
Chaa wali naa cha mchuuzi ii,
Nyaali Nyaalileee!
Nyaaliileee! Nyaaliileee! Nyaalii
Nyaaliileee! Nyaalii Nyaalileee!
Kibwe alipomaliza wimbo wake
ule, alimchungulia zimwi Nyalile,
ili atambue hisia zake baada ya
kusikia ule wimbo. Alimuona
Nyalile akiinua kichwa na
kuangalia juu ya lile bonde
kwenye miti mingi mirefu
alikokuwa yeye Kibwe! Lo! Kijana
yule alianza kutetemeka na jasho
likazidi kutoka! Ni dhahiri Nyalile
hakuona kitu chochote huko,
kwanza kwa kuwa Kibwe alikuwa
ni mdogo sana na miti
iliyomficha ilikuwa ni mikubwa,
na pili, jicho moja la Nyalile
halikuwa likiona vema! Kibwe
akapata faraja kidogo,
alipomuona nyalile kiogo kidogo
akianza kutabasamu, na hatimae
kutoa kicheko cha aina yake na
halafu akisema;
“Weee kidege weee! Uko wapi?
Wimbo wako ni mzuri sana.
Hebu imba tena nisikiye!” Kibwe
alizidi kujibanza mitini, akihisi
wakati wowote ule, Nyalile
angeweza kumuona! Pamoja na
hofu yake, Kibwe alijitahidi
kurudia kuimba ule wimbo wa
Nyalile, ili kumfurahisha. Na
halafu lo! Kwa jinsi zimwi
alivyofurahia wimbo ule, alikariri
maneno katika kiitikio, “Chaa
walii naa cha mchuziii, Nyaalii
nyaaliileee………!” Na kisha weee!
Zimwi Nyalile liliinuka na
kujikung’uta, huku likizidi
kutabasamu kusikia jina lake
likitajwa, na pia likifurahia uzuri
wa kiitikio cha wimbo ule. Basi
ikawa tena ni:
“Chaa wali na cha mchuchiiii,
Nyaalii Nyaaliileee! Chaa walii na
cha mchuuchiii, Nyaliii
nyaaliileee…….!”
Alipokua akirudia rudia kiitikio
hicho, zimwi Nyalile alikuwa
akicheza hatua mojamoja,
akifuatisha wimbo ule, na
kuitikia vile alivyoelewa yeye!
Alivyonogewa zaidi, akawa
anapiga hatua za haraka haraka
na kuendelea na kiitikio chake;
na hatimae likatimka mbio huku
likiitikia;
“Chaa wali na cha mchuchiiii,
Nyaalii Nyaaliileee! Chaa walii na
cha mchuuchuuchii, Nyaliii
nyaaliileee a!
Moja kwa moja zimwi Nyalile
likayoyoma na wimbo wake huku
likitimua vumbi na kuangusha
miti kwa kuikumba lilipopiga
mbio, huku likiimba. Hiloooo!
Likayoyoma, msitu na nyika
mguu nipe, hadi likafika mbali
mno, bila kujielewa, likielekea
kusini mwa dunia! Kibwe naye,
haraka alishuka bondeni na bila
kupoteza muda…… akaanza
kupiga mbio bila kusimama, hadi
alipovuka ule mpaka
uliotofautisha eneo la kule
kunako kuchwa jua, ambako ni
magharibi ya dunia, na kaskazini
ya mbali ya dunia. Kibwe alikuwa
akielekea kwa mzee wa busara
aliyeelekezwa na Bunga, ili
kupata maelekezo kuhusu
maendeleo ya safari yake ya
ajabu.
MZEE WA BUSARA.
Safari yake ikamfikisha mahali
kati ya milima miwili mirefu,
kwenye mazingira mazuri sana,
yenye mianguko na maporomoko
ya maji, mahali palipojaaliwa
ardhi iliyorutubika mno. Kule,
Kibwe alikuta miti ya matunda ya
makomamanga iliyostawi vizuri
sana. Aliona ndege wakirukaruka
na kuimba kwa furaha juu ya miti
hiyo, ambayo chini yake vilipita
vijito venye maji safi na ya
baridi, vikitokea juu ya milima.
Kibwe alifarijika mno na hali ile,
hususan baada ya kuona maeneo
mengi yaliyoathirika na ukame,
na pia yaliyokabiliwa na uwazi
uliotokana na mashambulizi ya
majabali na ardhi, baada ya
kuteketezwa na wala mawe.
Alishangaa kuona jinsi sehemu
ile ndogo ilivyotofautiana na
maeneo yale ya awali!
Mara Kibwe akakumbuka!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ahaaaaa! Sijui kwanini nilitaka
kusahau! Hapa ndipo Bunga
aliposema kuwa nitamkuta mzee
wa busara, ili nipate maelezo
kuhusu safari yangu! Sijui huyo
mzee wa busara ni nani? Lakini
nitafahamu baadae, kama kweli
hapa ndipo mahali penyewe.”
Hata hivyo kwa uchovu na njaa
aliyokuwa nayo, kijana yule
aliamua kuketi chini ya
mkomamanga , akawa anaokota
makomamanga yaliyoiva na
kudondoka chini, na kuanza kula.
Aliendelea kuketi chini ya ule mti
akipumzika, ili kupata nguvu
mpya. Alikuwa akitafakari
kuhusu hatima ya safari yake
wakati aliposikia mlio kama wa
pikipiki iliyokua ikianza
kuondoka! Alihisi kama mlio ule
ulikuwa ukitokea chini bondeni
hatua chache kutoka alipokuwa
ameketi, na alipotafakari kuhusu
mlio huo, akahisi kuwa ulikuwa
ni kama kikohozi cha jitu kubwa
sana! “Sijui ni kitu gani hicho
tena?” Kibwe aliwaza, na kwa
mara nyingine akaanza kupata
hofu. Alianza kujuta kwa nini
alikuwa kule mbali mno na
wazazi wake, ambao hata
hakukumbuka walikokuwa! Hata
hivyo, taratibu alinyanyuka na
kuanza kuangaza angaza,
akisogea bondeni uliposikika ule
mlio. Alitaka sana kufahamu ni
kitu gani kilichotoa mlio wa
labda tuseme….pikipiki? ……
Trekta……..?
Kila alipoangaza, hakuona kitu
chochote! Alisogea na kuzidi
kuchungulia chini bondeni, lakini
hakuona kitu licha ya ardhi ya
tope jeusi ambalo liliotesha
majani marefu, na pia
kulikuwepo lundo la kifusi
kilichoinuka mithili ya kilima
kidogo. Juu ya kilima hicho,
Kibwe aliona uyoga pori
umestawi vizuri sana. Taratibu
alisogea zaidi na kukichungulia
kile kilima, kuona kama
angeweza kushuka bondeni kwa
kurukia juu ya kilima hicho. Kwa
hiyo kutoka juu alikokuwa, kijana
yule alijirusha na kuangukia juu
ya hicho kilima. Hapo aliweza
kuangaza vema sehemu zote za
bondeni, ingawa bado alishindwa
kuona kitu chochote ambacho
kingeweza kutoa mlio wa
kustusha kama ule aliousikia
muda si mrefu uliopita.
Kibwe alishangaa sana, kwani
alikuwa na uhakika mkubwa
kuwa sauti aliyoisikia ilitokea
bondeni.
“Haya sasa ni maajabu makubwa!
Hivi ndio kusema kuwa labda
huo mlio sikuusikia? Au tuseme
haukutokea humu bondeni?”
Alijiuliza kwa mshangao mkubwa
juu ya muujiza ule wa aina yake.
Lakini kabla hajazidi kudadisi,
alisitushwa tena na mlio ule
usiofahamika, ila safari hii
alijikuta akirushwa hadi ng’ambo
kabisa juu ya bonde.
“Aaaaaaaaaaaaaaaaghh! Mama
yangu weeeeeeeeaaaagh…!” Alilia
kwa taharuki wakati alipokuwa
akielea hewani kabla ya
kuangukia kwenye matawi ya
mti, mbali na pale alipokuwa
awali.
Kijana aligwaya vibaya sana
akiwa ananing’inia juu ya mti
kama popo. Alikuwa akitweta na
kupumua kwa kasi, huku macho
yametoka pima, bila kufahamu
kilichomsibu! Halafu, kabla
hajatulia vema, kilisikika kitu
kama chafya ya nguvu
iliyoambatana na upepo mkali
kama wa gari moshi likifoka, na
hapohapo yeye alizolewa na huo
upepo na kujikuta akielea tena
hewani, na kisha akatupwa mbali
zaidi juu ya bonde kulikokuwa na
miti ya mikomamanga, akawa
amebanwa na matawi ya mmoja
kati ya mikomamanga ile!
Walisindikizwa na raia wa
Azarbajan kwa shangwe na
hoihoi hadi bandarini, na kule
wakaagana kwa upendo mkubwa,
na kisha merikebu ikaanza safari
nyingine ya ajabu ya Kibwe,
kumuokoa Bhaduri binti Sultani
Bashar wa Mashariki ya mbali ya
dunia!
Merikebu ya Mfalme KashKash
iliyoyoma usiku na mchana, na
hali ya bahari ilikuwa shwari
kabisa, kwa muda wote huo.
“Tuna bahati kubwa, kwani
mpaka sasa bado hali ni shwari
sana.” Hanga alimwambia
mwenzake Kibwe. “Kwa kawaida
mimi hutapika sana baharini,
lakini leo niko salama kabisa,”
Alieleza. Kibwe alimwambia
kuwa kwa kuwa bado safari ni
ndefu asijiamini sana. Kwa
maneno hayo, wote wawili
walicheka kwa pamoja. Meli hiyo
iliyowabeba vijana hao wawili,
wahudumu wakutosha wa meli
na manahodha, ilizidi kuyoyoma
hadi kufika katikati ya bahari,
halafu jambo la ajabu likatokea!
Ile meli ilisimama ghafla, kama
kwamba ilinasa mahali. Kibwe
alipomuuliza nahodha aliyekuwa
kwenye usukani ni nini
kilichotokea, akajibiwa kuwa
hakuelewa ni nini
kimeikwamisha meli yao.
“Huenda majani ya mwani
yamenasa kwenye pangaboi
linalozungusha maji huko chini
ya meli,” alisema nahodha.
Alipoambiwa hivyo kijana yule
alijitolea kwenda kuangalia kule
chini ya meli, ingawa wenzake
walimzuia sana.
“Ni hatari kwenda peke yako.
Labda tufuatane pamoja .” Hanga
na baadhi ya wahudumu wa
ndani ya meli walimwambia.
Ingawa Kibwe alipinga kufuatana
nao, lakini wenzake walishikilia
tu, hadi yule kijana akakubali
waende wote.
Naam, karibu watu wanne
walishuka na kuogelea kwenda
chini ya ile merikebu, kuangalia
hicho kilichonasa kwenye
pangaboi la meli yao. Wote
waliogelea, na Kibwe alikuwa
mbele zaidi, hivyo alitangulia
kuwasili pale lilipokuwa hilo
pangaboi. Lakini lo! Pangaboi
lenyewe lilikuwa limeshikiliwa
madhubuti na mtu mmoja
mwembamba kupita kiasi, na
mrefu kuliko utakavyofikiria!
Macho ya mtu yule yalikuwa
pembeni mwa sura yake,
iliyofanana na chura!
“Ahaa! Kumbe! Tunakutana tena
siyo?” Kibwe aliwaza, na bila
kupoteza muda, na haraka kama
mwendo wa mshale, kijana yule
alitoa rungu lililokuwa kwenye
mfuko alioubeba mgongoni, na
kulirusha kwa nguvu zake zote,
kumtupia yule mtu wa ajabu,
akilenga ule mkono ulioshikilia
lile panga boi! Kwa kishindo
kikubwa, lile rungu likamfikia
kwenye mkono wake huo, na
palepale akaachia lile panga boi,
na kama umeme, akapotelea
chini kabisa ya bahari!
Naam kwa mara nyingine, Kibwe
alikutana na mmoja kati ya jamii
ya majini wa bahari, jamaa zake
‘Makatta wa Makattani.’ Wakati
hayo yakitokea, wenzake wengine
waliokuwa wakija kuangalia chini
ya merikebu, walifika na
kumkosa yule jini wa bahari kwa
sekunde tu!
“Kwani kuna nini?” waliuliza, na
wakati huohuo, ile meli ikawa
inasogea mbele!
“Ilikuwa ni mwani tu, ulioshikilia
pangaboi! Nimekwisha uondoa ,
na ndio maana mnaona meli
inaondoka. Twendeni tuwahi!”
Kibwe alidanganya, akichelea
kuwatia hofu watu na hadithi za
majini wa bahari! Wote
wakarejea melini, na kuendelea
na safari.
Kibwe na wenzake waliendelea
na safari yao huko mashariki ya
katikati ya dunia, kwenye
majabali yaliyouzingira mto
mkubwa wa maji, mto Sakara,
ambako Bhaduri binti Sultani
kitinda mimba na mwana wa
saba wa Sultani Bashar, alikuwa
ameketi juu ya uwanda wa jabali
moja, akisubiri kutolewa kafara!
Kwa moyo wa ushujaa, na utiifu
kwa amri ya baba yake, mrembo
Bhaduri binti Sultani aliketi juu
ya jabali kwenye kiti kimoja
kizuri cha enzi, akiwa
amepambwa kwa sundusi za
hariri, mikufu, hereni na vikuku
vya dhahabu na vito vya
thamani, huku akinukia utuli
mchanganyiko kama udi, miski
na ambari, akisubiri wakati wake
wa kuchukuliwa na hicho
kitakachokuja kumchukua!
Kibwe na msafara wake ndani ya
merikebu yao ya fahari,
waliyoyoma kuelekea huko
mashariki ya katikati ya dunia,
wakati huo zikiwa zimebaki siku
chache tu, kuwasili mwisho wa
safari yao. Usiku mmoja
alipokuwa amelala na mwenzake
Hanga kwenye chumba chao,
Kibwe alimuota Bunga, akimpa
maelekezo ya safari yao hiyo.
“Lazima msafara huu usitishwe
haraka iwezekanavyo, mara tu
mtakapowasili kwenye bandari
yoyote ya jirani,” alisema Bunga.
Aliendelea kumwambia kuwa
itabidi wasubiri kwenye bandari
hiyo kwa siku mbili zaidi, kabla
ya kuanza tena safari yao. “Katika
muda huo mtakapo kuwa
mkisubiri kwenye bandari hiyo,
mtakuwa mmejinusuru na hatari
ya kupambana na mwamba wa
barafu majini, na pia
mtanusurika na tufani kubwa
itakayotokea mnamo saa ishirini
na nne zijazo.” Kibwe alimsikiliza
Bunga, aliyeonekana akielea
hewani kama ndege, na maneno
yake yakisikika kwa kukatika
katika, kwa sentensi
zisizokamilika!
Ndotoni Kibwe alikuwa
akimcheka Bunga, na
akimshangaa sana kwani kwa
mara hii alimuona ni wa ajabu
kabisa. Hakuamini maneno yake
hata kidogo, “Usinitanie mzee
Bunga! Unajua kwamba msafara
huu lazima uwahi nchini Shamsi
mashariki ya kati kati. Sasa
mbona unataka
kutuchelewesha?” Kibwe alianza
kulumbana na kile kijitu cha
ajabu.
“Tutaendelea tu……..na-
safa-”Lakini kabla hajamalizia
maneno yake, Kibwe akaona
ukuta uliokuwa mbele yake
ukipasuka, na maji mengi
yakianza kumwagika kama
mafuriko, na kumzoa Kibwe
kutoka pale alipokuwa, akajikuta
akitapatapa kujinusuru asizame!
Ingawa alikuwa anajitahidi
kuogelea, lakini alishindwa, na
hivyo akaanza kuzama---!
Akazama—akienda moja kwa
moja hadi chini kabisa ya dimbwi
la maji---! Pumzi zikamwishia
kabisa! Halafu ghafla, akajiibua
juu, na kutoa kichwa chake nje ya
dimbwi la maji, na kisha palepale
akasituka na kuamka, huku moyo
wake ukienda kwa kasi mno!
Aliinuka na kuketi kitako, akiwa
anapumua haraka haraka mno!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwenzake Hanga aliyekuwa
karibu yake, naye aliamka na
kumuona Kibwe akiwa katika hali
isiyo ya kawaida. “Vipi kibwe,
mbona uko hivyo, umeota ndoto
mbaya nini?” Kimya! Kibwe
hakujibu kitu, bali alizidi
kupumua kwa haraka haraka,
huku macho yake yakiangalia
mbele zaidi ya pale alipokuwa
mwenzake, kama kwamba
hakumuona wala kumsikia
Hanga! Haraka Hanga alichukua
gilasi ya maji na kumpa
mwenzake huyo anywe, akihisi
huenda akajisikia nafuu kidogo.
”Hebu kunywa maji kidoga, labda
yatakusaidia.” Kibwe aliyapokea
yale maji bila kumwangalia
mwenzake, na akanywa funda
mbili, na halafu akajilaza
kitandani. “Unajisikiaje hivi sasa
Kibwe? Ni ndoto gani uliyoota?”
Hanga aliuliza, akiwa na wasiwasi
na jinsi alivyomuona mwenzake.
Kibwe alikohoa kidogo, na kisha
akaanza kuongea.
ITAENDELEA
 
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nadhani huko mbele kuna tatizo
kubwa sana. Nimeota kuwa
kutakuwa na kimbunga kikubwa,
na meli yetu itapambana na
mwamba wa barafu majini,”
Kibwe alimwambia mwenzake,
ambaye alimshangaa,
akimwambia kuwa alichokiona
kilikuwa ndotoni tu, wala si
lazima kitokee. Lakini Kibwe
hakumsikiliza Hanga, bali
aliendelea kusema. “Kama
hatukusitisha safari yetu kwenye
bandari yoyote ya karibu angalau
kwa siku moja na nusu hadi
hatari hiyo ipite, wote tutapoteza
maisha yetu.” Hee! Hanga
akaduwaa akimwangalia
mwenzake huyo
aliyechanganyikiwa, au tuseme
vile alivyoamini Hanga kwa
wakati ule. Iweje tena jambo la
ndotoni, Kibwe akalichukulia
kuwa ni jambo kubwa na halisia?
Hanga alijaribu kuzungumza na
mwenzake akimsihi ajaribu
kutulia tu, na atasahau kuhusu
ndoto yake. “Na hata hivyo,
unadhani kuwa utaeleweka kwa
manahodha utakapowaambia
wasitishe safari kwa kuwa uliota
kuwa mbele kuna hatari? Jaribu
kufikiri vizuri Kibwe.” Kibwe
alishikilia palepale, akimwambia
Hanga kuwa lazima manahodha
wamwelewe, ama sivyo, wote
wamo hatarini!
Kwa hiyo, Hanga na Kibwe
walikwenda hadi kwenye
chumba cha manahodha, na
kuwaelezea kuhusu hatari iliyoko
mbele. “Lazima tusitishe huu
msafara, mara tu tutakapofika
bandari ndogo ya karibu, kabla
ya kuelekea nchini Shamsi, ama
sivyo, wote tutateketea.” Kibwe
aliwasihi wale manahodha, bila
kuwa na uthibitisho wa kutosha
wa hoja yake hiyo. Manahodha
wakamuona kuwa anafanya utoto
tu, hivyo kwa kebehi,
wakamwambia; “Hivi unadhani
kuwa katika maisha yetu kwenye
kazi hii, tungekuwa tunaamini
kila tulichokiota, tungeweza
kufanya safari kama hizi? Kijana,
kumbuka kuwa ndoto ni ndoto
tu. Hatuwezi kuacha kusafiri, eti
kwa kuwa mtu mmoja miongoni
mwetu ameota kuwa mbele kuna
hatari!” Pia manahodha wale
walisema kuwa kulikuwa na
umuhimu wa kuwahi kufika kule
waendako, ili waweze kugeuza
merikebu yao na kurudi makwao,
baada ya kumsindikiza Kibwe.
“Lakini jamani, mmejiuliza kuwa
huenda kuna ukweli kwenye
maneno ya kijana huyu?” Baadhi
ya wahudumu wa meli walihoji,
wakinong’ona chinichini. “Kweli
eti! Na labda tukiyadharau
maneno yake hayo, tutakuja
kujuta yatakapotokea hayo
anayoyatabiri!” Wahudumu wa
meli walisema hivyo, huku
wenzao wengine wakihofu sana,
walipokisia kuwa huenda kukawa
na ukweli kwenye hoja ya yule
kijana. ”Ndiyo kusema kuwa
wote tutakuwa hatarini!”
waliambiana. Hata hivyo wengine
miongoni mwa wahudumu wale
waliowaunga mkono manahodha
na hoja zao, wakasema kuwa
yule kijana aliota tu, na wala
hakuletewa onyo rasmi la
kimazingaombwe kutoka kokote.
“Haya jamani na tuendelee na
safari yetu, na tuachane na
mawazo ya kishirikina!” walisema
wahudumu hao, wakiwahimiza
manahodha wasipoteze muda.
Lakini lo! Laiti kama wangejua!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Haya, safari ikaendelea kama
ilivyoamuliwa, na hakuna
aliyejuwa kuhusu mkasa ambao
ungetokea mnamo saa ishirini na
nne zijazo! Kilometa kadhaa
kutoka pale walipokuwa, kwenye
mwamba mkubwa sana wa
barafu majini, pande moja kubwa
la barafu lilijigawa kutoka
kwenye mwamba huo mkubwa
wa barafu majini, uliokuwa kama
mlima mkubwa sana! Sehemu
hiyo ya mwamba iliyotanda
baharini, ilikuwa ikielea na
kusukasuka kuelekea kule
ilikokua merikebu ya mfalme
KashKash, walimokuwemo Kibwe
na abiria wengine! Wakati
huohuo, mawingu mazito na
meusi yakawa yanajikusanya, na
hivyo giza nene likaanza kutanda.
Upepo nao ukaanza kuchanganya
kasi ya mwendo wake,
iliyoongezeka kwa kila dakika, na
kuvuma kwa kuvuruga mawimbi
ya bahari, yaliyonyanyuliwa juu
kwa urefu mkubwa wa
kustaajabisha, kwani kimbunga
nacho kilikwishaanza! Lahaula!
Huko kulikokuwa kukijiandaa
katika hali hiyo, ndiko ilikokuwa
ikielekea merikebu iliyowabeba
kina Kibwe na wenzake!
Merikebu ile ilisafiri kwa
kilometa nyingi humo baharini,
na wakati wote huo, Kibwe akiwa
na wasiwasi mkubwa, kwani
aliamini kabisa kuwa huko mbele
sio kuzuri. “Nafahamu kuwa
Bunga hawezi kutokea waziwazi
ili kutuonya kuhusu hatari hiyo,
maana watu wote watashangaa
na pia kuhofu sana, mara
watakapomuona,” Kibwe aliwaza.
Lakini kwa bahati mbaya, ilibidi
kijana yule asubiri hatari hiyo
ifike, kwani hakuwa na la
kufanya! “Haya. Liwalo naliwe!”
alijiambia.
Mnamo majira ya saa kumi na
mbili asubuhi, abiria ndani ya
merikebu ile wakaona hali ya
hewa ikibadilika. Upepo ukawa
unavuma kwa kasi na kwa hasira,
huku bahari ikianza kuchafuka.
Maji ya mawimbi yaliyokuwa
yakijitupia na kupiga pembezoni
mwa merikebu, yaliingia sitahani
kwa wingi mno! Chini kabisa ya
sitaha humo melini, nako kuilijaa
maji tele! Kufikia hatua hiyo,
abiria wote wakaanza
kuhamanika, wakitoka vyumbani
mwao ili kujiunga na wenzao,
kuona jinsi hali ile iliyojitokeza,
ilivyoashiria kuhatarisha maisha
yao. “Haya sasa, tuone kama
hakuna atakaye amini maneno
yangu,” Kibwe alimwambia
mwenzake Hanga, aliyekuwa
ametowa macho pima
akimshangaa Kibwe kwa kuyajua
yote yale mapema! Ah! Laiti
kama watu wangemuamini na
ndoto yake! Mawazo hayo
yalikuwa yakipita kichwani mwa
Hanga. “Naam! Utabiri wa Bunga
umeanza kuwa kweli!” Kibwe
aliwaza, huku akiangalia jinsi
walivyokuwa wamezingirwa na
maji mle merikebuni.
“Haraka kawaambie abiria
waliokuwa chini ya staha
waondoke na kuja juu zaidi! Na
wa huku juu wawe waangalifu
wasisogee pembezoni mwa meli!”
Mmoja kati ya manahodha
aliwaambia wenzake. “Lo!
Kumbe yule kijana alisema kweli
kabisa.” Manahodha wale
waliambizana, huku wakikimbia
kwenda kuwatahadharisha abiria
kule walikokusanyika. Huko
waliwakuta baadhi ya abiria
wakiwa wamejeruhiwa kwa
kukimbia kutoka vyumbani
mwao, wakitafuta nusura sehemu
ambazo maji hayakufika.Wengi
wao walikuwa wakianguka na
kutereza mara kwa mara, kwani
ile merikebu ilikuwa ikisukasuka
kwa kusukumwa na mawimbi.
Kila ilipoegemea upande mmoja,
merikebu hiyo iliwamwaga abiria
kwa upande huo! “Kwa hakika
maneno yako yalikuwa sahihi
kibwe. Leo wote tuko hatarini!”
Hanga alimwambia mwenzake ,
wakati walipokuwa wakijishikiza
kwenye nguzo za ile meli, ili
wasiteleze na kuangukia sehemu
nyingine hatari zaidi. “Ndio hivyo
tena. Lakini haina haja kulilia
maji yaliyomwagika, kwani si
rahisi kuyazoa,” alisema Kibwe.
“Iliyobaki ni kuomba Mungu
atuvushe salama kutokana na
janga hili.”
Huko nchini Hazina mashariki ya
dunia jirani kabisa na
Azarbarjan, Sultan Hazari Basari,
alikuwa akisharehakea sikukuu
ya kuzaliwa mwanawe wa kiume,
kutokana na nadhiri aliyoiweka
miaka kumi na tano iliyopita,
baada ya kuota ndoto iliyoashiria
kuwa katika umri wa miaka kumi
na nne, kijana wake atakumbwa
na jini Makata na kupelekwa
mashariki ya mbali kwenye hewa
inayogeuza watu kuwa mawe!
HANGA BIN HAZARI
Katika zama zile za kale, kule
mashariki ya dunia nchini Hazina
jirani kabisa na nchi ya Azarbajan
kwa mfalme KashKash,
alikuwepo Sultani mmoja
mashuhuri sana, aliyeitwa Hazari
bin Basari. Sultani huyo alitawala
raia wake kwa amani, uaminifu
na upendo mkubwa, na kwa
sababu hiyo, raia wake
walimpenda sana. Kwa bahati
mbaya kwa miaka mingi sana
Sultani yule na mkewe
hawakujaaliwa kupata mwana
ambaye angekuwa mrithi wa kiti
cha utawala baada kuondoka
Sultani Hazar. Jambo hilo
liliwasonesha sana. Siku moja
Sultani Hazari aliwaita wazee na
washauri wake mashuhuri,
akawaelezea masikitiko yake.
“Sijui nifanye nini ili nami
niweze kupata mtoto
atakayekuwa mrithi wangu pindi
nitakapoitoka dunia hii.”
Aliwaambia.
Naam wale washauri
walipokutanisha vichwa vyao ili
kutafuta ufumbuzi wa jambo lile,
wote wakapata jibu moja.
“Ama kwa hakika tatizo la namna
hiyo hupatiwa ufumbuzi kwa njia
moja tu, nayo ni kumuomba
Mwenyezi Mungu mwenye kila
uwezo. Tunakushauri uandae
karamu kubwa na uwaalike
yatima, mafakiri na mawalii, ili
wamuombe Mwenyezi Mungu
akujaalie kupata ufumbuzi wa
jambo lako.” Walimshauri.
Sultani Hazari aliupokea ushauri
wao kwa dhati. Akaandaa
karamu mkubwa na kutoa sadaka
kwa wajane, yatima na mawalii,
ili kupata radhi za Mwenyezi
Mungu.
Naam haukupita muda mrefu,
mkewe akashika mimba na miezi
tisa baadae akajifungua mwana
wa kiume, waliyemwita Hanga.
Ndiye Hanga bin Hazari huyo!
Sultani na mkewe walifurahi
mno, na wakamlea mtoto wao
kwa uangalifu na mapenzi
makubwa sana hadi alipofikia
umri wa miaka kumi na nne.
Walimpa mtoto wao elimu bora
na mafunzo mbalimbali ya
mambo ya kimaisha, wakitarajia
kuwa iko siku angekuwa mtawala
wa nchi yake ya Hazina.
Siku moja wakati akiwa
usingizini, Sultani Hazari Basari
aliota ndoto ya kutisha sana
iliyohusiana na mwanawe
kipenzi, Hanga. Katika ndoto yake
alikuwa kwenye mji mmoja wa
ajabu uliokuwa chini kabisa ya
bahari, ambako huko alizingirwa
na wingu nene la moshi mweusi
kupita kiasi. Kila alipojitahadi
kukodoa macho ili aone vizuri
mbele yake, hakuweza kuona
chochote. Wahka ulimzidi
aliposikia sauti nzito ya kutisha
ikiunguruma masikioni mwake,
ikimwambia;“Ewe Hazari! Ewe
Hazari! Fahamu kuwa furaha
yako ya kupata mtoto
haitaendelea! Haitaendelea!
Haitaendeleaaaa…! Ha ha ha ha
ha…..!” Kile kicheko kilichofuatia
maneno yale mazito kilikuwa ni
cha kuogofya na kukata
matumbo!
Kile kicheko kilisita kidogo na
mchekaji yule asiyeonekana
akazidi kumshindilia maneno
mengine ya kutisha na ya
kukatisha tamaa zaidi.
“Kamwe huyo mwanao
hatafikisha umri wa miaka kumi
na tano, kwani kabla ya kufikia
muda huo, atakumbwa na pepo
mbaya na kupotelea kwenye
msitu wa hatari...msitu wa
kindumbwe!”
“Eeg Mungu wangu weee!”
Mfal,me Hazari alilalama ndotoni,
na wala ile sauti haikusitishwa na
mlalamo wake, ikaendelea, “…
katika msitu huo daima uovu
haulali wala hausinzii, na milima
ya huko ni maarufu kwa
maangamizi ya moto na hewa ya
huko haikuwa ila ni yenye wingi
wa sumu kali….Ha ha ha-ha-ha-
ha-aaaaaaaa! Huwezi kumnusuru
mwanao asilani wewe…huwezii…
huweziiiiiiii! HHha-ha-ha-ha-
haaaaaaa!”
Ile cheko mbaya ilivuma kwa
mudsa mrefu huku ikizidi kufifia
taratibu mpaka ikawa kimya cha
kutisha kuliko hata ile cheko
yenyewe.
Sultani Hazari aligutuka kutoka
usingizini na kwenye ndoto ile
akiwa na wahka na hofu kubwa!
Moyo ulikuwa ukimuenda kasi na
jasho lilikuwa likimtiririka kama
mtu aliyekuwa akikimbia! Mkewe
alipoamka na kumuona katika
hali ile, alipatwa na wasiwasi
mkubwa.
“Umepatwa na nini mahabuba
wangu? Mbona unanitisha?” Mke
akadadisi kutaka kujua
kilichomsibu Sultani usiku ule.
Sultani alikaa kimya kwa muda,
kisha akamwambia, “Kwa hakika
ndoto niliyoota inanipa wasiwasi
mkubwa.”
Na akamsimulia mkewe ndoto
yake.
“Usiogope sana mume wangu.
Asubuhi kutakapokucha
tutawaita waalimu waje
kumuombea dua mwanetu,
kwani ndoto hiyo ni ya uovu wa
majini tu, wapendao kutia
wasiwasi katika nyoyo za
wanadamu!”
Kwa hiyo siku iliyofuata Sultani
Hazari aliandaa kisomo kikubwa
cha maombi kwa Mwenyezi
Mungu, kilichohudhuriwa karibu
na raia wote wa nchi ya Hazina.
Siku ile Sultani akaweka nadhiri
ya pekee! “Mwanangu
atakapofikia umri wa miaka kumi
na tano bila kupatwa na madhara
yoyote, nitajaza fedha kwenye
visima saba, na mafuta ya kupikia
kwenye visima vingine saba, iwe
sadaka kwa raia wangu wote wa
Hazina kwa ajili ya nusura ya
mwanangu. Kila mmoja kwa
wakati wake atajichukulia kile
atakachojaaliwa iwe fedha au
mafuta, kadiri ya uwezo
wake!” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kufuatia kisomo kile, Hanga
alilelewa kwa uangalifu zaidi na
mapenzi makubwa kupita kiasi
hadi alipofikia umri wa miaka
kumi na tano na nusu, wakati
ambao tayari alikuwa amevuka
ule umri wa miaka kumi na tano
ambao Sultani aliota kuwa
angekuwa hatarini. Kwa bahati
Sultani Hazari Basari alikumbuka
nadhiri yake, hivyo akachimba
visima kumi na nne, saba kati
yake akavijaza fedha na saba
akavijaza mafuta ya kupikia.
Akatumwa mjumbe apite mitaani
kuwatangazia raia wote wafike
kwa Sultani na kujipatia sadaka.
Kama kawaida ya matangazo
kutoka kwa wafalme, mjumbe
yule akapiga la mgambo ambalo
kila likilia lazima huwa kuna
jambo.
“Naam ndugu zangu, Sultani
wenu anawatangazia kuwa
mwanawe Hanga bin Sultani kwa
bahati nzuri amefikisha umri wa
miaka kumi na tano bila kupatwa
na madhara yoyote, kama
ilivyodhaniwa awali! Ili
kudhihirisha furaha yake, kesho
Sultani atatimiza ahadi yake ya
kutoa sadaka ya fedha na mafuta
kwa raia wote wa nchi ya yake!
Wote mnatakiwa kufika kwenye
kasri lake bila kukosa!”
Naam baada ya ujumbe ule
kuwafikia raia wote
waliokusudiwa, watu kutoka
sehemu mbalimbali za milki ya
Sultani yule nchini Hazina
walikwenda katika kasri lake,
wakajizolea fedha na kujichotea
mafuta kwa ajili ya lishe yao
bora. Wake kwa waume wazee
kwa vijana na watoto kwa
wakubwa walifurahia zawadi
zile, na kila mmoja alishukuru na
kumuombea Hanga anusurike na
hasadi na kumtakia maisha
mema.
Lakini masikini bibi mmoja mzee
aliyejulikana na jamaa zake kwa
jina la ‘Ajuza’ aliyeishi nje kabisa
ya mji mkuu katika nchi ya
Hazina, alichelewa kuzipata
habari zile nzuri, na akasikitika
sana kwa wenzake waliobahatika.
“Mbona Sultani hakutangaza nchi
nzima kama ilivyo kawaida
yake?” Alidadisi kizee yule.
Wenzake walioshuhudia mjumbe
wa Sultani akipita mtaa kwa
mtaa kutangaza habari njema
kwa raia wa Hazina,
walishangazwa na lawama za
yule Ajuza.
“Kwani ulikuwa wapi hata
ukakosa kumsikia mjumbe
akitangaza mitaani?”
Walimuuliza. Walimshauri
aharakishe kwenda kwa Sultani
akajaribu bahati yake.
“Bila shaka utapata japo kidogo,
ama mafuta au fedha. Usikate
tamaa ndugu yangu.” Aliambiwa
na mzee mwenzake aliyeishi
jirani naye. Bila ajizi, wakati
uleule kibibi ‘Ajuza’ aliondoka na
kuelekea kwa Sultani Hazari,
ambaye masikini, hakuwa hata na
fununu kwamba ujio wa yule
‘Ajuza’ katika jumba lake
ungebadili kabisa mwelekeo wa
maisha ya Hanga, na kwamba
ungefuata mkondo wa njozi yake
aliyoiota awali!
Kizee yule alipofika kwenye kasri
la Sultani Hazari, bahati haikuwa
yake. Visima vyote saba vya
fedha havikuwa na kitu,
isipokuwa kisima kimoja tu kati
ya visima saba vya mafuta ndicho
kilichokuwa na mafuta kidogo
sana!
“Ah, masikini mimi! Sina la
kufanya kwani kila kitu huenda
kwa riziki ya mtu. Hii niliyoikuta
ndiyo riziki yangu. Nitashuka
humo kisimani nikadundulize
mafuta yaliyomo.” Alisema na
nafsi yake na huku taratibu
akijaribu kushuka kisimani kwa
ngazi maalum iliyojengewa
pembezoni, na huku kichwani
kwake akiwa amebeba mtungi.
Alipofika chini kabisa alichukua
muda mrefu sana kuujaza ule
mtungi. Hatimae alipofanikiwa
kuujaza, aliunyanyua na taratibu
akajitwika kichwani na kuanza
safari ya kutoka nje ya kisima,
kwa kutumia ile ngazi
aliyoshukia. Alitoka kwa mwendo
wa pole mno, kwani kutokana na
kazi aliyoifanya ya kuujaza
mafuta mtungi wake, alihisi
maumuvu makali mno kiunoni
na mgongoni!
Gorofani, juu kabisa ya kasri la
Sultani Hazari, Hanga bin Hazari
alikuwa akimwangalia ‘Ajuza’
yule kwa muda mrefu, tangu
aliposhuka kisimani, hadi
alipokuwa akijaza mafuta mtungi
wake na pia wakati alipokuwa
akitoka akiwa amejitwika mtungi
wake kichwani. Alitabasamu
kuona jinsi bibi yule alivyokuwa
akihangaika kufanya kazi ndogo
kabisa! Kwa utundu wa kitoto,
kijana yule aliyekuwa ameshikilia
manati, akaulenga mtungi wa
‘Ajuza’ na kuachia kijiwe
kilichofika moja kwa moja, tena
kwa kasi kubwa kwenye mtungi
wa yule bibi , na papo hapo
kuupasua mapande mapande, na
kumwacha ‘Ajuza’ akiwa
amelowa mafuta chapachapa
mwili mzima!
Hasira alizopata bibi yule
hazielezeki. Aliinua kichwa chake
juu kuangalia gorofa ya saba ya
jumba la Sultani, kuona ni nani
aliyemfanyia kitendo kile cha
kiburi! Hasira zake zilizidi
alipomuona Hanga bin Sultani
akimwangalia kutoka juu,
akimcheka!
“Ni mtoto wa nani wewe shetani
rajimi usiyekua na adabu wala
heshima kwa watu wazima? Hivi
hujafunzwa na wazazi wako
ukaambiwa kuwa heshima ni
kitu cha bure? Kama unajiona
kuwa wewe ni bora kuliko
wenzako, kwa nini hujaenda
Kaskazini mashariki kwenye ‘Paa
la dunia’, ukatekeleze yale
wanayoyafanya wenzako walio
bora, wanaojitahidi kuinusuru
sayari kutokana na majanga
yanayoikabili?” Bibi kizee
aliyaelekeza maneno yake kwa
Hanga kwa hasira kubwa,
akimwacha kijana yule akiwa
kimya, akitafakari kile
alichokuwa akikisikia.
“Wewe huwezi kuwa bora kuliko
Mwana Mteule ambaye licha ya
uwezo na vipaji alivyonavyo vya
kupambana na maovu, hata siku
moja hajawahi kuwavunjia
heshima wazee kama sisi!” Ajuza
yule alimalizia maneno yake kwa
kusisitiza kuwa ni wakati Hanga
atakapofika kule ambako uovu
umechukua nafasi kubwa kuliko
wema, ndipo atakapotambua
kwamba asiyefunzwa na mamaye
hufunzwa na ulimwengu!
Maneno haya ya hasira ya Ajuza
yalifuatiwa na msonyo mrefu
kupita kiasi, ulioufanya moyo wa
Hanga uzizime!
Yule bibi aliondoka akiwa
amechukia mno. Alikuwa
akijifutafuta mafuta usoni kwake
na mwilini, wakati Hanga akiwa
ameduwaa na kumwangalia kwa
tafakuri ya hali ya juu.
“Huyu ni nani? na anafahamu
vipi mambo yote yale
aliyoyasema?” Alijiuliza na
kutafakari kuhusu huyo Mwana
Mteule aliyetajwa, na hatari
iliyokuwa ikiikabili sayari yao.
Wakati huohuo, alijutia sana
utovu wake wa nidhamu
alioudhihirisha kwa bibi kizee
ambaye hakumkosea chochote.
Haraka sana akapata wazo la
kumfuata, kwanza akiazimia
kumuomba radhi kwa kosa lake
alilolifanya, na pili akitaka kupata
majibu ya majanga yanayoikabili
sayari yake. Akashuka ngazi za
kasri la baba yake mbilimbili kwa
wakati mmoja, ili aweze
kumuwahi yule kizee kabla
hajatoweka. Alipomkaribia
alikuwa akipumua kwa kasi mno
kwa jinsi alivyopiga mbio kutoka
gorofani hadi chini!
“Bibi…bibi…! Tafadhali nisamehe
bibi yangu! Nimekosea sana
kufanya vile nilivyofanya bibi…
naahidi sintarudia kukufanyia
vile nilivyokufanyia, na wala
sintamfanyia mtu mwingine
yeyote matendo ya utovu wa
heshima ya namna yoyote!”
Hanga alimuomba radhi yule bibi
huku machozi yakimtiririka.
Yule bibi alipomwangalia kijana
yule, alihisi kuwa ni kweli alijutia
kosa lake. Lakini pamoja na
kumsamehe alimwambia kuwa
mara nyingi ni bora kuzingatia
mafundisho ya wazazi, badala ya
kusubiri mafundisho ya
ulimwengu, kwani ulimwengu ni
mwalimu mkali mno kuliko
waalimu wote.
“Lazima kwanza uumie kabla
mafunzo ya ulimwengu
hayajazama akilini mwako.
Zingatia hivyo mjukuu wangu!”
Hanga akapiga magoti na kujibu,
“Sawa bibi, siku zote
nitakumbuka usia wako huu na
kuuzingatia”
Lakini kwa kuwa Hanga alipenda
sana kufahamu kazi anayoifanya
‘Mwana Mteule’ huko Kaskazini
Mashariki, na akatamani sana
naye apate fursa ya kumsaidia
mwenzake huyo katika kazi yake
ngumu, alimuuliza bibi Ajuza
jinsi ya kufika kule ‘Paa la Dunia’
Kaskazini Mashariki ya Sayari
yao.
Ingawa yule bibi alifahamu kuwa
kijana yule hakuwa na vipaji
wala uwezo kama alionao
'Mwana Mteule’, lakini alihisi
kuwa alikuwa na hamu na nia ya
kusaidia katika jukumu lile la
aina yake.
“Ingawa haitakuwa rahisi kufika
sehemu ile nyeti, lakini
utakapowasili Kaskazini
Mashariki katika eneo la Paa la
Dunia, utakuta limezingirwa na
majabali marefu sana yenye rangi
nyeusi”. Alimwambia kuwa
vilevile eneo lile hujulikana kwa
jina la ‘Bam i Dunya’.
“Utafuata njia nyembamba
iliyozungukwa na msitu mnene
kwa pande zote, na msitu huo ni
maarufu kwa jina la ‘Msitu wa
Kindumbwe’ au kwa maana
nyingine ‘msitu wa hatari’
Tahadhari sana kwani msitu huo
unakaliwa na viumbe wengi
hatari pamoja na mashetani na
vibwengo.” Yule Ajuza
alimweleza Hanga, na maelezo
yake yale yalijaza hofu kubwa
moyoni mwa yule kijana.
“Sasa bibi, ni nini hasa
ninachotakiwa kukitafuta huko?”
Alidodosa Hanga.
“Utakapofika mwisho wa njia
nyembamba kama uchochoro
wenye giza nene, utatokea katika
mlango wa kuingilia kwenye
pango lenye sanamu kubwa la
shaba la kichwa cha simba,
chenye mkufu mnene wa fedha
shingoni na wenye vidani vitatu
vya sanamu za fedha za kucha za
simba. Kimoja kati ya vidani
hivyo chenye kito cha rangi ya
samawati ndani yake, ndicho
chenye ujumbe ulioandikwa
kwenye upande uliopinda wa
sanamu ya ukucha huo”
Hanga alimsikiliza kwa makini
sana, na alipouliza ataelewa vipi
ni kidani kipi chenye kito
kinachohusika, alipewa
maelekezo ya kutosha kabisa.
“Usihofu lolote katika safari hii.
Wewe nenda tu na maelekezo
zaidi utayapata kadiri
utakavyokuwa safarini, kwani
huko kuna msaada hata
usioutarajiwa!”
Hanga alipowafahamisha wazazi
wake kuwa alitaka kufanya safari
kwenda Kaskazini Mashariki ya
dunia kufuatilia jambo muhimu
sana kuhusu usalama wa sayari
yao na jamii katika sayari,
Malkia, mama yake alipinga sana
jambo hilo. “Hapana mwanangu,
usithubutu hata kidogo kuchukua
hatua hiyo ya hatari.’” alionya.
huku akilia machozi. “Unafahamu
fika kuwa wewe ni mwana pekee
tuliyejaaliwa na Rahmani baada
ya miaka mingi ya kusubiri. Sasa
unataka kuondoka utokomee
sijui wapi huko mwanangu?
Ukipatwa na madhara huko
ughaibuni tutakusaidia vipi sisi?”
Lakini pamoja na mama yake
kumsihi sana, Hanga alishikilia
uamuzi wake, akisema; “Kama
mimi ni mwana pekee kwenu
ninyi wazazi wangu, hamuoni
fahari kama nikichukua hatua ya
kipekee kutekeleza jukumu
kubwa la kuinusuru sayari yetu?
Mbona nasikia kuwa tayari yuko
mwenzangu mwenye umri kama
mimi anayeshughulikia jambo
hilo na ambaye naye ni mwana
pekee wa wazazi wake? Tafadhali
mama niruhusu nami nikasaidie
jukumu hili muhimu!” CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuwasihi wazazi wake
wawili kwa muda mrefu hasa
mama yake, hatimae baba yake
Hanga Sultani Hazari,
akamuomba sana mkewe
amridhie kijana wao aweze
kulifuatilia jukumu lile zito lenye
umuhimu mkubwa na manufaa
kwa wengi. “Atakapojitosa katika
jambo hilo na kuchangia jitihada
za kuinusuru sayari yetu, bila
shaka yeye pamoja na sisi wazazi
wake tutapata sifa lukuki kwa
jamii ya mataifa mbalimbali!”
Sultani yule alimsisitizia Malkia
wake, basi,Malkia aliridhia
uamuzi wa mwanae. Kwa
muafaka ule, mama yake Hanga
aliandaa chakula rasmi kwa ajili
ya safari ya mwanawe, ambacho
ni mikate saba ya unga wa
mchele aliyomfungashia pamoja
na guduria la maji ya kunywa
njiani. Sultani naye akaandaa
farasi mkubwa madhubuti
ambaye angeweza kuhimili
mwendo mrefu wa safari
aliyoiazimia mwanawe!
“Mungu awe nawe katika safari
yako na akufanyie wepesi
kwenye shughuli yako nzito
mwanangu!” Mke wa Sultani
Hazari alimwombea dua njema
Hanga wakati akiagana naye,
akimkumbatia huku machozi
yakimtoka bila kizuizi. “Punguza
wahaka katika nafsi yako na kila
mara kumbuka kujiamini. Usikate
tamaa kwa jambo lolote
litakalotokea.” Sultani Hazari
naye alimwambia mwanawe,
akamshika mkono wake
madhubuti wakati ule wa
kuagana!
HANGA KATIKA PAA LA DUNIA.
Kwa muda wa siku saba Hanga
alisafiri usiku na mchana,
akavuka misitu, nyika na
majangwa makubwa kupita kiasi.
Alipita milimani na mabondeni
hadi baada ya miezi kadhaa ya
tabu na mnashaka, njiani akila
matunda waliyokula ndege,
alipofikamahali penye majabali
manne meusi marefu sana,
yaliyozingira uwanda wa milima
yenye urefu wa zaidi ya mita elfu
moja! Bondeni alikosimama chini
ya yale majabali, Hanga
alistaajabu sana kuona jinsi vilele
vya yale majabali vilivyoonekana
kama kwamba viligusa mbingu!
Alistaajabu pia kuona jinsi msitu
ulivyofunga katika lile eneo
alilokuwepo, hali
iliyomsababishia hofu kubwa
kwake kutokana na giza nene
lililosababishwa na miti mirefu
kupita kiasi! Miti ile ilitoa majani
kama mizizi katika matawi yake
na mizizi kwenye mashina yake.
Alishangaa kuona baadhi ya
majani yaliyokuwa na upana wa
ajabu mithili ya masikio ya
tembo!
“Sijapata kuona majani ya namna
hii tangu nizaliwe! Yamefunika
kama miavuli!” Aliwaza.
Kwa kuwa alikua na njaa sana,
aliketi chini ya kivuli cha majani
yale mapana akawa anakula
mkate wake wa unga wa mchele
alioubakiza, na kunywa maji
aliyofungashiwa na mama yake.
Baada ya kupumzika kwa muda
wa kutosha, Hanga akamwacha
farasi wake mahali alipomfunga,
na yeye akaanza kutafiti lile eneo
ajuwe ni upande gani aelekee
katika safari yake.
Alipoangalia kwenye jabali katika
upeo wa macho yake, yule kijana
akaona maporomoko ya maji
yaliyokua yakitokea mwambani
na kuanguka chini kwa kishindo
kikubwa, yakishindana na
michuruziko ya maji yaliyokuwa
yakitiririka chini kutoka kulekule
mwambani. Alitulia kidogo
akizidi kustaajabu aina ya msitu
ule wa kipekee, na vyote
vilivyohusika ndani yake!.Ghafla
wakati akitafakari kuhusu yote
aliyoyaona na jinsi
atakavyoendelea na safari yake,
akasikia mwaliko wa mawe
yakigongana gongana, yaliyotoa
mlio kama mtambo wa aina
fulani na sekunde chache baadae,
akasikia vishindo vya milipuko
kama mabomu, na alipoinua
kichwa chake kuangalia angani
kuona kilichokua kikitokea,
akaona moshi mnene na mweusi
sana umezagaa! Muda si mrefu
kijana yule akiwa na hofu kubwa,
aliona cheche za moto
zilizofuatiwa na mwanga mkali
wa moto juu kabisa ya anga!
Haraka sana Hanga aliruka na
kukimbilia sehemu alikohisi
kuwa kuna usalama, mbali na
eneo lile hatari, kwenye jabali
moja lililonekana katika upeo wa
macho yake! Alijaribu kukimbilia
nyuma ya mmoja kati ya milima
iliyo uzingira uwanda mrefu,
akivuka vijito, mawe na visiki
vya miti pamoja na miti mirefu
mno iliyoufanya ule msitu uwe
gizani. Miti katika ule msitu
ilijipanga katika safu mbili,
katikati ikiacha njia nyembamba
ambayo juu yake ilikutana na
kuonekana kama paa la nyumba.
Pembezoni mwa ile miti kwa
kiasi cha kama kilometa mia
mbili, ndiko yalikokuwepo yale
majabali marefu mno,
yaliyouzingira ule uwanda wa
‘Paa la Dunia’ alioutaja kibibi
Ajuza “Huu ndio ‘Msitu wa
Kindumbwe’ au ‘Msitu wa Hatari’
nilioambiwa na Ajuza!” aliwaza
Hanga, akishindwa kuzuia
kitetemeshi kwenye miguu yake
iliyokuwa inapoteza nguvu kwa
woga na wasiwasi aliokuwa nao!
Alipokuwa akikimbia kwa hofu
na wahaka, mguu wake mmoja
ulikamatwa na mizizi ya miti,
kwa hiyo akarushwa mbele zaidi,
na huko akajikwaa vibaya sana
katika kisiki. Puuuuuuh! Alipiga
mweleka wa nguvu na kufikia
kwenye mawe makali kama
wembe yaliyomchubua chubua
na kumpa machungu makali
mno! Kabla hajatulia kujisikilizia
machungu aliyoyapata, jambo
jingine la kushitusha na kumtia
hofu likatokea! Mahali
alipoangukia Hanga akasikia sauti
ya mtu! Mwili mzima ukazizima
kwa woga! “Hivi ni mwana wa
nani wewe unaenikwaa mimi
kizee cha Mungu? Nimekufanya
nini masikini?” Kwa mastaajabu
na hofu ya kusikia sauti ya
mwanadamu asiyeonekana,
Hanga alijizowazowa na kuruka
hatua moja ya kama mita mbili
nzima, akisahau kabisa
kuyasikilizia machungu
aliyoyapata muda mfupi uliopita,
akiangukia mwenye dimbwi la
maji lililokuwa mbele yake!
Alipogeuka kila upande kuangalia
ni mtu gani aliyemsemesha
maneno yale bila mafanikio, hofu
yake alizidi, akabaki akitetemeka
na miguu yake ikizidi
kunyong’onyea! Wakati ule
akakumbuka jinsi alivyomuudhi
‘Ajuza’ nyumbani kwao Hazina,
hivyo akaamua kumuomba radhi
mtu mwenye sauti ile iliyosikika
kama ya mzee wa kike.
“Nisamehe sana bibi yangu kwa
kukukosea. Kwa bahati mbaya
sikufahamu kama nilipojikwaa
nilikukwaa na wewe! Nisamehe
sana bibi!”
Baada ya kumtaka radhi yule bibi
ambaey wakati ule hakujua ni
wapi alikokuwa, alinyamaza
kimya kusikiliza kama bibi yule
angejibu kitu. Pale alipokuwa,
Hanga alizidi kupata wahaka kwa
ukimya uliotawala msitu ule,
baada ya ile milipuko ya awali
iliyotokea kwenye majabali saa
moja hivi iliyopita. Ni milio ya
sauti za ndege tu iliyosikika!
Wengine walilia “whu-whu-
whuuuu! Whu-whu- whuuuu!”
na wengine walilia “Tuu-tuuu
tutututuuu! tuu-tuuu-
tutututuuuu!” Mlio huu wa pili
aliusikia kama vile wimbo wenye
maneno aliyoyaelewa; ambayo ni
“Kuukuuu mifupa mitupuuu!
Kuukuuu mifupa mitupuuu!”
Lakini wala haikuwa hivyo, ila
alikwishaanza kubabaika na
kuchanganyikiwa kichwani.
Halafu ghafla katika ukimya ule,
akaisikia tena ile sauti ya kizee.“
“Nimekusamehe mjukuu wangu
na usihangaike kutafuta niliko
kwani ukifunua hiki kisiki
kilichokukwaa, utaona njia
inayoshuka chini ya ardhi. Ingia
na uje tuonane uso kwa uso
mjukuu wangu!” Lo! Hanga alitoa
macho kama nyanya chungu!
Aingie aridhini? Akaonane na
nani? Je kama huyo atakaemkuta
huko atakuwa si mwanaadamu?
Ingawa aliogopa sana kufuata
maelekezo ya ile sauti, Hanga
hakuwa na rai bali kufunua kile
kisiki huku mikono ikitetemeka
na moyo wake ukienda kasi mno!
Alikivuta kisiki kile kwa nguvu
zote na kisha hamadi!
Kilipofunuka tu, aliona ngazi
zikishuka chini kwenda sehemu
iliyokuwa na giza nene kupita
kiasi!. Alijishauri sana kwa kiasi
cha dakika mbili au tatu hivi, ‘je
ateremke na aende sehemu ile ya
kutisha?’ Alisita sana kufanya
vile. “Usihofu mjukuu wangu
njoo tu, kwani huenda majibu
mengi ya maswali yako
yakajibiwa huku.” Kwa sauti ile
yenye mikwaruzo, Hanga alihisi
kuwa bila shaka bibi yule
alikuwa ni kizee cha miaka mingi
sana. Pamoja na wasiwasi
aliokuwanao, Hanga aliamua
kuteremka zile ngazi za mawe
kuelekea kule kwenye giza la
kutisha, kwani ni kweli alitaka
sana kupata majibu ya maswali
mengi aliyokuwa nayo.
Kadiri Hanga alivyoshuka chini
zaidi ya zile ngazi, ndivyo giza
lilivyozidi kutanda. Alishuka
taratibu sana na kwa uangalifu
mkubwa, hatimae akafika
mwisho wa ngazi. Kule akaisikia
tena sauti ya yule bibi ikitokea
gizani,“Haya mjukuu wangu,
hebu keti kwenye kigoda
uniambie ulichokifuata katika
msitu huu wa kindumbwe,
unaodhibitiwa na viumbe waovu
wenye uhasama mkubwa na
wanadamu.” Hanga akapapasa
mahali palipokuwa na kigoda
akaketi, wakati macho yake
yakianza kulizowea giza lile nene
la kule chini. Mbele yake aliona
sehemu iliyokuwa na njia nyingi
kama vichochoro, au njia
zilizoelekea mapangoni.
“Nakwenda kwenye uwanda wa
‘Paa la Dunia’ kutafuta majibu
kuhusu athari zinazoikabili sayari
yetu. Je bibi nitafikaje sehemu
hiyo?” Yule kizee alimwangalia
Hanga akitathmini kiwango cha
ushujaa wake, akijua kuwa
masikini kijana yule hakufahamu
uzito wa jambo alilotaka
kulifanya. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mjukuu wangu wee! Kabla ya
yote kwanza lazima uelewe kuwa
mnamo miaka mia moja iliyopita,
nchi hii ya ‘Bam i Dunya’ ilikuwa
ni nchi ya amani sana,
iliyotawaliwa na Sultan Dhaman,
ambaye kama jina lake
linavyoashiria, alikuwa ni
mwajibikaji katika majukumu
kadhaa ya maendeleo ya nchi
yake na raia wake. Lakini
kutokana na hazina kubwa ya
vito vya thamani vilivyopatikana
katika mito, milima na
makorongo ya uwanda wa Paa la
Dunia, nchi hii ilihusudiwa na
viumbe waovu waliotoka sayari
nyingine, ambao baada ya kuifilisi
wakaamua kuiteketeza kwa moto
na kuwaathiri raia wake wote!”
Hanga aliutafakari muda wa
miaka mia moja iliyopita,
akamwangalia kwa makini yule
kizee aliyekuwa na umri wa zaidi
ya miaka hiyo iliyotajwa. “Lo!
Ndio maana ngozi yake
inaning’inia shingoni kwake na
mikono yake imekuwa mifupa
mitupu!” Aliwaza Hanga,
akimuona bibi yule kama kiunzi
cha mifupa tu! Kama kwamba
yule kizee alifahamu mawazo
yaliyopita kichwani mwa Hanga,
akasema; “Ndio mjukuu wangu,
nimekuwa humu pangoni kwa
miaka mingi sana! Nilipoona
kuwa nimepoteza ndugu na
jamaa zangu wote nikaamua
kujificha chini ya kisiki, ambacho
sikujua kama kiliyafunika
mapango mengi ndani yake,
yenye njia za kutokea kila upande
wa nchi yetu ya Bam i Dunya!”
Hanga hakuweza kukisia maisha
yalivyokuwa chini kabisa ya ardhi
kwa miaka mingi kama ile!
Aliwaza kuhusu wale viumbe
waovu waliotoka sayari nyingine
na kwenda kuvuruga amani
nchini kwa wenzao, eti kwa ajili
ya tamaa ya utajiri wao,
wakisababisha watu kama yule
bibi kuishi aridhini kama panya.
“Ni viumbe wa aina gani hasa
bibi, waliokuja kuiteketeza nchi
yenu?” Alidodosa Hanga,
akaambiwa kuwa ni viumbe
wasiokuwa wa kawaida wenye
maumbile ya ajabu sana, kwani
katika maumbile yao, kuanzia
tumboni hadi kichwani wako
kama joka kubwa sana, na
kuanzia tumboni kushuka
miguuni wako kama binaadamu
lakini wana mikia mirefu sana!
“Wengi wao ni waovu mno
ingawa miongoni mwao wamo
wachache waliokuwa wema
sana.” Kwa maelezo yale Hanga
alipata wasiwasi mkubwa. “Kama
miongoni mwa viumbe hao
wamo waliokua wema, je, wale
waovu wakijitokeza na kujifanya
kuwa ni wema, nitawatambua
vipi?” Alimuuliza yule kizee,
aliyemjibu kuwa atawatambua
waovu kutokana na lugha yao
wanayoongea isiyoeleweka na
mwanadamu yeyote.
“Mwanadamu pekee anayeelewa
lugha hiyo ni Mwana Mteule,
mwenye uwezo na vipaji vingi
vya kipekee!” Kizee yule alisema
Hanga alishituka kusikia habari
ya Mwana Mteule ambaye kwa
mara ya kwanza aliisikia kutoka
kwa bibi ‘Ajuza’ nchini kwao
Hazina. Hakufahamu jinsi ya
kumpata kijana huyo wa ajabu.
Alihisi kuwa yule bibi angeweza
kumsaidia kwa jambo lile.
“Nilipata msaada mkubwa kutoka
kwa viumbe wema miongoni
mwa viumbe waovu
ninaowasema,” bibi kizee
aliendelea kuelezea sifa za wale
viumbe wema, akipuuzia
mshangao wa Hanga mara baada
ya kutajwa Mwana Mteule.
“Viumbe wale wema ndio
walionileta humu pangoni
wakaninusuru na madhara
makubwa ya wenzao waovu.”
Kizee yule aliendelea na maelezo
yake, akimfahamisha Hanga kuwa
ni wale viumbe wema kati yao,
waliomwambia kuwa wenzao
waovu wameazimia kuzusha
janga kubwa katika sayari yao ili
isikalike, na kuwapa fundisho
wanadamu wanaojiona kuwa ni
bora kuliko wao!
Kizee yule aliendelea na maelezo
yake, akimfahamisha Hanga kuwa
ni wale viumbe wema kati yao,
waliomwambia kuwa wenzao
waovu wameazimia kuzusha
janga kubwa katika sayari yao ili
isikalike, na kuwapa fundisho
wanadamu wanaojiona kuwa ni
bora kuliko wao!
Pamoja na kupata hofu kubwa
kuhusu hali ilivyo katika msitu
wa kindumbwe, Hanga alitaka
kujua jinsi atakavyofika kwenye
pango la sanamu la kichwa cha
Simba, kama alivyoelekezwa na
‘Ajuza’. Kabla hajapewa jibu,
lilizuka kundi la bundi wengi
kupita kiasi waliotoka mwenye
vichochoro ambavyo ni njia za
kwenda katika mapango mengi
ya mle aridhini. Hanga alishtuka
na moyo wake ukawa kama
umesimama kwa nusu sekunde.
kwa woga. “Mama wee!” Hanga
alipiga ukulele, akajiangusha
chini kuwakwepa wale bundi
wasimkwaruze usoni! “Hao
mjukuu wangu, ndio wapelelezi
wa pepo mbaya wa ulimwengu
wa kale, naye ni mfalme mkuu
wa vidani vitatu katika sanamu la
shaba la kichwa cha Simba,
kilichokuwa na kile kidani
chenye ujumbe wa madhara
yanayoikabili sayari hii, na
ambacho ndicho unachokitafuta!
Pepo huyo mbaya wa ulimwengu
wa kale ambaye ni jamii ya
‘wanamoto’, hapendelei ujumbe
ule ujulikane na mtu yeyote
atakayebatilisha azma ya uovu
waliokusudiwa wanadamu,
ambao ni Wanahewa!” Hanga
aliduwaa tu, akabaki kinywa wazi
akitafakari. “Nikikifuata kidani
chenye huo ujumbe, nitakuwa
nimejitosa kwenye vita na pepo
huyo mbaya wa ulimwengu wa
kale!” aliwaza.
Wakati ule Hanga alipata hamu
ya kurudi kwa baba yake na
mama yake haraka
iwezekanavyo, kabla
hajapambana na viumbe wale wa
ulimwengu wa giza! Alipowaza
hivyo, akamsikia yule kizee
akisema; ”Kwa kuwa umefika
mpaka hapa, huna budi
kuendelea na safari yako, kwani
Mwana Mteule atahitaji sana
msaada wako!” Ni kama vile bibi
yule kwa mara nyingine alimsikia
Hanga alivyowaza moyoni
mwake! Kijana yule alimwangalia
bibi kizee kwa macho ya woga
mno! “Hivi huyu ni
mwanaadamu kama mimi au….!”
Hakuendelea na mawazo yake,
kwani alihofu kuwa yule bibi
alikuwa anayajuwa yote
aliyoyawaza! Alipoinua kichwa
kumwangalia, yule kizee naye
akamwangalia akiwa na
tabasamu kubwa usoni! Hanga
aliogopa mno!
SURA YA NANE
Kibwe Nchini Baharia
Akitokea kwa Mzee wa Busara;
Mzee Kaka, Kibwe alisafiri kwa
mtumbwi wake kwa masafa
marefu sana. Njiani alikuwa
akitafakari yote aliyoambiwa na
mzee yule. Aliambiwa kuwa
ingawa safari yake kule
Azarbajan kaskazini mashariki ya
mbali ya dunia itakuwa ngumu
sana, lakini ni wajibu kwake
kujitahidi kadiri ya uwezo wake
kufika kule ambapo msaada wake
unahitajika sana. “Maisha ya
watu wa huko yamo hatarini
kutokana na kuwepo kwa hewa
hatari mno, yenye uwezo wa
kuwakausha na kuwagandisha
watu au hata kuzifanya ngozi zao
zibambuke bambuke. Hewa hiyo
inayoweza kuwagandisha watu
na kuwageuza theluji ngumu
isiyoyeyuka, huhatarisha maisha
ya viumbe wote waishio
Azarbajan.” Kibwe aliambiwa
maneno hayo na Kakakuona
wakati walipokuwa kwenye
bonde la rutuba. Wakati huo,
kijana yule hakuelewa jinsi
atakavyotatua hilo tatizo la hewa
ile ya hatari!
“Sasa, nikifika huko nitafanya
nini kuliondoa tatizo hilo, ambalo
lipo hewani tu na wala haliko
mahali litakapodhibitiwa na
binadamu?” Kibwe alidadisi “Na
je, kwanini hewa hiyo
imekuwepo mahali hapo pekee
katika dunia nzima?” Maswali
hayo yalitupiwa kwa Mzee wa
Busara bila kituo!
“Kibweee! Kibweee mjukuu
wangu! Hebu niulize swali
mojamoja basi!” Mzee wa busara
alimwambia kijana yule, huku
akitabasamu kuona jinsi
alivyokuwa na hamu ya
kufahamu mambo mengi kwa
wakati mmoja. Kisha mzee yule
akafafanua kwa kusema. “Kuhusu
la kufanya ili kuliondoa tatizo
hilo la hewa hatari, ni kwamba
lazima uende nchini Baharia,
chini kabisa ya bahari
ukapambane na jini aitwae
‘Makatta wa Makattani’ na kundi
lake, wanaofanya uharibifu wa
kuchafua hewa iliyoko kwenye
anga hewa ya chini, katika tabaka
la hewa nzuri ya Ozoni, kwani
kitendo hicho husababisha
tabaka la hewa hiyo muhimu kwa
wanadamu, kupungua kwenye
maeneo ya makazi yao!” Lakini
hata baada ya ufafanuzi ule,
Kibwe bado alikuwa gizani, na
hakuelewa chochote kuhusu
chanzo cha tatizo lenyewe
alilolizungumzia Mzee wa Busara.
“Kwanza, sielewi uhusiano uliopo
kati ya watu kugeuzwa mawe ya
theluji, kuchafuliwa kwa hewa na
kupungua kwa tabaka la hewa
…..hewa gani….? Hewa ya
Ozo….?” Kibwe alidadisi.
Alishindwa kukumbuka jina la ile
hewa iliyotajwa na Mzee wa
Busara. “Hewa ya Ozoni Kibwe!
Inaelekea wewe si mpenzi wa
sayansi kabisa!” Mzee wa Busara
alimwambia kwa dhihaka kijana
yule mteule.
Kwa hiyo akimfafanulia Kibwe
kuhusu uhusiano wa matukio
yale yaliyomchanganya, mzee
yule mwenye busara alimweleza
kuwa baadhi ya wana sayansi
waligundua kuwa tabaka la hewa
ya Ozoni katika sehemu zenye
baridi kali za kaskazini ya mbali
ya dunia, hupungua mno mwaka
hadi mwaka, na hivyo
kusababisha uwazi au tundu
kwenye tabaka hilo la Ozoni.
Kitendo hicho, alisema,
kilisababisha hali ya hewa kuwa
ya baridi kali mno katika maeneo
hayo, na kuifanya hewa hiyo
kuzizima na wakati fulani kuwa
nzito kupita kiasi. Mzee yule
alisema kuwa hewa hiyo
inapoelea na kusafiri kwenda
kwenye makazi ya watu,
husababisha giza nene na la
kutisha, na inapofikia hatua hiyo,
hewa hiyo hatari kwa viumbe
huwa na uwezo mkubwa wa
kuwagandisha viumbe hao na
kuwageuza kuwa mawe ya theluji
isiyoyeyuka, mara
watakapopambana nayo!
Ingawa Kibwe alijaribu kuelewa
maelezo yale, lakini ilikuwa
vigumu sana kuupata ukweli huo
vilivyo, kwani kwanza kabisa,
hakuwa hata na fununu kuhusu
hewa hiyo ya Ozoni, kwa hiyo
haikuwa rahisi kuelewa kuwa eti
hewa ile asiyoijua inapochafuliwa
kwa namna fulani, matukio yale
yaliyotajwa hutokea. “Sasa mzee
‘Kaka’ ndio kusema hewa ya
Ozoni ni hewa gani? Mbona mimi
hufahamu kuwa hewa safi na
nzuri kwa binadamu ni hewa ya
Oksijeni?” Kijana kibwe
alidodosa, akimkosoa Mzee wa
Busara kuhusu hoja ya eti hewa
ya Ozoni ni hewa safi
inayotumiwa na wanaadamu,
akimtaja Kakakuona kwa
ufupisho wa jina lake, yaani
mzee’ Kaka, alipoona kuwa
wameanza kuzoweana “Ahaa!
Kumbe nawe wafahamu kidogo
mambo ya sayansi! Ni vizuri
sana! Sasa basi kwa kuwa tayari
unaelewa kuhusu hewa ya
Oksijeni, lazima pia uelewe kuwa
huko kwenye angahewa, liko
tabaka jingine ambalo ni la hewa
ya Ozoni, na hiyo ni aina fulani
ya hewa ya Oksijeni, iliopo kwa
kiasi kidogo sana, na ambayo
nayo huwawezesha viumbe
kuishi katika dunia hii!”
Kibwe alipotaka kufahamu kwa
nini Mzee wa Busara alisema
kuwa ufumbuzi wa tatizo la hewa
hatari kwa viumbe utapatikana
baada ya kupambana na jini
Makatta na wenzake, aliambiwa
kuwa jinni lile na wenzake ndio
wanaoweka vichafuzi vya hewa
kwenye anga hewa ya chini. Mzee
huyo wa busara alisema kuwa
vichafuzi hivyo vya hewa
vilivyomo ndani ya hewa ya
Ozoni huko kwenye anga hewa ya
chini, vinapopambana na mionzi
ya jua, mapambano hayo ya
kikemikali husababisha
mabadiliko kwenye hewa ya
Ozoni, na hivyo kuipa uwezo
mkubwa wa kuichafua hewa safi.
“Na wakati huohuo vichafuzi
hivyo huko kwenye anga hewa ya
chini vinapopambana na hiyo
mionzi ya jua, sehemu ya hewa ya
Oksijeni hugeuka na kuwa hewa
ya Ozoni ambayo hupatikana
kwenye anga hewa ya juu.” Mzee
wa busara aliendelea na maelezo
yake kwa Kibwe, akitofautisha
baina ya hewa ya Ozoni iliyopo
kwenye anga hewa ya juu,
ambayo ni safi, na hewa ileile ya
Ozoni iliyopo katika anga hewa
ya chini, ambayo hugeuzwa kuwa
hatarishi, akiongezea kwa
kusema, “Kumbuka kuwa
inapochafuliwa hewa ya Ozoni
iliyoko kwenye anga hewa ya
chini, huchangia mno katika
uchafuzi wa ile hewa
safi.” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe aliambiwa kuwa mara tu
baada ya kumshinda jini Makatta
na wenzake, na kuwazuia
wasiweke vichafuzi vya hewa
kwenye anga hewa ya chini,
atafanikiwa kuzuia mzizimo wa
hewa nzito na hatarishi, na hivyo
kuokoa maisha ya viumbe na
mimea! “Lo! Haya mambo ya
sayansi nayo, yanakwenda kwa
mzunguko hadi kumfikisha mtu
mahali pa kumchanganya kabisa
ki mawazo!” Kibwe alimwambia
Mzee wa Busara wakati ule,
kwani kufikia pale, tayari
alikwisha vurugikiwa kiwango
chake cha uelewa!
Lakini masikini, Kibwe
hakufahamu kwamba miaka mia
moja iliyopita alipozaliwa Mwana
Mteule wa awali nchini Sabaa
Kaskazini Mashariki ya mbali ya
dunia, ilipowadia siku ambayo
raia wa Sabaa, ‘Wanahewa’
waliandaa hafla maalum ya
kumkabidhi kijana wao mteule
kwa mwalimu wake ambaye
angempa maelekezo ya kutumia
vipaji vyake kwa nusura ya
viumbe kwenye sayari yao, ghafla
jamii ya falme za majini wa
bahari, chini ya uongozi wa
Mfalme wao Makatta wa
Makattani, waliivamia nchi ya
Sabaa na kuiteketeza kwa moto
waliopumua kutoka vinywani
mwao! Majini wale hawakusaza
chochote katika utajiri wa nchi ya
Sabaa, ikiwa ni pamoja na
kumteketeza Mwana yule Mteule
aliyetarajiwa kuipa matumaini
jamii katika sayari yao!
Kibwe hakufahamu kuhusu
mambo yote hayo, na wala
hakufahamishwa sababu kubwa
iliyowaponza raia wa Sabaa
waliofanyiwa unyonge ule,
ambayo ni neema na mafanikio
ya nchi yao pamoja na vipaji
vyao aliali vya kipekee
walivyojaaliwa, kwa faida ya
viumbe wote. Wala kijana yule
hakuwa na fununu kuhusu
azimio la mfalme wa majini dhidi
ya jamii yake! “Na kuanzia sasa,
asinusurike Mwanahewa yeyote
katika sayari hii! Lazima wote
wateketezwe popote
watakapokuwa, na kuwaondolea
amani katika maeneo yao!”
Mfalme Makatta aliwaambia raia
wake nchini Baharia, mara baada
ya kuiteketeza Sabaa. Vilevile,
Kibwe hakufahamu kuwa miaka
mia moja baada ya janga lile la
majini waovu wa nchi ya Baharia,
ndipo yeye alipozaliwa,
akitarajiwa kushika nafasi ya
mwenzake aliyeteketezwa! Kwa
hiyo alipopewa maelezo yale na
Mzee wa Busara kuhusu jukumu
lake zito alilotarajiwa
kulitekeleza, hakufahamu kuwa
zaidi ya kuelewa aliyoambiwa,
pia alikuwa na vipaji vya kipekee
vya kumsaidia kufanikisha yote
aliyotarajiwa kuyafanya!
Akiazimia kufuatilia jukumu lile
la mapambano na viumbe
wachafuzi wa hewa safi kwa
makusudi na walio hatarisha
maisha ya watu, Kibwe aliendelea
na safari yake kwa njia ya bahari,
akielekea kaskazini ya mbali ya
dunia. Alikuwa imara kabisa
katika safari ile ndefu na ngumu,
mara baada ya kuelewa barabara
tatizo lililokuwa likiwakabili raia
wa Azarbajan kwa Mfalme
Kashkash. Kwa hiyo alijiandaa
kulikomesha kabisa tatizo lile!
Katika maelekezo yake, Mzee wa
Busara alimwambia Kibwe kuwa
jini Makatta wa Makattani na
wenzake, huishi kwenye mji
ulioko chini kabisa ya bahari.
Alikumbuka maelezo yake,
wakati akimwambia, “Huko
nchini Baharia , chini kabisa ya
bahari, utakuta milima mikubwa
kabisa na mirefu, minne kati yake
ni myeusi kabisa. Yapo pia
mabonde na ardhi tambarare,
pamoja na makorongo
yatokanayo na mito mikubwa
inayoingiza maji baharini. Makazi
ya jini Makatta na wenzake ni
kwenye makasri ya thamani
katika baadhi ya milima hiyo iliyo
tambarare, na kwenye mabonde
na makorongo hayo.”
Kibwe alikumbuka maneno ya
Mzee wa Busara kuwa majini hao
hufanya kazi ya kuzalisha
vichafuzi vya hewa, wakitumia
mitungi mikubwa na masufuria
makubwa sana ya shaba,
kuchemshia madawa yao
yanayotoa vichafuzi hivyo kwa
njia ya moshi mchafu kupitia
mabomba makubwa!
“Wanaoutoa moshi huo nje ya
bahari ni majini wa upepo,
ambao huuvumisha upepo kwa
kuupulizia nje ya bahari,
wakiutumia kwa kuyazungusha
maji ya bahari , na kusababisha
kutokea mawimbi yanayokwenda
sanjari na bahari hiyo.” Kibwe
alitafakari maelezo hayo ya Mzee
Kaka, aliyeongezea maelezo yake
kwa kusema kuwa wakati fulani
yale mawimbi huinuliwa kwa
urefu wa takriban mita mia mbili
au zaidi, na hivyo hatimae
kuweza kuusindikiza moshi huo
kwenye angahewa ya chini, kwa
kupitia kwenye mabomba
maalum yaliyoko juu kabisa
kwenye minara pacha mitatu,
katika uwanda wa ‘Paa la Dunia!’
“Baada ya hapo, Majini hao wa
upepo huupuliza tena upepo ule
unaosukuma maji mithili ya
mawimbi, na kuyarudisha
mawimbi hayo chini kabisa ya
bahari, ili kukusanya tena ile
hewa ya vichafuzi inayozalishwa
na majini wa chini ya bahari, na
kisha kuipandisha tena juu ya
bahari kwa njia ya mawimbi
hayo, ili kuendelea na zoezi la
kuifikisha hewa hiyo ya vichafuzi
huko kwenye anga hewa ya
chini.” Mzee wa Busara
alimfafanulia Kibwe, akimsisitizia
kutumia upanga wake wa radi
kutatua matatizo mengine mengi
yatakayojitokeza bila kutarajia .
Kibwe alizidi kutafakari maelezo
ya awali ya Mzee wa Busara,
‘kwamba mapambano ya
kikemikali baina ya mionzi ya jua,
husababisha kupatikana kwa
kiasi kidogo cha hewa nzuri ya
Ozoni kwenye anga hewa ya juu
ya dunia, na kupatikana kwa
hewa chafu na hatarishi kwenye
anga hewa ya chini’. Kibwe
alimaizi kuwa kwa hakika majini
wale walikuwa ni waovu mno
kiasi cha kudiriki kuyafanya yote
hayo, ili mradi tu, kuhatarisha
maisha ya watu!
“Ama kweli, hasidi hana sababu!”
Aliwaza Kibwe huku akiendelea
kusukuma makasia ya ngalawa
yake kwa nguvu zote, wakati
akikumbuka moja katika methali
za mama yake alizopenda
kuzitumia.
Kijana yule aliendelea na safari
yake hadi alipoatokea kwenye
kisiwa chenye msitu mnene sana
wenye miti mirefu iliyokuwa na
matawi marefu mno,
yaliyoning’inia mithili ya mizizi
minene, na mashina yake nayo
yalishikiliwa na mizizi yenye
unene kama yale matawi ya
kipekee, iliyojitokeza nje ya
aridhi, na kufungana kama
utanda wa buibui! Miti mingine
iliyokuwepo katika msitu ule wa
ajabu ilikuwa na majani mapana
kama masikio ya tembo, na
mingine ilikuwa na majani ya
rangirangi yaliyofanana na
myavuli kwa ukubwa na
maumbile. Kibwe aliufunga
mtumbwi wake kwenye kisiki, ,
akaanza kutembea kwa miguu,
ingawa alipata shida sana
kutokana na matawi na mizizi
katika msitu ule kujifunga juu na
chini yake kama utando wa
buibui! Kijana yule alilazimika
kupenya kama panya, akitumia
upanga wake kuikatakata ile
mizizi ili kurahisisha safari yake
iliyokuwa ya utata. Msitu wote
ulikuwa kimya, isipokuwa kwa
sauti za ndege wa aina
mbalimbali, ambao baadhi yao
walisikika kama vile walitamka
maneno aliyoyaelewa Kibwe
“Kuukuuu mifupa mituupuuu!
Kuukuuu mifupa mituupuuu!”
Kibwe alishangaa sana!
“Kama videge vinaona kuku ni
mifupa mitupu, venyewe ndio
vina nyama?” Alijiuliza, huku
akitabasamu.
Kibwe hakufahamu kuwa katika
msitu ule alikuwepo kijana
mwenzake Hanga, ambaye kama
yeye, naye alisikia sauti za ndege
walioimba kwa kusema maneno
aliyoyasikia yeye, yaani, “kuku
mifupa mitupu!”. Kwa sababu
hiyo, huenda Kibwe na Hanga
wote walikuwa katika ‘Msitu wa
Kindumbwe’ bila kuelewa! Kibwe
pia alisikia milio ya wadudu
kama Nyenze, mvumo wa bahari
na upepo uliosikika ukivuma kwa
mbali kidogo “Ili kufika nchini
Baharia, chini kabisa ya bahari,
kwanza utavuka kisiwa chenye
msitu wa miti ya mizizi” Mzee
Kaka alimwambia Kibwe wakati
akijiandaa na safari ile,
isipokuwa hakumtajia jina la
msitu wenyewe,.isipokuwa
mwenzake Hanga aliambiwa na
kizee aridhini kuwa ni ‘Msitu wa
Kindumbwe!
Alitembea kutwa nzima hadi
alipotokea kwenye bonde
lililozungukwa kila upande na
majabali marefu mno.
Alipoangalia huku na kule kuona
jinsi atakavyoendelea na safari
yake, hakuona mahali pa
kutokea! Alihofu sana alipojikuta
katika ngome ya majabali kama
gereza! Kwakuwa miti ya msitu
ule ilikuwa na mizizi
iliyoning’inia mithili ya kamba
nene imara, Kibwe aliamua
kujishikiza kwenye mizizi,
ambayo kwa bahati ilibebelea
malundo ya udongo wa mfinyanzi
ulioganda madhubuti, alioutumia
kama vikanyagio au ngazi.
Alining’inia kwenye mzizi kama
aliyetaka kubembea, halafu
akainua miguu yake juu kichwa
chake kikiwa chini, akiitumia
miguu yake kulibana lundo moja
la udongo lililokuwa juu yake, na
kisha moja baada ya jingine
aliyatumia malundo yale kwa
kupanda juu zaidi ya miti,
akilenga kufika katika kilele cha
moja ya majabali. Taratibu na
kwa makini, alipanda kwa mbinu
ile ya kushikilia matawi ya mizizi.
Mara kwa mara alipapasa
kiunoni kuona kama ule upanga
wake muhimu katika safari yake
bado alikuwa nao. Kwa hekima
kubwa na nguvu zake zote Kibwe
aliendelea kupanda juu kabisa ya
jabali lenye urefu usiokadiriwa!
Alipofika kileleni alianza kushuka
kwa upande wa pili wa jabali lile,
akitarajia kushukia korongoni
upande ilikokuwa bahari, ili
aweze kufika chini kabisa ya kina
cha bahari, kama alivyoelekezwa
na Mzee Kaka.
“Utakapokuta mwanguko au
mteremko wa ardhi, ufuate na
ushuke nao hadi ufike chini
kabisa ya bahari.” Kakakuona
alimwambia Kibwe walipokuwa
katika bonde la rutuba. Kabla
hajaanza kushuka chini ya lile
jabali, alishtuka kusikia sauti za
watu wengi kwa pamoja,
wakiongea na kukubaliana
kuhusu jambo ambalo Kibwe
alihisi lilikuwa la maana sana
kwao. Haraka alijibanza nyuma
ya lundo la udongo katika tawi
kama mzizi alilolishikilia,
akijiandaa kushuka. Alisita
kidogo na taratibu akachungulia
kule kulikotokea zile sauti! Lo!
Alipowaona waliohusika Kibwe
alipata hofu kupita kiasi….! Moyo
wake ulichupa, miguu yake
ikapooza na kinywa chake
kikawa wazi kwa mshangao!
Aliowaona kwa hakika hawakuwa
binadamu wa kawaida, bali
walikuwa ni viumbe ambao
kuanzia kifuani hadi kichwani
walikuwa na maumbile ya nyoka,
na kuanzia tumboni kushuka
chini walikuwa na maumbile ya
binadamu lakini wakiwa na
mikia mirefu mno! Hakufahamu
kuwa katika msitu uleule, kijana
mwenzake ‘Hanga’ naye
angeshuhudia maajabu yale siku
chache baada yake! CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe aliogopa sana wakati
viumbe wale wa ajabu
walipogeuza sura zao upande
aliojificha! Hakuamini macho
yake alipowaangalia vema
viumbe wale na kuona kuwa
macho yao yalikuwa pembezoni
mwa sura zao, na walipojifuta
jasho kijana yule alishangaa zaidi
alipoona mikono yao imefanana
na mikono ya vyura! Alipata
hofu, wahaka na taharuki kubwa!
“Ni jambo la kutisha na
kushangaza mno!.” Aliwaza
Kibwe, misuli ya mwili mzima
ikitetemeka! Alipozidi
kuwachunguza zaidi viumbe
wale, aliona kuwa walikuwa na
midomo mithili ya midomo ya
vyura! Aaa--hapana! Labda
tuseme sura zao zilikuwa ni za
vyura kabisa, kuanzia kwenye
vipaji vya nyuso zao hadi
kushuka kwenye shingo zao!
Kuanzia shingoni kwenda kifuani
walikuwa na umbo la nyoka, na
kushuka miguuni walikuwa ni
binadamu wembamba mno,
wenye mikia mirefu sana!
“Sijapata kuona viumbe wa aina
hii katika muda wote nilioishi
hadi leo, na wala sijasikia habari
zao zikizungumzwa na yeyote!”
Aliwaza kijana yule, akiwa
amezidiwa na hofu na mshangao
mkubwa! “Bila shaka hawa ndio
majini nilioambiwa na Mzee
Kaka” Alitafakari, na wakati
uleule alipata jibu lake, kwani
viumbe wale walikuwa
wakipumua mienge ya moto!
Alipohakikisha hilo ingawa
alikuwa na hofu kubwa, Kibwe
aliazimia kuwafuata viumbe wale
popote walikokuwa wakienda,
kwani aliamini kabisa kwamba
wangemfikisha kwenye maabara
yao ya maandalizi ya hewa ya
uchafuzi wa angahewa. Kwa
wakati ule alitulia tuli ili
kunusuru maisha yake, huku
akiyapelemba yale majitu au
wale viumbe, kwa mbali!
Viumbe wale walipokaribia
mahali alipokuwa Kibwe juu
kabisa ya jabali, na wao wakiwa
chini bondeni, yalisikika maneno
yasiyoeleweka kabisa na
binadamu yeyote! Kibwe alizidi
kujibanza nyuma ya lundo la
udongo uliogandana na matawi
ya mizizi, juu ya jabali. Chini ya
majabali yale majinni yalisimama
kwa mduara mpana, na kisha
mmoja wao aliyeonekana kuwa
kiongozi wa msafara na aliyevalia
taji la matumbawe ya rangirangi
za kuvutia, alianza
kuwanyamazisha wenzake
waliokuwa wakielezana mambo
yao kwa lugha yao, wakibishana
kwa ukali kabisa.
“Nimaja! Nimaja! Myaki tewo!
Myakitewo!” Mara moja zile
kelele na zogo lililokuwa
likisikika, vikaanza kupungua.
Wote waliponyamaza kimya,
ndipo kiongozi wao alipoanza
kuwaeleza kwa maneno yaleyale
yasiyoeleweka kwa Kibwe,
akiwasihi wahakikishe kuwa
wanatekeleza malengo yao
waliyoyaweka miaka mia moja
iliyopita. “Nguzangudu! Mazila
shelizatu shimo ngimwi aw
wadama okatao ndakwe kanifu
wahengaa…….” Kiongozi huyo wa
viumbe wale wa ajabu alisema
maneno hayo ya ajabu
yaliyokuwa na ujumbe mzito
ambao kwa wakati ule, Kibwe
hakuuelewa! Walimalizia hotuba
yao kwa kauli mbiu iliyoanzishwa
na kiongozi wao na kuitikiwa na
wengine wote kwa furaha.
“Fovi awk wahenawa!”
“Fovi awk wahenawa!”
Baada ya kusema hivyo, yale
majini yote kwa pamoja yalitoa
pumzi ya moto, wakaunguza
sehemu kubwa kabisa ya msitu!
Pale alipojificha huku
akitetemeka, Kibwe alitafakari
sana kuhusu maneno ya viumbe
wale, na kitendo walichokifanya
muda mfupi uliopita. “Sijui
walikua wakiambiana nini waovu
wale! Bila shaka walipoyasema
waliyoyasema, walikua
wakipanga mkakati wa uharibifu
wa mazingira kama huu
uliotokea.” Aliwaza kijana yule
bila kufahamu kuwa kule mbele
aendako ataipata maana nzima ya
yale maneno waliyoyasema wale
viumbe, ili kumrahisishia
utekelezaji mzuri wa malengo
yake!
Alipowaangalia viumbe wale
chini ya jabali na kuwaona
wakianza kuondoka na kuendelea
na safari yao, taratibu Kibwe
naye alianza kushuka kwa
kutumia moja katika yale matawi
mithili ya mizizi. Alipofika chini
katika upande wa pili wa jabali,
alisubiri kwa muda fulani ili yale
majini yafike mbali, halafu
akawafuata taratibu, akitarajia
kuwa walikuwa wakienda
kwenye maabara yao. Nia yake
ilikuwa ni kufika kwenye
maabara yao na kuzuia mchakato
wao mzima wa uzalishaji wa
moshi uletao madhara makubwa
duniani. Alipokuwa akiwafuata,
mara kwa mara walikuwa
wakigeuka nyuma kama kwamba
walihisi kuwa walikuwa
wakifuatwa na kitu au mtu.
Kibwe aliogopa sana, na alijificha
vichakani akihofu kuonekana na
kutiwa nguvuni na mazabania
yale. Baada ya mwendo wa saa
nzima katika msitu wa giza nene
uliojifunga kwa matawi na mizizi,
wakati majini wakienda kwa
hatua kubwakubwa kutokana na
urefu wao, na Kibwe naye
akiwafuata nyumanyuma, mara
akitembea na mara akikimbia,
walitokea katika ufukwe wa
bahari walikokuta mteremko wa
ardhi, ambako yale majini
yalishuka na kuanza kuzama
chini kabisa ya bahari Kibwe
alitulia tuli mahali alipojificha
katikati ya matawi na mizizi
mirefu akiwaangalia. “Bila shaka
hapa ndipo pale mahali Mzee wa
Busara aliponielekeza jinsi ya
kushuka baharini na kuingia
chini ya bahari, ili kufika nchi ya
majini ya Baharia.” Aliwaza
Kibwe, akitafakari mazungumzo
kati yake na mzee yule mwenye
busaranyingi.
“Utakapofika mwambao wa
ufukwe, utakuta mwanguko au
mteremko wa ardhi. Shuka kwa
njia ya mteremko huo hadi ufike
chini kabisa ya bahari.” Wakati
wa maagizo hayo ya Mzee wa
Busara, Kibwe alipata wasiwasi
kuhusu jinsi atakavyopumua
atakapokuwa huko chini ya
bahari. “Nitawezaje kuwepo
kwenye maji kwa muda mrefu
wa utekelezaji wa shughuli
yangu? Je,nitaweza kupumua
kama samaki?” Mzee wa busara
alimcheka Kibwe kwa kiwango
chake kidogo cha uelewa wa
mambo mengi ya dunia.
“Nimesema kuwa huko chini
kuna mji wa majini, kwa hiyo
wewe nenda tu, na utakuta mji
kama miji mingine uijuwayo.
Hakuna maji huko!”
Kibwe aliambiwa kuwa akifika
kule kwenye mji wa majini chini
kabisa ya bahari, aende kwenye
maabara yao, ambako viumbe
wale huendesha shughuli zao za
kuchemsha vichafuzi vya hewa.
Kibwe hakujua atafikaje kwenye
maabara hiyo, ndio maana
alipobahatika kuyaona yale
majini, akaamua kuyafuata.Na ili
kukamilisha kazi yake ya
kuyateketeza majini yale maovu,
Kibwe alipewa fuko zima la
uvumba, ubani na udi,
akaambiwa kuwa anachotakiwa
kufanya ni kumwaga
mchanganyiko ule kwenye moto
mara atakapofika katika maabara
hiyo ya kipekee ya majini, ili
kuifukiza hewa yote katika
sehemu ile. “Hakikisha kuwa
unatupia mchanganyiko huu
kwenye moto, kwa kuwa moshi
wake wenye harufu kali,
utawachanganya akili hao majini.
“ Mzee Kaka alifafanua, na
vilevile akamwambia Kibwe
kuwa asishangae kama kitatokea
kimbunga cha chini ya bahari au
‘tsunami’ na kuteketeza eneo hilo
na vifaa vyote vya uharibifu wa
hewa.
Kibwe alisubiri kwa muda wa
kutosha tangu yale majini
yalipozama baharini, akichelea
kupambana nayo kabla
hajajiandaa. Mwishowe naye
alianza safari yake ya kushuka
chini ya bahari kwenye ule mji
wa majini nchini Baharia. Kama
alivyoambiwa na Mzee Kaka,
chini kabisa ya bahari Kibwe
hakukuta maji, bali alikutana na
msitu mwingine wa ajabu sana,
uliopambwa na miti ya
matumbawe ya rangi rangi,
mingine mirefu sana mingine ya
kawaida iliyopendezesha
mandhari kwa rangi zake za
kuvutia kama manjano,
machungwa, samawati, damu ya
mzee na nyinginezo. Mara kwa
mara Kibwe alipishana na
viumbe wengine wa ajabu ambao
kutoka tumboni hadi kichwani
walikuwa ni binadamu, na
kutoka tumboni kuja miguuni
walikuwa samaki! Walimvutia
mno Kibwe, aliyewapungia
mkono, lakini walimshangaza
zaidi walipomsalimia. “Habari
yako Kibwe! Karibu kwenye jiji
letu kuu 1nchini Baharia!” Ha!
Kibwe alibutwaika mno! “Habari
nzuri sana! Nashukuru
kunikaribisha. Siku njema.”
Aliwaambia, huku akiwa na
maswali chungu nzima ya
kujiuliza. “Haa! Kumbe nguva ni
viumbe wa kweli! Nilidhani wapo
katika hadithi tu. Na tena
wanaongea kama sisi!” Aliwaza
kwa mshangao mkubwa, ingawa
hakufahamu kuwa aliweza
kuwaona na kusalimiana nao kwa
sababu yeye mwenyewe hakuwa
mwana wa kawaida!
Kijana yule shujaa alijizamisha
chini zaidi ya bahari hadi
alipofika mahali ambapo maji
yalikomea juu ya kichwa
chake.Baada ya kuzama, kwenye
upeo wa macho yake akaona
ngome ndefu ya shaba
iliyozunguka kwa kilometa nyingi
mno! Alihisi kuwa bila shaka ile
ilikuwa ni maabara ya majini
aliyotarajia kuiteketeza. Ingawa
alikuwa na hofu ya kupambana
na wale viumbe wanaoweza
kujigeuza katika maumbile
yoyote wayatakayo, lakini
aliamua kwenda moja kwa moja
hadi mahali pale. Njia aliyopitia
kufika huko ilinakshiwa kwa
tumbawe za aina aina na
marumaru za thamani kubwa.
Mbele zaidi aliona makasri
makubwa ya kifalme
yaliyojengwa kwa marumaru za
rangi mbalimbali. Mengine kati
ya makasri hayo yalijengwa kwa
mawe na majabali yaliyojaa chini
ya bahari. Kule alikuta mabonde
yenye ukubwa uliotofautiana,
yaliyotokana na miamba
iliyoonekana kama rafu. CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kwenda mbele zaidi,
kabla ya kufika kwenye maabara
iliyozungushiwa ngome ya shaba
iliyong’ara mno kwa mwanga wa
jua, alikuta sehemu ambayo
miamba imekusanya takataka,
matope na mchanga. Ajabu ni
kwamba mchanga ule
ulichanganyika na vumbi la
dhahabu! Alipozidi kusonga
mbele, aliona kuwa mchanga wa
kawaida ulizidi kupungua na
badala yake, kiwango cha vumbi
la dhahabu kiliongezeka,
kuelekea bondeni. Kadiri
alivyoikaribia ile maabara,
ndivyo alivyoshuhudia utajiri
mwingi usioelezeka, wa johari
kama vile lulu na vito vingi vya
thamani pamoja na dhahabu na
fedha, vyote vikiwa
vimelundikana kandokando ya
njia. Kibwe alibutwaika,
akistaajabu kuona yote yale,
ambayo ni mageni kabisa katika
maisha yake.
“Sijui nimo ndotoni….au
ninayoyaona ni kweli nayaona”!
Aliwaza, na akimaizi kuwa safari
yake yote ilikuwa ni ya maajabu
makubwa.
Alipofika ngomeni alikuta lango
kuu limefungwa.
ITAENDELEA
 
Sehemu Ya Tatu (3)
“Naona huu ni wakati muafaka
wa kutumia upanga wangu.”
Kibwe aliwaza, halafu akatoa
upanga wake katika ala na
kugusa ile sehemu ya vitasa vya
lango kuu, na mara zikatokea
cheche, halafu lango likajiachia
na Kibwe akaweza kulifungua
kwa urahisi mkubwa. Taratibu
aliingia ndani ya uzio, alikokuta
sebule kama uwanja mkubwa
mno, iliyojengewa mabomba
mapana na marefu kupita kiasi,
yaliyotoa moshi mnene mweusi
mno!. Moshi ule ulionekana
ukipotelea juu mno kwenye
majabali na miamba iliyouzingira
mji wa Baharia. Mabomba katika
ile maabara yaliunganishwa
kwenye maguduria makubwa na
mitungi ya shaba vilivyoinjikwa
kwenye majiko au mafiga
yaliyotowa moto mwingi mkali
sana! CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nitakapofika karibu na yale
mafiga tu, kazi yangu
itakamilika.” Aliwaza Kibwe
lakini akiwa na hofu na wahaka
mkubwa. Je, yale majini
yakitokea kabla hajatekeleza kazi
yake ya kumwaga mavumba
kwenye moto? Itakuwaje? Hata
hivyo, alipiga moyo konde na
kwa umakini mkubwa, alinyata
hadi mahali palipoinjikwa yale
masufuria, maguduria na mitungi
ya shaba, moyo wake ukikimbia
kwa kasi mno! Aliangalia huku
na kule kuhakikisha kuwa
hakukuwa na hatari yoyote.
Alipoona kuna amani, akatoa
fumba la mchanganyiko wa
uvumba , udi na ubani kutoka
kwenye mfuko wake alioubeba
mgongoni na haraka alilitupia
motoni. Halafu lo! Mara moja
ulitokea moshi mnene uliotanda
eneo lote, na uliopanda juu
kabisa ambako ule moshi wa
vichafuzi vya hewa ulikokuwa
ukiyoyoma!
Moshi ule wa mavumba ambao ni
hatari kwa wale viumbe wa
ajabu, ulikwenda hadi kwenye
yale makasri ya majini ya fahari ,
yaliyojengwa juu ya vilima
tambarare, na ukayaathiri vibaya
sana majini hayo kwani
walipaliwa na wakakohoa bila
kizuizi, huku wakishindwa
kupumua vizuri. Wote
walipaparika, na kuamanika,
wakigombea milango ya kutokea
nje ya majumba yao, ili
kujinusuru. Baadhi yao
waliofanikiwa kutoka wakiwa
katika maumbile ya majoka
kamili, walimuona Kibwe
akitokea kwenye maabara yao,
na wakatambua kuwa
mwanadamu yule ndiye
aliyehusika na janga
linalowasibu.” Niteaufm karaha!
Niteaufm vihi asas!”(mfuateni
haraka! Mfuteni sasa hivi!) Majini
yale yaliamrishana kwa lugha
yao, huku yale yaliyogeuka nyoka
halisi yakitambaa kwa kasi
kumfuata Kibwe, na yale
yaliyobaki kuwa nusu watu na
nusu majoka, yalimkimbilia kama
upepo, yakitowa pumzi ya moto
uliofika mbali mno, na
kumkosakosa Kibwe kwa
sentimita chache sana!
Wakati majini yakiazimia
kumuadhibu mwanadamu yule
mchokozi, Kibwe naye alikimbia
kufa na kupona, kwani alitambua
kuwa tayari nyuma yake kwa yale
majini, aliacha maafa makubwa
na hasara isiyoelezeka .
“Wakinikamata tu, utakuwa ndio
mwisho wang……” Kabla
hajamalizia kusema neno la
mwisho, moto mkubwa
ulioelekezwa kwake ulimjia kwa
nguvu na kasi ya ajabu!
“Ooooooo! Whuuuu.uuuuuu!”
Kibwe alipiga ukulele
uliochanganyika na pumzi
aliyoitowa kama mluzi, kama mtu
anayepumua, akihofia kile
kitakachofuatia, na akijitahidi
kuukwepa ule moto! Assalalaaaa!
Kibwe alishangaa kupita kiasi!
Mara moja aliona mambo
yakibadilika, kwani ule moto
waliopumua majini, uligeuza njia
na kuwarudia wenyewe, wengi
wao wakiungua vibaya sana!
Kilichotokea ni kwamba wakati
Kibwe aliposhtuka na kuona
mienge ya moto ikimwandama,
na alipopumua kwa nguvu kwa
kupiga mluzi mkali, mluzi ule
ulisababisha hewa iliyomzunguka
kujikusanya mbele yake, na
halafu wakati uleule nguvu za
mluzi wake ukasukuma hewa
iliyopeperusha mienge ya moto
uliokuwa ukimfuata kwa ajili ya
kumteketeza! Kwa mastaajabu
makubwa, alishuhudia moto
ukiyageukia yale majini na
kuyaunguza unguza vibaya sana!
Tukio lile la kimiujiza lilihusika
sana na maajabu ya Mwana
Mteule ambayo Kibwe hakuwa na
habari nayo asilani! Hata hivyo
Kibwe hakutaka kuwa karibu
wakati wale viumbe hatari
walipoanza kumfuata ili kulipizia
kisasi! Hakupoteza muda bali
alitimua mbio za ajabu na wakati
ule aligundua muujiza mwingine
tena. Alipokuwa akikimbia alihisi
kwamba ingawa wakati fulani
alikuwa akikimbia kama mtu wa
kawaida, lakini mara nyingine
alijiona akielea angani kama
mwewe! Hakuwa na muda wa
kujiuliza chochote kuhusiana na
maajabu yale mengine, bali
alikimbia tu, mara akipeperuka
kama kipepeo na mara akikimbia
kwa kutumia miguu yake kama
kawaida, akifuata njia
iliyomfikisha nchini Baharia, ili
aweze kutokea ufukweni
alikoingilia. Lakini lo! Kwa bahati
mbaya Kibwe alipotea njia na
kutokea kwenye eneo la
makorongo ambayo awali
hakuyaona! Makorongo yale
yalipasua miteremko ya ardhi
iliyotoka kwenye mwambao wa
ufukwe!
Kibwe alizidi kufuata njia ile ya
korongoni kwani hakuwa na
muda wa kuamua vinginevyo.
Lakini kwa bahati, wakati fulani
alihisi kuwa aliruka juu mno
kama mtu aliyekuwa na mbawa,
na kisha kama samaki nyangumi,
akayavuka maji ya bahari
ambayo awali yalikuwa juu ya
kichwa chake kama paa la
nyumba. Kwa kuyavuka yale maji
ya bahari, Kibwe akajikuta nje
kabisa ya maji yale, na kufikia
juu kabisa ya moja kati ya
majabali aliyoyaona awali kabla
ya kuingia nchini Baharia.
“Wooo—woooo—wooooo
Aaaaaaaaagh! Wooooo—woooo—
woooo…..Aaaaaaaa!!” Kibwe
alilalama wakati akipaa juu
kimiujiza! Alimshukuru sana
Mungu wake kwani tukio lile
lisilokuwa la kawaida
lilimrahisishia mno azma yake ya
kuwakimbia wale viumbe wa
kipekee, pamoja na kwamba
lilimstaajabisha sana.
“Hakika leo ni siku ya maajabu
makubwa kwangu!” Kijana yule
alisema na nafsi yake, moyo wake
ukidunda kwa kasi!
Akiwa juu ya jabali na baada ya
kuangaza huku na kule, Kibwe
aliaona mlango wa pango kubwa
la tumbawe na mawe magumu.
“Yoohu! Yoohuu!
Nieizum….nieizum (Mzuieni!
Mzuieni! Huyoo! Huyooo)!”
Kelele za majini zilisikika nyuma
ya Kibwe, wakati mienge ya moto
ikielekezwa kule alikokuwa.
Majinni yaliyonusurika na moshi
wa mavumba, nayo yaliruka
kama popo kumfuata Kibwe kwa
hasira, ambaye alijaribu tena zile
mbinu za kuupuliza ule moto wa
majini kwa nguvu zake zote. Lo!
Faraja ilioje! Mbinu zile
zilifanikiwa na kusababisha moto
uliokusudiwa kumteketeza Kibwe
kuyarudia yale majini kama
ilivyokuwa mwanzoni, na
kuyaunguza vibaya sana. Kibwe
alitumia wakati ule kuingia
haraka kwenye ule mlango wa
pango aliloliona, ili kunusuru
maisha yake. Alipoangalia mle
pangoni hakuweza kuona
chochote kutokana na giza nene
lililotanda. Alipokodoa macho
yake kwa muda mrefu ili
kujaribu kuyalazimisha kulizowea
lile giza, taratibu alifanikiwa
kuona njia nyembamba mbele
yake. Bila kusita haraka sana
alianza kutembea kwa hatua za
haraka haraka akiifuata ile njia,
bila kujua ilikua akielekea wapi.
Halafu akaanza kukimbia
kutokana na hofu ya yale majini
aliyoyaacha nyuma yake. Hata
hivyo, kadiri alivyozidi kukimbia
na kuifuata njia ile nyembamba
mle pangoni, ndivyo giza nene
lilivyozidi kutanda upya!
Alipokuwa katika lile giza nene,
Kibwe akakanyaga mahali
palipojiachia ghafla, na mawe ya
mahali pale yakaanza
kuporomoka pamoja naye kwa
mwendo wa kasi bila kizuizi,
yakienda sanjari na ufa uliokuwa
juu ya miamba minne
iliyoning’inia, ikibembea huku na
kule, kila mwamba ukiiinuka kwa
uimara mkubwa, na kuishia
katika wangwa wa maji, kama
mita thelethini chini ya mahali
ambapo Kibwe alianzia
kuporomoka.
“Aaaaaagh! Aaaagh! Mama yangu
weee! Nakufaaaa….mim
mimiiiii!” Kibwe alipiga ukelele
huo kwa taharuki na alipojaribu
kukamata mizizi iliyokuwa
ikining’inia kutoka juu yake
alishindwa, kutokana na kasi ya
kuporomoka kwenda chini.
Lakini ghafla bila kutarajia,
mkono wake ukakamatwa
madhubuti na kitu
asichokifahamu! Kibwe alishituka
mno! Wakati ule alikuwa
akining’inia baina ya juu na chini
ya jabali refu mno! Alipata hofu
zaidi alipohisi joto kali juu ya
kichwa chake, lililotokana na
moto waliopumua wale viumbe
wenye hasira naye….majini!
Kile kitu kilichomshika mkono
wake kilimning’iniza kwa nguvu
kama mtu anaebembea, na kisha
kikamrushia kwenye jabali
jingine upande wa pili, katika
mwamba uliokuwa na sehemu
ndogo ya ardhi tambarare mithili
ya rafu, na hivyo kumnusuru
asiangukie kwenye wangwa, chini
ya lile jabali refu kupita kiasi!
Alipoangalia upande wa jabali
alikotokea, Kibwe aliona kitu cha
ajabu kikibembea, na kikijirusha
kutoka katika mti mmoja kwenda
mwengine, kwa kutumia mizizi
ya miti iliyokua ikining’inia,
kama kwamba kitu kile kilikua
kikijiandaa kurudi juu ya lile
jabali refu kabisa mithili ya
gorofa. Halafu Kibwe akatambua!
“Haa! Ndio maana
nimenusurika!” aliwaza kwa
furaha!
Mbele ya macho yake, kile
alichodhania kuwa ni kitu cha
ajabu kikibembea huku na kule,
hakikuwa kitu, bali alikuwa ni
rafiki yake mpenzi ‘Bunga!’
Alimrukia na kumkubatia kwa
furaha kubwa sana, na Bunga
akawa anamcheka tu.
HANGA NA NJIA YA MAKUTANO.
Kule pangoni kwa bibi kizee,
Hanga aliyatafakari maelekezo
yake kabla hajaendelea na safari.
“Huko mjukuu wangu ni kwenye
milima ya moto ya maangamizi
kwa binadamu. Daima uovu
haulali mahali pale wala
hausinzii! Hewa ya huko ni ya
sumu hatari! Ni mahali ambapo
licha ya kunyesha mvua ya
kawaida, mara nyingine
hunyesha mvua ya mawe na
majabali. Kumbuka tu kuwa
mahali unapotaka kwenda
hakuna heri, bali kumetawaliwa
na uovu mtupu!”
Usia ule wa bibi wa pangoni
ulimtia wasiwasi mkubwa yule
kijana, hasa bibi yule
alipomalizia usia wake kwa
msisitizo kwamba ‘kila waendao
kule hawarudi wao, ila hurudi
majina yao tu!’
Dah! Hanga alijilaumu sana kwa
uamuzi wake wa kwenda ‘Msitu
wa Kindumbwe’.
“Ama kwa hakika nimejitosa
katika janga kubwa mno!”
Alijisikitikia moyoni.
Lakini pia alitambua kuwa ‘maji
ukiyavulia nguo, lazima uyaoge’.
Kwa hiyo alimwambia yule bibi
mzee kuwa angejitahidi kuwa
mwangalifu sana katika safari
yake, kwa hiyo amwelekeze tu,
jinsi ya kufika mahali
panapohusika. Yule Kizee
alinyoosha mkono na kuonesha
kidole chake kwenye moja ya
vichochoro vya mle pangoni
akasema, “ Fuata ile njia katika
uwazi unaoelekea kwenye
uchochoro wa upande wa
kaskazini. Njia hiyo ni ndefu mno
na yenye giza nene. Watu huiita
njia ile, ‘Njia ya makutano,’ kwani
njiani hukutana na vitu au watu
wasiowatarajia. Baada ya
kutembea kwa masafa marefu
sana utatokea kwenye kuta ndefu
za moja kati ya majabali meusi
kwa upande wa ndani wa
uwanda wa ‘Paa la Dunia’, na
humo utakuta ngazi za mawe.
Ukipanda kwenda juu kabisa ya
uwanda ukiwa humo ndani,
utakuta mlango wa kuingilia
kwenye hilo pango unalolitafuta,
la sanamu la kichwa cha Simba. ”
Woga ukamtawala Hanga. Hii
safari ilizidi kuelekea kuwa
ngumu kwake.
Ukipanda kwenda juu kabisa ya
uwanda ukiwa humo ndani,
utakuta mlango wa kuingilia
kwenye hilo pango unalolitafuta,
la sanamu la kichwa cha Simba.
” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Woga ukamtawala Hanga. Hii
safari ilizidi kuelekea kuwa
ngumu kwake.
Baada ya maelekezo yale bibi
yule aliendelea kumtahadharisha
kuwa humo atakamopita huenda
akakutana na kibwengo mmoja
mbaya na laghai sana, ambaye
naye ni mjumbe wa shetani au
pepo muovu wa ‘ulimwengu wa
zama za kale’ ambaye pia ni
mfalme wa kidani anachokifuata.
“Anaweza kukudanganya ili
akichukue yeye kile kidani kwa
lengo la kuuficha ukweli
ulioandikwa ndani ya kidani
hicho, ili tu kuipotosha jamii
katika sayari yetu.” Bibi
alimtanabahisha kuhusu huyo
Kibwengo laghai, na macho
yakazidi kumtumbuka Hanga.
Jambo jingine lililompa hofu zaidi
Hanga ni kufahamu kuwa huko
aendako, wapo mazimwi
wanaoongozwa na shetani au
pepo huyo muovu wa
‘ulimwengu wa zama za kale,’
wanaokilinda kidani kile
kisiangukie mikononi mwa watu
wema. Nia yao, alisema yule bibi,
ni kukitekeza kwa moto kwenye
milima ya maangamizi, kusiwepo
na uwezekano wowote wa mtu
yeyote kufanikisha nusra ya
sayari yao. “Kwa kuwa wao
hawawezi kukifikia pale kilipo’
kutokana na laana waliyoipata
miaka mia moja iliyopita kwa
kusaidia kuiteketeza nchi moja
mashuhuri ya Sabaa
wakishirikiana na majini wa nchi
ya Baharia, ndio maana
wanawavizia watu wema
watakaofanikwaa kukichukua
kidani hicho, ili wawapore.”
Kutokana na maelezo yote yale,
Hanga alimaizi uovu mkubwa
unaoikabili sayari yao na watu
wake, akihofu kwamba huenda
kazi ya kuipata nusura ya jamii
yake ikawa ni ngumu mno!
Wakiagana pale pangoni yule
bibi kizee alitoa kito kimoja
kikubwa cha thamani chenye
ukubwa wa komamanga na
chenye umbile la alimasi,
akamkabidhi kijana yule na
kumwambia, “Kwa kuwa njia
yote kuanzia hapa tulipo ni giza
tupu, na kwa kuwa mara kwa
mara huenda ukakabiliana na
viumbe wengi waovu, kito hiki
kitakuwa ni mwanga katika
sehemu za giza nene si kwa
kuwamulika tu viumbe hao, bali
pia kwa kuwadhibiti wote
wasioitakia heri sayari yetu!”
Pia alimwambia kuwa
atakapofika langoni mwa pango
analolitafuta, lazima aseme neno
la mazingaombwe ndipo lango
lile litafunguka ili aingie kwenye
sanamu la kichwa cha shaba cha
simba. “Lazima useme neno
“Lyang’andu” mara tatu.”
Alimwambia, na kumuuliza mara
mbili iwapo amemuelewa.
Hanga akamhakikishia kuwa
amemuelewa.
“Haya buriani mjukuu wangu,
nenda salama.” Hatimaye bibi
alimuaga.
“Buriani dawa bibi yangu.
Tutaonana Mungu akipenda!”
Hanga alimjibu kwa shukurani
kubwa . Wakati akimuaga kwa
maneno hayo, hakuacha pia
kuwaza na kujiuliza kuhusu
ubinadamu wa bibi yule, kwani
alimuona kuwa hakuwa wa
kawaida. Haraka sana aliondoka
na kuelekea kwenye moja kati ya
vile vichochoro vilivyokuwa na
giza totorooo, ili aachane na
kizee yule wa pangoni
aliyemhofu sana!
Hanga alivipita vichochoro vya
mle pangoni vilivyomfikisha
kwenye mapango mengine
mengi. Aliifuata njia ya makutano
kama alivyoelekezwa, akavuka
vijito vilivyoshehena mawe na
tope, hali iliyoifanya safari yake
mle mapangoni kuwa ngumu
sana. Hapa na pale kwenye njia
ile nyembamba iliyogubikwa na
giza la ajabu, miti mirefu mno na
minene iliupamba msitu ule wa
kipekee. Ingawa alikuwa na hofu
kubwa, lakini Hanga aliendelea
na safari yake, wakati macho
yake yakimudu kuona mahali
alipokanyaga tu kutokana na lile
giza. Mara nyingine alitumia kile
kito alichopewa na mzee wa
pangoni, lakini hata hivyo bibi
yule alimtahadharisha kuwa
asikitoe mfukoni kito hicho mara
kwa mara, kwani huenda
mwanga wake ukamfanya
aonekane kwa urahisi na
wajumbe wa shetani au ‘pepo wa
ulimwengu wa zama za kale.’
Kwa hiyo mara nyingi Hanga
alilazimika kutembea kwa shida
sana gizani.
Wakati Hanga akitafakari kuhusu
onyo la yule kizee, mara moyo
wake ulichupa, kwani ghafla
alihisi kama kwamba ameona
vivuli vya watu!
“Ni watu kweli?” aliwaza.
“Lakini labda si watu! Au tuseme
wanyama! Lakini mmh….labda si
wanyama…….! Mbona wana
mikia mirefu sana?” Mawazo
hayo yalipita kichwani kwa
Hanga huku akitetemeka na
kugwaya kwa hofu.
Kwa bahati mbaya hakuweza
kuona vizuri ni vivuli vya
viumbe wa aina gani alivyoviona
kwa sababu ya lile giza. Katika
njia ile ya Makutano, vivuli hivyo
vilipita katika upeo wa macho
yake kwa kasi kama upepo!
“Chukua kito hiki na inshaallah
kitakuwa ni mwanga wakati kila
mahali patakapokua giza…..”
Hanga alipoyakumbuka maneno
ya yule bibi wa pangoni haraka
akakitoa kile kito na halafu mara
moja katika sekunde chache
zilizofuata, nuru ilizagaa msitu
wote wa mle pangoni na
kumwezesha kuwaona vizuri
sana viumbe waliokuwa
wakubwa mno na wa ajabu,
wenye maumbule ya nyoka
kuanzia tumboni kwenda
kichwani, na maumbile ya
wanadamu kushuka miguuni,
isipokua walikuwa na mikia
mirefu sana! Katika muda ule wa
sekunde chache sana viumbe
wale walitokomea msituni,
wakimwacha Hanga dhoful hali
kwa hofu, mwili wake wote
ukizizima!
***
Naam, Hanga alipokuwa pangoni
chini ya ‘Paa la dunia,’ Kibwe
naye alikuwa nje ya lile pango
juu ya ‘Paa la Dunia’, kulikokuwa
na minara pacha mitatu mirefu
kupita kiasi! Minara ile
ilisimikwa kama mafiga, na
katikati yake kilikuwepo kitu
kama kigoda cha vito vya
thamani. Ile ilikuwa ni sehemu
maalum iliyoutoa moshi mnene
wa vichafuizi vya hewa ya ozoni
kutoka kwenye maabara ya
majini kule chini kabisa ya bahari
nchini Baharia, ambako Kibwe
alipambana na majini na
kuiteketeza maabara yao.
“Lazima nifike juu ya kile kigoda
kwenye minara mitatu, kama
nilivyoelekezwa na mzee Bunga.”
Kibwe aliwaza. Kibwe alilazimika
kufika kwenye minara akitokea
juu ya uwanda mrefu kupita
kiasi, uliogawanyika katika safu
kama ngazi kwenye miamba
minne, kila mmoja ukianzia
pembezoni mwa uwanda kwa
utaratibu maalum. Ilimlazimu
Kijana yule kuivuka miamba ile
myembamba iliyokuwa
ikining’inia, kwa kubembea huku
na kule. Kwa hiyo alijishusha kwa
umakini mkubwa sana akiponea
chupuchupu kuangukia chini
kabisa kwenye umbali wa zaidi
ya mita alfu moja!
Kwa kuwa kila mwamba uliinuka
kwa uimara mkubwa kutokea
korongoni, kwa kufuata
maelekezo ya Bunga, Kibwe
alijitahidi kwa nguvu na hekima
zake alizokuwa nazo, kuifikia
ngazi ya mawe iliyokuwa katika
moja ya ile miamba, na kutafuta
mbinu za kufika karibu na usawa
wa ile minara pacha, ingawa
chini ya ile miamba kuliwa na
korongo moja kubwa mno la
hatari, kama mtu angeangukia
humo kutokea juu alikokuwa
yeye. Kijana yule shujaa aliweza
kuifikia ile ngazi ya mawe katika
moja ya ile miamba. Lakini
masikini, kwa sababu maji ya
kijito yalitiririka kila siku
yakamwagikia kwenye zile ngazi
na kusababisha utelezi hatari,
mara Kibwe alipokanyaga jiwe
moja la ngazi za moja kati ya
miamba ile, mguu wake uliteleza,
akaanza kuporomoka! Moja kwa
moja alianguka akipitia eneo
lenye mwanya au ufa
mwembamba ulioongezeka
upana kwa chini alikokuwa
akiporomokea. Katika safari ile
hatari akiporomoka kwenda
chini, alipambana na maji
yaliyokuwa yakiporomoka kwa
nguvu mno kutokea juu kabisa ya
uwanda! Aliogopa kupita kiasi na
wakati alipokuwa akitapatapa
kutafuta njia ya kujinusuru,
haraka alikamata mzizi mwingine
mnene uliokuwa ukining’inia,
akabembea nao akiangalia kwa
uangalifu na kutafuta ni mahali
gani pa kurukia.
Kibwe alifahamu kwamba kwa
kujining’iniza vile, alikuwa katika
hatari ya kuporomokea chini kwa
umbali mkubwa sana, ambako
yalikuwepo mawe makali na
sehemu nyingine kukiwa na
mchanga didimizi hatari. Kibwe
alihofia sana kupoteza maisha
yake! Kwa kuwa alitishika mno
na mawazo hayo, alibembea na
kujirusha upande mwingine wa
ule ufa wa mwambani, akafikia
kwa kishindo kwenye lango la
pango moja jingine kubwa, katika
moja ya safu iliyoligawanya moja
ya majabali meusi. Pale langoni
alipofikia, Kibwe alijaribu
kuangalia ndani ya pango lakini
kwa giza lililokuwa mle ndani
hakuweza kuona chochote, bali
alihisi kama kwamba amemuona
mtu amesimama kwa mbali
kidogo, akiangalia kwenye
mlangoni wa pango alikofikia
yeye. Kibwe alipatwa na hofu na
wahaka mkubwa. CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ni nani tena yule mle pangoni?
Ni mtu au ni jini? Au ni mmoja
kati ya yale majini yaliyokuwa
nyuma yangu, anaesubiri
kulipizia kisasi kwa matatizo
niliyowasababishia kwao? Sijui
nimejitosa wapi tena?” Maswali
mengi yalimzonga kichwani
mwake. Alijaribu kugeuka ili
kutafuta njia ya kuondoka pale
alipokuwa na kurudi alikotoka,
lakini lo! Mara akasikia mlipuko
mkubwa wa kushtusha
ulioambatana na mviringo
mkubwa wa moto iliomwelekea
pale alipokuwa! Hapo hapo
akajirusha haraka ndani kabisa
ya lile pango kubwa kujinusuru!
MAANDIKO YA AJABU.
Wakati Kibwe anakurupushwa na
lile viringo kubwa la moto kule
alipokuwa, huku kwa Hanga nako
kulikuwa kuna yake.
Hanga alikuwa akizipanda zile
ngazi za mawe zilizojitokeza mle
pangoni chini ya ‘Paa la Dunia,’
ndani ya ule uwanda mrefu
akiwa mwingi wa wahaka na
aliyetekwa na hofu kubwa.
“Labda hizi ngazi zitanifikisha
sehemu ya ule mlango
alioniambia bibi kizee wa
pangoni.” Aliwaza, huku taratibu
na kwa tahadhari kubwa, akienda
juu zaidi ya lile jabali.
Giza lilipozidi kijana yule alitoa
kile kito alichopewa na kizee
pangoni, kilichotoa nuru kali
iliyomuonesha njia. Alipanda kwa
masafa marefu sana hadi miguu
yake ikapooza na kupata ganzi
kwa uchovu! Alikuwa akipanda
jabali la urefu wa takriban gorofa
ishirini, na wala hakuwa na
fununu ya mwisha wa safari
yake!
“Subira mjukuu wangu! Subira
pekee ndiyo itakayokusaidia
kukamilisha jukumu lako!”
Alikumbuka usia wa bibi kizee
wa pangoni, mara baada ya
kupewa maelekezo ya safari yake.
Akiwa katika tafakuri ya usia ule,
mara hatua chache mbele yake
akaona mlango mkubwa wa
mawe ya tumbawe! Alihisi kuwa
bila shaka ule ulikuwa ndio
mlango wa kuingilia kwenye
pango la sanamu la shaba la
kichwa cha Simba, ambako ndiko
alikokuwa akielekea.
Pale langoni alijaribu kukumbuka
lile neno la mazingaombwe
aliloambiwa aliseme, ili mlango
wa kuingilia pangoni
ufunguke….! Kwa bahati nzuri
baada ya kukuna kichwa kwa
muda fulani, Hanga alilikumbuka
lile neno na akalitamka mara
tatu.
“Lyang’andu! Lyang’andu!
Lyang’andu!”
Lo!
Kama muujiza baada ya kama
sekunde thelathini hivi, jiwe la
pango lilianza kuzunguka
taratibu likitoa mlio kama mtu
anayesaga mtama kwa jiwe!
Lango lile lilipofunguka Hanga
hakuamini macho yake! Mle
pangoni aliona sanamu kubwa
kupita kiasi la kichwa cha shaba
cha Simba, lenye urefu uliokuwa
mara tatu ya urefu wake yeye!
Iilikuwa na sura ya Simba kabisa,
lenye macho mekundu kutokana
na vito maalum vilivyong’ara,
ndevu za shaba na vidani vitatu
vya fedha vya sanamu za kucha
za simba vyenye ukubwa wa
tunda la zaituni, vikining’inia
kwenye mkufu mrefu wa fedha.
Naam, Hanga alifarijika mno
kujikuta mahali pale ambapo
ndipo hasa palipokuwa kiini cha
safari yake! Pamoja na wahaka na
wasiwasi wa hatari nyingi
zilizohusiana na sehemu ile
aliyofika kwa mujibu wa onyo la
bibi kizee wa mle pangoni,
kwamba daima mahali pale uovu
hausinzii wala haulali, na hewa
ya sehemu ile kuwa ya sumu,
lakini Hanga alihisi kuwa jambo
muhimu ni kwamba alikaribia
kupata jibu la uovu na majanga
yanayoikabili sayari yake!
Lakini kwa bahati mbaya, kati ya
mahali aliposimama Hanga na
mahali lilipokuwa lile sanamu,
ulikuwepo uchochoro au ufa
kama mfereji. Wakati akiwaza
jinsi ya kuvuka na kufika pale
lilipokuwa lile sanamu, ulisikika
mwaliko wa mawe yaliyogongana
na kutoa mlio kama mtambo wa
aina fulani. Mwaliko ule
ulipoendelea ulifuatiwa na
mtikisiko mkubwa wa ardhi!
Hanga aliduwaa! Aliogopa sana.
Alijaribu kuelewa ni nini
kilichosababisha mwaliko ule, na
ulianzia wapi! Alihisi kuwa
huenda ulitokea kwenye Paa la
lile pango! Wakati yote yale
yakitokea, Hanga alikuwa juu
kabisa ya jabali, alikofika kwa
kupitia pangoni, ndani ya jabali
hilo la uwanda wa Paa la Dunia!
Akiwa kule alibaini jambo moja
la kutisha sana! “Haa! Hivi hapa
nilipo ni baina ya milima ya
maangamizi na uwanda wa Paa la
Dunia kama alivyosema ….”
Kabla hajatafakari zaidi, taratibu
paa katika lile pango lilianza
kuporomoka, na mawe ya
matumbawe yakajiachia,
yakisababisha nafasi ya chini
alikosimama Hanga kupungua,
wakati paa lile likikaribia
kichwani kwake!
Haraka sana kijana yule aliinama
kujinusuru, na wakati uleule
akijaribu kuuvuka ule ufa
miguuni mwake, ulioandaa
hifadhi ya maji kama kijito!
Ingawa Hanga hakuwa na
uhakika wa kina cha kijito kile,
hakuwa na la kufanya bali
kujitosa na kuvuka!
“Huenda nikivuka kijito hiki
itakuwa ni mwisho wa maisha
yangu lakini kurudi nyuma siwezi
kwani paa limeshuka mno!”
Aliwaza kwa hofu, akihisi kuwa
angeweza kuzama kwenye kile
kijito, na lile pango likawa ndiyo
kaburi lake!
Kwa simanzi kubwa, na kwa
mara ya kwanza kabisa kijana
yule alikumbuka maneno ya
kibibi Ajuza nyumbani kwao
Hazina, aliyemwambia, “Nenda
mjukuu wangu na utakapokuwa
huko ndipo utakapotambua kuwa
asiyefunzwa na mamaye
hufunzwa na ulimwengu!”
Hanga aliyekuwa mgumu
kuelewa kwa haraka maana za
methali, mara kwa mara alijiuliza
kuhusu maneno ya busara ya
kibibi Ajuza, kila alipopambana
na matukio kadhaa katika safari
yake.
“Ndio kusema kuwa hivi sasa
ulimwengu unanifunza? Na je,
ulimwengu wenyewe uko wapi
sasa? Maana….” Hakuendelea na
tafakuri yake kwani ghafla
liliporomoka jiwe kubwa kutoka
juu na alipotaharuki, aliona paa
likizidi kushuka kwa mwanguko
wa hatari mno! Bila kuwaza,
alijitosa ndani ya kile kijito! La
haula! Karibu mwili wake wote
uligubikwa na yale maji, yakasaza
sehemu ya kifua na kichwa tu!
Alijaribu kutembea ili avuke kwa
upande wa pili wa kijito
kulikokuwa na lile sanamu, lakini
hakuweza kufanya vile kutokana
na kina cha maji, na kwa bahati
mbaya hakuweza kuogelea!
Alianguka chini akatambaa
kwenye kijito huku mara kwa
mara akimeza maji na kukosa
uwezo wa kupumua vizuri.
Alijaribu kutembea ili avuke kwa
upande wa pili wa kijito
kulikokuwa na lile sanamu, lakini
hakuweza kufanya vile kutokana
na kina cha maji, na kwa bahati
mbaya hakuweza kuogelea!
Alianguka chini akatambaa
kwenye kijito huku mara kwa
mara akimeza maji na kukosa
uwezo wa kupumua vizuri. Kina
cha maji kilipoongezeka kilitishia
zaidi maisha ya Hanga. Kadiri
kina kilivyozidi kuongezeka,
ndivyo alivyoinuliwa kwenda juu.
Kwa bahati lile paa la pango kwa
upande aliokuwa akipelekwa na
maji, lilishikiliwa barabara na lile
sanamu kubwa la shaba la kichwa
cha Simba, likazuia paa lile
kuporomoka zaidi.
Maji yalipozidi kujaa yalimwinua
Hanga hadi juu kabisa ya ule
mwinuko wa matumbawe,
uliokuwa sanjari na lile sanamu
kwa juu ya paa la lile pango. Kwa
bahati kule juu ndiko kulikokuwa
na kifyatuzi cha kukamilisha kazi
iliyompeleka Hanga sehemu ile
hatari.
“Ah! ni bahati ilioje hii!” Aliwaza
kwa furaha, pamoja na uchovu
mkubwa aliokuwanao.
Alipoangaza angaza aligundua
kuwa nyuma ya, lile sanamu
lilikogubika sehemu kubwa ya
pango, kulikuwa na uwazi
mwingine mkubwa kama
mlango, ambao Hanga alihisi
kuwa bila shaka mtu angeweza
kutoka mle pangoni kwa kutumia
njia ya upande ule, baada ya
kuingia kwa kupitia kwenye ule
mlango uliofunguka kwa neno la
mazingaombwe, ‘Lyang’andu!’.
Hanga alihisi upepo mwanana
ukivuma kutokea kwenye uwazi
ule, ulioashiria kuwa ule uwazi
ulikuwa umeelekea kwenye
ufukwe wa bahari. Hata hivyo
Hanga alibaini moshi mnene sana
uliotanda nje ya pango katika
upeo wa macho yake kuelekea
baharini! Jambo lile lilimkatisha
tamaa kabisa!
“AH! Ndio kusema nimechelewa
kufika mahali hapa? Mbona
tayari sayari yetu imeanza
kuteketea jamani? Hivi safari yote
niliyoifanya ni ya bure?”
Alijiuliza maswali hayo kwa
kusononeka kukubwa kabisa.
“Kama kazi hii sikuifanya mimi
ataifanya nani tena? Hapana, si
vizuri kukata tamaa! Lazima
nifanye kile ninachoweza
kukifanya ili kufuatilia jambo hili
kwa makini!” Alikata shauri.
Akajitosa kutafuta faraja, ingawa
kwa kawaida yeye alikuwa
mwoga sana na mwenye
wasiwasi mkubwa yanapotokea
mambo ya kutatanisha .CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa kuwa maji ya kijito
yaliyoongezeka, yalimfanya
Hanga ainuliwe hadi kwenye
mwinuko wa ardhi tambarare
kwa upande mmoja wa sanamu
la kichwa cha Simba, taratibu
kijana yule alijisogeza na
kujipandisha juu zaidi ya
matumbawe yaliyokuwa
yakitereza mno na kuifanya kazi
ile kuwa ngumu sana. Hatimae
aliposimama juu kabisa na
kuweza kufikia kwenye usawa wa
masikio ya lile sanamu la Simba
lililoegemea pembezoni mwa
ukuta wa lile pango, akaona
kifyatuzi cha pembe tatu.
“Ni kifyatuzi kitakacho elekeza ni
kipi katika vidani vitatu vya
sanamu za kucha za Simba
vinavyoning’inia katika mkufu wa
fedha kina ujumbe maalum!”
Hanga aliwaza, akikumbuka
maelekezo ya awali ya kibibi
Ajuza kuhusu sahamu lile la aina
yake.
“Ili kutambua ni kipi katika
vidani vile kina ujumbe
unaohusika, utazungusha
kifyatuzi maalum cha jiwe
chenye umbo la pembe tatu,
kilichopo pembezoni mwa
sanamu. Kwa kufanya hivyo,
utafyatua mtego uliopo juu ya
sanamu lenyewe katika paa la
pango lile. Kitendo hicho
kitasababisha mwanga wa jua
kutoka mbinguni upenye na
kung’ara kwenye vidani vya
fedha vya kucha za simba, na ni
kimoja tu, kati ya vidani hivyo na
chenye kito cha rangi ya
samawati ndani yake, kitatoa
nuru. Hiyo itaashiria kuwa hicho
ndicho kidani unachokihitaji, na
ndicho kilichoandikwa huo
ujumbe wa kuitahadharisha jamii
kuhusu madhara yanayoikabili
sayari yao, na ni kwa sababu
gani…”
Baada ya tafakari ya maneno yale,
Hanga alijisogeza taratibu
akisaidiwa na ujazo wa maji ya
kijito, ambayo hakufahamu
yalitokea wapi, akajikweza juu ya
mwinuko wa matumbawe,
akijaribu kufika kwenye kile
kifyatuzi, ili kuendelea na zoezi
aliloazimia kulifanya.
Alipofanya kama alivyoelekezwa
na kizee Ajuza ili kukitambua
kidani chenye yale maelezo
muhimu, mtego ulijitegua na jiwe
moja katika sehemu ndogo ya paa
la pango likajiachia na
kudondoka, likiacha wazi tundu
dogo lililopenyeza mwanga wa
jua kutoka mbinguni. Mwanga
ule ulipovimulika vile vidani
vitatu vya fedha vya kucha za
simba, kimoja miongoni mwavyo
kilianza kutoa nuru ya rangi ya
samawati, iliyotokana na kito
maalum cha rangi hiyo
kilichokuwa ndani yake. Ghafla
katika upande uliojikunja wa
kidani kile cha umbile la ukucha
wa Simba, yalijidhihirisha
maandiko makubwa ya rangi ya
samawati! “Enheee! Haya ndiyo
maandiko yenyewe
ninayoyataka!” Hanga alisema
kwa furaha, akitabasamu
kutokana na faraja aliyoipata.
Alizidi kujisogeza karibu zaidi ya
kile kidani ili aweze kuyasoma
maandiko yale na kutegua
kitendawili cha miaka mingi sana
kuhusu sayari yao.
Lakini Loh, masikini!
Alipoyaangalia vizuri yale
maandiko, moyo wake
ukagutuka! Maandiko yale
yalionekana kama michoro tu,
isiyo na maana yoyote! Hii
iliashiria kuwa Hanga asingeweza
kuuelewa ujumbe alioufuata kwa
kilometa nyinga kutoka kwao,
njiani akipitia hatari za kila aina
hadi kufika pale alipokuwa!
Alipofikia uamuzi huo, hakuwa
na la kufanya. Alikata tamaa
kabisa ingawa awali hakuazimia
kufanya hivyo! Taratibu akaketi
juu ya ule mwinuko wa
matumbawe mbele ya lile
sanamu, akitafakari kuhusu
hatima ile, huku akitokwa
machozi.
“Maneno ya bibi 'Ajuza’ ni kweli
tupu! Jibu la kitendawili hiki
chote analo Mwana Mteule, na
wala si mimi! Bila ya yeye kufikia
hatima nzuri ya tatizo hili ni
kama ndoto tu!”
Baada ya kutafakari kwa muda
wa kutosha, aliamua kuondoka
taratibu kutoka mle pangoni kwa
kutumia upande wa pili wa lile
pango. Pole pole alielekea
kwenye ule uwazi mwingine wa
kutokea nje. Alitembea polepole
akiwa ameinamisha kichwa chake
chini.
Ghafla kishindo kikubwa
kikasikika na alipoinua kichwa
chake kuangalia mbele
kilikotokea na ambako ndiko
alikokuwa akielekea, hakuamini
macho yake! Kwenye uwazi wa
lile pango kwa umbali wa kama
mita mia moja hivi kutoka pale
alipofika, kilianguka kitu kutoka
mahali pasipojulikana lakini nje
ya uwazi wa lile pango! Aliruka
hatua moja nyuma moyo wake
ukikimbia kwa kasi. Alipojaribu
kuelewa ni kitu gani
kilichoanguka kwa kishindo
kikubwa vile na kilichoonekena
kuwa na umbile la mtu, mviringo
mkubwa wa moto uliotoa
mwanga mkali na joto la ajabu
ulioambatana na cheche nyingi
uliangukia nje ya ule uwazi,
ukiacha ndimi za moto
zikipeperuka juu. Hanga alihofu
kuwa huenda msitu wote
kuelekea ufukwe wa bahari
umeshika moto. Aliogopa sana
lakini zaidi ya yote, alisikitika
mno moyoni.
“Yote haya ni kwa sababu
sikuweza kuusoma ule ujumbe
kwenye kidani!” aliwaza.
“Lakini kama kweli yupo huyo
Mwana Mteule anasubiri nini
kufika huku ambako bila shaka
ndilo eneo la utekelezaji wa
jukumu Lake? Amekaa tu huko
alipo, raha mustarehe akifurahia
wadhifa aliopewa, wakati mambo
yanaharibika kiasi hiki! Watu
wengine bwana! Hawana haya na
wala hawaoni vibaya! Angalau
mimi nimejaribu kufanya
nilivyoweza!” Hanga aliyawaza
yote hayo kwa hasira nyingi, na
wakati ule akawa anarudi nyuma
haraka kule alikotokea ili
kunusuru maisha yake kutokana
na ule moto hatari uliozuka
pamoja na sijui kiumbe gani tu
kilichoanguka kwenye lango la
lile pango.
KIBWE, HANGA NA MINARA
PACHA.
Kutoka baharini nje ya lile pango
la Sanamu la Kichwa cha Simba,
moshi mnene ulizidi kutanda, na
wakati Hanga akihofu na kupata
wasiwasi baada ya kuhisi kuwa
aliona mtu au kitu kimesimama
kwa ndani ya mlango wa kutokea
mle pangoni, mlipuko mkubwa
uliotokana na mviringo mwingine
wa moto ulisikika.
Moto mwekundu sana mithili ya
zaha ya volkeno ulijidhihirisha,
ukiacha eneo lote likimweka kwa
mwanga mkali na kutukutia kwa
mvuke hatarishi mno! Ndimi za
moto mkali zilitanda pale langoni
mwa lile pango, hatua chache
kabisa na mahali kilipoangukia
kile kitu alichokiona Hanga…!
Mara kijana yule akashuhudia
maajabu makubwa.
Wakati ule moto ulipoelekea
pangoni alimokuwa Hanga, kile
kiumbe kilichoangukia kwenye
mlango wa lile pango kilitoa
pumzi zisizokuwa za kawaida,
zilizo upuliza ule moto kwa
nguvu, na hivyo kusababisha zile
ndimi za moto kupeperuka na
kurejea kule zilikotoka! Hanga
aliyekuwa pangoni amekodoa
macho yake kwenye ule mlango
wa pango, alishangaa sana huku
akihofia mno maisha yake kwani
hakuelewa kilichokuwa
kikitokea! Lakini mara, taratibu
aliweza kutambua kuwa muujiza
aliouishuhudia kwenye mlango
wa kutokea pangoni haukutokana
na kitu chochote, bali ulitokana
na mwanadamu kama yeye,
lakini si wa kawaida!
Hakufahamu tu kuwa mtu yule
wa ajabu aliyeangukia kwenye
mlango wa pango alikuwa ni
‘Mwana Mteule,’ Kibwe!’
Hanga alibaki akiwa amesimama
kama kisiki. Hakujua iwapo
amkimbie yule mtu ambaye
wakati ule naye alikuwa
akikimbilia kule alikokuwa yeye,
au amsubiri ili amfahamu kuwa
yeye ni nani hasa?
Kibwe naye alipofika karibu na
lile sanamu la kichwa cha Simba
akashtuka na kushangaa sana
kumuona kijana wa rika lake
akiwa amesimama mbele yake,
akiwa na uso uliojaa hofu
isiyosemeka. Huku akipumua
kwa kasi kutokana na
kuyakimbia yale majini, Kibwe
alitumbua macho kama tunguja
kumshangaa mwenzake, akili
ikimzunguka.
“Huyu ni binadamu kabisa huyu!
Sasa amefuata nini huku?”
Alijiuliza bila kuamini kuwa
baada ya siku kadhaa za
kupambana na viumbe
wasiokuwa wa kawaida, hatimae
amekutana na mwanadamu!
Wakati akijiuliza haya, akamsikia
Hanga akitoa sauti ya hofu,
iliyotetemeka kwa woga,
akimuuliza; “W-wewe n-ni
Jini….au n-ni m-mwanadamu…
enhh s-samah-han-ni…s-sa-ana!”
Wakati akiuliza swali lile, Hanga
alikuwa akirudi nyuma kidogo
kidogo, akijaribu kuwa mbali na
Kibwe, aliyemdhania kuwa si
mwanadamu wa kawaida.
“Mimi ni mwanadamu kama
wewe ndugu yangu isipokuwa
nashangaa kukukuta katika
sehemu hii isiyokuwa ya kawaida,
maana…” Kabla hajaendelea,
Hanga alimkatiza.
“Ndugu yangu? Ndugu yako
mimi? Ah, wee vipi? Sidhani
kama wewe na mimi ni ndugu.
Hatuko sawa asilani! Mtu dakika
chache tu zilizopita nimekuona
kwa macho yangu ukizipuliza
ndimi za moto mkubwa namna
ile kama unayezima mshumaa
tu?. Hebu niambie, ni
mwanadamu gani mwenye
uwezo kama ule, eenh?”
Kibwe alisita, kwani matukio yale
ya ajabu hata yeye
yalimkanganya.
“Amini usiamini ndugu yangu…
mimi ni mwanadamu kama wewe
na ningependa unitazame kama
nduguyo tu…kwani hakika
kukutana na binadamu
mwenzangu eneo hili ni jambo la
faraja isiyo kifani kwangu…”
Kibwe alimjibu, na kuendelea
kumwambia mwenzake kwamba
kwa kuwa tukio lile lilihitaji
maelezo marefu, kwanza
alipenda kujua ni kitu gani
kilichompeleka yeye Hanga
mahali pale hatari!
“Huku ndugu yangu, daima uovu
haulali wala kusinzia! Ni mahali
ambapo milima yake ina kazi ya
kuangamiza watu wema tu, ikiwa
ni pamoja na wewe na mimi!”
Hanga aliyatambua yale maneno
kwani aliyasikia awali kutoka
kwa bibi kizee wa mlemle
pangoni, kwa hiyo alihisi kuwa
bila shaka yule kijana ni
miongoni mwa wahusika wa
eneo lile.
“Ah! Ndugu yangu wee!
Kilichonileta huku ni kusaidia
jitihada za kuinusuru sayari yetu,
ingawa katika hatua niliyofikia,
uwezekano wa kutimiza azma
hiyo haupo tena.” Hanga alijieleza
kwa masikitiko, na Kibwe
alishangaa kusikia vile, kwani
mpaka wakati ule, hakufahamu
kuwa alikuwepo mtu mwingine
mwenye jukumu la kuinusuru
sayari, na ambae ni kijana kama
yeye.
Lakini alipomwangalia mwenzake
yule aliona kuwa amekata tamaa
kabisa, na tena mapema mno
katika utekelezaji wa kazi ile
nzito.
“Na kwanini usiwepo uwezekano
wa kukamilisha lengo hilo?”
Kibwe alidodosa. Hanga
alimweleza kuwa katika
ufuatiliaji wake wa jambo lile,
alipokuta ujumbe uliohusu
madhara yanayoikabili sayari
yao, hakuweza kuusoma ili
aufikishe kwa wahusika
watakaoufanyia kazi.
“Maana maandiko yaliyotumika
hayakuwa maandiko yanayoweza
kueleweka na mtu wa kawaida
kama mimi isipokuwa Mwana
Mteule pekee, ambaye kwa kweli
sina hata fununu ya mahali
alipo!”
Lo! Kibwe alizidi kushangaa!
Bunga asilani hakumwambia vile!
Au ndiyo sababu ya yeye
kufikishwa kwenye uwanda wa
‘Paa la Dunia’? Alitafakari, na
halafu akamwambia Hanga,
“Ahhhm! Sasa mwenzangu,
kwanza hata jina lako
nani?” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wale vijana wakatambulishana
majina. Baada ya kutambuana,
Kibwe akamtoa wasiwasi yule
mwenzake kwa kumpa moyo
kwamba huenda ukapatikana
ufumbuzi, mara baada ya yeye
kuyaangalia maandiko yale.
“Haya…hebu twende ukayaone.”
Hanga alimjibu huku
akimuongoza kule kwenye
kifyatuzi pembezoni mwa
sanamu la kichwa cha simba,
baada ya kuupanda ule mwinuko
wa mawe ya tumbawe ili kufikia
pale mahali. Kwa pamoja
walipokizungusha kifyatuzi, kama
kawaida kikaachia mwanya juu
ya paa la pango na kuingiza
mionzi ya jua, iliyosababisha
kimoja kati ya vidani vitatu venye
umbile la kucha za Simba, kitoe
nuru ya rangi ya samawati na
wakati uleule katika upande
uliojikunja wa kidani kile,
yalijidhihirisha maandiko ya
rangi ya samawati!
Kwa mshangao mkubwa, Hanga
alimsikia Kibwe akitamka
maneno haya;
“Kuungua Sayari, Kuteketea
Misitu, Kuongezeka vina vya
Bahari!
Kupotea Visiwa, wanasayari
kuteseka!
Lazima wema uushinde uovu,
heshima ikiuke dharau, imani
ilete tumaini, na kwa hekima,
wanasayari wazitawale tamaa
zao!”
Hanga alipagawa.
“Hapana! Haiwezekani!
Umewezaje kuyasoma haya
maandiko? Kama wewe si Mwana
Mteule usingeweza kuyasoma
maandiko haya hata kidogo! Bila
shaka wewe ndiye mteule
niliyeambiwa! Ni wewe! Ni wewe
nakwambia!” Hanga aliropoka
kwa hamaniko dhahiri
lililochanganyika na furaha kwa
jambo aliloligundua. Alijiona
kuwa ni mwenye bahati kubwa
na akataka sana kuelewa ni vipi
watafuatilia jambo lile baada ya
kupata undani walioupata.
“Huu ni ujumbe wenye maana
pana sana Kibwe! Je, tuanzie
wapi kuyatekeleza
yanayohusika?” Alidadisi Hanga.
Kibwe alimwangalia kijana
mwenzake aliyejawa na shauku
ya kuanza harakati za kuinusuru
sayari yao. Alijiuliza ni wapi
alikotokea mwenzake yule
aliyemuongezea nguvu na
matumaini makubwa katika kazi
yake.
“Hebu nieleze kisa chako rafiki
yangu…ilikuwaje hata ukafika
hapa? Na vipi unaonekana kuwa
ulikuwa unajua juu ya habari
zangu kabla hata hatujaonana?”
Hatimaye alimuuliza yule
mwenzake.
Hanga akaketi chini huku
akitabasamu.
“Hakika nitakueleza mwana
mteule…kwani na mimi ia nina
hamu ya kujua ni vipi ilikuwa
hata ukateuliwa kwa jukumu
kubwa kama hili…na…na
ulifikaje hapa kwa namna ile
ulivyofika/ Oh, mbona nina
maswali mengi kwako, ewe
mwana mteule usifikaye kila
kona?” Hanga alimjibu kwa
kiherehere.
Kibwe alimtazama tena yule
mwenzake.
“Dunia inateketea kila dakika
zinavyosonga Hanga. Sidhani
kama tutakuwa na muda mrefu
sana wa kupeana habari zetu.
Naomba unieleze kwa kifupi,
nami nitafanya hivyo baada ya
wewe kumaliza.” Alimjibu.
Ndipo Hanga bin Sultan
alipomueleza kisa chake…kisa
kilichomsababisha apate
msukumo wa kuifanya safari ile
ya ajabu kumtafuta mwana
mteule.
“Na sasa nashukuru kuwa
nimekutana nawe Kibwe. Hakika
wewe ni mwana mteule wa
kweli. Hebu na wewe nieleze kisa
chako sasa.” Hanga alimwambia
baada ya kumaliza kisa chake,
ambacho Kibwe alikisikiliza
akiwa kimya kabisa.
Sasa Kibwe alishusha pumzi
ndefu, akajiadaa kumueleza
mwenzake kisa chake. Kisa
kilichoanzia na nyoka wa baba…
nyoka wa baba yake…nyoka
kunyenge.
Na wakati akimsimulia, kwa
kifupi kwa kadiri alivyoweza
kuifupisha hadithi ile ya maisha
yake kabla ya kuwa mwana
mteule, Kibwe alijikuta akihama
kifikra kutoka kwenye ile sehemu
ya ajabu, vitisho, maafa na
maangamizo, na kurudi
nyumbani kwa baba na mama
yake, ambako sasa kulionekana
kama kwamba ni sayari nyingine
kabisa…
KUNYENGE NYOKA WA BABA.
Kibwe alitafakari kuhusu mambo
mengi ya ajabu aliyopambana
nayo. Aliwakumbuka kwa hofu
viumbe wengi wasiokuwa wa
kawaida aliowaona, hasa majini
waliojigeuza katika maumbile
mbalimbali, mara nusu watu na
nusu wakiwa ama vyura kuanzia
tumboni kwenda vichwani au
nyoka wakubwa, au binadamu
ambao hugeuka wakawa na mikia
mirefu sana! Aliogopa mno!
“Sikujua Kama majini wanaweza
kujigeuza katika maumbile
yoyote wanayopenda, na hata
kuwa nyoka!” aliwaza.
“Labda hata yule nyoka wa baba
yangu naye alikuwa ni jinni…”
Alitafakari na kukumbuka mkasa
uliomsibu alipokuwa mdogo
sana, nyumbani kwa wazazi
wake, wakati alipokutana uso
kwa uso na kichwa cha joka
kubwa lililofugwa kwenye
chumba kimoja kwenye nyumba
ya baba yake, mzee Ilunga.
Aliwaza jinsi mvuvi mmoja
alivyompelekea baba yake nyoka
mdogo badala ya samaki
aliozowea kumpelekea siku zote,
na jinsi baba yake alivyoamua
kumchukua na kumfuga nyoka
huyo, aliyeonekana kuwa mzuri
na wa kupendeza! Mkutano wa
ghafla baina ya Kibwe na nyoka
huyo, ulikuwa siku ambapo
kijana yule alipovunja amri ya
baba yake na kufungua chumba
kimoja miongoni mwa vyumba
saba vya jumba la wazazi wake
alichokatazwa kukifungua. Tukio
hilo lilimtia kihoro kikubwa
kijana huyu kwa muda mrefu
sana!
Kwa zaidi ya miaka kama sita
hivi, Kibwe hakukumbuka mkasa
wa joka kubwa nyumbani kwa
wazazi wake, hadi wakati ule
alipowaona wale nyoka wa
kipekee katika msitu wa ajabu
kuelekea nchini Baharia.
Alikumbuka kuwa mara ya
mwisho alipowaona nyoka wa
kawaida lakini katika makundi,
walikuwa wa rangi mbalimbali,
yaani wenye rangirangi kama
ushanga uliotungwa kwa
mpangilio, wenye mistari ya
rangirangi mithili ya pundamilia,
wenye rangi mojamoja
zisizochanganywa kama vile
weusi, kijivu, kahawia, kijani
hudhurungi na wengine wengi
wa rangi nyingine mbalimbali,
wote wakijitokeza kwenye
ufukwe wa mito ya maji ambako
Kibwe alipitia, akihangaika
kumtafuta nyoka wa baba yake
aliyempoteza, aliyeitwa
‘Kunyenge.’ Wakati ule, kila
alipowaona nyoka wale, Kibwe
aliimba na kuwalilia wamsaidie
kumpata nyoka huyo, kwani baba
yake alimfukuza Kibwe nyumbani
kwao, akimwambia kuwa asirudi
bila nyoka wake!
Siku ile, Kibwe alikumbuka jinsi
alivyokuwa akimtafuta nyoka
huyo wa baba yake, jinsi
alivyotembea kwa masafa
marefu, akienda msitu na nyika
mguu nipe, na kila alipotokea
kando kando ya mito, kwenye
ufukwe wa bahari na maziwa ya
maji, akilia na kuimba kwa
maneno haya;
“Nyoka wa baba nyoka wa baba,
lawa nkuloleex2
Nkulolee! Nkulolee! Lawaa
Nkuloleee!”
Yaani aliita na kumuomba nyoka
wa baba yake atoke ili waonane.
Na wale nyoka waliojaa kando ya
maji nao walimjibu kwa kuimba
kwa maneno haya;
“Nakunyengapo nakunyengapo,
kawa Kunyenge!x2
Kunyengee! Kunyengee!
Kaliwaa na nyama!
Yaani nyoka hao walimjibu kuwa
kama huyo nyoka anayemtafuta
ni ‘Kunyenge,’ basi ajuwe kuwa
ameliwa na wanyama! Na kila
lipoambiwa hivyo, Kibwe alilia
sana, na kisha akaendelea na
safari yake ya kumtafuta
‘Kunyenge’, nyoka wa baba yake.
Kwa kuwa kijana yule alitembea
usiku na mchana akimsaka nyoka
huyo wa baba yake, alichoka
sana, na hatimaye alianguka,
akazirai na kupoteza fahamu.
Alipozinduka, alijikuta yuko
kwenye ule mji wa wala mawe,
kwa Bunga, ambako safari yake
ya kisiwa cha mazimwi pamoja
na ile ya Azarbajan, kwenye mji
wa majini chini ya bahari,
zilikoanzia. Alipokuwa chini ya
bahari, Kibwe alikumbuka sana
nyumbani kwao kwa mzee Ilunga
kwenye mkutano wa nchi tatu,
katika mji mdogo wenye
mazingira mazuri sana,
uliozungukwa na milima
iliyotiririka vijito vya maji,
yaliyomiminika kwenye mto
mkubwa na maarufu, Mto Mbezi!
Ingawa mto huo ulikuwa na
samaki wengi, lakini Kibwe
alikumbuka kuwa mto huo pia
ulikuwa ni makazi ya nyoka wa
aina mbalimbali.
Kwa kuwa baba yake Kibwe Mzee
Ilunga alipenda sana samaki, kila
siku mvuvi mmoja maalum
alimpelekea samaki wa
kitoweleo. Siku moja mvuvi huyo
alikosa samaki, na akabahatika
kuvua nyoka yule mdogo.
“Bwana wangu, seyidi yangu wee!
Leo sikupata samaki kabisa.
Katika uvuvi wangu wote, bali
siku ya leo nimejaaliwa kuvua
nyoka huyu mdogo. Kwa hakika
sielewi kwa nini imekuwa hivyo.”
Lakini yule mvuvi alishangaa
sana, kwani Mzee Ilunga hakujali
kabisa kuhusu hali ile
iliyojitokeza, na akasema
kumwambia yule mvuvi; “Kama
leo hii ulichoweza kuvua ni huyu
nyoka, basi huyuhuyu ndiyo riziki
yangu. Nitamchukua na
kumfuga!”Kwa hiyo mzee Ilunga
alipomfungia yule nyoka kwenye
chumba kimoja kati ya vyumba
vyake saba, hakuna aliyejua,
kwani jambo hilo alilifanya siri.
Siku moja baba yake Kibwe alitoa
onyo kwa familia yake,
Alipowaita ukumbini na
kuwaambia; “Nimewaita
kuwaeleza kuwa mnaweza
kufungua vyumba vyote sita
katika nyumba hii, lakini kamwe
msifungue kile chumba cha saba.
Lazima mzingatie jambo hilo!”
Kwa pamoja Kibwe na mama
yake wakasema, “Tutazingatia
jambo hilo bila
wasiwasi.Hatutafanya kinyume
na amri yako.” Kwa hiyo kila siku
mzee Ilunga alihakikisha kuwa
anapeleka chakula cha nyoka
yule kwa siri, katika chumba cha
saba. Alianza zoezi hilokwa
kumpelekea yule nyoka kuku
mmoja, na kisha kila alivyozidi
kukua nyoka yule, ndivyo idadi
ya kuku aliokula livyozidi
kuongezeka. Hatimae yule
akakuwa s mno, hadi akaanza
kupewa mbuzi mzima! Huyo
alikuwa ni nyoka mwenye
ukubwa wa kutisha mno!
Hata hivyo, Kibwe hakuridhika
kila alipoona kufuli ikining’inia
kwenye chumba alichokatazwa
kukifungua. “Sijui baba ameficha
nini mle ndani?” Kibwe aliwaza
mara kwa mara. “Siku moja baba
akisahau ufunguo wa chumba
hicho tu, lazima nitakifungua
nichungulie ndani!” Basi naam,
hiyo siku ilipowadia, kijana
Kibwe hakufanya ajizi, bali
haraka aliunyakua ule ufunguo
na moja kwa moja akaenda
kufungua kufuli ya chumba kile,
na kuingiza mguu wake, ili aone
hicho kilichofichwa! Lakini lo!
Mguu wake huo haukudiriki
kuingia mle ndani asilan, kwani
ulizuwiwa palepale kizingitini, na
kitu kilichojaa chumba chote! Na
alipoinua kichwa chake kuangalia
juu ili aone ni kitu gani hicho,
kilichojilundika mle ndani kama
matairi ya gari yaliyopangwa
moja juu ya jingine, Kibwe
alishituka na kutaka kukimbia!
Aliponyanyua kichwa juu,
alikutana na macho ya joka
kubwa lililokuwa na kichwa
kikubwa kama boga! CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Leo ni leo Kibwe! Ama zako ama
zangu! Utaona jinsi watoto
wapekepeke wanavyofanywa!
Kwa hiyo kwa sasa, ni bora
uingie ndani tu, maana ukitoka
nje umekufa, na hata ukiingia
ndani umekufa! Uchaguzi ni
wako. Nimetambua kuwa wewe
ni mtoto mtukutu sana, usiyesikia
makanyo ya wazazi wako. Leo
ndio utahakikisha kuwa asiyesikia
la mkuu huvunjika guu!” Joka lile
lilimfokea Kibwe. Halafu
likajigamba na kusema; “Mimi
ndiye nyoka ‘Kunyenge,’ na
kwetu, kwa baba na mama yangu
ni bahari ya kina kirefu. Kuanzia
hivi sasa naondoka kwenda
kwetu, na wewe Kibwe utajua
utakalomwambia baba yako!”
Kibwe hakuwa na la kujibu, bali
alisimama pale alipokuwa kama
aliyepigiliwa misumari, akizidi
kuogopa na kushangaa! “Sielewi
hata kidogo, sababu iliyomfanya
baba yangu kumfuga mnyama
huyu hatari nyumbani kwetu!”
aliwaza kijana yule, bila kupata
jibu. Alimshangaa baba yake
kwelikweli!
Wakati Kibwe akisimama pale
mlangoni huku akigwaya na
akimwangalia yule nyoka,
akitafakari na kubutwaika na
maajabu yale mbele yake, mara
upepo mkali ulizuka, ukavuma
kwa nguvu sana, hadi ukatingisha
paa la nyumba kama kwamba
litang’oka! Punde si punde,
Kibwe alipopepesa macho, na
kisha kuangalia chumbani kwa
huyo Kunyenge, akaona chumba
kimekuwa kitupu! Yule nyoka wa
ajabu alipotea ghafla na
kutoweka kimuujiza! Si hivyo tu,
bali mazingira aliyopotelea
yalikuwa ni ya kutisha, kwani
mpaka wakati ule, bado nyumba
ilikuwa ikitingishika kama
kwamba lilipita tetemeko la
ardhi. Jambo jingine ni kwamba
Kibwe hakujua atamwambia nini
baba yake kuhusu kupotea kwa
nyoka Kunyenge! “Baba
alinikataza kufungua hiki
chumba! Nitamwambia nini leo?”
Haraka alifunga kile chumba na
kurudisha ule ufunguo pale pale
alipouchukua!
Kibwe alihofu sana kuhusu jinsi
baba yake atakavyokasirika mara
atakapopata taarifa ya kupotea
kwa nyoka wake. Hofu hiyo
ilikamilika na kuongezeka wakati
mzee wake huyo aliporejea
nyumbani, na haraka kuutafuta
ufunguo wake aliousahau, na
kisha moja kwa moja
akaharakisha kwenda kule
chumbani kumwangalia nyoka
wake! Alipofungua mlango na
kumaizi kuwa kunyenge
hakuwamo mle chumbani, Ilunga
alibaki kinywa wazi kwa
mshangao! Hakuamini macho
yake kumkosa yule nyoka mle
ndani, jambo ambalo kwake
halikuwa la kawaida. Alisimama
pale mlangoni akiduwaa na
kuwaza ni kitu gani kimemtokea
nyoka wake! Kisha, hasira
zilimpanda pamoja na ghadhabu,
na mara moja akatoka na
kumwendea mwanae Kibwe,
ambaye ndiye pekee aliyekuwa
nyumbani wakati alipotoka na
kuusahau ufunguo wa chumba
cha Kunyenge.
“Hivi wee Kibwe, umempeleka
wapi nyoka wangu?”
Kibwe hakusema lolote, kwani
hakika hakujua nyoka huyo
alipokwenda.
Mzee yule alipaza sauti zaidi kwa
hasira na kusema; “Hivi mimi
nasema na nani? Si ninasema na
wewe Kibwe? Haraka sana
niambie ulichomfanya nyoka
wangu!”
Kimya tena!
Kibwe hakujibu.
Hapo ndipo mzee Ilunga alipozidi
kukasirika, na ndipo aliposema
maneno haya;
“Wewe ni mtoto mbaya sana
usiyesikia unayoambiwa na
wakubwa! Pamoja na kukukataza
kufungua kile chumba, wewe
umefanya hivyo hivyo
nilivyokukataza. Hivyo basi
kuanzia sasa toka hapa ndani,
uende ukamtafute nyoka wangu
na umlete hapa! Usipompata,
hakikisha na wewe unapotelea
huko huko!”
Kibwe aliduwaa na pia kushangaa
kusikia baba yake
anavyomthamini nyoka zaidi
yake. Alilia sana, na kumsihi baba
yake amsamehe kwa kosa hilo.
Mama yake Kibwe nae aliyelia
pamoja na mwanawe, na yeye pia
akamsihi sana mumewe
amsamehe mtoto wao.
“Achilia mbali hasira hizo mume
wangu! Utampoteza mwanao bila
sababu ya maana. Hivi aende
wapi kumtafuta huyo nyoka?
Kumbuka kuwa aliyepotea ni
nyoka tu, na huyu ni mwanao
Baba Kibwe! Tafadhali rudisha
moyo wako umsamehe!”
Baba yake Kibwe hakutaka
kusikia lolote, bali alishikilia uzi
uleule, akasema; “Mtoto akililia
wembe, mwachie umkate!
Lazima aende akamtafute nyoka
wangu na amrudishe hapa bila
kukosa.”
Kwa hiyo Kibwe hakuwa na la
kufanya, isipokuwa kufanya
safari ya kumtafuta nyoka wa
baba yake, ‘Kunyenge.’ Kabla ya
kuanza safari hiyo, mama yake
alimtayarishia mwanae mikate
saba ya kumimina ya kula njiani,
na akamfungashia guduria la maji
ya kunywa.
Naam, Ndipo Kibwe alipoanza
safari yake. Akitembea mchana
kutwa , na usiku akilala juu ya
miti, akimtafuta nyoka Kunyenge.
Kwa kuwa awali yule nyoka
alimwambia Kibwe kuwa
nyumbani kwa wazazi wake ni
chini kabisa ya bahari kuu, kila
alipofika kwenye bahari na mito
mikuu ambako nyoka
walionekana wakiota jua, Kibwe
alisimama na kuanza kumwita
nyoka wa baba yake, alilia
akimsihi kwa kuimba kwa
maneno haya;
“Nyoka wa baba nyoka wa babaa,
Lawa nkuloleee!x2
Nkuloleee! Nkuloleee! Lawaa
nkuloleee!”
Na nyoka wakamjibu kwa
maneno haya;
“Nakunyengapo, nakunyengapo!
Kawaa Kunyengeex2
Kunyengee! Kunyengee! Kawaa
Kunyengee!
Kaliwaa na nyamaa!”
Alipochoka sana kwa kazi nzito
ya kumtafuta yule nyoka,
alianguka, akazirai na kupoteza
fahamu kabisa! Alipozindukana,
hakukumbuka safari ya
kumtafuta ‘Kunyenge,’ bali
wakati ule ndipo alipokutana na
Bunga, akaambiwa kuwa yeye ni
Mteule atakaye inusuru dunia
kutokana na ukame, vifo na
uovu! Baada ya kutoka katika mji
wa majini wa chini ya bahari,
ambako majini huhatarisha
maisha ya watu kwa uchafuzi wa
hewa safi.
“Sijui hivi sasa ‘Kunyenge’ bado
yuko chini ya bahari au la!”
Kibwe aliwaza. Wakati ule Kijana
yule alimkumbuka sana mama
yake, na pia kujiuliza kama baba
yake alikuwa bado akimsubiri
nyoka wake ‘Kunyenge.’ Vilevile
alihisi kuwa labda yule
‘Kunyenge’ ni mmoja miongoni
mwa yale majini ya bahari, na
labda wale nyoka wengi
aliokutana nao, baadhi yao
walikuwa ni familia yake! “Bila
shaka Bunga atakuwa anaelewa
zaidi kuhusu habari hizi”
Aliwaza.
“Duh! Ama hakika kisa chako ni
cha kushangaza sana
mwenzangu!” Hanga alimshitua
kutoka kwenye mawazo yale, na
hapo Kibwe akamaizi kuwa
kumbe alikuwa ameshamaliza
kumsimulia mwenzake kile kisa
chake.
Aliguna na kutikisa kichwa.
“Ama hakika sikujua kuwa kule
kutoka kumtafuta nyoka wa baba,
ndio ulikuwa wito wangu wa
kutoka kuja kwenye hii safari ya
kuinusiri dunia!” Alisema kwa
mastaajabu.
Kimya kilipita kidogo baina yao,
kisha Hanga akauliza.
“Sasa nini kinafuata Kibwe.
Ulisema kuwa muda
unavyokwenda ndio dunia
inateketea…tunaendeleaje
kutokea hapa?”
“Ni kweli. Kwanza mahali hapa
tulipo pana uovu mkubwa
ulioniandama kila nilipokwenda
na unaoendelea kuniandama,
kwa nia ya kufifiza jitihada za
kuwanusuru raia wa nchi ya
Azarbajan, kutokana na hewa
hatari inayowageuza mawe ya
theluji! Mwana yule Mteule
alimjibu mwenzake.
“Kwa hiyo haraka tuongozane
kwenye milima pacha
nilikoazimia kufika, ili
nikakamilishe jukumu hilo!”
Kibwe alizidi kumwambia
mwenzake.
Kwahiyo kwa pamoja vijana wale
walishikana mikono na kutimua
mbio! Wakati ule, Hanga alikuwa
akitafakari maneno ya Kibwe
yaliyomfanya abutwaike kidogo!
Nchi ya Azarbajan?
Mbona ni nchi inayopakana na
Hazina ambako ni Milki ya baba
yake Sultani Hazari bin Basari?
Kama jirani zao tayari
wamekwisha kumbwa na janga la
kugeuzwa mawe, bila shaka hata
nchi yao iko hatarini! CHANZO:
https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nina kila sababu ya kumsaidia
mwenzangu huyu kutatatua tatizo
hilo!” Hanga aliwaza bila kusema
lolote kwa Kibwe.
Kibwe na Hanga waliongozana
wakitoka mle pangoni kwa
kupitia mlango wa pili wa pango
kwenye sehemu aliyoingilia
Kibwe. Pale mlangoni ilining’inia
mizizi iliyotokana na miti
mikubwa mno na yaajabu,
iliyounda msitu mnene, ‘Msitu
wa Kindumbwe,’uliotanda kila
upande wa majabali.
“Kamata madhubuti mzizi mmoja
na ujishikize ili uweze kubembea
na kujirusha kwenye uleee
mwamba unaoonekana mbele
yetu.” Kibwe alimfahamisha
mwenzake, akimwambia kuwa
watakapofika pale mwambani,
anatarajia kukuta ngazi za mawe
zinazoelekea chini ya minara
pacha.
ITAENDELEA
 
Sehemu Ya Nne (4)

“Kwa kuwa huku tuliko ni juusana kwa urefu wa zaidi yakilometa elfu moja, hatuatunayoichukua ni ya hatari mno,kwani kama tutaanguka, huendaama tukafikia juu ya jabali lenyemawe makali ya kukata, nakupoteza maisha yetu, autukaangukia kwenye mchangadidimizi na kuzama humo!” Alisisitiza Kibwe, wakati Hangaakionesha sura ya hofu. Kwakuwa alifahamu kwambamwenzake alikuwa ni mteule,alijuwa wazi kuwa atakayekuwahatarini zaidi ni yeye!

Kwa moyo mzito sana Hangaaliukamata mzizi mnenealioamini kuwa ungembeba bilakumbwaga chini. Aliuvutavutakuhakikisha uimara wake, nakisha akabembea kwa nguvu zakezote, akilenga kufikia kwenyemwamba alioambiwa namwenzake. Kwa bahati,alifanikiwa kujikita katika eneotambarare la mwamba uliokuambele yake. Alitulia kwa dakikakama tano hivi, moyo ukiendakasi kupita kiasi, kwa kazi yakubembea na kujirusha hadikufika pale mwambani, na piakwa woga na hofu!

Alimshukuru Mungu wake kwa kumsaidiakufika mahali pale salamasalimini. Muda mchache baadae,Kibwe naye aliwasili mahali palekwa njia ileile aliyoitumia Hanga.Kwa pamoja huku wakiwa hoi,walianza kupanda juu zaidi ya ulemwamba wakielekea kwenyekilele cha uwanda, mahaliambapo ni karibu zaidi naminara pacha.“Kibwe! Kibwe! Nyuma yetu kunamtu anatufuata….!” Hangaalisema kwa hofu, akiwa ametoamacho kungalia upandealikoelekeza kidole chake. Kibwealigeuka haraka!

Lakini kwa jinsimsitu ulivyofunga haikuwa rahisikuona hata hatua kumi mbeleyao.“Hata mimi nahisi kama kunawatu wanatufuata lakini usijali.Tuendelee na safari yetu na walatusigeuke nyuma!” Kibwe alisemahuku akimkokota mwenzake. Mara kwa mara wale vijanawaliona vivuli kama watu,vilivyopotea hata kabla hawajatambua kama vilikuwa nivivuli vya watu, majini auvibwengo!Wakiwa na hofu kubwa, vijanawale waliendelea moja kwa mojana safari yao, kwa mashaka nataabu, wakipanda jabalilililokuwa na mawe makaliyaliyowachubua chubua mikonoyao magoti na miguu, hadiwalipofika juu kabisa ya uwanda.

Kwa furaha kubwa, hukowaliiona ile minara pacha mitatu,iliyosimikwa kamamafiga….iliyokuwa mirefu kupitakiasi!“Lazima nifike juu kabisa ya vilevilele vya minara ili niwezekusimama juu ya kigoda chadhahabu, ambako nitawezakuelekeza upanga wangu wa radijuu zaidi kwenye angahewa yachini.” Kibwe alimwambiamwenzake, ambaye alimsikilizamteule yule kwa makini.“Kwa kufanya hivyo unakusudianini?” Alidodosa Hanga, kwaniyeye alielekeza imani yake yotekwa Kibwe, aliyeonesha maajabuya kusoma maandiko kamamichoro tu, isiyoeleweka namwanadamu wa kawaida.“Upanga huu utakapotoa chechezitauathiri moshi wa vichafuzivya hewa ya Ozoni, ambayondiyo inayowadhuru raia waAzarbajan kwa kuwageuza maweya theluji!”Kusikia vile Hanga aliduwaa!

Ingawa Azarbajani ni nchiiliyopakana na nchi yake yaHazina, lakini hakufahamu kamakatika pwani ya nchi hiyo, raiawengi walikuwa wakiteketezwakwa moshi wa ajabu! Mara nyingiHanga hakuwa mfuatiliaji wamambo kama yale.“Lo! Bila shaka hayo ndiyosehemu ya madhara tuliyotahadharishwa katika ujumbe ulemaalum kwenye vidani vyasanamu za fedha ya kucha zaSimba zinazoning’inia kwenyemkufu shingoni mwa sanamu lashaba la kichwa chaSimba!”

Kijana yule aliwaza kwamshangao, huku akipata jibukuwa ni yule mwenzake mteuleatakayesaidia kutatua tatizo lilehatari, pamoja na matatizomengine makubwa zaidi.Alitambua pia kuwa msaadawake yeye pamoja na msaada wavijana wengine kama wao, naoulihitajika mno. Alitulia tuli, ilikuona jinsi Kibwe atakavyowezakufika kule juu ya minara pacha,mahali penye urefu wa zaidi yakilometa alfu nne, palipoonekana kama kwamba pamepakana nambingu!

Lakini kufumba nakufumbua baada ya Kibwekukusanya nguvu kule chini yaminara pacha, aliweza kujirushana kuelea hewani kama Kipanga,akapaa juu kabisa hadi kileleni,na aliponyoosha upanga wakekuuelekeza mbinguni, chechezilianza kutoka na kusababishamoto uliozingira sehemu kubwaya anga hewa ya chini, ilikofikahewa ya vichafuzi kutoka kwenyemaabara ya majini nchiniBaharia!Hanga hakuwa na la kusema balialiduwaa tu!“Haya ni maajabu makubwa!”Aliwaza.

BAADA YA DHIKI FARAJA.Muda mfupi baadae Hangaalimuona Kibwe akishuka tenaardhini kama jinsi kipangaashukavyo, na kutua kwa ustadimkubwa.“Kazi imekamilika Hanga…kamamaelekezo niliyopewa yatakuwasahihi, na sina sababu ya kuaminivinginevyo, basi tatizo la hewachafuzi kule nchini Azarbajanlitakuwa limekomea hapa!”Kibwe alisema kwa ushindi.“Kweli?”

Hanga aliuliza si kwakutoamini, bali kw akutaka tukujithibitishia tena kuwa hakikapale alikuwa amesimama begakwa bega na mwana mteule.“Twen’zetu Azarbajantukajihakikishie…” Kibwealimwambia, na kwa pamojavijana wale waliendelea na safariyao hadi ufukwe wa nchi yaAzarbajan kwa Mfalme Kashkash,ambako eneo lote lilikuwa na ilemitumbwi iliyopakia wavuviwaliopambana na janga la hewanzito, iliyowagandisha nakuwageuza masanamu ya maweya theluji isiyoyeyuka.Kibwe alishuhudia pia mlolongowa masanamu ya theluji yawanawake na wazee paleufukweni.“Heh! Mbona hali bado ni mbayavile vile Kibwe?”

Hanga aliulizakwa hamaniko.Kibwe hakujibu. Alibakiakiitazama hali ile kwa masikitikomakubwa sana.Alijua kuwa kutokana na kilekitendo cha kuulenga upangawake wa radi na kuutingisha juuya anga hewa ya chini akiwakwenye kigoda cha dhahabukwenye milima pacha mitatukama alivyoelekezwa na Mzee waBusara, kitendo kilichosababishakutokea kwa cheche za motozilizozusha kwenye angahewa ile,na vienge vilivyotoa mvukeulioelekezwa kwa wale wotewaliogeuka mawe ya theluji,theluji ingeanza kuyeyuka namaji yangeanza kuchuruzikaardhini.“Sasa mbona…”

Alianza kuwaza.Na hata pale walipokuwawakiitazama hali ile, wale vijanawaliwashuhudia wale watuwakianza kuamka. Wote wakatoachafya wakati mmoja, kuashiriauzima wao! Bila kukumbukamkasa uliowasibu, wote walianzakutawanyika kama vile kila kitukilikuwa ni kawaida tu! Nchi yoteilichangamka kutokana nakupishana kwa wavuvi wengikatika maeneo ya Ufukweni!Hanga aliangalia maajabu yalebila kutia neno!Kilichotokea ni kwamba hewa yajoto kutoka kwenye vienge vyamoto wa upanga wa radi, ilieleakutoka kwenye milima pacha nakupanda juu kwenye anga hewaya chini, na huko ikapambana nahewa ya Ozoni, ambayo ilianzakuyeyuka na mzizimo wakekupungua, wakati vichafuzi vyahewa kutoka chini ya bahari kwakina Makatta wa Makattani,navyo vilipopungua taratibu, nakisha kutoweka kabisa!

Tatizo lahewa ya mzizimo ya kugandishaviumbe likakomea hapo!Siku hiyo Sultani KashKashalifurahi sana akamshukuruKibwe kwa msaada wake wotealioutoa kwa raia wake,akishirikiana na mwenziyeHanga.“Lazima kesho tusheherekeepamoja kwa chakula na vinywaji,kwani hakika mnastahilikupongezwa mno!”Kibwe alipokea shukurani zilekutoka kwa Sultani kwaniaba yamwenzake Hanga, nayeyeakamshukuru sana mtawala yulewa Azarbajan kwa mwaliko wakekwao.

Siku iliyofuata, mjumbe wajumba la Mfalme alipiga mbiu yamgambo, ambayo hupigwa amawakati wa karaha, au raha! Kablakijumbe huyo kuanza tangazolake, alipiga goma lake alilolibebakifuani, na kisha ndipoalipotangaza kutangaza; “Lamgambooo! La mgambooo!Likilia lina jambo! La mgambooo!La mgambooo! Asiye mwanaaeleke jiwe! Wanachi wotemnatangaziwa na Mfalme kuwakesho wote mjumuike pamojakwenye uwanja wa sanaa, ilikusheherekea kupatikanaufumbuzi wa tatizo la hewahatari iliyowageuza mawe yatheluji raia wan chi hii! Kesho,kijana shujaa aliyetufikia kwetuna utatuzi wa tatizo hilo, kibwe,atatunukiwa tuzo ya ushujaa yakaskazini ya mbali ya dunia!

Lamgambooo! Wote mnatakiwakuhudhuria!” Mjumbe yulealikamilisha tangazo lake kwakulipiga piga goma lake.Ama kwa hakika ile shereheilifana mno, na watu walikulawakasaza, na wakanywa mvinyona togwa safi nyingi sana!Mwishowe, Mfalme KashKashakamkabidhi kibwe tuzo ya ainayake, ya sanamu la kijanaaliyeshika upanga, iliyochongwakwa dhahabu tupu! Siku hiyoilikuwa ni siku ya furaha kubwakwa Kibwe, na kwa raia wa palena Mfalme wao. Hatimae baadaya tafrija ile ya kihistoria, kijanayule na mwenzake waliagana nawatu wote pamoja na mtawalawao, wakiwaambia kuwawalikuwa na jukumu jinginekubwa kule mashariki ya katikatiya dunia.

“Huko kuna shida kubwa ya maji,na nahofia kuwa katika sikuchache zijazo, binti Sultani wanchi ya majabali atakuwa hatarinikutolewa mhanga!” Kibwealimwambia Sultani Kashkash, naalipotakiwa kutoa maelezo zaidi,alijibu kuwa hafahamu zaidikuhusu habari hiyo, kwani yeyehupewa muhtasari tu, wamatukio, na wale wanaomwelekeza kufanya kazi hiyo.Kwa furaha na shukurani kubwaaliyokuwa nayo MfalmeKashKash, aliandaa merikebukubwa yenye wahudumu wakutosha, kwa ajili ya usafiri waakina Kibwe, kuwapeleka kulemashariki ya katikati ya dunia, iliaendelee na majukumu mengineya huduma kwa watu.“Ndani ya merikebu hii vipovyakula vya kila aina, vitakavyowasaidia njiani.

Zipo chapati,yapo maandazi, kuna visheti nabajia, pia zipo jelebi, katlesi nakachori,” Mfalme alimwambiaKibwe, akiongezea kuwa humopia kuna nyama zilizoandaliwakwa mapishi tofauti, kama vilenyama ya kubanika, nyama yakukaanga, nyama ya kuchemsha,ikiwa ni pamoja na nyama yakuku, nyama ya mbuzi na pianyama ya ng’ombe! Mfalmealiazimia kumfurahisha Kibwekwa ushujaa wake!Mfalme yule alimwambia Kibwekuwa kwenye merikebu ilewalikuwemo manahodha hodarisana, na wahudumu watiifukabisa. Kibwe alifurahia ukarimuwa mfalme.“Sijui niseme nini mtukufuMfalme kwa ukarimu wote huuunaonionyesha.

Nakushukurusana kwa yote.” Kibwe alisemakwa dhati na kwa unyenyekevukabisa. Kijana yule shujaa na yulerafikiye mwaminifu Hanga,walisindikizwa na raia waAzarbajan kwa shangwe nahoihoi hadi bandarini, na kulewakaagana kwa upendo mkubwa,na kisha merikebu ikaanza safarinyingine ya ajabu ya Kibwe,kumuokoa Bhaduri binti SultaniBashar wa Mashariki ya mbali yadunia!Walisindikizwa na raia wa Azarbajan kwa shangwe nahoihoi hadi bandarini, na kulewakaagana kwa upendo mkubwa,na kisha merikebu ikaanza safarinyingine ya ajabu ya Kibwe, kumuokoa Bhaduri binti SultaniBashar wa Mashariki ya mbali yadunia!Merikebu ya Mfalme KashKashiliyoyoma usiku na mchana, nahali ya bahari ilikuwa shwarikabisa, kwa muda wote huo.“Tuna bahati kubwa, kwanimpaka sasa bado hali ni shwarisana.” Hanga alimwambiamwenzake Kibwe.

“Kwa kawaidamimi hutapika sana baharini,lakini leo niko salama kabisa,”Alieleza. Kibwe alimwambiakuwa kwa kuwa bado safari nindefu asijiamini sana. Kwamaneno hayo, wote wawiliwalicheka kwa pamoja. Meli hiyoiliyowabeba vijana hao wawili,wahudumu wakutosha wa melina manahodha, ilizidi kuyoyomahadi kufika katikati ya bahari,halafu jambo la ajabu likatokea!Ile meli ilisimama ghafla, kamakwamba ilinasa mahali. Kibwealipomuuliza nahodha aliyekuwakwenye usukani ni ninikilichotokea, akajibiwa kuwahakuelewa ni ninikimeikwamisha meli yao.“Huenda majani ya mwaniyamenasa kwenye pangaboilinalozungusha maji huko chiniya meli,” alisema nahodha.

Alipoambiwa hivyo kijana yulealijitolea kwenda kuangalia kulechini ya meli, ingawa wenzakewalimzuia sana.“Ni hatari kwenda peke yako.Labda tufuatane pamoja .” Hangana baadhi ya wahudumu wandani ya meli walimwambia.Ingawa Kibwe alipinga kufuatananao, lakini wenzake walishikiliatu, hadi yule kijana akakubaliwaende wote.Naam, karibu watu wannewalishuka na kuogelea kwendachini ya ile merikebu, kuangaliahicho kilichonasa kwenyepangaboi la meli yao. Wotewaliogelea, na Kibwe alikuwambele zaidi, hivyo alitanguliakuwasili pale lilipokuwa hilopangaboi. Lakini lo! Pangaboilenyewe lilikuwa limeshikiliwamadhubuti na mtu mmojamwembamba kupita kiasi, namrefu kuliko utakavyofikiria!Macho ya mtu yule yalikuwapembeni mwa sura yake,iliyofanana na chura!“Ahaa! Kumbe! Tunakutana tenasiyo?”

Kibwe aliwaza, na bilakupoteza muda, na haraka kamamwendo wa mshale, kijana yulealitoa rungu lililokuwa kwenyemfuko alioubeba mgongoni, nakulirusha kwa nguvu zake zote,kumtupia yule mtu wa ajabu,akilenga ule mkono ulioshikilialile panga boi! Kwa kishindokikubwa, lile rungu likamfikiakwenye mkono wake huo, napalepale akaachia lile panga boi,na kama umeme, akapoteleachini kabisa ya bahari!Naam kwa mara nyingine, Kibwealikutana na mmoja kati ya jamiiya majini wa bahari, jamaa zake‘Makatta wa Makattani.’

Wakatihayo yakitokea, wenzake wenginewaliokuwa wakija kuangalia chiniya merikebu, walifika nakumkosa yule jini wa bahari kwasekunde tu!“Kwani kuna nini?” waliuliza, nawakati huohuo, ile meli ikawainasogea mbele!“Ilikuwa ni mwani tu, ulioshikiliapangaboi! Nimekwisha uondoa ,na ndio maana mnaona meliinaondoka. Twendeni tuwahi!”Kibwe alidanganya, akicheleakuwatia hofu watu na hadithi zamajini wa bahari! Wotewakarejea melini, na kuendeleana safari.

Kibwe na wenzake waliendeleana safari yao huko mashariki yakatikati ya dunia, kwenyemajabali yaliyouzingira mtomkubwa wa maji, mto Sakara,ambako Bhaduri binti Sultanikitinda mimba na mwana wasaba wa Sultani Bashar, alikuwaameketi juu ya uwanda wa jabalimoja, akisubiri kutolewa kafara! Kwa moyo wa ushujaa, na utiifukwa amri ya baba yake, mrembo Bhaduri binti Sultani aliketi juuya jabali kwenye kiti kimojakizuri cha enzi, akiwaamepambwa kwa sundusi zahariri, mikufu, hereni na vikukuvya dhahabu na vito vyathamani, huku akinukia utulimchanganyiko kama udi, miskina ambari, akisubiri wakati wakewa kuchukuliwa na hichokitakachokuja kumchukua!Kibwe na msafara wake ndani yamerikebu yao ya fahari,waliyoyoma kuelekea hukomashariki ya katikati ya dunia,wakati huo zikiwa zimebaki sikuchache tu, kuwasili mwisho wasafari yao.

Usiku mmojaalipokuwa amelala na mwenzakeHanga kwenye chumba chao,Kibwe alimuota Bunga, akimpamaelekezo ya safari yao hiyo.“Lazima msafara huu usitishweharaka iwezekanavyo, mara tumtakapowasili kwenye bandariyoyote ya jirani,” alisema Bunga.Aliendelea kumwambia kuwaitabidi wasubiri kwenye bandarihiyo kwa siku mbili zaidi, kablaya kuanza tena safari yao. “Katikamuda huo mtakapo kuwamkisubiri kwenye bandari hiyo,mtakuwa mmejinusuru na hatariya kupambana na mwamba wabarafu majini, na piamtanusurika na tufani kubwaitakayotokea mnamo saa ishirinina nne zijazo.” Kibwe alimsikilizaBunga, aliyeonekana akieleahewani kama ndege, na manenoyake yakisikika kwa kukatikakatika, kwa sentensizisizokamilika!Ndotoni Kibwe alikuwaakimcheka Bunga, naakimshangaa sana kwani kwamara hii alimuona ni wa ajabukabisa. Hakuamini maneno yakehata kidogo, “Usinitanie mzeeBunga! Unajua kwamba msafarahuu lazima uwahi nchini Shamsimashariki ya kati kati. Sasambona unatakakutuchelewesha?” Kibwe alianzakulumbana na kile kijitu chaajabu.

“Tutaendelea tu……..na-safa-”Lakini kabla hajamaliziamaneno yake, Kibwe akaonaukuta uliokuwa mbele yakeukipasuka, na maji mengiyakianza kumwagika kamamafuriko, na kumzoa Kibwekutoka pale alipokuwa, akajikutaakitapatapa kujinusuru asizame!Ingawa alikuwa anajitahidikuogelea, lakini alishindwa, nahivyo akaanza kuzama---!Akazama—akienda moja kwamoja hadi chini kabisa ya dimbwila maji---! Pumzi zikamwishiakabisa! Halafu ghafla, akajiibuajuu, na kutoa kichwa chake nje yadimbwi la maji, na kisha palepaleakasituka na kuamka, huku moyowake ukienda kwa kasi mno!Aliinuka na kuketi kitako, akiwaanapumua haraka haraka mno!Mwenzake Hanga aliyekuwakaribu yake, naye aliamka nakumuona Kibwe akiwa katika haliisiyo ya kawaida.

“Vipi kibwe,mbona uko hivyo, umeota ndotombaya nini?” Kimya! Kibwehakujibu kitu, bali alizidikupumua kwa haraka haraka,huku macho yake yakiangaliambele zaidi ya pale alipokuwamwenzake, kama kwambahakumuona wala kumsikiaHanga! Haraka Hanga alichukuagilasi ya maji na kumpamwenzake huyo anywe, akihisihuenda akajisikia nafuu kidogo.”Hebu kunywa maji kidoga, labdayatakusaidia.” Kibwe aliyapokeayale maji bila kumwangaliamwenzake, na akanywa fundambili, na halafu akajilazakitandani. “Unajisikiaje hivi sasaKibwe? Ni ndoto gani uliyoota?”Hanga aliuliza, akiwa na wasiwasina jinsi alivyomuona mwenzake.

Kibwe alikohoa kidogo, na kishaakaanza kuongea.“Nadhani huko mbele kuna tatizokubwa sana. Nimeota kuwakutakuwa na kimbunga kikubwa,na meli yetu itapambana namwamba wa barafu majini,”Kibwe alimwambia mwenzake,ambaye alimshangaa,akimwambia kuwa alichokionakilikuwa ndotoni tu, wala silazima kitokee. Lakini Kibwehakumsikiliza Hanga, balialiendelea kusema. “Kamahatukusitisha safari yetu kwenyebandari yoyote ya karibu angalaukwa siku moja na nusu hadihatari hiyo ipite, wote tutapotezamaisha yetu.” Hee!

Hangaakaduwaa akimwangaliamwenzake huyoaliyechanganyikiwa, au tusemevile alivyoamini Hanga kwawakati ule. Iweje tena jambo landotoni, Kibwe akalichukuliakuwa ni jambo kubwa na halisia?Hanga alijaribu kuzungumza namwenzake akimsihi ajaribukutulia tu, na atasahau kuhusundoto yake. “Na hata hivyo,unadhani kuwa utaeleweka kwamanahodha utakapowaambiawasitishe safari kwa kuwa uliotakuwa mbele kuna hatari? Jaribukufikiri vizuri Kibwe.” Kibwealishikilia palepale, akimwambiaHanga kuwa lazima manahodhawamwelewe, ama sivyo, wotewamo hatarini!Kwa hiyo, Hanga na Kibwewalikwenda hadi kwenyechumba cha manahodha, nakuwaelezea kuhusu hatari iliyokombele. “Lazima tusitishe huumsafara, mara tu tutakapofikabandari ndogo ya karibu, kablaya kuelekea nchini Shamsi, amasivyo, wote tutateketea.”

Kibwealiwasihi wale manahodha, bilakuwa na uthibitisho wa kutoshawa hoja yake hiyo. Manahodhawakamuona kuwa anafanya utototu, hivyo kwa kebehi,wakamwambia; “Hivi unadhanikuwa katika maisha yetu kwenyekazi hii, tungekuwa tunaaminikila tulichokiota, tungewezakufanya safari kama hizi? Kijana,kumbuka kuwa ndoto ni ndototu. Hatuwezi kuacha kusafiri, etikwa kuwa mtu mmoja miongonimwetu ameota kuwa mbele kunahatari!” Pia manahodha walewalisema kuwa kulikuwa naumuhimu wa kuwahi kufika kulewaendako, ili waweze kugeuzamerikebu yao na kurudi makwao,baada ya kumsindikiza Kibwe.“Lakini jamani, mmejiuliza kuwahuenda kuna ukweli kwenyemaneno ya kijana huyu?” Baadhiya wahudumu wa meli walihoji,wakinong’ona chinichini.

“Kwelieti! Na labda tukiyadharaumaneno yake hayo, tutakujakujuta yatakapotokea hayoanayoyatabiri!” Wahudumu wameli walisema hivyo, hukuwenzao wengine wakihofu sana,walipokisia kuwa huenda kukawana ukweli kwenye hoja ya yulekijana. ”Ndiyo kusema kuwawote tutakuwa hatarini!”waliambiana. Hata hivyo wenginemiongoni mwa wahudumu walewaliowaunga mkono manahodhana hoja zao, wakasema kuwayule kijana aliota tu, na walahakuletewa onyo rasmi lakimazingaombwe kutoka kokote.“Haya jamani na tuendelee nasafari yetu, na tuachane namawazo ya kishirikina!” walisemawahudumu hao, wakiwahimizamanahodha wasipoteze muda.

Lakini lo! Laiti kama wangejua!Haya, safari ikaendelea kamailivyoamuliwa, na hakunaaliyejuwa kuhusu mkasa ambaoungetokea mnamo saa ishirini nanne zijazo! Kilometa kadhaakutoka pale walipokuwa, kwenyemwamba mkubwa sana wabarafu majini, pande moja kubwala barafu lilijigawa kutokakwenye mwamba huo mkubwawa barafu majini, uliokuwa kamamlima mkubwa sana! Sehemuhiyo ya mwamba iliyotandabaharini, ilikuwa ikielea nakusukasuka kuelekea kuleilikokua merikebu ya mfalmeKashKash, walimokuwemo Kibwena abiria wengine! Wakatihuohuo, mawingu mazito nameusi yakawa yanajikusanya, nahivyo giza nene likaanza kutanda.

Upepo nao ukaanza kuchanganyakasi ya mwendo wake,iliyoongezeka kwa kila dakika, nakuvuma kwa kuvuruga mawimbiya bahari, yaliyonyanyuliwa juukwa urefu mkubwa wakustaajabisha, kwani kimbunganacho kilikwishaanza! Lahaula!Huko kulikokuwa kukijiandaakatika hali hiyo, ndiko ilikokuwaikielekea merikebu iliyowabebakina Kibwe na wenzake!Merikebu ile ilisafiri kwakilometa nyingi humo baharini,na wakati wote huo, Kibwe akiwana wasiwasi mkubwa, kwanialiamini kabisa kuwa huko mbelesio kuzuri.

“Nafahamu kuwaBunga hawezi kutokea waziwaziili kutuonya kuhusu hatari hiyo,maana watu wote watashangaana pia kuhofu sana, marawatakapomuona,” Kibwe aliwaza.Lakini kwa bahati mbaya, ilibidikijana yule asubiri hatari hiyoifike, kwani hakuwa na lakufanya! “Haya. Liwalo naliwe!”alijiambia.Mnamo majira ya saa kumi nambili asubuhi, abiria ndani yamerikebu ile wakaona hali yahewa ikibadilika. Upepo ukawaunavuma kwa kasi na kwa hasira,huku bahari ikianza kuchafuka.Maji ya mawimbi yaliyokuwayakijitupia na kupiga pembezonimwa merikebu, yaliingia sitahanikwa wingi mno! Chini kabisa yasitaha humo melini, nako kuilijaamaji tele!

Kufikia hatua hiyo,abiria wote wakaanzakuhamanika, wakitoka vyumbanimwao ili kujiunga na wenzao,kuona jinsi hali ile iliyojitokeza,ilivyoashiria kuhatarisha maishayao. “Haya sasa, tuone kamahakuna atakaye amini manenoyangu,” Kibwe alimwambiamwenzake Hanga, aliyekuwaametowa macho pimaakimshangaa Kibwe kwa kuyajuayote yale mapema! Ah! Laitikama watu wangemuamini nandoto yake! Mawazo hayoyalikuwa yakipita kichwani mwaHanga. “Naam! Utabiri wa Bungaumeanza kuwa kweli!” Kibwealiwaza, huku akiangalia jinsiwalivyokuwa wamezingirwa namaji mle merikebuni.“Haraka kawaambie abiriawaliokuwa chini ya stahawaondoke na kuja juu zaidi!

Nawa huku juu wawe waangalifuwasisogee pembezoni mwa meli!”Mmoja kati ya manahodhaaliwaambia wenzake. “Lo!Kumbe yule kijana alisema kwelikabisa.” Manahodha walewaliambizana, huku wakikimbiakwenda kuwatahadharisha abiriakule walikokusanyika. Hukowaliwakuta baadhi ya abiriawakiwa wamejeruhiwa kwakukimbia kutoka vyumbanimwao, wakitafuta nusura sehemuambazo maji hayakufika.Wengiwao walikuwa wakianguka nakutereza mara kwa mara, kwaniile merikebu ilikuwa ikisukasukakwa kusukumwa na mawimbi.Kila ilipoegemea upande mmoja,merikebu hiyo iliwamwaga abiriakwa upande huo! “Kwa hakikamaneno yako yalikuwa sahihikibwe.

Leo wote tuko hatarini!”Hanga alimwambia mwenzake ,wakati walipokuwa wakijishikizakwenye nguzo za ile meli, iliwasiteleze na kuangukia sehemunyingine hatari zaidi. “Ndio hivyotena. Lakini haina haja kuliliamaji yaliyomwagika, kwani sirahisi kuyazoa,” alisema Kibwe.“Iliyobaki ni kuomba Munguatuvushe salama kutokana najanga hili.”Ile merikebu ilikwisha potezamwelekeo wa mwendo wake,kwani injini ilikwisha zimika.Abiria walijishikiza mle ndaniwakisubiri maajabu tu yatokee.Wakati ule wakisukasuka na meliyao kwa msukumo wa mawimbi,ghafla , Hanga akapiga ukulele,akionyesha kidole kwenye upeowa macho yake.

“Jamani, hebuangalieni kule!” Wote wakageukiakule alikoangalia kijana huyo. Lo!Si taharuki hiyo iliyowapata!Waliona pandikizi la barafulililokua kubwa kupita kiasi,likielea na kuelekea kulewalikokuwa wao! Abiria wotewakaanza kulalama kwa hofu.“Sasa tutafanyaje jamani?Manahodha, hebu jitahidinikufufua injini tuondoke!” Walitoawazo hilo bila kufikiri, maanawalifahamu fika kuwa tanguhapo awali, injini ya meli ileilishindikana kabisa kuwaka. Nawakati wakilalama, waliuona ulemwamba wa barafu ukiwaendeakwa kasi sana. Wote wakapigakelele kwa pamoja “ Mungu weewa mbingu na ardhi! Tusaidiewaja wako sisi!”

Walitafutamahali pa kukimbilia lakinihawakupaona. Wakaenda hukuna huko, ingawa walipofanya vilewalijiweka kwenye hatari yakuanguka na kukanyagana,maana ile merikebu ilikuwaikisuwa suwa kila upande! “Tulieni mahali pamoja jamani,mkienda huku na huko,mtaumizana!” Manahodhawaliwaonya abiria wao, ambaohawakuwasikiliza hata kidogo

Kibwe alinyamaza kimya akiwaza, kwani miongoni mwa watu wotewaliokuwa ndani ya merikebuile, ni yeye peke yake aliyekuaanaelewa kinachoendelea. Alifahamu fika kwamba baharinikulikuwa na majini ambaoingawa baadhi yao walikuwa niwema, lakini wengine hawakuwana nia njema na binaadamu.Alikumbuka jinsi jini Makatta nawenzake walivyowezakuyadhibiti mawimbi ya bahari.“Sijui majini hao watakuwawamechangia vipi katika jangahili mbele yetu!” Kibwe aliwaza.

Lakini muda si muda wakatiKibwe akitafakari kuhusu yotehayo, ghafla ile merikebu yaoikapigwa kumbo na mwamba wabarafu baharini! Lilikuwa nikumbo kubwa mno, kiasikwamba merikebu ileiligawanyika vipande viwili, naabiria wakagawanyika sehemutatu! Huku kelele na mayowevikitawala anga ile ya eneo latukio, baadhi ya abiriawaliporomoka na kuangukiabaharini, wakawa wanatapatapakujinusuru wasife maji, wenginewakawa wanashikilia vipandevya mbao zilizobomoka kutokamerikebuni, na wenginewalikuwa katika mabaki ya ilemerikebu, lakini wakieleakwenye maji yaliyojaa mle ndani!Kibwe alikuwa miongoni mwawale walioangukia baharini, na Hanga akawa ananing’inia,akijishikiza kwenye nguzo yamerikebu, na kuponeachupuchupu kuangukia majini!

Hata hivyo, hakunusurika kwamuda mrefu, kwani kwa maranyingine, mwamba mwingine wabarafu uliokuwa ukiwajia,ukayakumba yale mabaki yamerikebu na kuwabwaga watuwaliokuwa ndani ya chombo kile,na wale waliokuwa wakining’iniakwenye nguzo na mbao, akiwemoHanga! “Mama wee! Tunakufa leojamani!” Kelele zilisikika, nawengine walilia kwa zogo, bilakusema lolote!Wengi miongoni mwa abiriawalioangukia bahariniwalijitahidi kuogelea ilikujinusuru na kuzama, lakiniwapi! Wengi walikufa maji!Kibwe naye akawa anazama chiniya maji, na kama vile yukondotoni, akajihisi akizidi kwendachini bila kizuizi, kwani wakatiwa zile heka heka za vikumbovya miamba ya barafu, Kibwe alijigonga kichwani na kitukisichojulikana na kupotezafahamu.

Kwa hiyo alivyokuwaanazama, alikwenda moja kwamoja……akaenda! Akaenda! Hadiakafika mbali mno chini yabahari. Lakini alipokuwa akiendachini, Kibwe alikua akisikia sautikwa mbali, ikimwita jina lake.“Kibwe! Kibwe! Amka Kibwee!Amka!” Wakati likitajwa jina lake,Kibwe pia alihisi kuwaameshikiliwa na hukuakitingishwa tingishwa. KumbeHanga aliyeporomoka baharini baada ya Kibwe kuangukia humo,alimuwahi mwenzake kablahajafika chini zaidi ya bahari bilafahamu. Kijana huyo alikuwaakijitahidi kumsaidia mwenzakeasizame, kwa hiyo ingawahakufahamu kuogelea, kwamastaajabu makubwa akawaanaogelea kwa mkono mmoja, nakwa mkono mwengine akijaribukumkokota Kibwe na kupandanaye juu ya bahari ili kupatahewa safi!

Hanga alihisi kuwatukio lile la uwezo mkubwa wakuogelea lilihusiana sana naupekee wa Mwana Mteulealiyeshirikiana naye!Wakati Hanga akifanya jitihada zakujinusuru yeye na mwenzake,mara mbele yake akaona kitukipana mno, labda kama kinywacha mnyama gani sijui! Labda niaina fulani ya mnyama wabahari, aliyekuwa anajiandaakuwameza yeye na mwenzake!Hanga aliogopa sana. Akajaribukugeuka na kumkokotamwenzake, lakini yule mnyamaakamuwahi! Akafunua kinywachake zaidi, na bila kupotezamuda, akawameza vijana walewote kwa urahisi mkubwa! Mojakwa moja Hanga na Kibwewakaporomoka kwenye tobo lagiza nene, wakipita katika njianyembamba, na hatimae kutuwachini! Walikua tumboni mwamnyama mmoja wa ajabu!Muda fulani baadae, Hanga nakibwe wakawa wamelala kwamuda mrefu kwenye nyasi.


Kwakuwa jua lilikuwa likiwamulikausoni, taratibu wakaanza kuamka. Kibwe aliamka mwanzo, naakawa anaangaza angaza huku nahuko, aweze kuelewa mahalialipokuwa. Hakukumbuka maramoja mikasa iliyowasibu.Pembeni kwake, Hanga nayeakafumbua macho, akaamka nakuketi kitako. Hakujua mahalialipokuwa, mpaka alipomuonakibwe pembeni yake.Akakumbuka kuwa wakati fulaniKibwe alikuwa amezimia. “Ah,kibwe rafiki yangu, umepona?Unajisikiajae sasa?” kibwe nayealifurahi kumuona Hanga, naakamwambia kuwa yeye hakuwana tatizo lolote. Isipokuwa kwapamoja walisikitika kuwahawakuwa na taarifa yoyotekuhusu wenzao waliokuwa naobaharini, baada ya lile jangalililotokea katika meli ya mfalme KashKash.

Kabla ya kubadilishanamawazo, ghafla Hanga akapigaukulele wa kukata matumbo!Kilima kidogo alichokiona mbeleyake kwa muda wote waliokuwapale na mwenzake, kilikuwakinatembea kuwafuata palewalipokuwa! Hanga akagunduapia kuwa kilima hicho kilkuwa nashingo…hapana! Siyo shingo tu!Kilima hicho kilikuwa na umbo laKobe, kwa hiyo sehemu mojakulikuwa na kichwa chenyemacho yaliyokuwayakizungushwa zungushwa! Lo!Kilima chenye uhai!Bila ajizi Hanga akainuka nakuanza kukimbia, hukuakimkokota Kibwe pamoja naye!“Haraka Kibwe! Tukimbie nduguyangu! Hatari hiyo mbele yetu!Jamani, mbona tuna mkosi hivi!”Hanga alilalamika huku akihofukupita kiasi.

Kibwe alisimama nakumfuata mwenzake, hukuakiangalia kule mwenzake huyoalikokua anaelekeza kidole chake.Lakini mara Kibwe akasita nakukodoa macho kwenye kilekilima. “Kimbia Kibwe! Unangojanini sasa? Twende bwana weee!”Hanga alimsisitizia mwenzakehuku akimburuza. Kibwealimuonyesha ishara Hanga kuwaasubiri kidogo. Ingawamwenzake yule alikubalikusubiri, lakini alijiweka mbalikabisa na Kibwe na kile kilimacha ajabu. Aliwaza kuwa kama Kibwe alikuwa tayari kujitosakwenye janga jinginelitakalotokana na kitu kile chenyeuhai kilichofanana na kilima chaaina yake, yeye Hanga hakuwatayari kujitoa kafara namna hiyo!Kwa mshangao mkubwauliochanganyika na furaha, Kibwealisogea karibu zaidi na kilekilima cha hatari!

Halafu, eti kwafuraha kubwa zaidi, kijana yuleakakirukia kile kitu ambachoHanga alikiita kilima cha ajabu,na ingawa alianguka chini kwakufanya hivyo, Hanga akamuonaakiinuka na kuanza kupapasakwenye kile kilma kama mtualiyechanganyikiwa! “Amepatwana nini mwenzangu huyujamani?” Hanga aliwaza hukuakihisi kuwa wakati wowote ule,jambo la hatari lingetokea. “Ah!Kumbe ni wewe! Shikamoo babu!Hivi umefika vipi huku?Nimefurahi sana kukuona rafikiyangu!” Kibwe alirukaruka kwafuraha, wakati mwenzake Hangaakimwangalia bila kumuelewa.“Bila shaka mwenzangu huyualipojigonga kichwani tulipotupwa baharini kutokakwenye merikebu, akili yakealiathirika masikini weee!”

Hangaaliwaza, akijua kuwa mwenzakeyule amepata kichaa, ndio maanahata hakujali kuhatarisha maishayake!Baada ya kuelewa kuwa kile‘kilima’ hakikuwa dude la hatari,Hanga akauliza. “Sasa, kamawewe ni Mzee wa Busara, hebutueleze, kwa busara zako, hivi sisitulitoka vipi kwenye tumbo layule mnyama mkubwa baharini,na je alikuwa ni mnyama ganiyule?” Mzee wa Busaraakamwangalia Hanga, na kishaakacheka sana! Kibwe hakujuakama walimezwa na mnyama wabahari, kwani yeye alizirai baadaya kujigonga na nguzo yamerikebu, baada ya meli ilekuvunjika kwa tufani namwamba wa barafu majini.Hivyo, alistaajabu sana, na kishaakasikiliza kwa makini maelezoya Mzee wa Busara.

Baada yakucheka sana, Mzee wa Busaraalisema, “Mlipotumbukiabaharini wakati Kibwe alipokuwaanazama, kulikuwa hakunauwezekano wa wewe Hanga pekeyako kumuokoa na piakujinusuru nafsi yako, kwakuzingatia hata kuogeleahukufahamu vizuri!. Kwa kuwanilifahamu hivyo nilifika hukoharaka kuwaokoa nyote wawili,kwa hiyo nikawameza, na kishakuwaleta hapa kwenye ardhiiliyorutubika.” Hanga namwenzake Kibwewakamwangalia Mzee wa Busarakwa faraja kubwa, na Hangahakuamini aliyoyasema,isipokuwa mwenzake Kibwealiyemfahamu.. ,

Kibwe alifahamukuwa Mzee ‘Kaka’ hakuwaKakakuona wa kawaida, balialikuwa ni mnyama wakimazingaombwe kamaalivyokuwa Bunga.“Tunakushukuru sana mzee‘Kaka,’ kwani bila ya wewetungekufa maji” Kibwe alisema,na Hanga naye, hukuakimwangalia Kibwe na hukuakihofu kuuliza chochote,akajiuliza kwa nini mwenzakeyule hakuhoji kabisa kuhusu iletaarifa ya ajabu ya Mzee ‘Kaka?’Hata hivyo, kwa kufuataalivyosema Kibwe, naye akatoashukurani zake kwa Mzee waBusara.

Baada ya hapo, Kibweakataka kujua hatua inayofuatakatika safari yake ya ajabu.Mzee wa Busara alimwambiaKibwe aende hadi nchi ya shamsi,upande wa mashariki ya katikatiya dunia, kilometa chache tukutoka pale walipokuwa. “Tunzaupanga wako huo wa radi, maanautauhitaji sana. Huko uendako.Utakwenda katika sehemu yenyemajabali yaliyozingira mtoSakura, yaani mto mkubwa wamaji, ambako utakutana na jokala vichwa saba na ambaloutapigana nalo na kulikatavichwa sita, kwa urahisi.

Lakinikichwa cha mwisho ambacho nicha shaba, kitakusumbua sanakukikata. Kwa msaada wa upangahuu, hatimae utafanikiwakukikata, isipokuwa baada yahapo, utaanguka na kuzirai!”Hanga akatoa macho kwa hofu,kwanza ya kuambiwa kuwawatakukutana na hilo joka kubwala ajabu, na pili kusikia habarikwamba mwenzake Kibwe,atazirai tena! “Sasa asipoamka je?Itakuwaje?” alimuuliza mzee‘Kaka.’

“Hapo ndipo msaadawako utahitajika. Mara tuatakapoanguka, harakautachukua ndoo ya maji nakummwagia mwili mzima, nayeatazinduka baada ya muda”Hanga hakujua watapata wapihiyo ndoo ya maji huko kwenyemajabali matupu, naalipomuuliza Mzee wa Busara,mzee yule akamjibu kwa methaliya busara, kwamba ‘mwenyemacho haambiwi tazama,’ kwanihuko huko waendako, wataelewawatakapopata hiyo ndoo ya maji.Pamoja na mawaidha hayo,Kibwe na Hangawakafahamishwa kuwa hilo jokawatakalokutana nalo, sio joka lakawaida. “Joka hilo ni Maimuni,mwana wa mfalme wa majini yabahari na mito ya maji, anaeishichini ya huo mto Sakara!”

Lo! Mikasa juu ya mikasa. Hangaakawa dhoful hali kwa hofu!Hanga alipata wasiwasi tmkubwa.Katika maisha yake, alimsikia bibiyake akisema kuwa majini niviumbe wabaya sana ambaohugeuka upepo na kuwakumbawanaadamu, na baada yakukumbwa na jinni, mara nyingiwanadamu hupata ugonjwa wakiharusi. Mwanzoni Hangahakuelewa kuhusu huo ugonjwawa kiharusi, lakini baadaealifahamu kuwa huo ni ugonjwaambao watu hupooza upandemmoja wa mwili. “Mtoto wajirani yetu ……alikumbwa naupepo mbaya alipokuwa anapitanjia panda, ndio maana amepatakiharusi.” Bibi yake alisemawakati mmoja, na alipomuulizakuwa upepo mbaya ndio upepogani, bibi yule alimwambia kuwani majini waovu.

Na sasa etiMzee wa Busara anasema kuwamajini ni majoka ya baharini.Inakuwaje? Alitaka sana kujua,kwa hiyo akamuuliza Mzee‘Kaka.’ “Hivi babu, ni kweliduniani kuna majini? Na majinini nyoka au ni upepo mbaya? Naje wanaishi wapi?” Mzee waBusara alimwambia kuwa majinini wa aina mbalimbali, naakamfafanulia kwa undani zaidi,akisema; “Kijana , kumbukakwamba duniani hawaishiwanaadamu peke yao, bali majininayo huishi miongoni mwao,lakini hawaonekani kwa macho .

Kama vile ilivyo kwawanaadamu, utaona kuwa wapowaliokuwa wema na wapo ambaoni waovu sana, na kwa majinni,wapo waliokuwa wema nawanaotenda matendo mazuri, nawapo ambao ni waovuwanaotenda matendo ya uovu.Kwa hiyo, wale waovuwanapotaka kuwazuruwanaadamu, hujigeuza katikamaumbile yatakayo wasaidiakutekeleza uovu waowalioukusudia. Mara nyinginehugeuka maji, mara upepo, marawanyama wa aina waipendayo,na kadhalika. Si rahisikuwatambua majini wanapofanyauovu wao.” Kibwe na Hangawakaduwaa, wakitafakarimaelezo hayo ya Mzee wa Busara.Kibwe aliogopa sana kupambanana adui mwenye hila kama hizo

Kibwe na Hanga walitembea kwasaa nyingi, na kutokana naukame wa jangwani, njianiwakanywa na kumaliza maji yotewaliyofungasha kutoka kule kwaMzee ‘Kaka.’ Hivyo, baada yahapo, walikosa kabisa maji yakuondoa kiu, kwani kwa jinsiukame mkubwa ulivyotawalasehemu hizo, kwenye maeneoyote waliyokuwa wakipita,hawakukuta mto wala vijito vyamaji. Huku na huko walizingirwana jangwa, na ardhi haikuwa nammea hata mmoja! “Hivitutafanyaje Kibwe? Koo langulimekauka kabisa, na hata nguvusina,” Hanga alimwambiamwenzake. “Tujitahidi kutembeakidogo, maana huenda njianitutawakuta wenyeji ambao niwakazi wa nchi hii, nawatatuelekeza sehemu ya kupatamaji.”

Kibwe alimfarijimwenzake, na hivyo wakasongambele na safari yao. Baada yamwendo wa saa moja hivi, Hangaakaona kwa mbali, nyumba mojaya tope iliyojitenga, na iliyokuwakwenye kichaka, ambakohawakuona nyumba nyingineyoyote zaidi ya ile. “Angalia!Kuna nyumba kule mbele!Huenda tukapata maji huko,hebu tuharakishe!” kijana yulealiyekuwa na kiu sana,alimuhimiza mwenzake Kibwe.Kwa hiyo kwa moyo wamatumaini, wawili haowaliharakisha na kufika kwenyehiyo nyumba.

Hapo, walibishahodi ili waweze kumpatamwenyeji, watakaye muombahayo maji.“Hooodiiiii! Hooodi humu ndani,Hodiii!” Kibwe na Hanga wakawawanapokezana kubisha hodi,lakini hakuna mtu aliyejibukutoka ndani. “Hooodiiii! Humu ndani hakuna watu? Hooodiii!”Waliendelea kubisha hodi, kwasababu pale palikuwa ni mahalipekee walipopatarajia kupatamsaada, maana kilawalipoangalia huku na huko,hawakuona dalili yoyotekuashiria kuwa sehemu ileilikuwa na watu. “Wenyewe mpoo?” waliuliza tena kwa sautiya juu zaidi. Hata hivyohawakujibiwa. Wakabisha tenahodi kwa sauti ya juu zaidi, namara hii wakasikia sauti hafifu yamwanamke aliyesikika kamamzee.

Akawakaribisha ndani kwafuraha. ”Karibu! Karibuni ndani!”Kusikia hivyo, haraka wale vijanawakaingia ndani, wakijua kuwabaada ya muda, tatizo lao la kiuya maji litapatiwa ufumbuzi.Walipofika ndani wakaonamwenyeji wao alikuwa ni bibimmoja kizee, hivyowakamwamkia; “Shikamoo bibi.Habari za hapa?” Kizee yuleakaitikia, “Marahaba, wajukuuzangu, Hamjambo? Na je,mnatokea wapi, maana si maranyingi watu kupitia huku kwetu,na mnakwenda wapi.”“Kusema kweli bibi, hatujuitutokako wala tuendako.Isipokuwa katika safari yetundefu, tumeishiwa maji yakunywa, na ndio tukaja hukukuomba maji, maana tuna kiusana, na safari yetu nadhani badoni ndefu,” Kibwe alisema kwaniaba ya mwenzake Hanga.

“Ndio bibi, tutashukuru sana ukitupatiahata robo kikombe tu ya maji,yatatutosha,” Hanga akaongezea .“Ah! Wajukuu zangu wee! Sijuiniwaambie nini! Maana hiyonusu kikombe ya maji ndiyoniliyobaki nayo. Kwa hakikakatika nchi hii, tuna shida kubwaya maji. Hivi ninavyoongea, leohii Sultani wetu anamtoa kafarabinti yake kitinda mimba, ili raiawake tuweze kuchota maji mtonikwa kipindi cha mwaka mmojazaidi.” Yule bibi aliwafahamishawale vijana. “Kabla ya hapo,Sultani aliwatoa kafara mabintizake sita, mmoja kila mwaka,nasi tukaweza kupata maji kilamwaka kila baada ya tukio hilo lakusikitisha,” alieleza bibi kizee.“Sasa bibi, hao mabintiwanatolewa vipi kafara?

Wanakatwa vichwa, auwanatoswa mtoni? na je, ilikumridhisha nani ambayeakifurahi ndio ataruhusu watuwachote maji?Eti tuliambiwa kuwa mabinti haohupelekwa kwa Mfalme wamajini!” Vijana wale walijaribukupata majibu kutoka kwa yulebibi kizee.“Kwenye mto mkubwa ambaondio pekee unaotupatia maji,huishi joka moja kubwa sana.Joka hilo na wenzake huwazuiaraia wa nchi hii kuchota majimtoni mle, na limewezakuwadhuru raia wengi sana hapoawali.” Bibi yule aliwaeleza walevijana, waliopenda sana kujuaSultani Bashar wa jiji la Majabalihuko Shamsi alifahamu vipi kuwatatizo lile lingetatuliwa kwakuwatoa kafara mabinti zake.

“Ama kwa hakika baada ya shidakubwa ya maji kuligubika jiji laMajabali nchini Shamsi kwa zaidiya miaka kumi, ambapowananchi wake waliotegemeamaji ya mto Sakara kwamatumizi ya kila sikuwalishindwa kuyapata kutokanana kuwepo katika mto ule ndulihuyo niliyewaambia, raia wotewalielekeza masikitiko yao kwamtawala wao Sultan Bashar, kilayalipotokea maafa kwa baadhiyao yaliyosababishwa na jokahilo. Mara kwa marawalilazimika kupiga mbiokwenye kasri la mtawala waowakilia machozi na kulalamawakitafuta msaada, jamboambalo lilimsikitisha mnokiongozi wao Bashar…..”JINI MAIMUNI WA MAJABALI.

“Maulana Sultani! MaulanaSultani! Yametokea tena maafa!Baadhi ya waliokwenda mtonikuchota maji wameshambuliwana lile dude lisiliojulikana nakuuawa! Aah! Mtukufu Sultani!Tutafutie ufumbuzi wa haraka wajanga hili, maana raia wakotunamalizika!” Vilio hivyo namaombolezo vilitawala mno kuleMajabali mara kwa mara kwakipindi cha zaidi ya miaka kumi.Lakini masikini kwa muda wotehuo, Sultani Bashar hakuwa naufumbuzi wala jawabu kwa tatizolile.”Sijui nifanye ninikuyanusuru maisha ya raiawangu kutokana na dude hiloambalo kwa mtu wa kawaida sirahisi kupambana nalo.” Sultanializungumza kwa masikitiko nawashauri katika baraza lake laushauri.

Nao washauri wakewenye busara na hekima kubwa,hawakuweza kumpa matumainiyoyote Mtawala wao, ya utatuziwa suala lile. “Ama kwa hakikamtukufu Sultani huu ni msibamkubwa kwa nchi yetu, ambaohadi sasa ni kitendawilikisichoteguka.” Walimjibu kwamasikitiko. “Ingawa upoumuhimu mkubwa wakuwanusuru raia dhidi ya nduliyule hatari, lakini pia ni muhimuzaidi na ni wajibu kwetukuwaondolea tatizo la kukosamaji. Kwa bahati mbaya yotemawili yana ugumu mkubwakwetu kwani hatuna majawabunayo!”

Walijieleza kwa Sultaniwao wakiwa na majonzi kupitakiasi! Naam, hiyo ilikuwa ndiyohali katika nchi ya Shamsi kamawalivyoelezewa Kibwe na Hangana yule kizee waliyemuombamaji. Ni hali iliyoisononesha jamiinzima ya Shamsi kwa muda huowa zaidi ya muongo mmoja!Siku moja Sultani Basharalipokuwa usingizini aliota ndotoya kutisha mno! Katika ndoto ilealisikia sauti nzito ya ajabuiliyotokea nje ya kasri lake. Uzitowa sauti ile ulilitetemesha kasrizima lililo sukwasukwa kamameli iliyopambana na mawimbimakubwa ya bahari au dhoruba!Ilikuwa ni sauti yenye mwangwiwa kipekee!

‘Mmmmmmhhhh!Tetteeetetetettee!Mmmmmmhhh! Tetteeeteeettee!Heneee Maimuni ( mimi niMaimuni ) wa Makatta waMakattani! Mmmmmhhhh!Amani haipatikani Shamsiii!Eeeehuuun! Eeeehuuun! Sakaraitatoa maji na kuleta amani kamakila mwaka ataletwa kwenye mtohuo, mmoja kati ya mabinti zakosaba na kumwacha ufukwenimwa mto! Ukifanya hivyo maafaya raia wako yataondoka!Watachota maji kwa amani nausalama…….!Tattaaaatattaaaatattaaahh! Nausipofanya hivyo nitawafuata raiawako hadi nchi kavu nakuwateketeza kwamakundiiiii….! .Taaaattaaaataaaattaaaaaahh! Ha ha ha hahaaaaaaaa!”Sultani aliingiwa na hofu kubwasana, na wakati ule akawaanaisikia sauti hiyo ya aina yakeikitoweka taratibu, na kasri lakenalo likipunguza kasi yamsukosuko, na palepaleakashituka na kuinuka kitandanihuku moyo wake ukidunda, naakijaribu kuelewa kamaaliyoyasikia yalitokana na ndotoau ni ukweli.

Lakini alipoyatafakari maneno yamaagizo ya vitisho yaliyotolewa,aliona kuwa yamehusiana mnona hali ya nchi yake.“Hhhhhaaaa! Hhhhhaaaa!Hhhhhaaaa!” Sultani alipumuawakati mke wake, Malkia nayeakigutuka na kumkumbatiamumewe kwa wasiwasi. “Aaaaa!mume wangu! Umepatwa na ninitena usiku huu laazizi? Mbonahivi?” Sultani hakujibu balialiendelea kuhema isivyokawaida. Baada ya muda wakutosha, akamweleza mkewekuhusu ndoto aliyoota.

Lo! Malkia naye aliogopa mnohususan aliposikia habari yakuwatoa mhanga mabinti zake!“Hapana mume wangu! Hatuwezikufanya hivyo asilani! Kamwesintakubali!” Mama yule mzaziwa wana alimaka. Lakini Sultanikwa maneno ya busara,alimtuliza mkewe akimkumbushakuwa ingawa wao ni wazazi wamabinti zao saba, lakini wao piani watawala wa raia wengi mnoambao wamo kwenye matatizomakubwa. “Mmoja mmoja raiawetu wanapoteza maisha yaoama kwa kushambuliwa na nduliwa mto Sakara, au wanateketeakwa makundi kwa kukosa maji.Je, unadhani ni nani atakayewanusuru na janga hilo kama simimi, wewe, na mabinti zetu?Kama kujitolea wanetu ndioufumbuzi wa tatizo hili sugu, basina iwe hivyo!” Alisema kiongoziyule mwema.

Masikini Malkia alilia sana kwauchungu, lakini hatimaewatawala wale wawili wakaamuakujitolea binti yao mmoja kilamwaka, mabinti waliopoteleakwenye mton Sakara, na hivyobaba yao Sultani Basharkufanikiwa kuwanusuru raiawake kwa miaka sita. Sultani namkewe walibaki na binti yaommoja kitinda mimbawaliyempenda sana, Bhaduribinti Sultani! Maelezo ya mkasaule wa nduli Maimuni wa Sakarana Sultani Bashar wa Shamsiyaliyotolewa na bibi kizee,yaliyosadikisha taarifa ya Mzeewa Busara kwa Kibwe na Hanga.

Vijana wale waliduwaa kabisa nakubutwaika, wakasahau kiu yamaji waliyokuwa nayo! Kutokanana maelezo ya awali ya Mzee waBusara Kibwe aligundua kuwawamekwisha wasili nchiniShamsi, na akatanabahi nakutambua kuwa kazi yakeiliyompeleka kule haitakuwanyepesi!Ama kwa hakika maajabu yalizidikumtokea Kibwe, kila mojalikizidi la awali! Kwanza walamawe, kisha kisiwa cha mazimwiwala watu, halafu majiniwageuzao watu kuwa mawe yatheluji…… na sasa….. eti kunajoka kubwa linalozuia watukuchota maji, hadilitakapopelekewa warembomabinti Sultani kama kafara! Nimabalaa makubwa! Vijana wotewawili walizidi kubutwaika,waliposikia ile habari ya mwishoisiyokuwa ya kawaida, ya mabintiSultani wanaotolewa kafara aumuhanga!

Na kwa sababu hiyo,hawakutaka tena kuomba maji yakunywa, kitu ambacho kilikuwana utata mkubwa katika sehemuile ya mashariki ya katikati yadunia. Kibwe na Hanga walizidikupata unyonge mkubwa kuhusujambo lile kwani wakati ule yulebibi alipokuwa akizungumza nao,alikuwa akikwangua kwa kata yamaji, chini kabisa ya mtungi nakisha kutoa maji yaliyokuwa navumbivumbi na uchafu, nakuanza kuyanywa! Huku wakishangaa, na piakusikitika, Kibwe na Hangawalimuuliza yule kizee, “Hivi lilejoka huwafanya nini walemabinti baada ya kuwachukua?” Yule bibi alikohoa kidogo,akapapasa kata yake ya maji, nakunywa funda moja ya maji,kisha akaendelea kusema; “Sidhani kama kuna yeyoteanayefahamu yanayowasibu walemabinti baada ya kuchukuliwa nalile joka Hata Sultani mwenyewehajafuatilia kujua zaidi mamboyanayowasibu mabinti zake.

Nimsiba mkubwa sana huowajukuu zangu!” Wale vijanawalipata majonzi makubwa,hususan waliposhuhudia yulebibi akihangaika kunywa majikidogo sana ambayo ni machafuyaliyobakia mtungini. Kibwealipiga moyo konde ‘liwalo naliwe’, na akasema; “Subiri kidogobibi, baada ya muda si mrefu,tutakuletea maji ya kunywa. Vutasubira kidogo tu!” Hangaakamwangalia mwenzake kwakumshangaa. “Sasa tena Kibweanaanzisha nini kingine?”alijiuliza, huku akihofu kuwamwenzake yule alitaka kufanyavile alivyoambiwa na mzee wabusara, yaani kupambana na jokala vichwa saba! Hivyo, bila yulekizee kuona, kijana huyo muogaakawa akimfinya Kibwe, akiashiria kuwa aachane namambo hayo! Na bibi kizee naye,hakuwa tayari kumwachia yulekijana ajitose kwenye hatari hukomtoni.

“Hapana mjukuu wangu,usifanye hivyo hata kidogo, kwaniutajitafutia madhila makubwa.Nadhani leo jioni baada ya hilojoka kumpata Bhaduri bintiSultani, kila mtu atapata maji yakutosha. Kwa hiyo nadhani wewendiye unayestahili kuvuta subirakidogo!” Hanga alimuunga mkonobibi kizee, kwa kusema; “Nikweli kabisa Kibwe, kwani kwakujipeleka huko, unawezakuhatarisha maisha yako.” Kibwenaye hakuwa tayari kusubiri etimpaka lile joka limchukue yulebinti. “Lakini bibi nadhani badohujaelewa nia yangu. Nataka leoiwe mwisho wa joka hilo kudaikafara. Umesema kuwa huyo nibinti wa mwisho wa Sultani.

Sasabaada ya yeye kutolewa kafaramwakani mtapataje hayo maji?Au Sultani ataanza kuwatoakafara raia wake mmoja mmoja?Sidhani kama hilo litakuwa nijambo la busara. Yule bibialishangaa sana kuona jinsi yulekijana alivyojiamini.Akamwombea Mungu, aende nakurudi salama. “Mjukuu wangu,kama unadhani kuwa unawezakulipatia ufumbuzi tatizo hilo,sina la kusema, isipokuwanakuombea kila la heri, na bilashaka Mungu atakuwa pamojanawe!” Bibi yule alimuombeahivyo, akihisi kuwa labda Kibweanaweza kuwafikisha raia wa Shamsi kwenye hatima ya tatizolao sugu, ingawa pia alihofu mnokuwa huenda kijana huyoakapotelea hukohuko mtoni,kama ilivyokuwa kwa mabintiSultani sita!Hanga alifuatana na Kibwe shingoupande, na wakaondoka wakiwawamebeba ndoo mbili za maji,wakielekea mtoni.

Kijana yulealishangaa sana, kwani wakatiwalipokuwa wakienda mtoni kwajoka la vichwa saba, Kibwehakuwa na wasiwasi asilani!Hanga hakufahamu kwambamwenzake alikuwa anakumbukamawaidha ya Mzee wa Busara,kuwa upanga wa radi humpanguvu ya ushindi kila anayeutumia. Alikumbuka sikualipoutumia upanga ule kulekaskazini ya mbali kwa MfalmeKashKash, na jinsialivyouzungusha hewani kwamaelekezo ya Mzee Kaka, ilikujinusuru na majini wa upepowa bahari. Bila kutegemea,upanga huo ulitoa cheche zamoto zilizogeuka kuwa viengevya moto mkali, vilivyowateketeza majini hao.“Usipoangalia, upanga huounaweza kukudhuru mwenyewebadala ya kumdhuru adui unayepigana naye” Mzee wa Busaraalimuonya Kibwe.

“ Nitajitahidikuwa mwangalifu Mzee ‘Kaka’.Kibwe aliahidi. Mzee wa Busaraalikohoa kidogo kama kawaidayake na kisha akasema, “Ninafuraha kubwa kuweza kukusaidiaKibwe, isipokuwa kuhusukujichunga usidhurike na huoupanga wa radi, usijitahidi tu,kuwa mwangalifu na upanga huo,bali KUWA MWANGALIFU.”akasema kwa msisitizo! Kibwealimuelewa vizuri sana Mzee waBusara!Kibwe, akiwa na upanga wakekiunoni, uliofungwa vizurikwenye ala yake, akifuatana naHanga wakiwa na ndoo zaowalizozichukua kwa bibi kizee ilikumpelekea maji watakapoyapata, walianza kuelekea mtoni,ambako Bhaduri binti Sultan,kitinda mimba wa Sultani Basharalikuwa akisubiri kuchukuliwa najoka kuu, akiwa ni kafara kwanyoka huyo.

Walipokaribiakufika, macho yao yalivutiwa naukubwa wa majabali yaliyokuwambele yao. Waliposogea karibuzaidi, macho hayo yalizidikuvutiwa, walipomuona bintimrembo wa ajabu, aliyeketikwenye kiti kikubwa cha enzi juuya jabali. Wakazidi kumsogelea,na hapo ndipo walipogunduajinsi binti huyo alivyopambwa!Na pale alipokuwa, upepomororo wa manukatomchanganyiko, ulienea sehemuyote !

“Ama kwa hakika Sultaniameamua kuwavutia nakuwafurahisha majiniwanaowachukua binti zake,maana nakumbuka bibi alisemakuwa majini hupenda sanamanukato!” Hangaalimnong’oneza Kibwe, ambayehakujibu kitu, bali alizidikumsogelea Bhaduri binti SultaniBashar!“Habari za asubuhi binti Sultani,” Kibwe alimsalimia Bhaduri.“Habari nzuri kaka yangu. Vipi,mbona mnakuja na ndoo za majiwakati huu ambapo hata badohawajaja kunichukua? Mnatakakusababisha matatizo kwa raiawa Shamsi? Au tuseme ninyi niwageni katika nchi hii?”

Bhadurialimuuliza Kibwe, hukuakiwashangaa yeye namwenzake. “Nadhani ni boramsubiri hadi nitakapo chukuliwa,ndipo mje kuchota maji kwaamani kaka zangu, na sivinginevyo!” Binti Sultanialiwasihi vijana wale wawili.Lakini Kibwe alitabasamu tu, nakusema, “Naona leo tutasubiripamoja, tujue mwisho wa tatizola jamii ya nchi hii.” .Wakati akisema hivyo, alikuwaameanza kuitumbukiza ndoo zabibi kizee mtoni ili kuzijaza maji, na alifanya hivyo kwa fujo mno,akiyakoroga koroga yale maji nandoo yake, kama kwambaalikuwa akilichokoza lile jokahuko lilikokuwa! Hangahakupenda kitendo hicho asilani,kwani kilimpa hofu kubwa.Alihisi kama vile wakati wowotewangevamiwa na lile dude lavichwa saba kutoka mtoni!

Palealiposimama, jasho jembambalilimtiririka kwa hofu, akawaanaangalia huku na huko,akitarajia dude kuwa jokamaimuni litatokea upandewowote! “Leo ndio mwishowetu,” aliwaza, huku akitetemekabila kizuizi.Binti Sultani hakuelewa kijanayule mkorofi alitokea wapi,aliyetaka kuleta matatizo kati yaraia wa baba yake na hilo joka lakutisha, ambalo awali kabla dadazake hawajatolewa kafara,liliwateketeza raia wengi wa nchiyao waliojaribu kuchota majipale mtoni. Hakuelewa nia yakeilikuwa ni nini.

Alimshangaa sanaalipoendelea kuchota maji kwafujo, akaweka ndoo zakepembeni, na kisha kumwamurumwenzake kwa kujiamini.“Mpelekee yule bibi kizee ndoomoja, halafu urudi hapa harakaili tusubiri pamoja.” Hangaaliifurahia mno amri ile, ilimraditu, aondoke pale mahali pahatari. “Sawasawa, ngojaniwahi....” Bila kupoteza muda,Hanga akachukua ndoo ya majina kutokomea vichakani, akirejeakwa bibi kizee!Kibwe naye, akaketi karibu nabinti Sultani, panga lake kiunoni,akisubiri kitakachotokea!

Punde si punde, upepo mkaliukaanza kuvuma, kamailivyokuwa kawaida kila mwaka,wakati binti Sultani alipofuatwana yule nduli wa vichwa saba.Dalili hizo mara nyingi ziliwatiahofu raia wote, ambaowalikomelea milango yao,wakihofu dhoruba ambayo maranyingine iliezua mapaa yanyumba zao na kung’oa milangoya nyumba zilizokuwa hafifu.Siku ile ilipotokea dhoruba hiyona kimbunga kibaya, vikachafuamno maji ya mtoni.

Muda simrefu, maji ya ule mto yakawa nimawimbi makubwa yaliyoinukajuu sana na kumwaga maji kwakuyarusha kila sehemu! Kutokapale walipokuwa, Kibwe naBhaduri wakatupwa chini nahayo mawimbi. Punde,ukajitokeza mlima mkubwa waumbile la lile joka lililokuwalikisubiriwa! likajinyonga nyongana kujitoa mtoni kwa hasira,likijileta juu ya jabali! Mara,kimoja kati ya vichwa vyake saba,kikaonekana kikifoka, kikimakana kutoa povu! Alipoona kinywakipana cha yule nduli, Bhaduriakapiga ukulele mmoja wakusisimua, akihofu kuteketezwa“Mama yangu weeee! Tunakufaleo jamani!” Binti huyoalibabaika, bila kujua akimbiliewapi, kwani lile joka lilitandapande zote!

ITAENDELEA
 
Sehemu Ya Tano (5)
Wakati lile joka lilipofunua
kinywa chake kwa hasira, Kibwe
akasimama kishujaa , akainua
upanga wake wa radi na
kuuzungusha, na kwa kufanya
hivyo, mara moja, kama muujiza
upanga huo ulitoa ngurumo za
radi za kusisimua, na wakati
uleule Kibwe akalibwaga panga
lile shingoni kwa hilo joka, na
sekunde chache baadae, kichwa
chake kikadondokea nchi kavu!
Lakini Joka likazidi kujitoa nje ya
maji kwa ghadhabu, na kutoa
kichwa chake cha pili, kilichokua
kikifoka na kutoa povu jingi.
Kibwe akasema, “Leo ni leo, ama
zako ama zangu.” Akainua tena
panga lake la radi ambalo safari
hii, pamoja na kutoa ngurumo,
likatoa cheche za moto wakati
lilituwa shingoni kwenye kichwa
cha pili cha lile joka lenye hasira.
Vivyo hivyo, vichwa vingine vya
joka hilo vikachakazwa kimoja
kimoja kwa dhoruba moja tu,
kwa kila kichwa, wakati upanga
ulipotoa ngurumo na cheche,
hadi kilipobaki kichwa cha saba!
Wakati huo, Hanga naye,
aliyeagizwa na Kibwe kwa bibi
kizee hapo awali, akatokea!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kimoja kati ya vichwa vyake
hivyo saba yaani cha mwisho, ni
cha shaba.” Kakakuona, Mzee wa
Busara alimwambia Kibwe.
Kichwa hicho kitakusumbua sana
kukikata, na hatimae
utakapokikata, utaanguka na
kuzirai.” Akakumbuka vile Mzee
wa Busara alivyomwambia
Hanga, kuwa atakapomuona yeye
amezirai, ammwagie ndoo nzima
ya maji, ndipo atakapozinduka.
Alipomuona Hanga akitokea
wakati akikumbuka maneno yale
ya mzee wa busara,
akamtahadharisha mwenzake
yule kuhusu jambo hilo.
“Usisahau maagizo ya mzee wa
busara. Nitakapozirai tu, mara
moja unimwagie ndoo nzima ya
maji.” Hanga akajibu kuwa
hajasahau.
Baada ya hapo, Kibwe alisimama
tena, na kuanza kupambana na
kichwa hicho cha shaba, na
wakati ule, lile joka lilikua
limekwisha choka! Kila
aliponyanyua upanga na
kuubwaga kwenye shingo ya kile
kichwa cha shaba, ulisikika mlio
kama vile panga lililopigwa
kwenye mataruma ya reli, lakini
kichwa hakikutetereka! Kibwe
hakukata tamaa, bali alizidisha
nguvu kila mara hadi katika
dhoruba ya saba, kichwa hicho
cha saba kilipoanguka, na Kibwe
naye akaporomoka chini na
kuzira! Palepale, Hanga akaruka
na ndoo ya maji na kummwagia
Kibwe mwili mzima! Lakini mara
tu baada ya kitendo hicho,
kikasikika kishindo nyuma yake
na alipogeuka, akamuona
Bhaduri naye kaporomoka chini
na kuzirai kama Kibwe! Hanga
ambaye anaposhtukizwa na kwa
ghafla kama vile hushindwa
kupata ufumbuzi wa haraka,
kwahiyo akaanza kubabaika bila
kujua la kufanya. “Sasa mbona na
huyu naye amezirai? Nifanye nini
sasa?” aliwaza, na mara,
akajishauri na kuamua kuchota
maji, huku akihofu mno, akihisi
kuwa huenda likazuka kutoka
mtoni joka jingine, labda lenye
vichwa zaidi ya saba, na
kuwazowa wote kwa kafara! Hata
hivyo, hatimae kijana huyo
aliyapata maji na kummwagia
binti Sultani. Baada ya nusu saa
ya kusubiri kwa wasiwasi huku
vichwa saba vya lile joka
vilivyoangukia nchi kavu
vikimtolea macho, punde kidogo
akawaona Bhaduri na Kibwe
wakizinduka, huku Kibwe akiwa
hoi, lakini mwenye tabasamu
kubwa usoni kwake!
Hanga na Kibwe walipokamilisha
kazi hiyo nzito, wakiuacha
mtumba wa lile joka
umejilundika nchi kavu baada ya
kujitoa wakati wa mapambano,
Kibwe akakusanya vichwa vyote
vya lile joka, na kuviweka
kwenye fuko lake kubwa la gunia
mbalo yeye hulibeba mgongoni
kila anakokwenda. Alifanya hivyo
kutokana na ushauri wa mzee wa
busara.
“Lazima ukusanye vichwa vyote
na uvichukue…kohoo..kohooo
(kikohozi) maana hivyo ni
ushahidi wako………usisahau
kabisa jambo hilo!”
Kibwe hakuelewa maana yake, na
alipouliza sababu ya kufanya
hivyo, Mzee wa Busara
alitabasamu tu, na kisha
kumalizia na kikohozi
kinachomjia mara kwa mara.
Lakini hatimae Kibwe alifahamu
kwa nini aliambiwa avikusanye
vichwa vile na kuvichukuwa.
Kibwe alimwambia Bhaduri
asubiri pale pale juu ya jabali,
kwani alitaka kuingia chini
kabisa ya mto alikotoka yule
nyoka wa aina yake, ili aweze
kupata majibu ya maswali mengi
aliyokuwa akijiuliza. Alikumbuka
pia kuwa Kakakuona, yaani Mzee
wa Busara, alimwambia kuwa lile
joka sio la kawaida, bali ni
mwana wa mfalme wa majini ya
bahari na mito. Alimwambia
kuwa majini hayo hujigeuza
katika maumbile yoyote
wanayotaka, hata maumbile ya
kibinaadamu. “Majini hao wana
miji yao chini kabisa ya mito na
bahari.” Kibwe aliambiwa na
mzee yule wa busara, na
alikumbuka jinsi alivyo pambana
na jini makata na wenzake
kwenye mji mmoja wa chini ya
bahari huko kaskazini ya mbali
ya dunia. “Huoni kwamba
kuingia huko chini ya mto ni
hatari ?” Binti Sultani alimuuliza
Kibwe, akihofu kuwa huenda
akakutana na nyoka wengi wa
aina ile. Lakini Kibwe alishikilia
jambo hilo, akisema, “Ili niweze
kuzuia matukio mengine kama
haya yasitokee tena, ni muhimu
sana nikafanye utafiti na kujua
asili ya nyoka huyu
niliyemuuwa,” Bhaduri na Hanga
wakatazamana, kuona jinsi Kibwe
alivyokuwa amejiamini kupita
kiasi!
Hanga aliogopa mno,
alipoambiwa na Kibwe kuwa
lazima wafuatane huko chini ya
mto. “Mmi-mmi-mi na-ddhani- t-
tuonndoke tu, K-ibwe! N-ni
hatari k-kuin-gia humo n-dani!”
Alisema Hanga huku akitetemeka
kupita kiasi kwa hofu. “Twende
bwana wee! Tutajua jinsi ya
kujihami tukifika huko.” Kibwe
alisema huku akimkokota
mwenzake kuelekea upande wa
mto , sehemu ya korongoni,
ambako ndiko walikoingilia
kwenda chini kabisa ya ule mto.
Bhaduri binti Sultani akabaki
kando ya mto juu ya jabali,
akisubiri.
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Twende bwana wee! Tutajua
jinsi ya kujihami tukifika huko.”
Kibwe alisema huku akimkokota
mwenzake kuelekea upande wa
mto , sehemu ya korongoni,
ambako ndiko walikoingilia
kwenda chini kabisa ya ule mto.
Bhaduri binti Sultani akabaki
kando ya mto juu ya jabali,
akisubiri.
Vijana wale walizama chini
kabisa ya mto kwa kupitia kule
korongoni, na hatimae bila
kuamini macho yake, Hanga
aliona nchi kavu! “Ha! Kibwe,
huku ni wapi tena?” aliuliza kwa
mastaajabu, kwani chini ya ule
mto, kulikuwepo mji mkubwa
wenye majumba makubwa
makubwa ya fahari! Majumba
hayo yaliyofanana, yalijengwa
katika eneo kubwa juu ya
mwinuko wa milima iliyotanda
kwa hekari nyingi mno. Mjengo
wa hizo nyumba ulifuata
mzunguko wa nusu miduara
kama saba hivi, yaani nyumba
nyingine zilikuwa katika mduara
wa kwanza kwa ndani ambao
ulikuwa mdogo, zikafuatiwa na
nyumba zilizojengwa kwa
kufuata miduara iliyoongezeka
ukubwa, kutokana na kuongezeka
kwa idadi ya miduara yenye
nyumba hizo. Nyumba zenyewe
zilijengwa kwa matufali ya mawe
ya vito vya thamani pamoja na
marumaru. Milango na madirisha
ya nyumba vilikuwa vya fedha na
dhahabu. Kwa kufuata mjengo
wa mizunguko hiyo ya aina yake,
nyumba hizo zilijengwa karibu
karibu mno. “Hee! Maajabu
makubwa haya!” Hanga alizidi
kushangaa, lakini Kibwe hakuona
ajabu, kwani tayari alikwishaona
mji wa jini Makatta na wenzake
chini ya bahari, kulikokuwa
kunatengenezwa vichafuzi vya
hewa safi iliyoko kwenye tabaka
la hewa ya ozoni. Lakini Kibwe
hakumwambia Hanga habari hiyo
wakati ule.
Huku akizidiwa na maajabu kule
chini ya mto, Hanga aliuliza.
“Lakini mbona kuko kimya hivi?
Ndio kusema wenye mji huu
wote hawapo?” Aliuliza hivyo
akihofu wasije wakavamiwa na
kutiwa hatiani na hao wenyeji,
bila tahadhari. Mwenzake
hakumjibu, ila akamuonesha
ishara ya kwamba anyamaze, ili
polepole waweze kuchunguza
wakazi hao walipo. Kwa pamoja
Kibwe na Hanga wakaambaa na
yale majengo marefu yaliyokuwa
karibu karibu, hadi walipotokea
kwenye jengo lililoonekana kama
msikiti! “La haula! Ni nini hiki?
Yaani ni msikiti au---?” Hanga
alianza udadisi wake wa kipuuzi,
na hapohapo Kibwe akamkatiza
kwa kusema, “Ndio! Ni msikiti
huo, na kama unavyoona,
takriban wenyeji wote wa mji
huu wamo humo ndani
wanasali!” Kibwe alizidi
kumfafanulia mwenzake yule,
kwa kunong’ona, akimwambia
kuwa wale wote aliowaona mle
msikitini walikuwa ni majini wa
mtoni, na ambao pia hugeuka
kuwa nyoka, wanyama
mbalimbali, upepo, au kujigeuza
katika maumbile mengine
wanayoyapenda, kulingana na
mahitaji yao kwa nyakati
zinazohusika. Kama kawaida
yake, Hanga akatoa macho pima
kwa hofu, na kisha naye
akanong’ona kama alivyofanya
mwenzake, akisema, “Ah! Ni
Kweli kabisa! Hivi sasa wana
maumbile ya binaadamu kama
alivyotuambia Kakakuona. Na lo!
wote wamevalia majoho meupe.
Haa! Ndiyo!ndiyo! Sasa
nimeelewa! Ni kwa sababu leo ni
siku ya Ijumaa, kwa hiyo watu
wote wamekuja kusali pamoja,
ndio maana mji wao wote
umepooza !” Kwa sababu ya
maajabu yale, wakati ule Hanga
alisahau kabisa hofu zake za
kawaida.
Tofauti na Kibwe aliyekuwa si
mgeni na mambo yale, Hanga
alifarijika kuyaona yale
aliyokuwa akiyasikia tu, lakini
hakuyafahamu, na ambayo
yalimshangaza kila
alipoyatambua. Mzee wa Busara
aliwaambia pia kuwa kama ilivyo
miongoni mwa binaadamu, wapo
majini wacha Mungu na wapo
wanaomuasi Mungu wao, na
kama walivyokuwapo wanadamu
wema na waovu, hali kadhalika
miongoni mwa majini, wapo
waliokuwa waovu, na wengine
ambao ni wema. “Bila shaka yule
aliyehusika na kuwachukua
mabinti Sultani waliotolewa
kafara, anatokana na jamii ya
majini waovu na wenye kumuasi
Mungu wao,” Hanga alimwambia
Kibwe, ambaye alimjibu kuwa
alihisi kuwa mabinti Sultani hao
mpaka sasa wamo mikononi mwa
majini hao waovu!
Hanga hakuamini kuwa wale
mabinti Sultani walikuwa hai
mpaka wakati ule, akihoji kuwa
ni muda mrefu sana uliopita
tangu mabinti hao wachukuliwe
na yule nduli. Iweje tena hadi
wakati ule wawe bado wako hai ?
“Kama chini ya huu mto kuna mji
mkubwa kama huu, ambao yule
nduli huwaleta wana wa Sultani,
mji ambao wakazi wake ni
viumbe wanaoweza kujibadili na
kuwa kama wanaadamu,
watashindwa vipi kuwahifadhi
kibinaadamu mabinti hao wa
Sultani, na kuwaficha miongoni
mwao, labda wakiwatumia kama
watumwa? Sasa, ikiwa kama lile
joka ni mwana wa mfalme wa
majini ya bahari na mito, basi
bila shaka chini ya mto huu yupo
baba yake, ambaye ndiye mfalme
mwenyewe, na bila shaka wale
mabinti watakuwa wapo kwenye
milki yake ya kifalme katika
himaya hii, wakifanyishwa kazi
fulani.…! Na huko ndiko
tutakakowakuta hao mabinti.
Lazima tuwahi kuwatafuta kabla
wenyeji hawajatoka msikitini!
Kibwe na mwenzake walianza
kutembea tembea katika mitaa ya
ule mji wa chini ya mto, wakiwa
macho kabisa, ili wasisitukizwe
na wenyeji na kutiwa msukosuko.
Walipokuwa wakitafuta tafuta ili
waone jumba lenye hadhi ya
kifalme, mara wakasikia sauti za
watu nyuma yao. Lo! Wakati ule
wale majini walikuwa wakitoka
msikitini, wakiwa wamevalia
majoho yao meupe kama
yangeyange! Kibwe na Hanga
walijibanza kwenye ukuta wa
nyumba moja kubwa, wakisubiri
watu wale wapite. Hanga ambaye
aliwaona viumbe wale kwa mara
ya kwanza, alistaajabu kuona
jinsi walivyokuwa warefu kupita
kiasi! Alipojifananisha nao,
alijihisi kama paka na chui! “Lo!
Ni maajabu ambayo sijawahi
kuyaona tangu nitoke tumboni
kwa mama yangu!” Hanga
alinong’ona, na Kibwe
akamfunika mdomo wake kwa
mkono ili asiendelee na maneno
yake ya mshangao, na hali wale
majini hawakuwa mbali sana na
pale walipokuwa!
Mara, miongoni mwa viumbe
wale wa ajabu, Kibwe na Hanga
wakawasikia baadhi yao
wakiulizana. “Hivi Maimuni
alirudi na yule binti sultani
kutoka majabalini?” Mwengine
akajibu, “Leo ni ajabu sana,
maana inaelekea kuwa mpaka
sasa bado hajarejea. Sijui
amepatwa na nini.”
“Usiulize kama amepatwa na nini
au vipi, maana kama huko juu
alikutana na yule kijana Ibilisi,
sidhani kama atarudi salama na
huyo binti.”
“Kijana gani tena ambaye ni
Ibilisi, na kwa nini akikutana
naye asiweze kurudi salama?”
“Kwa sababu huyo ndiye kijana
aliyenivunja huu mkono kwa
kunipiga na rungu. Sina hamu
naye asilani.”
“Hivi tuseme ulikuwa wapi
mpaka ukakutana naye, na
akakufaniya hivyo?”
“Unajua, nilipotumwa kwenda
kuzamisha meli ili kuwapata
watu wengi watakao letwa huku
kutufanyia kazi, na nikaweza
kuikamata ile meli ya Mfalme
KashKash, nilipoanza kuizamisha
tu, alitokea huyo kijana, ambaye
ghafla alinipiga na rungu
mkononi kwa nguvu za ajabu!
Nilipata machungu makubwa,
nikakimbia na kujizamisha
baharini. Sasa, kama kijana huyo
amefika huku, na akamkuta
Maimuni akimchukua binaadamu
mwenzake, bila shaka mwenzetu
huyo yumo hatiani wakati huu!”
Lo! Kibwe hakuamini masikio
yake! Hivi wale majini walikua
wameweka baraza kabisa,
barabarani, eti wakimzungumzia
yeye! Mwenyewe Kibwe alijizuia
kuporomosha kicheko! “Hivi ni
kijana gani huyo wanayemsema?
Ni wewe?” Hanga alianza
kudodosa, na hakuamini
aliposikia kuwa eti Kibwe ndiye
aliyefanya hivyo alivyoelezea yule
jinni. “Ama kweli mwenzangu
wewe una ujasiri wa ajabu
kabisa!” Hanga alimsifu Kibwe,
na akiamini kuwa kwa hakika
alikuwa ni mwana mteule, na
wala si kijana wa kawaida.
Wakati wakiwa wamejibanza
pembezoni mwa yale majengo
wakiwasikiliza wale majini,
wengine miongoni mwao
waliokuwa wakitoka msikitini,
nao wakasimama pale
walipokuwa wakizungumza
wenzao. Baada ya kusikia mkasa
uliomsibu yule aliyepigwa na
rungu, mmoja wao naye akaanza
kusimulia mkasa wake.“Labda
kijana huyo ndiye yule kijana
balaa aliyefika mjini kwetu,
akatuwekea hewa ya uvumba
iliyowateketeza wenzetu wengi,”
alisema, na kujieleza kuwa yeye
alikuwa ni miongoni mwa
kikundi kilichomfuata kijana
huyo juu ya bahari alipokuwa
akitoka mjini kwao chini ya
bahari, baada ya kuwateketeza
wenzake. “Tulishambuliwa na
cheche za moto zilizogeuka kuwa
miali ya moto, mara kijana huyo
alipotoa upanga wake wa ajabu
na kuanza kutupiga nao. Wengi
kati yetu waliunguzwa vibaya, na
wengine tulidiriki kukimbia. Kwa
hiyo, ni kweli kuna wasiwasi
kuwa kama binti wa mfalme
wetu amekutana na mtu huyo,
basi bila shaka atakuwa hatarini
hivi sasa!” alisisitiza.
Mahali walipojibanza, Kibwe na
Hanga waliweza kupata taarifa
kamili kuhusu jamii ile ya ajabu
ya majini. Kumbe wengi wao
hupatikana kwenye maji ya mito,
bahari na mabwawa. Kumbe wao
huendesha vitendo vya ukatili
kwa wanaadamu, na kwamba
pamoja na ukweli huo, zipo njia
mbalimbali ambazo wanaadamu
hutumia ili kujilinda na uharibifu
wao dhidi yao. “Watu wanao
kumbwa na majini hufukizwa
moshi wa uvumba, kwani bibi
yangu alimfanyia hivyo jirani
yetu, na baada ya hapo, , jini
huyo alikimbia na kumwacha
mhanga yule akiwa salama
salimini.” Kibwe akamfinya
Hanga kumnyamazisha, kwani
alijua kuwa endapo wale majini
wangewasikia na kuwaona,
wangewateketeza kama
walivyofanyiwa wao. Baada ya
kuyasikia yote yaliyosemwa na
wale majini, Kibwe akaelewa
kuwa pale walipo ndio hasa
mahali penyewe alipokuwa
akipatafuta, ili kuwapata mabinti
wa Sultani.
Mara tu baada ya wale majini
kuvunja baraza lao na kuondoka
mahali pale, Kibwe alimshika
mkono Hanga na kuongoza njia,
akiharakisha waondoke mahali
pale hatari, ili kuendelea na
utafiti wao wa kuwatafuta
mabinti Sultani sita. Walielekea
kwenye lile jumba la kifalme,
ambako walihisi kuwa ndiko
walikokuwa. Walipokuwa
wanaambaa kwenye majengo
marefu yaliyojipanga kwa safu,
walitembea kwa tahadhari
kubwa, huku wakinyata, ili
kujinusuru wasije wakaonwa na
wale watu wa kijini. Katika
tembea yao, ghafla Kibwe
akamuona mmoja wa wale majini
akigeuza shingo yake, kuangalia
kule walikokuwa yeye na
mwenzake! Wasiwasi mkubwa
ulimpata, kwani alihofu kuwa
katika eneo lililopambwa na
weupe wa majoho ya wale majini
hapa na pale, na kwamba katika
eneo hilo ambalo watu wote ni
warefu, Kibwe alihisi kuwa
isingekuwa vigumu kwa majini
wale kuwatambuwa kwa mbali
kabisa yeye na Hanga, na
kuwaona kuwa wao sio miongoni
mwao! Kwa kutambua hilo,
vijana wale wakaitambua pia
hatari iliyokuwa mbele yao!
“Kama hatukutafuta njia ya
kuondoka haraka katika eneo hili,
kaumu yote ile ya majini
itatuandama na kutushambulia”
Kibwe alimwambia mwenzake.
Maneno yale hayakumfurahisha
Hanga hata kidogo, kwa kuwa
yeye alikuwa ni mwoga kupita
mwenzake. “Sasa tutafanya nini
kujinusuru?” aliuliza, huku akiwa
anaangalia huku na huko kwa
hofu aliyokuwa nayo. “Kwa sasa
ni kujibanza tu, pembezoni mwa
haya majengo, mpaka wote
watakapoondoka mitaani,” Kibwe
alimjibu. Kwa hiyo walijibanza na
kuwa kimya, wakisubiri hadi hali
itakapokuwa shwari.”Sijui
wakituona na kutukamata
watatufanya nini masikini!”
Hanga alijisemesha, kama vile
hakutarajia jibu lolote kutoka
kwa Kibwe, ambaye kwa mara hii
tena, alimwashiria mwenzake
huyo anyamaze,
“sssssshhhhh!” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe naye alikuwa na hofu
kubwa, kwani alijua kuwa kwa
bahati mbaya, yeye na Hanga
hawataweza kuwatambua majini
waovu miongoni mwa kundi lile
la majini wale waliovalia sare ya
majoho meupe, isipokuwa pale
watakapoanza kuwashambulia
yeye na mwenzake. Lo! Salalee!
Wakati akiwaza hivyo, akasikia
sauti kama mluzi iliyotoka nyuma
yao, ikisema, “Angalieni kule!
Hivi wale sio binaadamu?”
Wengine wakawa wanaangalia
huko alikokuwa akionesha kidole
mwenzao, na kisha wakanena,
“Ndiyo! Wale ni binaadamu
kabisa! Wakamateni na
muhakikishe kuwa hawakimbii!
Kama mmoja wao ni yule kijana
mkorofi, lazima aadhibiwe!”
Maneno hayo yalipowafikia
Kibwe na Hanga, hawakupoteza
hata sekunde moja, kwani
walitimua mbio za ajabu, kama
upepo, wakifuata vichochoro
vilivyokuwa baina ya majengo
marefu kupita kiasi, ambayo ni
nyumba za thamani za wale
majini!
Hanga na Kibwe walikimbia kwa
nguvu zao zote bila kugeuka
nyuma, kwani walijua kuwa wale
majini nao walikuwa wakikimbia
kwa mbio za kasi ili kuwakamata.
Walipokimbia kwa muda mrefu
wakizunguka kwenye vichochoro
vya yale majengo, Kibwe aligeuka
ili kujua wale majini walikuwa
umbali gani kutoka pale
walipokuwa wao. Hanga
alipomuona mwenzake anageuka
na yeye akafanya hivyo, na halafu
lo! Kile alichokiona kilimfanya
akose nguvu miguuni,
akanyong’onyea viungo vyote,
kwa sababu ya mshituko wa hofu
na woga. Alianza kupunguza kasi
ya mbio zake! Wakati ule, ndipo
kijana huyo alipohakikisha kabisa
kuwa wale hawakuwa viumbe wa
kawaida hata kidogo, kwani
aliona macho yao yakianza
kumweka mithili ya macho ya
paka yanavyoonekana gizani! “La
haula! Sidhani kama leo
tutanusurika na hawa majini!”
alisema Hanga wakati akijaribu
kukimbia, lakini miguu yake
ikikataa kunyanyuka! Kibwe
aliyeona kuwa tayari kulikuwa na
ucheleweshaji wa mbio zao
kutokana na woga na hofu kwa
upande wa Hanga, na pia
ucheleweshaji wa mazungumzo
ya mwenzake ya mara kwa mara
kama kawaida yake, akamaka
kwa hasira, na kumwambia,
“Nyamaza na uongeze kasi ya
mbio kunusuru maisha yetu!
Acha mazungumzo Hanga!”
alisema hivyo huku akimkokota
mwenzake yule, na kwa pamoja
wakakoleza mbio za kufa na
kupona!
Wakati fulani Kibwe na Hanga
walikimbia mbio za kawaida, na
walipokuta sehemu kulikokuwa
na mapipa mengi yaliyofungwa
pamoja, waliyafungua na
kuyaachia yaporomoke kwa
nyuma yao ili kuwababaisha wale
majini. Wakati mwingine
waliruka kama ngedere hasa kwa
uwezo wa ajabu wa Kibwe
alipomkamata mwenzake
madhubuti, kila walipotokea
sehemu za miinuko ambako
waliweza kujirushia juu ya
madirisha kwenye sehemu ya
chini ya majumba yale marefu,
na kuambaa humo hadi kwenye
madirisha mengine, na kisha
kujiangusha chini kwenye
miinuko mingine. Waliporukia
madirishani, walishikilia maeneo
yaliyojitokeza kwenye madirisha
hayo, wakitambaa kwa kwenda
juu ya jengo, hatua kwa hatua,
kwa wepesi mkubwa! Vijana
wote wawili walikuwa ni hodari
sana wa michezo ya kuruka juu,
na Hanga alitumia urefu wake
kwa hodari zaidi kwani alikuwa
mrefu kuliko Kibwe, wakati
Kibwe akisaidiwa na ule uwezo
wake wa ajabu! Lakini wale
majinni waovu nao walizidi
kuwaandama, huku wenzao
wema wakiwaangalia na
kuwashangaa. Mmoja kati ya
majini wale waovu alikuwa
akiwakaribia mno wale vijana!
“Mungu wangu wee! Asitufikie….!
Asitukamate…..! Tujitahidi Kibwe
ndugu yangu!” Hanga alikuwa
akisema huku akikimbia.
“Ukinyamaza ndio utakuwa na
nguvu ya kukimbia zaidi!” Kibwe
alimwambia, huku akimkokota,
na kupaa naye, wakirukia
kwenye paa la nyumba moja,
ambako kwa bahati walikuta
kamba ndefu iliyokunjwa.
Haraka Kibwe aliikunjua ile
kamba, akafunga ncha moja
kwenye nguzo ya chuma cha
jengo.. Akamwambia Hanga
ashuke kwa kutumia ile kamba,
na kisha yeye akafuatia kwa
kuelea kushuka chini, akiponea
chupuchupu kukamatwa na yule
jini aliyekuwa karibu nao. Wawili
hao walijidondosha chini kama
buibui anavyojidondosha na
utando wake. Badala ya kuanguka
chini kabisa, walibembea na
kisha kwa msaada wa Kibwe kwa
nguvu zake zote, wakajirusha
hewani, wakilenga kuangukia
kwenye dirisha la jengo
lililokuwa mbele yao.
Wakitanguliza miguu yao, wawili
wale wakabamiza kioo cha hilo
dirisha, na wakati wakiangukia
ndani ya chumba cha jengo hilo,
vipande vya vioo navyo
vikamwagika kwenye chumba
hicho kikubwa walichoangukia,
vikitoa mlio wa kelele za
kusitusha!
Mle walimoangukia walifikia
kwenye zulia moja la fahari mno,
“Whuuuuuu!” Hanga alipumua
na huku akiinuka na kurudi
dirishani walikoingilia, ili aone
kama wale majini walikuwa
wakiwafuata au la. Alichokiona
kwenye lile paa la nyumba
walikotoka, kilifanya mwili wake
wote uzizime, kwani aligeuka
wakati muafaka, kuona jinsi
vichwa vya viumbe wale wa
ajabu sana vilivyoanza kuchukua
maumbile ya vichwa vikubwa
vya nyoka! Alimvuta mkono
Kibwe, na pamoja wakakodoa
macho, huku misuli ya Hanga
ikitetemeka, akiwa kinywa wazi,
na kubutwaika kwa kile
alichokua akikiangalia! Ilikuwa ni
mara ya kwanza kwa Hanga
kushuhudia kitu kama kile,
ukiachilia mbali pale alipomuona
yule nyoka aliyeuawa na Kibwe.
Hanga alishuhudia vichwa hivyo
vya nyoka, ambavyo awali
vilikuwa ni vichwa vya wale
viumbe wa ajabu, vikitokeza juu
ya majoho yao waliyovaa, na
kujiangusha chini kwenye lile
paa, na taratibu miili ya nyoka
wakubwa ikaanza kujidhihirisha,
iliyotambaa kwa kuambaa na
ukuta wa lile jengo, na kisha
kushuka chini! Kinywa wazi,
Hanga alishuhudia majoka yale
yakiporomoka huku yakijivua
kutoka mwenye yale majoho
Yaliyokuwa Yamevaa awali,
Yalipokuwa katika maumbile ya
wanaadamu! Yalipofika chini,
ndipo yalipokuwa majoka kamili!
“Ama kwa hakika ni ubishi wako
uliotufanya tuje kwenye mji huu
wa majoka, ambao sasa unatutosa
katika hatari hii kubwa!” Hanga
alimlaumu Kibwe, ambaye
hakusema lolote wakati ule, bali
alinyamaza tu!
Baada ya Hanga kusema maneno
hayo, mara Kibwe akashituka
ghafla, kwani alihisi kama
ameshikwa bega lake na mtu!
Alipogeuka, kitu cha kwanza
ambacho macho yake yalikiona,
kilikuwa ni urembo usiokadiriwa,
uliokuwa kwenye sura ya
mrembo mwenye uzuri wa shani!
Binti huyo mrembo alikuwa na
macho manene, ambayo kila
alipoyapepesa, yalifunikwa na
kope ndefu. Juu kidogo ya macho
hayo yenye kope ndefu,
zilionekana nyusi zilizokaa kwa
mpangilio mzuri mno, mithili ya
upinde! Mashavu yote mawili ya
yule binti yalikuwa na vibonye,
vilivyo kamilisha kazi nzima ya
urembo wa maumbile yake, na
kuifanya sura ile iliyotokea mbele
ya Kibwe na Hanga, kuwa ni ya
kipekee, na ambayo wote wawili,
hawajawahi kuona mfano wake!
“Eh……! Ah……!” Hanga alijaribu
kusema lakini hakuweza kupata
la kusema. Kibwe akasafisha koo
lake kwa kikohozi hafifu, bila
kutia neno! Wote wakasahau
kuwa yalikuweko mapandikizi ya
majoka yakiwafuata kule waliko!
“Nadhani huyu ni binti mfalme
wa majini!” Hanga
alimnong’oneza Kibwe, ambaye
alimfinya kidogo, ili
kumnyamazisha….., na wakati
huo, ikasikika sauti nyororo
ikisema,
“Hivi katika mji huu wa hatari
mmefuata nini hasa…..? Hususan
kwenye jumba hili? Na ninyi hasa
ni kina nani?” Yule binti mrembo
aliwauliza Kibwe na Hanga. Huku
wakimshangalia huyo binti,
Kibwe na Hanga walikuwa
wakijikung’uta kung’uta nguo
zao zilizokuwa zimechafuka kwa
vumbi kutokana na lile sakata la
mbio za kuwakimbia nyoka wa
kijini. Kibwe alimshangaa yule
binti kwa kuwashangaa wao
kuwepo pale, wakati na yeye
mwenyewe alikuwa kwenye
sehemu ileile ya hatari, lakini
hakudhurika kwa namna yoyote,
bali alizidi kuwa mrembo tu!
“Sasa dada yangu, mbona na
wewe uko huku? Kwani wewe ni
nani, na hapa ni wapi?” Kibwe
aliuliza .
“Kwa hakika siko hapa kwa
kupenda. Mimi ni Jasmin binti
Sultani, na hapa ni kwa mfalme
wa majini wote, yaani mfalme
“Makattani.” Alijieleza Jasmin,
akimwachia Kibwe aunganishe
mwenyewe kuhusu je, mfalme
‘Makattani’ ni nani. Kibwe
alimjua na kumuona jini
‘Makatta’ kule kwenye mji wa
chini ya bahari, aliyeitwa
‘Makatta wa Makattani.’ Hivyo
basi, akatambua kuwa mwenye
milki ile waliyokuwepo wakati
ule, alikuwa ni baba yake jini
‘Makatta!’ Kwa hiyo awali baada
ya kumteketeza jini yule ‘Makatta
wa Makattani’ kwenye mji wa
chini ya bahari kulikokuwa
kukitengenezwa vichafuzi vya
hewa safi kwa binaadamu, mara
hii ya pili yaelekea kuwa Kibwe
alimteketeza nduguye jini
Makatta, Maimuni, ambaye naye
alikuwa akifanya uovu wa
kuwachukua wana wa Sultani!
“Kwa hiyo Jasmin, unafanya nini
katika milki ya mfalme
‘Makattani’ na umefikaje hapa
bila ridhaa yako?” Hanga
alimuuliza mrembo yule
aliyemuona kama mwanamke
mwenye urembo wa kijini.
“Mimi ni mwana wa kwanza wa
Sultani wa nchi ya Shamsi. Niko
huku nafanya kazi za kitumwa
kwa mfalme ‘Makattani.’
Alijieleza Jasmin, na halafu
akawapa taarifa ambayo haikuwa
nzuri kwao!
”Ningependa pia muelewe kuwa
siku ya leo sio siku nzuri kwenu
kuwepo huku.” Aliwafahamisha
binti huyo. “Kwa kuwa Binti yake
Mfalme ‘Makattani’ yaani
‘Maimuni’ aliyetumwa kwenda
kumchukua Bhaduri binti Sultani
na kumleta huku kutumikia
kwenye milki ya baba yake,
hajaonekana tangu alipoondoka
saa tano asubuhi” Jasmin
aliwaeleza wale vijana, akisisitiza
kuwa ujio wao kule
hautatafsiriwa vizuri na jamii ya
majini, kwani raia na jamaa zake,
wana wasiwasi kuwa huenda
wanaadamu wamemdhuru!”
Kama kawaida, Hanga akaanza
kukosa raha kwa hofu. “Kwani
mabinti Sultani wengine
waliochukuliwa mwanzoni
wamewekwa wapi?” H alidodosa,
ili afahamu kama wanaadamu
wafikapo kule huuawa, au la.
“Wako kwenye sebule maalum
anayopumzikia mfalme
‘Makattani.’
“Na huyo Mfalme ‘Makattani’
mwenyewe yuko wapi hivi sasa?”
Hanga aliuliza, akitaka kujua jinsi
atakavyojihami, endapo mfalme
huyo atatokea pale ghafla!
“Mfalme huyo wa majini yuko
pamoja na wadogo zangu, ambao
hivi sasa wanaendelea na kazi ya
kumkanda , wakati yeye
amelala.” Jasmin aliwaambia,
akimwacha Hanga hoi,
akiwahofia hao mabinti
wanaokaa pamoja na hilo nduli,
bila kujua ni wakati gani
litawageukia na kuwadhuru!
Kibwe naye alibutwaika mno
kusikia hivyo, akiwaza kuwa pale
walipokuwa, ni mahali pa kutia
hofu sana. Wakati huohuo,
Jasmin akawatanabahisha kuwa
mpaka wakati ule walikwisha
poteza muda wa kutosha, kwani
wale majini waliokuwa
wakiwafuata, ni askari wa
Mfalme Makattani, na walipewa
amri ya kufuatilia habari ya
Maimuni binti Makattani. “, Haya,
twende huko kwa wadogo zako,
haraka!” Kibwe alimwambia
Jasmin, huku akamshika mkono
ili wakimbie, na wakati huohuo
akimwashiria Hanga afuate
nyuma. “Leo nimekuja
kuwachukuweni wewe na
nduguzo.” Kibwe alisema kwa
kujiamini, wakati Jazmin na
Hanga wakishangaa kumsikia
akisema hivyo. Hawakuelewa
jinsi gani alivyopanga kukimbia
na Jasmin na nduguze watano,
wakati kundi zima la askari wa
kijini lilikuwa likiwafuata kwa
kasi kubwa. “Sidhani kama
unaelewa unachokisema ndugu
yangu. Hivi unadhani utapita
wapi baada ya kutuchukua?”
Binti Sultani yule alimuuliza.
Lakini Kibwe hakumjibu, bali
alimwonyesha ishara ya kwamba
yeye aongoze njia tu, kuelekea
huko walikokuwa
nduguze. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipoingia kwenye hiyo sebule
kubwa ya mfalme ‘Makattani,’
wale vijana wakashangaa kweli
kweli, kwani kwenye kitanda
kikubwa kupita kiasi, lilionekana
joka kubwa mno, kuliko hata lile
lililokuwa na vichwa saba,
aliloliua kibwe! Joka hilo ambalo
ni mfalme wa majini, lilienea
sebule nzima kwenye kitanda
hicho kikubwa cha ajabu. Kitanda
hicho kilizungukwa na mabinti
Sultani watano waliochukuliwa
awali na joka kuu, ‘Maimuni’ wa
Makattani, pamoja na mabinti
wengine wengi warembo,
waliopelekwa kule baada ya
majini kuzamisha mitumbwi na
ngalawa zipitazo kwenye mito, na
pia meli kubwakubwa
zinazosafiri kwa njia ya bahari.
Ajabu ni kwamba kila mmoja
alishikilia mchi mdogo wa
kutwangia vitunguu na viungo
vingine jikoni, na wote walikuwa
wakimtwanga mfululizo, mfalme
‘Makattani!’ Kilichowashangaza
zaidi ni kwamba wakati mabinti
Sultani walipokuwa
wakimtwanga Mfalme yule wa
majini, ‘Makattani,’ yeye alikuwa
amelala fo, fo, fo!
Kule nje kwenye majabali
alikokuwa ameketi Bhaduri binti
Sultan, alisubiri kwa muda mrefu
sana, hadi akahisi kuwa huenda
Kibwe na mwenzake
walimtelekeza. “Yule mmoja
aliyepambana na lile joka,
ameondoka na fuko lake
mgongoni, kwa hiyo sidhani
kama anayo sababu ya kurudi
tena huku. Labda amekwisha
kwenda zake, au labda ameuawa
na majoka ya mtoni….” Hayo ni
mawazo yaliyokuwa yakipita
kichwani kwa Bhaduri, na wala
hakupata jibu. Akapata hofu
kubwa kwamba anaweza kutokea
nyoka mwengine mkubwa na
kumchukua!
Lakini masikini! Laiti kama
angefahamu yaliyokuwa
yakiendelea kule chini ya mto,
ambako ni himaya ya jamii ya
majini, na ambako ndugu zake
wote walikuwa ni watumwa wa
Mfalme Makattani, angetaharuki
zaidi!
Wakati Kibwe, Hanga na Jasmin
wakikimbilia kwenye hiyo sebule
kubwa ya jini Makattani, mara,
kama muujiza, wakasituka
kuwaona wale majini, askari wa
Mfalme Makatta, wamekwisha
ingia kwenye sehemu ya gorofa
ya juu walipoangukia kibwe na
Hanga, wakati walipojibembeza
na kamba kutoka kwenye jengo
la jirani!
“Haaa! Wameingia jamani! Na sio
majoka tena bali sasa ni yale
majini marefu! Harakisheni
jamani!” alisema Hanga
kuwatahadharisha wenzake.
Wakati wakikimbia ili kuingia
kwa Makattani, Kibwe
alikumbuka maneno ya muhimu
sana ya mzee wa busara.
“Kwenye bustani ya jumba la
Makatta, ipo chemchemi ya maji,
na kwenye chemchemi hiyo,
huelea kibatali kidogo chenye
mwenge mdogo wa moto.
Mwenge huo ndio roho za majini
yote ya huko, isipokuwa mfalme
wao ambaye roho yake
hushikiliwa na hirizi kubwa sana
inayoning’inia chini ya mti
uliopandwa karibu na
chemchemi hiyo. Ili kuwateketeza
majini wa huko, lazima uzime
hicho kibatali, na uikate kate hiyo
hirizi yenye roho ya mfalme wa
majini.” Mzee wa busara
alifahamisha kuwa kwa kufanya
hivyo, majini wataathirika kwa
njia mbalimbali.
Kibwe alimgeukia Jasmin na
kumuuliza, “Ni mlango upi
unatokea kwenye bustani ya
mfalme Makatta?” Yule binti
akanyoosha mkono wake,
kumwelekeza ulipo.
“Wewe nenda kwa wadogo zako
na mnisubiri huko. Hanga, haraka
nifuate!” Moja kwa moja kibwe
aliongoza hadi bustanini,
akifuatiwa na mwenzake Hanga.
Nyuma yao, kama upepo, wale
askari wa Makattani walielea na
kuwatangulia vijana wale,
wakiizingira ile chemchemi ya
uhai wao. “Haraka sana irukie ile
hirizi mtini, na uizungushe
hewani mara nyingi!” Kibwe
alimwambia Hanga, aliyekuwa
hodari kwa kuruka. Bila kupoteza
muda, kijana yule akainua miguu
yake mirefu na kuchukua hatua
mbili kabla ya kujirusha na
kuning’inia mtini, akizuka na ile
hirizi kubwa ya
kimazingaombwe! Wakati ule
wale majini waliojitahidi kuelea
kama upepo ili kumzuia Hanga,
walikwisha chelewa kwa
sekunde! Walipohisi hatari
iliyokuwa mbele yao, wakaanza
kurudi nyuma, wakijiweka mbali
na Hanga, kabla hawajatahamaki
na kumuona kijana yule
akiizungusha ile hirizi! Hamadi,
mara ukazuka upepo mkali mno
uiliowakumba wale majini na
kuwamwaga upande mmoja!
Kibwe naye aliruka na kujaribu
kukiwahi kile kibatali
kilichokuwa kikielea kwenye
chemchemi! Mmoja kati ya majini
aliyeangukia karibu na Kibwe,
alimshika mguu wake! Hanga
alipoona vile, haraka
akaizungusha ile hirizi mara
nyingi sana, na tena kwa nguvu
zake zote! Afana aleik! Kwa mara
hii, upepo mkali zaidi ulitokea na
kuwazowazowa wale majini,
ukawabwaga upande mmoja,
walibaki wakielea sehemu moja,
wakikosa uwezo wa kwenda
popote!
Wakati huo, mfalme Makattani
alianza kuamka pale mahali
alipokuwa amelala fo fo fo kwa
kipindi cha miaka mingi iliyopita,
bila kuamka! Kadiri alivyokuwa
akitwangwa na wale mabinti,
ndivyo alivyozidi kulala! Siku ile
alipoanza kuamka, wale mabinti
wote wakasituka na kushangaa
sana. Mara wakamuona mfalme
yule wa majini akianza
kubadilika kutoka kwenye umbo
la joka kubwa la ajabu, na kuwa
kiumbe mmoja mwenye umbo la
ajabu sana! Alionekana akiwa na
kichwa kirefu na kipana sana,
chenye uso wenye macho manne
makubwa, yaliyofunikwa na
sehemu ya nyusi iliyokuwa kama
nundu kubwa mbili! Kiumbe
huyo alikuwa na mikono mine
mirefu kupita kiasi, miwili kila
upande,iliyokuwa haina mifupa,
kwani ilikuwa na uwezo wa
kujinyonga nyonga kama nyoka!
Kila mkono uilikuwa na vidole
sita, vilivyoning’inia mithili ya
mikia ya pweza! Na miguu yake
minne, miwili kila upande, nayo
ilikuwa na uwezo wa kutambaa
kama nyoka, na pia kukamata
kitu chochote kwa nguvu za
ajabu. Ama kwa hakika, umbo
lake zima baada ya kubadilika,
lilifanana na umbo la buibui,
lakini katika mwili mkubwa mno
kuliko buibui!
Kwa kutumia mdomo wake
ulioonekana kama wa sokwe mtu,
Mfalme wa majinni, Makattani
alipiga ukelele uliorindima hadi
matumboni mwa kila
mwanaadamu aliyeusikia, na
kisha kwa mlio wa hasira wa
kukoroma uliotingisha miti yote
na kudondosha matunda
yaliyokuwa kwenye bustani yake,
jinni huyo akanena. “Ni nani
huyo anayethubutu kuniamsha
mimi Makattani wa Samsuri!”
Wale mabinti wote waliokuwa
wakimkanda Makattani bin
Samsuri, walianguka na kuzirai!
Jinni hilo katika umbo lake la
ajabu, likainuka kitandani na
kujitingisha, na kisha likaiongoza
miguu yake mirefu iliyokuwa
kama nyoka wanne, na miguu
hiyo kama nyoka, ikaanza
kutambaa na kumfanya
Makattani taratibu atoke kule
ndani, akielekea kwenye bustani,
huku mikono yake nayo
ikikamata nguzo na vikuta, ili
kujirahisishia mwendo!
Alipotokea kwenye bustani katika
umbo hilo na mwendo wa
kustaajabisha, Hanga aliyeanza
kumuona, akashikilia mdomo
wake kwa mastaajabu! Wakati
huo hakukumbuka kuwa alikuwa
ameshikilia hirizi ambayo ndiyo
iliyokuwa ikiwanusuru na vitimbi
vya majini! Bila kuelewa,
akaiachia hirizi ile ya miujiza,
iliyoanguka chini karibu ya
miguu yake. Kwa tukio hilo, wale
majini i ambao ni askari wa
Makattani, wakaanza kukusanya
nguvu, na taratibu wakamfuata
Kibwe, aliyekuwa akifuata kile
kibatali kieleacho kwenye
chemchemi, kwa nia ya kukizima.
“Moshi wa hicho kibatali baada
ya kuzimika, utawazingira majini
wote, ambao nao watageuka
kuwa moshi, na kuchanganyika
na moshi wa kibatali kabla ya
kuyeyukia angani!” Kibwe
aliambiwa na Mzee wa Busara
hapo awali. Alikumbuka pia
kuwa mzee huyo alimwambia
Hanga atahadhari kwa vyovyote
vile, asithubutu kudondosha ile
hirizi, na kwamba akifanya hivyo,
majini watapata nguvu upya, na
hivyo kumshambulia Kibwe
atakayeonekana kuwa anatishia
maisha yao!
Masikini Kibwe alikwisha kuwa
mikononi mwa yale majini ambao
ni askari maalum wa Makattani!
Wakati huohuo jini Makattani
naye alikuwa akijitoa sebuleni
kwake na kuwasili kwenye ile
bustani. Alijiburuza na kutambaa
mithili ya buibui, na kisha akatoa
ukelele mwingine wa aina yake,
kama vile mtu anaye kuna nazi
kubwa sana kwenye mbuzi
kubwa!
“Kirrrrrrraaah! Kirrrrrrrraah!
Kirrrrrrraaah!” Jini makattani
lilikoroma hivyo, na huku
likimaka kwa hasira likisema;
“Mleteni hapa kwangu huyo
kijana mkorofi!” Aliwaamuru
askari wake. Wakati huo, Hanga
alizinduka kutokana na lile
butwaa alilolipata baada ya
kumuona jini Makattani katika
umbile lake la kustaajabisha! Na
hapohapo, Kibwe naye akapiga
kelele za kumzindua Hanga,
wakati wale askari wa kijini
walipokuwa wakimpeleka kwa
mfalme wao kama
walivyoamrishwa. “Hangaaaa!
Hangaaa! Acha kushangaa!
Haraka sana okota hiyo hirizi!”
Hanga akagutuka na kwa wepesi
usio kuwa wa kawaida, akadiriki
kuiokota hirizi ile wakati ambapo
mmoja kati ya askari wa kijini
aliwasili akielea hewani kama
samaki baharini, pale mahali
alipokuwepo Hanga, ili
kumuwahi. Lakini wapi!
Alikwisha chelewa! Baada ya yule
kijana kuidhibiti ile hirizi, alianza
kuisukasuka na kuitingisha kwa
nguvu zake zote, zaidi ya vile
alivyoelekezwa na Mzee wa
Busara, Kakakuona! Alizidisha
nguvu na kuisukasuka ile hirizi
mara chungu nzima! Halafu wee!
Kasi ya upepo uliotokea kwa
mara ile ya tatu, ilikiuka ile kasi
ya awali, na badala yake, upepo
huo ukachanganyika na tufani
kubwa, iliyotingisha ardhi na
kuipasua, na wakati huohuo
kusababisha mafuriko makubwa
ya maji!
Wakati yakitokea hayo
yaliyosababishwa na Hanga,
majini wengi walizolewa na
upepo mkali, na wakati huohuo,
baada ya Kibwe kuachiwa huru,
akawahi kukifikia kile kibatali
kilichokuwa kwenye chemchemi
na kukizima! Lo! Moshi uliotoka
kwenye kibatali hicho kidogo,
ulianza kufunga na kutanda
katika bustani, na kuwafunika
wale majinni, waliogeuka moshi
uliojiunga na ule uliotoka kwenye
kibatali! Kibwe na Hanga
wakauona moshi ule ukiyoyoma
angani na kupotelea huko! Hata
hivyo, hali hiyo iliyotokea
haikumdhuru mfalme wa majini
asilani. Wakati Kibwe alipotaka
kuwahi kwenda kwa Hanga na
upanga wake ili kusaidia kuikata
kata ile hirizi, Makattani ghafla
aligeuka ndege aliyeruka moja
kwa moja hadi kwa Hanga,
akikusudia kumpokonya ile hirizi.
“Irushie kwangu upesi!” Kibwe
alimwambia Hanga, ambaye
haraka alifanya hivyo. Bila
kupoteza muda, Kibwe alitoa
upanga wake kiunoni, na
kuuzungusha hewani, na wakati
hirizi ile bado iko hewani,
akaiwahi kabla haijatuwa, na
hivyo kuikata katika mapande
mawili!
“Aaaaaaaaaagh! Aaaaaaaaaggh!
Jini Makattani aliugulia huku
akigaagaa chini mithili ya buibui
anaposhambuliwa! Baada ya robo
saa, jini yule akayeyuka kama
kwamba hakuwepo pale kabisa!
Katika saa moja iliyofuatia, kila
kitu katika jumba lile la mfalme
wa majini kikawa kimya na
shwari, wakati wale mabinti
waliokuwa wakifanya kazi ya
kumkanda mfalme yule,
wakizinduka baada ya kuzirai!
“Jamani, kimetokea nini hapa?”
Waliulizana kwa mshangao,
kwani kulikuwepo uharibifu
mkubwa wa vitu na mazingira.
Hali ile ilipotulia na wale mabinti
Sultani wote sita walipotoka nje
kwenye bustani, Kibwe na Hanga
waliduwaa,kuona jinsi mabinti
wale walivyoshindana kwa uzuri!
Dada yao Jasmin aliligundua hilo
mara moja, akaelewa kuwa wale
vijana walibabaishwa na wadogo
zake, kama walivyobabaika mara
baada ya kumuona yeye!
“Hawa watano ni wadogo zangu,
na majina yao ni Sabrina, Samiya,
Samira, Shamshir, na Shabnam.”
Binti yule aliwatambulisha
nduguze. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vijana wale walishangaa kusikia
majina yale mazuri, na
yaliyoanzia na herufi ‘S.’ Ila
walitaka kujua kwanini majina ya
Jasmnin na Bhaduri yalitengwa
na yale ya wenzao watano.
“Kwa sababu wazazi wetu
walitaka majina ya mabinti wao
wa katikati yafanane, na kuwepo
tofauti baina ya binti zao wa
kwanza na kitinda mimba.”
Alijibu Jasmin.
Wakati mabinti wale wakiendelea
na utambulisho, masikini
hawakuwa hata na fununu
kuhusu mambo yaliyokuwa
yanatendeka kule nchi kavu
kwenye majabali, alikobaki
mdogo wao Bhaduri!
Binti Sultani ambaye ni kitinda
mimba, alisubiri kwa muda
mrefu sana pale alipoachwa na
Kibwe na Hanga. Hatimae
akatokea mchungaji mmoja na
mifugo yake, waliokuwa
malishoni, na wakati ule, aliileta
mifugo hiyo pale mtoni ili
kuinywesha maji, kwani alivizia
wakati ule maalum, akitarajia
kuwa tayari yule binti Sultani
atakuwa amekwisha chukuliwa
na lile joka kuu! Mchungaji yule
aliyeshikilia fimbo mkono mmoja
na mkuki mkono wa pili,
alishtuka sana alipoona mwili wa
lile joka liliokuwa likihofiwa nchi
nzima, eti umelala kwenye
majabali bila uhai! Mara,
akagundua kwamba yule binti
Sultani ambaye angetolewa
kafara, hakuchukuliwa kama
walivyochukuliwa wenzake wa
awali! Bahati ilioje kwake!
Lazima ajifanye kuwa yeye ndiye
aliyeliua lile joka ! Palepale
akachukua mkuki na kuanza
kuuchoma choma ule mwili wa
lile joka , huku akipiga kelele
kuita watu washuhudie kazi
aliyoifanya!
“Jamani eeh! Jamani!
Nimekwisha muua yule nduli
aliyekuwa akisumbua jamii yetu
kwa miaka kadha wa kadha! Leo
nimemuua jamani! Njooni
mshuhudie!” Yule mchungaji
alichacharika kama punguani,
akilalama bila kuwaza kuwa
huenda yule aliyeifanya ile kazi
yuko jirani na pale. Vilevile bila
kuwaza kuwa huenda Bhaduri
akasema ukweli kuhusu hali
halisi ya mambo yalivyotokea,
mtu yule mnafiki aliendelea
kujitangaza kwa kelelele!
Alichokifikiria yeye ni kwamba
mara tu, Sultani Bashar
atakaposikia kuwa yeye ndiye
aliyemuua yule nduli, bila shaka
atamuoza yule binti Sultani, na
kumfanya awe tajiri! Ajabu ni
kwamba, Bhaduri naye,
alinyamaza kimya, akimwangalia
mchungaji huyo aliyekuwa
akilalama na kujigamba!Yule
mchungaji akaukusanya ule
mwili wa lile joka, akauweka
kwenye gari lake la ng’ombe na
kuondoka nao hadi kwa Sultani,
ambako alipokewa kwa shangwe
na hoihoi! Haya, wapi na wapi!
Kazi afanye mwingine, sifa apewe
mwingine. Lakini kwa wakati ule,
hivyo ndivyo ilivyokuwa!
Sultani alituma watumishi wake
na gari la farasi kumfuata binti
yake kule mtoni! Furaha
aliyokuwa nayo haikuwa na
mfano, kwanza kwa kumpata
mwanae, na pili kwamba raia
wake hawatasumbuliwa tena na
lile joka, na watachota maji kwa
amani!
“Wee Nokora! Haraka sana piga
mbiu ya mgambo uwatangazie
raia wangu habari hii njema! Na
pia uwaambie kuwa kutakuwa na
sherehe kubwa ya kumuoza
mwanagu kitinda mimba kwa
shujaa aliyetuokoa na tatizo lile la
kudumu!” Sultani alimwamuru
mtumishi wake.
Shamrashamra zikaanza, nchi
nzima ikachangamka, na raia
wote wakasherehekea habari zile
nzuri kwa furaha. Bhaduri binti
Sultani akaweka mkono wake
shavuni, bila kuamini jinsi
wanaadamu wanavyoweza
kukosa haya, na wakaweza
kudhulumu jasho la wenzao
kimacho macho! Alinyamaza tu,
ili aone mwisho wake!
Kibwe na kundi la wasichana
waliochukuliwa na majini na
kutumikishwa kwa mfalme
Makatta, Jasmin na wadogo zake
pamoja na Hanga, walipotoka
kwenye mji wa majini chini ya
mto, hawakumkuta Bhaduri pale
walipomuacha!
“Bila shaka alichoka kusubiri
akaamua kurudi nyumbani.”
Jasmin aliwaambia wenzake, na
akashauri kuwa na wao lazima
warudi haraka
wakawafahaimishe wazazi wao
kuwa wako hai, waweze
kuwatambulisha kwa baba yao
wale wasichana wengine
waliochukuliwa na majini kutoka
sehemu mbalimbali za dunia bila
ridhaa yao, ili wafanyiwe mpango
wa kurudishwa kwa wazazi wao.
Wakati binti yule akiyasema
hayo, Hanga alikuwa akiangaza
kila sehemu, akijaribu kuelewa
kuwa je, ule mwili wa lile joka la
kutisha ulipelekwa wapi? “Hivi
Kibwe ulibeba vichwa tu vya yule
nyoka Maimuni, au uliubeba na
mwili wake wote? Mbona siuoni
mahali popote?” Kibwe alicheka
sana kwa mas-khara hayo ya
Hanga.
“Ningetembea nao vipi mwili ule,
na hapohapo niweze kufanya
yote tuliyoyafanya huko
tulikotoka? Mwili kama ule
unahitaji kubebwa kwa gari la
farasi au gari la ng’ombe! Na bila
shaka aliyeuondoa hapa
aliuondoa kwa kutumia kitu
kama hicho!” Kibwe alimjibu
Hanga, ambaye kama kawaida
alidodosa kutaka kujua je, Kibwe
anafikiri kuwa ni nani
aliyeuondoa huo mwili?
“Tusubiri tu, na bila shaka
tutafahamu baada ya muda si
mrefu,” alijibiwa na Kibwe, na
kisha, wote wakaondoka kule
mtoni kuelekea kwenye jumba la
Sultani Bashar, ambako
hawakujua kuwa kulikuwa na
sherehe kubwa kupita kiasi!
Kila walikopita, Kibwe na
wenzake walikuta shamrashamra
mitaani. Kila mtu alionekana
kuwa mwenye furaha kubwa, na
kwa mara ya kwanza baada ya
miaka mingi, mji ya Majabali
katika nchi ya Shamsi,
ulichangamka kupita kiasi.
Jasmin binti Sultani na nduguze
waliwaambia Hanga na Kibwe
kuwa awali, hali ya mji wao
haikuwa ya kawaida hata kidogo.
“Bila shaka kuna hafla ya aina
fulani,” alinena Sabrina binti
Sultani, na Samiya na Samira
nao, waliomfuatia Sabrina kwa
kuzaliwa, wakashangaa kusikia
neno hafla, ambalo katika muda
wote wa utoto wao, hawakuwahi
kulisikia, kwani mji wao
umekuwa kwenye hali ya misiba
kila mwaka!
“Au tuseme baba ameandaa hafla
maalum ya kumpokea Bhaduri?”
aliuliza Samiya.
“Kama hivyo ndivyo, subirini
muone jinsi sherehe hizo
zitakavyozidi, mara baba
atakapotuona tukiwasili
nyumbani!” Sabrina naye
akawaambia wadogo zake kuwa
wajiandae kuona jinsi wazazi
wao watakavyosituka na
kushangaa kwa kuona sura za
mabinti zao waliodhaniwa kuwa
wameitoka dunia kwa miaka
mingi sasa! Mara tu baada ya
maneno hayo ya Sabrina binti
Sultani, ukasikika mdundo wa
goma kubwa likiwazindua raia
kusogea karibu kupokea taarifa
za Sulitani wao. Waliyoyasikia
kina Sabrina hayakuwa ya
kawaida!
“La mgambooo! La mgambooo!
Likilia lina jamboo! La
mgambooo! Leo jamani asiye
mwana aeleke jiwe! (abebe jiwe)
Raia wote wa mji huu wa
majabali nchini Shamsi,
mnaalikwa kwenye viwanja vya
tamasha katika kasri la Sultani,
kusherehekea ndoa ya mwanae
kitinda mimba, aliyenusurika
kuchukuliwa na lile joka kuu!
Wote msikose kuhudhuria!”
Waliposikia tangazo hilo, Jasmin
na wadogo zake wakaupata
ukweli wa mambo. Lakini sasa,
anayemuoa mdogo wao ni nani?
Shabnam, binti Sultani
aliyemuachia ziwa Bhadura,
yaani bibi harusi mtarajiwa,
akavunja ukimya uliotawala
wakati wote walipokuwa
wanajaribu kuelewa ni nini hasa
kiini cha lile ‘lamgambo’.
“Nadhani hii ndoa ya haraka
haraka hivi, mara tu baada ya
Bhaduri kurejea nyumbani, ina
walakini kabisa!” Samiya na
Shamshir hawakumuunga mkono
kwa kutia neno lolote, bali wote
wawili wakaitikia kwa vichwa na
mguno wa pamoja;
“Mmmmhuuuu!” Na kisha Hanga
aliyenyamaza kwa muda mrefu
pamoja na mwenzake Kibwe,
akasema kuwa kwa kuwa hali ile
inaelekea kuwa ni ya kutatanisha,
hususan kwa kuzingatia kupotea
kwa mwili wa lile joka, ni
muhimu sana waharakishe kufika
kwenye hilo jumba la Sultani.
Kibwe naye, huku akilipapasa
fuko lake mgongoni, alitabasamu
tu, alipotafakari kuhusu wingi wa
busara za Kakakuona!
Bhaduri binti Sultani kwa mara
nyingine, alipambwa kama
alivyopambwa awali ili kutolewa
kafara kwa joka kuu la mtoni,
kwa faida ya raia wa mji wao wa
Majabali, katika nchi ya Shamsi.
Mara hii tena, baada ya
kunusurika na nduli wa mtoni,
binti yule alikuwa akitayarishwa
kama vile kwa kutolewa tena
kafara, kwa mtu aliyedai kumuua
huyo nduli ambaye angemchukua
kule mtoni kama kafara! Kwa
Bhaduri hali zote mbili zilikuwa
zikimkandamiza tu. Bahati
mbaya, kitinda mimba yule
hakuweza kusema lolote, kwani
hakuwa na ushahidi wowote wa
hoja yoyote atakayoitowa kuhusu
mtu aliyefanya kazi kubwa ya
kumuua yule nduli. Tatizo ni
kwamba, yule kijana na
mwenzake, wote walipotelea
chini ya mto! “Nitaelezea vipi
habari zao kwa kadamnasi hii ya
watu, wakati ambapo sina
uhakika wowote wa uhai wao,
kwani sijui kama wazima au
wameuawa na majoka ya huko
baharini.” Binti Sultani yule
alizidi kutafakari, na hatimae
kuamua kukaa kimya tu, liwalo
na liwe!
Katika jukwaa maalum, yule
bwana harusi aliketi akisubiri
ndoa ifungwe. Kwenye uwanja
wa matamasha, raia walifurika
kushuhudia shujaa wao
aliyewaokoa na msukosuko wa
kupata maji, akimuoa binti
mrembo wa Sultani wao! Nyimbo
na ngoma mbalimbali zilitawala
eneo lile, pamoja na mashairi na
tenzi bila kusahau vicheko na
furaha. Walichokua
hawakukifahamu ni kwamba
punde, hali ile yote ingebadilika,
kama kupepesa kwa macho!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe na wale mabinti sita wa
Sultani pamoja na mabinti
wengine waliochukuliwa bila
ridhaa zao na kutumikishwa na
majini, waliwasili kwenye ile
hafla maalum ya ndoa ya
Bhaduri, katika wakati muafaka
kabisa! Walipowasili, Sultani
alikuwa akimsifu shujaa
aliyemuua nyoka, aliyeisumbua
jamii ya mji wa Majabali nchini
Shamsi, wakati mtu yule aliyedai
kuwa ndiye aliyefanya kazi ile
ngumu, akiwa amesimamishwa
kadamnasi, juu kabisa ya
membari, ili watu wote
wamuone!
“Bila ushujaa wake, licha ya raia
wote kuendelea kusumbuka
kutafuta maji, lakini pia
ningempoteza binti yangu mmoja
aliyebaki, baada ya kuwapoteza
wanangu sita katika kipindi cha
miaka sita!” Sultani aliwaambia
raia wake, kabla ya ndoa
kufungwa. Wakati hayo
yakisemwa, msururu wa takriban
mabinti ishirini na sita, uliingia
mahali pale, wakifuatiwa na
vijana wawili. Watu wote
wakasahau kwa muda, kuhusu
hafla maalum iliyoandaliwa kwa
heshima ya shujaa wao, na
macho yote yaliwageukia hao
walioongozana wakiingia kwenye
uwanja wa sherehe, kama
kwamba ile sherehe iliandaliwa
kwa ajili yao! Baada ya hapo,
kukawa kimya! Kilikuwa ni kimya
kizito mno, kiasi kwamba hata
pumzi ya watu wakipumua
iliweza kusikika! Sultani alipigwa
butwaa lisiloelezeka! Bwana
harusi mtarajiwa naye,
akatahayari kuwaona mabinti
sultani sita miongoni mwa kundi
la wale mabinti walioingia pale!
“Sijui wale vijana wawili ni kina
nani?” alijiuliza yule mfugaji,
huku akianza kugwaya kwa hofu
na tahayuri!
“Naam, Maulana, Mheshimiwa
Sultani! Tuwie radhi sana kwa
kuivamia hafla hii bila taarifa,”
Kibwe alianza kujieleza, alipoona
kaumu nzima iliyokuwepo pale
ikiwashangaa! Na pia alipoona
kuwa kila mtu aliyehudhuria
mahali pale, ghafla hakuelewa
kilichokuwa kikiendelea! Sultani
alifungua mdomo kusema, lakini
hakuna maneno yaliyotoka.
Malkia akashuka kwenye kiti cha
enzi na moja kwa moja
akakimbilia kule walikokuwa
wale wasichana, na alipofika
karibu yao, hakujua amkumbatie
nani! “Aah! Ama kweli Mwenyezi
Mungu ni mkubwa! Hivi hawa ni
wanangu kweli?” Mke huyo wa
Sultani alihamanika na
kubabaika, akiwaita majina
wanawe mmoja mmoja, huku
akikagua na kuzingira sura ya
kila mmoja kwa viganja vya
mikono yake miwili, kila
alipomtaja jina lake. “Ah!
Mwanangu Samira….! Mwanangu
Sabrina…! Jamani Samiya wangu
wee! Nawe ni Shabnam kipenzi
changu! Shamshir nawe
hujabadilika kabisa! Ooooh!
Mama huyoo! Jasmin mashavu
wangu! Umewalinda wadogo
zako wote na kuwalea vema hadi
mkarejea na afya nzuri kabisa!
Kisha akawageukia Hanga na
Kibwe na kuwaambia, “Sidhani
kama kuna haja ya kuuliza kuwa
mabinti zetu waliwezaje
kunusurika na kurejea salama
nyumbani! Kabla hamjajieleza
zaidi, natoa shukurani zangu za
dhati kwa kunirejeshea
wanangu!” Vijana Kibwe na
Hanga wakanyamaza kimya,
wakipata faraja kubwa kuona
jinsi mzazi yule alivyofurahi!
Wakati huo, Sultani naye
akazinduka kutoka kwenye
msituko alioupata baada ya
kuwaona mabinti zake. Alihisi
kuwa kutokana na hali ile
iliyojitokeza, yalikuwepo maelezo
ya kina ambayo kila mmoja
alistahili kuyasikia! Muda wote
wa yale matukio pamoja na
taharuki ya Malkia, watu wote
walikuwa kimya. Baada ya Malkia
kuwashukuru kibwe na Hanga na
kwenda kuchukua nafasi yake
katika kiti cha enzi ubavuni mwa
Sultani, minong’ono ikaanza!
“Jamani, haya ni maajabu
makubwa! Mabinti hawa sio wale
walioliwa na nduli wa mtoni?
Sasa leo hii wametoka wapi
tena?” Mmoja alimuuliza
mwenzake, ambaye alimkatisha
asiendelee na maneno yale,
akihofia wasije wakaeleweka
vibaya na jamii ya Sultani.
“Nahisi mwenzangu wewe
hujipendi kabisa! Aliyekwambia
kuwa mabinti wale waliliwa na
nduli ni nani? Achana na uvumi
utakaokutosa mahali pabaya
ndugu yangu wee!”
“Eeeh! Kwani nani amenisikia
jamani na nilikuwa
nakunong’oneza wewe tu? Haya!
nimenyamaza!” Wengine
walinong’ona kuhusu lile kundi
la wasichana wasiowajua! “Aisee!
Hivi wale vimwana ndo kina
nani? Nao ni wana wa masultani,
nini? Maana wanarusha roho
kwelikweli! Laiti kama…”
Mwenzake akamzuia kuendelea
na maneno yale, na kumwambia,
“Ndiyo! Kama kawaida yako!
Laiti kama ungepata fursa ya
kuongea na mmoja …..na hivi na
hivi! Siku moja utaponzeka nawe!
Hebu achana na mambo hayo, na
tusikilize hatima ya matukio ya
leo!” Mara, kijumbe mtangazaji
wa taarifa za jumba la Sultani
akaanza kupiga goma lake, ili
kupata usikivu wa raia wote!
“Haya, haya! Mabibi na
mabwana! Tunyamaze na tutulie
ili kumpa nafasi Mheshimiwa
Maulana Sultani aongee. Kama
mlivyoona, kumekuwa na
mabadiliko ya matukio, tofauti na
mpangilio wa awali. Baada ya
muda si mrefu, kila mmoja wenu
atapata majibu ya maswali yake.
Karibu Mukufu Waziri Mkuu
umkaribishe mtukufu Sultani
aendelee.” Sultani alipoanza
kuongea, kwanza kabisa
aliwataka Kibwe na Hanga
wajieleze na kuweka wazi
kitendawili kilichojitokeza mahali
pale.
“Ningependa kujua kuwa ninyi ni
kina nani, na mmewapata wapi
hawa mabinti zangu waliopotea
miaka mingi iliyopita.”
Minong’ono ikarudia palepale!
“Eeheee! Hilo neno jamani!
Lazima tupate maelezo hayo!”
walisema baadhi ya watu, na
wengine wakawa wanagunaguna
na kutingisha vichwa. “Hebu
tusikilizane! Hamtayasikia
mnayotaka kuyasikia kama
mtaendelea hivyo! Tusikilizane
jamani!” Alisema kijumbe wa
Sultani. Baada ya muda, Kibwe
akaanza kujieleza.
“Mtukufu Sultani wa nchi hii ya
Shamsi, jina langu ni Kibwe
mwana wa Ilunga Mbuyu wa
Kala, na mwenzangu ni Hanga
mwana wa Hazari Basari Nkulu.
Tulikutana tulipokuwa katika
harakati zetu za kutafuta hali ya
maendeleo ya kijamii, na tangu
wakati huo, tumekuwa
tukitembea pamoja,” Kibwe
alieleza pia kuwa yeye na
mwenzake Hanga walikutana na
wale mabinti zake kwenye nchi
ya majini, ambako walikuwa ni
watumwa! Maneno hayo
hayakuaminiwa kabisa na kaumu
iliyohudhuria mahali pale.
“Bwana mdogo, heshimu mahali
hapa, maana ni mahali pa
heshima na utukufu mkubwa.
Acha maskhara na tueleze
yaliyojiri huko utokako. Mbona
uyasemayo ni kama simulizi za
paukwa pakawa?”aliuliza waziri
wa Sultani, akimshangaa yule
kijana kwa kuanzisha porojo zile.
Hanga alicheka kusikia maneno
ya waziri, na kisha, kama vile
kuongezea mafuta ya taa kwenye
moto uliokwisha washwa,
akasema; “Kwa hiyo mheshimiwa
waziri, ukiambiwa kuwa huyo
kijana mwenye maskhara na
simulizi za kale, ndiye aliyemuua
yule nduli kule mtoni, na wala si
huyo bwana harusi wenu
mtarajiwa, utasema nini?”
Kimya!
Katika watu waliohudhuria hafla
ile, hakuna hata mmoja
aliyesema kitu! Kila mtu alizama
kwenye dimbwi la mawazo
mazito!
“Kijana, hebu sogea hapa mara
moja!” Waziri wa Sultani
alimwita Hanga aende karibu
yake.
“Wewe unao ushahidi gani wa
maneno uliyoyasema hivi sasa?
Tuonesheni ushahidi kwamba
huyo kijana ndiye aliyemuua yule
nyoka, maana mwenzenu
ametuletea ushahidi wa nyoka
mzima. Ninyi mnasemaje kwa
hilo?” Waziri alitoa rai zake.
Wakati ule, Kibwe naye
akajisogeza kwa waziri, akapanda
kwenye membari alikokuwa yule
aliyedai kuwa ndiye aliyemuua
nyoka maimuni, na kisha
akasema kwa sauti ya juu ili kila
mtu asikie. “Nasema kwa
ushahidi kwamba mimi ndiye
niliyemuua yule nyoka. Na kama
mheshimiwa waziri na baraza
lako mliamini kuwa mwenzangu
huyu ndiye aliyeifanya kazi hiyo,
tafadhali naomba mmwambie
awaoneshe na vichwa vya huyo
nyoka mwenye mwili aliouleta
kwenu kuwa ni ushahidi!”
Kimya tena.
Watu wote wakaduwaa, hususan
Sultani ambaye awali, hakufikiria
kuulizia jambo kama hilo . Lo!
Yule laghai aliyechangamkia ile
nafasi ya Kibwe, kijana aliyefanya
kazi yote ya kupambana na joka
la ajabu, akatamani mno ardhi
ipasuke ili ajifiche humo, kwa
jinsi alivyofedheheka, pia kwa
jinsi alivyohofu hatima ya uongo
wake!
Wakati huo, waziri naye
akazinduka, baada ya kuipata
habari ambayo hakutarajia kuwa
itatoka kwa wale vijana wa
kawaida, na ili kuwabana,
alimuuliza Kibwe, “je, unaweza
kuvionesha vichwa vya joka hilo?
Palepale Kibwe akashusha lile
fuko lake kubwa alilolibeba
mgongoni, akalifungua na kisha
kumwaga chini vichwa saba vya
lile joka! Kwa hakika mahali pale
hapakukalika! Watu wote
walitimka kila mmoja akitafuta
njia ya kupitia, kwani vichwa vile
vilionekana kama vina uhai!
Kichwa cha saba kilizidi
kuwachanganya raia wote, jinsi
kilivyong’ara kama bati la shaba!
Ilikuwa ni pata shika na nguo
kuchanika. Ama kwa hakika
penye kweli uongo hujitenga, na
njia ya muongo, siku zote ni fupi
mno!
Ukweli ulipofichuka, Sultani
alitoa hukumu kali sana kwa yule
mnafiki aliyedai kuwa alikuwa
mkombozi wa raia wa Shamsi, na
wale mabinti waliochukuliwa na
majini kutoka sehemu
mbalimbali za dunia,
wakapelekwa nchini kwao kwa
wazazi wao. “Kwa hakika, pamoja
na kuwashukuru ninyi vijana
wawili shujaa, nawapa fursa hii,
ya kila mmoja kujichagulia mke
ampendaye miongoni mwa
mabinti zangu ili nimuozeshe,
tuweze kuunda udugu wa
kudumu!” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe alitabasamu, halafu
akasema, “Nafikiri
tutakapokamilisha kazi yetu na
tutakaporejea huku, tutawaachia
wao mabinti zako wachague yule
wampendaye kati yetu, ndipo
tuweze kufunga ndoa nao!”
Sultani, mkewe na mabinti zake
walicheka sana, wakikubaliana na
wazo la Kibwe, wakati Hanga
akigugumia kwa kutoridhika na
uamuzi ule wa Kibwe. Yeye
alimpenda sana Sabrina! Wakati
vijana wale walipokuwa
wakifurahi na kucheka pamoja
na mabinti Sultani, mambo kule
kusini magharibi ya mbali ya
dunia, katika eneo lililokuwa
sanjari na sehemu ya machweo ya
jua, Malkia Sharara alipungukiwa
na kichwa cha mtu mmoja, ili
kukamilisha ujenzi wa jumba
lake la ajabu la matofali ya
vichwa vya watu!
Kibwe na mwenzake wakaagana
na Sultani wa nchini Shamsi na
familia yake, na baada ya hapo
wakaanza safari yao, wakielekea
kusini, kutoka pale Kaskazini ya
mbali katika mji wa Majabali.
MWISHO
 
Sehemu Ya Tano (5)
Wakati lile joka lilipofunua
kinywa chake kwa hasira, Kibwe
akasimama kishujaa , akainua
upanga wake wa radi na
kuuzungusha, na kwa kufanya
hivyo, mara moja, kama muujiza
upanga huo ulitoa ngurumo za
radi za kusisimua, na wakati
uleule Kibwe akalibwaga panga
lile shingoni kwa hilo joka, na
sekunde chache baadae, kichwa
chake kikadondokea nchi kavu!
Lakini Joka likazidi kujitoa nje ya
maji kwa ghadhabu, na kutoa
kichwa chake cha pili, kilichokua
kikifoka na kutoa povu jingi.
Kibwe akasema, “Leo ni leo, ama
zako ama zangu.” Akainua tena
panga lake la radi ambalo safari
hii, pamoja na kutoa ngurumo,
likatoa cheche za moto wakati
lilituwa shingoni kwenye kichwa
cha pili cha lile joka lenye hasira.
Vivyo hivyo, vichwa vingine vya
joka hilo vikachakazwa kimoja
kimoja kwa dhoruba moja tu,
kwa kila kichwa, wakati upanga
ulipotoa ngurumo na cheche,
hadi kilipobaki kichwa cha saba!
Wakati huo, Hanga naye,
aliyeagizwa na Kibwe kwa bibi
kizee hapo awali, akatokea!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kimoja kati ya vichwa vyake
hivyo saba yaani cha mwisho, ni
cha shaba.” Kakakuona, Mzee wa
Busara alimwambia Kibwe.
Kichwa hicho kitakusumbua sana
kukikata, na hatimae
utakapokikata, utaanguka na
kuzirai.” Akakumbuka vile Mzee
wa Busara alivyomwambia
Hanga, kuwa atakapomuona yeye
amezirai, ammwagie ndoo nzima
ya maji, ndipo atakapozinduka.
Alipomuona Hanga akitokea
wakati akikumbuka maneno yale
ya mzee wa busara,
akamtahadharisha mwenzake
yule kuhusu jambo hilo.
“Usisahau maagizo ya mzee wa
busara. Nitakapozirai tu, mara
moja unimwagie ndoo nzima ya
maji.” Hanga akajibu kuwa
hajasahau.
Baada ya hapo, Kibwe alisimama
tena, na kuanza kupambana na
kichwa hicho cha shaba, na
wakati ule, lile joka lilikua
limekwisha choka! Kila
aliponyanyua upanga na
kuubwaga kwenye shingo ya kile
kichwa cha shaba, ulisikika mlio
kama vile panga lililopigwa
kwenye mataruma ya reli, lakini
kichwa hakikutetereka! Kibwe
hakukata tamaa, bali alizidisha
nguvu kila mara hadi katika
dhoruba ya saba, kichwa hicho
cha saba kilipoanguka, na Kibwe
naye akaporomoka chini na
kuzira! Palepale, Hanga akaruka
na ndoo ya maji na kummwagia
Kibwe mwili mzima! Lakini mara
tu baada ya kitendo hicho,
kikasikika kishindo nyuma yake
na alipogeuka, akamuona
Bhaduri naye kaporomoka chini
na kuzirai kama Kibwe! Hanga
ambaye anaposhtukizwa na kwa
ghafla kama vile hushindwa
kupata ufumbuzi wa haraka,
kwahiyo akaanza kubabaika bila
kujua la kufanya. “Sasa mbona na
huyu naye amezirai? Nifanye nini
sasa?” aliwaza, na mara,
akajishauri na kuamua kuchota
maji, huku akihofu mno, akihisi
kuwa huenda likazuka kutoka
mtoni joka jingine, labda lenye
vichwa zaidi ya saba, na
kuwazowa wote kwa kafara! Hata
hivyo, hatimae kijana huyo
aliyapata maji na kummwagia
binti Sultani. Baada ya nusu saa
ya kusubiri kwa wasiwasi huku
vichwa saba vya lile joka
vilivyoangukia nchi kavu
vikimtolea macho, punde kidogo
akawaona Bhaduri na Kibwe
wakizinduka, huku Kibwe akiwa
hoi, lakini mwenye tabasamu
kubwa usoni kwake!
Hanga na Kibwe walipokamilisha
kazi hiyo nzito, wakiuacha
mtumba wa lile joka
umejilundika nchi kavu baada ya
kujitoa wakati wa mapambano,
Kibwe akakusanya vichwa vyote
vya lile joka, na kuviweka
kwenye fuko lake kubwa la gunia
mbalo yeye hulibeba mgongoni
kila anakokwenda. Alifanya hivyo
kutokana na ushauri wa mzee wa
busara.
“Lazima ukusanye vichwa vyote
na uvichukue…kohoo..kohooo
(kikohozi) maana hivyo ni
ushahidi wako………usisahau
kabisa jambo hilo!”
Kibwe hakuelewa maana yake, na
alipouliza sababu ya kufanya
hivyo, Mzee wa Busara
alitabasamu tu, na kisha
kumalizia na kikohozi
kinachomjia mara kwa mara.
Lakini hatimae Kibwe alifahamu
kwa nini aliambiwa avikusanye
vichwa vile na kuvichukuwa.
Kibwe alimwambia Bhaduri
asubiri pale pale juu ya jabali,
kwani alitaka kuingia chini
kabisa ya mto alikotoka yule
nyoka wa aina yake, ili aweze
kupata majibu ya maswali mengi
aliyokuwa akijiuliza. Alikumbuka
pia kuwa Kakakuona, yaani Mzee
wa Busara, alimwambia kuwa lile
joka sio la kawaida, bali ni
mwana wa mfalme wa majini ya
bahari na mito. Alimwambia
kuwa majini hayo hujigeuza
katika maumbile yoyote
wanayotaka, hata maumbile ya
kibinaadamu. “Majini hao wana
miji yao chini kabisa ya mito na
bahari.” Kibwe aliambiwa na
mzee yule wa busara, na
alikumbuka jinsi alivyo pambana
na jini makata na wenzake
kwenye mji mmoja wa chini ya
bahari huko kaskazini ya mbali
ya dunia. “Huoni kwamba
kuingia huko chini ya mto ni
hatari ?” Binti Sultani alimuuliza
Kibwe, akihofu kuwa huenda
akakutana na nyoka wengi wa
aina ile. Lakini Kibwe alishikilia
jambo hilo, akisema, “Ili niweze
kuzuia matukio mengine kama
haya yasitokee tena, ni muhimu
sana nikafanye utafiti na kujua
asili ya nyoka huyu
niliyemuuwa,” Bhaduri na Hanga
wakatazamana, kuona jinsi Kibwe
alivyokuwa amejiamini kupita
kiasi!
Hanga aliogopa mno,
alipoambiwa na Kibwe kuwa
lazima wafuatane huko chini ya
mto. “Mmi-mmi-mi na-ddhani- t-
tuonndoke tu, K-ibwe! N-ni
hatari k-kuin-gia humo n-dani!”
Alisema Hanga huku akitetemeka
kupita kiasi kwa hofu. “Twende
bwana wee! Tutajua jinsi ya
kujihami tukifika huko.” Kibwe
alisema huku akimkokota
mwenzake kuelekea upande wa
mto , sehemu ya korongoni,
ambako ndiko walikoingilia
kwenda chini kabisa ya ule mto.
Bhaduri binti Sultani akabaki
kando ya mto juu ya jabali,
akisubiri.
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Twende bwana wee! Tutajua
jinsi ya kujihami tukifika huko.”
Kibwe alisema huku akimkokota
mwenzake kuelekea upande wa
mto , sehemu ya korongoni,
ambako ndiko walikoingilia
kwenda chini kabisa ya ule mto.
Bhaduri binti Sultani akabaki
kando ya mto juu ya jabali,
akisubiri.
Vijana wale walizama chini
kabisa ya mto kwa kupitia kule
korongoni, na hatimae bila
kuamini macho yake, Hanga
aliona nchi kavu! “Ha! Kibwe,
huku ni wapi tena?” aliuliza kwa
mastaajabu, kwani chini ya ule
mto, kulikuwepo mji mkubwa
wenye majumba makubwa
makubwa ya fahari! Majumba
hayo yaliyofanana, yalijengwa
katika eneo kubwa juu ya
mwinuko wa milima iliyotanda
kwa hekari nyingi mno. Mjengo
wa hizo nyumba ulifuata
mzunguko wa nusu miduara
kama saba hivi, yaani nyumba
nyingine zilikuwa katika mduara
wa kwanza kwa ndani ambao
ulikuwa mdogo, zikafuatiwa na
nyumba zilizojengwa kwa
kufuata miduara iliyoongezeka
ukubwa, kutokana na kuongezeka
kwa idadi ya miduara yenye
nyumba hizo. Nyumba zenyewe
zilijengwa kwa matufali ya mawe
ya vito vya thamani pamoja na
marumaru. Milango na madirisha
ya nyumba vilikuwa vya fedha na
dhahabu. Kwa kufuata mjengo
wa mizunguko hiyo ya aina yake,
nyumba hizo zilijengwa karibu
karibu mno. “Hee! Maajabu
makubwa haya!” Hanga alizidi
kushangaa, lakini Kibwe hakuona
ajabu, kwani tayari alikwishaona
mji wa jini Makatta na wenzake
chini ya bahari, kulikokuwa
kunatengenezwa vichafuzi vya
hewa safi iliyoko kwenye tabaka
la hewa ya ozoni. Lakini Kibwe
hakumwambia Hanga habari hiyo
wakati ule.
Huku akizidiwa na maajabu kule
chini ya mto, Hanga aliuliza.
“Lakini mbona kuko kimya hivi?
Ndio kusema wenye mji huu
wote hawapo?” Aliuliza hivyo
akihofu wasije wakavamiwa na
kutiwa hatiani na hao wenyeji,
bila tahadhari. Mwenzake
hakumjibu, ila akamuonesha
ishara ya kwamba anyamaze, ili
polepole waweze kuchunguza
wakazi hao walipo. Kwa pamoja
Kibwe na Hanga wakaambaa na
yale majengo marefu yaliyokuwa
karibu karibu, hadi walipotokea
kwenye jengo lililoonekana kama
msikiti! “La haula! Ni nini hiki?
Yaani ni msikiti au---?” Hanga
alianza udadisi wake wa kipuuzi,
na hapohapo Kibwe akamkatiza
kwa kusema, “Ndio! Ni msikiti
huo, na kama unavyoona,
takriban wenyeji wote wa mji
huu wamo humo ndani
wanasali!” Kibwe alizidi
kumfafanulia mwenzake yule,
kwa kunong’ona, akimwambia
kuwa wale wote aliowaona mle
msikitini walikuwa ni majini wa
mtoni, na ambao pia hugeuka
kuwa nyoka, wanyama
mbalimbali, upepo, au kujigeuza
katika maumbile mengine
wanayoyapenda, kulingana na
mahitaji yao kwa nyakati
zinazohusika. Kama kawaida
yake, Hanga akatoa macho pima
kwa hofu, na kisha naye
akanong’ona kama alivyofanya
mwenzake, akisema, “Ah! Ni
Kweli kabisa! Hivi sasa wana
maumbile ya binaadamu kama
alivyotuambia Kakakuona. Na lo!
wote wamevalia majoho meupe.
Haa! Ndiyo!ndiyo! Sasa
nimeelewa! Ni kwa sababu leo ni
siku ya Ijumaa, kwa hiyo watu
wote wamekuja kusali pamoja,
ndio maana mji wao wote
umepooza !” Kwa sababu ya
maajabu yale, wakati ule Hanga
alisahau kabisa hofu zake za
kawaida.
Tofauti na Kibwe aliyekuwa si
mgeni na mambo yale, Hanga
alifarijika kuyaona yale
aliyokuwa akiyasikia tu, lakini
hakuyafahamu, na ambayo
yalimshangaza kila
alipoyatambua. Mzee wa Busara
aliwaambia pia kuwa kama ilivyo
miongoni mwa binaadamu, wapo
majini wacha Mungu na wapo
wanaomuasi Mungu wao, na
kama walivyokuwapo wanadamu
wema na waovu, hali kadhalika
miongoni mwa majini, wapo
waliokuwa waovu, na wengine
ambao ni wema. “Bila shaka yule
aliyehusika na kuwachukua
mabinti Sultani waliotolewa
kafara, anatokana na jamii ya
majini waovu na wenye kumuasi
Mungu wao,” Hanga alimwambia
Kibwe, ambaye alimjibu kuwa
alihisi kuwa mabinti Sultani hao
mpaka sasa wamo mikononi mwa
majini hao waovu!
Hanga hakuamini kuwa wale
mabinti Sultani walikuwa hai
mpaka wakati ule, akihoji kuwa
ni muda mrefu sana uliopita
tangu mabinti hao wachukuliwe
na yule nduli. Iweje tena hadi
wakati ule wawe bado wako hai ?
“Kama chini ya huu mto kuna mji
mkubwa kama huu, ambao yule
nduli huwaleta wana wa Sultani,
mji ambao wakazi wake ni
viumbe wanaoweza kujibadili na
kuwa kama wanaadamu,
watashindwa vipi kuwahifadhi
kibinaadamu mabinti hao wa
Sultani, na kuwaficha miongoni
mwao, labda wakiwatumia kama
watumwa? Sasa, ikiwa kama lile
joka ni mwana wa mfalme wa
majini ya bahari na mito, basi
bila shaka chini ya mto huu yupo
baba yake, ambaye ndiye mfalme
mwenyewe, na bila shaka wale
mabinti watakuwa wapo kwenye
milki yake ya kifalme katika
himaya hii, wakifanyishwa kazi
fulani.…! Na huko ndiko
tutakakowakuta hao mabinti.
Lazima tuwahi kuwatafuta kabla
wenyeji hawajatoka msikitini!
Kibwe na mwenzake walianza
kutembea tembea katika mitaa ya
ule mji wa chini ya mto, wakiwa
macho kabisa, ili wasisitukizwe
na wenyeji na kutiwa msukosuko.
Walipokuwa wakitafuta tafuta ili
waone jumba lenye hadhi ya
kifalme, mara wakasikia sauti za
watu nyuma yao. Lo! Wakati ule
wale majini walikuwa wakitoka
msikitini, wakiwa wamevalia
majoho yao meupe kama
yangeyange! Kibwe na Hanga
walijibanza kwenye ukuta wa
nyumba moja kubwa, wakisubiri
watu wale wapite. Hanga ambaye
aliwaona viumbe wale kwa mara
ya kwanza, alistaajabu kuona
jinsi walivyokuwa warefu kupita
kiasi! Alipojifananisha nao,
alijihisi kama paka na chui! “Lo!
Ni maajabu ambayo sijawahi
kuyaona tangu nitoke tumboni
kwa mama yangu!” Hanga
alinong’ona, na Kibwe
akamfunika mdomo wake kwa
mkono ili asiendelee na maneno
yake ya mshangao, na hali wale
majini hawakuwa mbali sana na
pale walipokuwa!
Mara, miongoni mwa viumbe
wale wa ajabu, Kibwe na Hanga
wakawasikia baadhi yao
wakiulizana. “Hivi Maimuni
alirudi na yule binti sultani
kutoka majabalini?” Mwengine
akajibu, “Leo ni ajabu sana,
maana inaelekea kuwa mpaka
sasa bado hajarejea. Sijui
amepatwa na nini.”
“Usiulize kama amepatwa na nini
au vipi, maana kama huko juu
alikutana na yule kijana Ibilisi,
sidhani kama atarudi salama na
huyo binti.”
“Kijana gani tena ambaye ni
Ibilisi, na kwa nini akikutana
naye asiweze kurudi salama?”
“Kwa sababu huyo ndiye kijana
aliyenivunja huu mkono kwa
kunipiga na rungu. Sina hamu
naye asilani.”
“Hivi tuseme ulikuwa wapi
mpaka ukakutana naye, na
akakufaniya hivyo?”
“Unajua, nilipotumwa kwenda
kuzamisha meli ili kuwapata
watu wengi watakao letwa huku
kutufanyia kazi, na nikaweza
kuikamata ile meli ya Mfalme
KashKash, nilipoanza kuizamisha
tu, alitokea huyo kijana, ambaye
ghafla alinipiga na rungu
mkononi kwa nguvu za ajabu!
Nilipata machungu makubwa,
nikakimbia na kujizamisha
baharini. Sasa, kama kijana huyo
amefika huku, na akamkuta
Maimuni akimchukua binaadamu
mwenzake, bila shaka mwenzetu
huyo yumo hatiani wakati huu!”
Lo! Kibwe hakuamini masikio
yake! Hivi wale majini walikua
wameweka baraza kabisa,
barabarani, eti wakimzungumzia
yeye! Mwenyewe Kibwe alijizuia
kuporomosha kicheko! “Hivi ni
kijana gani huyo wanayemsema?
Ni wewe?” Hanga alianza
kudodosa, na hakuamini
aliposikia kuwa eti Kibwe ndiye
aliyefanya hivyo alivyoelezea yule
jinni. “Ama kweli mwenzangu
wewe una ujasiri wa ajabu
kabisa!” Hanga alimsifu Kibwe,
na akiamini kuwa kwa hakika
alikuwa ni mwana mteule, na
wala si kijana wa kawaida.
Wakati wakiwa wamejibanza
pembezoni mwa yale majengo
wakiwasikiliza wale majini,
wengine miongoni mwao
waliokuwa wakitoka msikitini,
nao wakasimama pale
walipokuwa wakizungumza
wenzao. Baada ya kusikia mkasa
uliomsibu yule aliyepigwa na
rungu, mmoja wao naye akaanza
kusimulia mkasa wake.“Labda
kijana huyo ndiye yule kijana
balaa aliyefika mjini kwetu,
akatuwekea hewa ya uvumba
iliyowateketeza wenzetu wengi,”
alisema, na kujieleza kuwa yeye
alikuwa ni miongoni mwa
kikundi kilichomfuata kijana
huyo juu ya bahari alipokuwa
akitoka mjini kwao chini ya
bahari, baada ya kuwateketeza
wenzake. “Tulishambuliwa na
cheche za moto zilizogeuka kuwa
miali ya moto, mara kijana huyo
alipotoa upanga wake wa ajabu
na kuanza kutupiga nao. Wengi
kati yetu waliunguzwa vibaya, na
wengine tulidiriki kukimbia. Kwa
hiyo, ni kweli kuna wasiwasi
kuwa kama binti wa mfalme
wetu amekutana na mtu huyo,
basi bila shaka atakuwa hatarini
hivi sasa!” alisisitiza.
Mahali walipojibanza, Kibwe na
Hanga waliweza kupata taarifa
kamili kuhusu jamii ile ya ajabu
ya majini. Kumbe wengi wao
hupatikana kwenye maji ya mito,
bahari na mabwawa. Kumbe wao
huendesha vitendo vya ukatili
kwa wanaadamu, na kwamba
pamoja na ukweli huo, zipo njia
mbalimbali ambazo wanaadamu
hutumia ili kujilinda na uharibifu
wao dhidi yao. “Watu wanao
kumbwa na majini hufukizwa
moshi wa uvumba, kwani bibi
yangu alimfanyia hivyo jirani
yetu, na baada ya hapo, , jini
huyo alikimbia na kumwacha
mhanga yule akiwa salama
salimini.” Kibwe akamfinya
Hanga kumnyamazisha, kwani
alijua kuwa endapo wale majini
wangewasikia na kuwaona,
wangewateketeza kama
walivyofanyiwa wao. Baada ya
kuyasikia yote yaliyosemwa na
wale majini, Kibwe akaelewa
kuwa pale walipo ndio hasa
mahali penyewe alipokuwa
akipatafuta, ili kuwapata mabinti
wa Sultani.
Mara tu baada ya wale majini
kuvunja baraza lao na kuondoka
mahali pale, Kibwe alimshika
mkono Hanga na kuongoza njia,
akiharakisha waondoke mahali
pale hatari, ili kuendelea na
utafiti wao wa kuwatafuta
mabinti Sultani sita. Walielekea
kwenye lile jumba la kifalme,
ambako walihisi kuwa ndiko
walikokuwa. Walipokuwa
wanaambaa kwenye majengo
marefu yaliyojipanga kwa safu,
walitembea kwa tahadhari
kubwa, huku wakinyata, ili
kujinusuru wasije wakaonwa na
wale watu wa kijini. Katika
tembea yao, ghafla Kibwe
akamuona mmoja wa wale majini
akigeuza shingo yake, kuangalia
kule walikokuwa yeye na
mwenzake! Wasiwasi mkubwa
ulimpata, kwani alihofu kuwa
katika eneo lililopambwa na
weupe wa majoho ya wale majini
hapa na pale, na kwamba katika
eneo hilo ambalo watu wote ni
warefu, Kibwe alihisi kuwa
isingekuwa vigumu kwa majini
wale kuwatambuwa kwa mbali
kabisa yeye na Hanga, na
kuwaona kuwa wao sio miongoni
mwao! Kwa kutambua hilo,
vijana wale wakaitambua pia
hatari iliyokuwa mbele yao!
“Kama hatukutafuta njia ya
kuondoka haraka katika eneo hili,
kaumu yote ile ya majini
itatuandama na kutushambulia”
Kibwe alimwambia mwenzake.
Maneno yale hayakumfurahisha
Hanga hata kidogo, kwa kuwa
yeye alikuwa ni mwoga kupita
mwenzake. “Sasa tutafanya nini
kujinusuru?” aliuliza, huku akiwa
anaangalia huku na huko kwa
hofu aliyokuwa nayo. “Kwa sasa
ni kujibanza tu, pembezoni mwa
haya majengo, mpaka wote
watakapoondoka mitaani,” Kibwe
alimjibu. Kwa hiyo walijibanza na
kuwa kimya, wakisubiri hadi hali
itakapokuwa shwari.”Sijui
wakituona na kutukamata
watatufanya nini masikini!”
Hanga alijisemesha, kama vile
hakutarajia jibu lolote kutoka
kwa Kibwe, ambaye kwa mara hii
tena, alimwashiria mwenzake
huyo anyamaze,
“sssssshhhhh!” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe naye alikuwa na hofu
kubwa, kwani alijua kuwa kwa
bahati mbaya, yeye na Hanga
hawataweza kuwatambua majini
waovu miongoni mwa kundi lile
la majini wale waliovalia sare ya
majoho meupe, isipokuwa pale
watakapoanza kuwashambulia
yeye na mwenzake. Lo! Salalee!
Wakati akiwaza hivyo, akasikia
sauti kama mluzi iliyotoka nyuma
yao, ikisema, “Angalieni kule!
Hivi wale sio binaadamu?”
Wengine wakawa wanaangalia
huko alikokuwa akionesha kidole
mwenzao, na kisha wakanena,
“Ndiyo! Wale ni binaadamu
kabisa! Wakamateni na
muhakikishe kuwa hawakimbii!
Kama mmoja wao ni yule kijana
mkorofi, lazima aadhibiwe!”
Maneno hayo yalipowafikia
Kibwe na Hanga, hawakupoteza
hata sekunde moja, kwani
walitimua mbio za ajabu, kama
upepo, wakifuata vichochoro
vilivyokuwa baina ya majengo
marefu kupita kiasi, ambayo ni
nyumba za thamani za wale
majini!
Hanga na Kibwe walikimbia kwa
nguvu zao zote bila kugeuka
nyuma, kwani walijua kuwa wale
majini nao walikuwa wakikimbia
kwa mbio za kasi ili kuwakamata.
Walipokimbia kwa muda mrefu
wakizunguka kwenye vichochoro
vya yale majengo, Kibwe aligeuka
ili kujua wale majini walikuwa
umbali gani kutoka pale
walipokuwa wao. Hanga
alipomuona mwenzake anageuka
na yeye akafanya hivyo, na halafu
lo! Kile alichokiona kilimfanya
akose nguvu miguuni,
akanyong’onyea viungo vyote,
kwa sababu ya mshituko wa hofu
na woga. Alianza kupunguza kasi
ya mbio zake! Wakati ule, ndipo
kijana huyo alipohakikisha kabisa
kuwa wale hawakuwa viumbe wa
kawaida hata kidogo, kwani
aliona macho yao yakianza
kumweka mithili ya macho ya
paka yanavyoonekana gizani! “La
haula! Sidhani kama leo
tutanusurika na hawa majini!”
alisema Hanga wakati akijaribu
kukimbia, lakini miguu yake
ikikataa kunyanyuka! Kibwe
aliyeona kuwa tayari kulikuwa na
ucheleweshaji wa mbio zao
kutokana na woga na hofu kwa
upande wa Hanga, na pia
ucheleweshaji wa mazungumzo
ya mwenzake ya mara kwa mara
kama kawaida yake, akamaka
kwa hasira, na kumwambia,
“Nyamaza na uongeze kasi ya
mbio kunusuru maisha yetu!
Acha mazungumzo Hanga!”
alisema hivyo huku akimkokota
mwenzake yule, na kwa pamoja
wakakoleza mbio za kufa na
kupona!
Wakati fulani Kibwe na Hanga
walikimbia mbio za kawaida, na
walipokuta sehemu kulikokuwa
na mapipa mengi yaliyofungwa
pamoja, waliyafungua na
kuyaachia yaporomoke kwa
nyuma yao ili kuwababaisha wale
majini. Wakati mwingine
waliruka kama ngedere hasa kwa
uwezo wa ajabu wa Kibwe
alipomkamata mwenzake
madhubuti, kila walipotokea
sehemu za miinuko ambako
waliweza kujirushia juu ya
madirisha kwenye sehemu ya
chini ya majumba yale marefu,
na kuambaa humo hadi kwenye
madirisha mengine, na kisha
kujiangusha chini kwenye
miinuko mingine. Waliporukia
madirishani, walishikilia maeneo
yaliyojitokeza kwenye madirisha
hayo, wakitambaa kwa kwenda
juu ya jengo, hatua kwa hatua,
kwa wepesi mkubwa! Vijana
wote wawili walikuwa ni hodari
sana wa michezo ya kuruka juu,
na Hanga alitumia urefu wake
kwa hodari zaidi kwani alikuwa
mrefu kuliko Kibwe, wakati
Kibwe akisaidiwa na ule uwezo
wake wa ajabu! Lakini wale
majinni waovu nao walizidi
kuwaandama, huku wenzao
wema wakiwaangalia na
kuwashangaa. Mmoja kati ya
majini wale waovu alikuwa
akiwakaribia mno wale vijana!
“Mungu wangu wee! Asitufikie….!
Asitukamate…..! Tujitahidi Kibwe
ndugu yangu!” Hanga alikuwa
akisema huku akikimbia.
“Ukinyamaza ndio utakuwa na
nguvu ya kukimbia zaidi!” Kibwe
alimwambia, huku akimkokota,
na kupaa naye, wakirukia
kwenye paa la nyumba moja,
ambako kwa bahati walikuta
kamba ndefu iliyokunjwa.
Haraka Kibwe aliikunjua ile
kamba, akafunga ncha moja
kwenye nguzo ya chuma cha
jengo.. Akamwambia Hanga
ashuke kwa kutumia ile kamba,
na kisha yeye akafuatia kwa
kuelea kushuka chini, akiponea
chupuchupu kukamatwa na yule
jini aliyekuwa karibu nao. Wawili
hao walijidondosha chini kama
buibui anavyojidondosha na
utando wake. Badala ya kuanguka
chini kabisa, walibembea na
kisha kwa msaada wa Kibwe kwa
nguvu zake zote, wakajirusha
hewani, wakilenga kuangukia
kwenye dirisha la jengo
lililokuwa mbele yao.
Wakitanguliza miguu yao, wawili
wale wakabamiza kioo cha hilo
dirisha, na wakati wakiangukia
ndani ya chumba cha jengo hilo,
vipande vya vioo navyo
vikamwagika kwenye chumba
hicho kikubwa walichoangukia,
vikitoa mlio wa kelele za
kusitusha!
Mle walimoangukia walifikia
kwenye zulia moja la fahari mno,
“Whuuuuuu!” Hanga alipumua
na huku akiinuka na kurudi
dirishani walikoingilia, ili aone
kama wale majini walikuwa
wakiwafuata au la. Alichokiona
kwenye lile paa la nyumba
walikotoka, kilifanya mwili wake
wote uzizime, kwani aligeuka
wakati muafaka, kuona jinsi
vichwa vya viumbe wale wa
ajabu sana vilivyoanza kuchukua
maumbile ya vichwa vikubwa
vya nyoka! Alimvuta mkono
Kibwe, na pamoja wakakodoa
macho, huku misuli ya Hanga
ikitetemeka, akiwa kinywa wazi,
na kubutwaika kwa kile
alichokua akikiangalia! Ilikuwa ni
mara ya kwanza kwa Hanga
kushuhudia kitu kama kile,
ukiachilia mbali pale alipomuona
yule nyoka aliyeuawa na Kibwe.
Hanga alishuhudia vichwa hivyo
vya nyoka, ambavyo awali
vilikuwa ni vichwa vya wale
viumbe wa ajabu, vikitokeza juu
ya majoho yao waliyovaa, na
kujiangusha chini kwenye lile
paa, na taratibu miili ya nyoka
wakubwa ikaanza kujidhihirisha,
iliyotambaa kwa kuambaa na
ukuta wa lile jengo, na kisha
kushuka chini! Kinywa wazi,
Hanga alishuhudia majoka yale
yakiporomoka huku yakijivua
kutoka mwenye yale majoho
Yaliyokuwa Yamevaa awali,
Yalipokuwa katika maumbile ya
wanaadamu! Yalipofika chini,
ndipo yalipokuwa majoka kamili!
“Ama kwa hakika ni ubishi wako
uliotufanya tuje kwenye mji huu
wa majoka, ambao sasa unatutosa
katika hatari hii kubwa!” Hanga
alimlaumu Kibwe, ambaye
hakusema lolote wakati ule, bali
alinyamaza tu!
Baada ya Hanga kusema maneno
hayo, mara Kibwe akashituka
ghafla, kwani alihisi kama
ameshikwa bega lake na mtu!
Alipogeuka, kitu cha kwanza
ambacho macho yake yalikiona,
kilikuwa ni urembo usiokadiriwa,
uliokuwa kwenye sura ya
mrembo mwenye uzuri wa shani!
Binti huyo mrembo alikuwa na
macho manene, ambayo kila
alipoyapepesa, yalifunikwa na
kope ndefu. Juu kidogo ya macho
hayo yenye kope ndefu,
zilionekana nyusi zilizokaa kwa
mpangilio mzuri mno, mithili ya
upinde! Mashavu yote mawili ya
yule binti yalikuwa na vibonye,
vilivyo kamilisha kazi nzima ya
urembo wa maumbile yake, na
kuifanya sura ile iliyotokea mbele
ya Kibwe na Hanga, kuwa ni ya
kipekee, na ambayo wote wawili,
hawajawahi kuona mfano wake!
“Eh……! Ah……!” Hanga alijaribu
kusema lakini hakuweza kupata
la kusema. Kibwe akasafisha koo
lake kwa kikohozi hafifu, bila
kutia neno! Wote wakasahau
kuwa yalikuweko mapandikizi ya
majoka yakiwafuata kule waliko!
“Nadhani huyu ni binti mfalme
wa majini!” Hanga
alimnong’oneza Kibwe, ambaye
alimfinya kidogo, ili
kumnyamazisha….., na wakati
huo, ikasikika sauti nyororo
ikisema,
“Hivi katika mji huu wa hatari
mmefuata nini hasa…..? Hususan
kwenye jumba hili? Na ninyi hasa
ni kina nani?” Yule binti mrembo
aliwauliza Kibwe na Hanga. Huku
wakimshangalia huyo binti,
Kibwe na Hanga walikuwa
wakijikung’uta kung’uta nguo
zao zilizokuwa zimechafuka kwa
vumbi kutokana na lile sakata la
mbio za kuwakimbia nyoka wa
kijini. Kibwe alimshangaa yule
binti kwa kuwashangaa wao
kuwepo pale, wakati na yeye
mwenyewe alikuwa kwenye
sehemu ileile ya hatari, lakini
hakudhurika kwa namna yoyote,
bali alizidi kuwa mrembo tu!
“Sasa dada yangu, mbona na
wewe uko huku? Kwani wewe ni
nani, na hapa ni wapi?” Kibwe
aliuliza .
“Kwa hakika siko hapa kwa
kupenda. Mimi ni Jasmin binti
Sultani, na hapa ni kwa mfalme
wa majini wote, yaani mfalme
“Makattani.” Alijieleza Jasmin,
akimwachia Kibwe aunganishe
mwenyewe kuhusu je, mfalme
‘Makattani’ ni nani. Kibwe
alimjua na kumuona jini
‘Makatta’ kule kwenye mji wa
chini ya bahari, aliyeitwa
‘Makatta wa Makattani.’ Hivyo
basi, akatambua kuwa mwenye
milki ile waliyokuwepo wakati
ule, alikuwa ni baba yake jini
‘Makatta!’ Kwa hiyo awali baada
ya kumteketeza jini yule ‘Makatta
wa Makattani’ kwenye mji wa
chini ya bahari kulikokuwa
kukitengenezwa vichafuzi vya
hewa safi kwa binaadamu, mara
hii ya pili yaelekea kuwa Kibwe
alimteketeza nduguye jini
Makatta, Maimuni, ambaye naye
alikuwa akifanya uovu wa
kuwachukua wana wa Sultani!
“Kwa hiyo Jasmin, unafanya nini
katika milki ya mfalme
‘Makattani’ na umefikaje hapa
bila ridhaa yako?” Hanga
alimuuliza mrembo yule
aliyemuona kama mwanamke
mwenye urembo wa kijini.
“Mimi ni mwana wa kwanza wa
Sultani wa nchi ya Shamsi. Niko
huku nafanya kazi za kitumwa
kwa mfalme ‘Makattani.’
Alijieleza Jasmin, na halafu
akawapa taarifa ambayo haikuwa
nzuri kwao!
”Ningependa pia muelewe kuwa
siku ya leo sio siku nzuri kwenu
kuwepo huku.” Aliwafahamisha
binti huyo. “Kwa kuwa Binti yake
Mfalme ‘Makattani’ yaani
‘Maimuni’ aliyetumwa kwenda
kumchukua Bhaduri binti Sultani
na kumleta huku kutumikia
kwenye milki ya baba yake,
hajaonekana tangu alipoondoka
saa tano asubuhi” Jasmin
aliwaeleza wale vijana, akisisitiza
kuwa ujio wao kule
hautatafsiriwa vizuri na jamii ya
majini, kwani raia na jamaa zake,
wana wasiwasi kuwa huenda
wanaadamu wamemdhuru!”
Kama kawaida, Hanga akaanza
kukosa raha kwa hofu. “Kwani
mabinti Sultani wengine
waliochukuliwa mwanzoni
wamewekwa wapi?” H alidodosa,
ili afahamu kama wanaadamu
wafikapo kule huuawa, au la.
“Wako kwenye sebule maalum
anayopumzikia mfalme
‘Makattani.’
“Na huyo Mfalme ‘Makattani’
mwenyewe yuko wapi hivi sasa?”
Hanga aliuliza, akitaka kujua jinsi
atakavyojihami, endapo mfalme
huyo atatokea pale ghafla!
“Mfalme huyo wa majini yuko
pamoja na wadogo zangu, ambao
hivi sasa wanaendelea na kazi ya
kumkanda , wakati yeye
amelala.” Jasmin aliwaambia,
akimwacha Hanga hoi,
akiwahofia hao mabinti
wanaokaa pamoja na hilo nduli,
bila kujua ni wakati gani
litawageukia na kuwadhuru!
Kibwe naye alibutwaika mno
kusikia hivyo, akiwaza kuwa pale
walipokuwa, ni mahali pa kutia
hofu sana. Wakati huohuo,
Jasmin akawatanabahisha kuwa
mpaka wakati ule walikwisha
poteza muda wa kutosha, kwani
wale majini waliokuwa
wakiwafuata, ni askari wa
Mfalme Makattani, na walipewa
amri ya kufuatilia habari ya
Maimuni binti Makattani. “, Haya,
twende huko kwa wadogo zako,
haraka!” Kibwe alimwambia
Jasmin, huku akamshika mkono
ili wakimbie, na wakati huohuo
akimwashiria Hanga afuate
nyuma. “Leo nimekuja
kuwachukuweni wewe na
nduguzo.” Kibwe alisema kwa
kujiamini, wakati Jazmin na
Hanga wakishangaa kumsikia
akisema hivyo. Hawakuelewa
jinsi gani alivyopanga kukimbia
na Jasmin na nduguze watano,
wakati kundi zima la askari wa
kijini lilikuwa likiwafuata kwa
kasi kubwa. “Sidhani kama
unaelewa unachokisema ndugu
yangu. Hivi unadhani utapita
wapi baada ya kutuchukua?”
Binti Sultani yule alimuuliza.
Lakini Kibwe hakumjibu, bali
alimwonyesha ishara ya kwamba
yeye aongoze njia tu, kuelekea
huko walikokuwa
nduguze. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipoingia kwenye hiyo sebule
kubwa ya mfalme ‘Makattani,’
wale vijana wakashangaa kweli
kweli, kwani kwenye kitanda
kikubwa kupita kiasi, lilionekana
joka kubwa mno, kuliko hata lile
lililokuwa na vichwa saba,
aliloliua kibwe! Joka hilo ambalo
ni mfalme wa majini, lilienea
sebule nzima kwenye kitanda
hicho kikubwa cha ajabu. Kitanda
hicho kilizungukwa na mabinti
Sultani watano waliochukuliwa
awali na joka kuu, ‘Maimuni’ wa
Makattani, pamoja na mabinti
wengine wengi warembo,
waliopelekwa kule baada ya
majini kuzamisha mitumbwi na
ngalawa zipitazo kwenye mito, na
pia meli kubwakubwa
zinazosafiri kwa njia ya bahari.
Ajabu ni kwamba kila mmoja
alishikilia mchi mdogo wa
kutwangia vitunguu na viungo
vingine jikoni, na wote walikuwa
wakimtwanga mfululizo, mfalme
‘Makattani!’ Kilichowashangaza
zaidi ni kwamba wakati mabinti
Sultani walipokuwa
wakimtwanga Mfalme yule wa
majini, ‘Makattani,’ yeye alikuwa
amelala fo, fo, fo!
Kule nje kwenye majabali
alikokuwa ameketi Bhaduri binti
Sultan, alisubiri kwa muda mrefu
sana, hadi akahisi kuwa huenda
Kibwe na mwenzake
walimtelekeza. “Yule mmoja
aliyepambana na lile joka,
ameondoka na fuko lake
mgongoni, kwa hiyo sidhani
kama anayo sababu ya kurudi
tena huku. Labda amekwisha
kwenda zake, au labda ameuawa
na majoka ya mtoni….” Hayo ni
mawazo yaliyokuwa yakipita
kichwani kwa Bhaduri, na wala
hakupata jibu. Akapata hofu
kubwa kwamba anaweza kutokea
nyoka mwengine mkubwa na
kumchukua!
Lakini masikini! Laiti kama
angefahamu yaliyokuwa
yakiendelea kule chini ya mto,
ambako ni himaya ya jamii ya
majini, na ambako ndugu zake
wote walikuwa ni watumwa wa
Mfalme Makattani, angetaharuki
zaidi!
Wakati Kibwe, Hanga na Jasmin
wakikimbilia kwenye hiyo sebule
kubwa ya jini Makattani, mara,
kama muujiza, wakasituka
kuwaona wale majini, askari wa
Mfalme Makatta, wamekwisha
ingia kwenye sehemu ya gorofa
ya juu walipoangukia kibwe na
Hanga, wakati walipojibembeza
na kamba kutoka kwenye jengo
la jirani!
“Haaa! Wameingia jamani! Na sio
majoka tena bali sasa ni yale
majini marefu! Harakisheni
jamani!” alisema Hanga
kuwatahadharisha wenzake.
Wakati wakikimbia ili kuingia
kwa Makattani, Kibwe
alikumbuka maneno ya muhimu
sana ya mzee wa busara.
“Kwenye bustani ya jumba la
Makatta, ipo chemchemi ya maji,
na kwenye chemchemi hiyo,
huelea kibatali kidogo chenye
mwenge mdogo wa moto.
Mwenge huo ndio roho za majini
yote ya huko, isipokuwa mfalme
wao ambaye roho yake
hushikiliwa na hirizi kubwa sana
inayoning’inia chini ya mti
uliopandwa karibu na
chemchemi hiyo. Ili kuwateketeza
majini wa huko, lazima uzime
hicho kibatali, na uikate kate hiyo
hirizi yenye roho ya mfalme wa
majini.” Mzee wa busara
alifahamisha kuwa kwa kufanya
hivyo, majini wataathirika kwa
njia mbalimbali.
Kibwe alimgeukia Jasmin na
kumuuliza, “Ni mlango upi
unatokea kwenye bustani ya
mfalme Makatta?” Yule binti
akanyoosha mkono wake,
kumwelekeza ulipo.
“Wewe nenda kwa wadogo zako
na mnisubiri huko. Hanga, haraka
nifuate!” Moja kwa moja kibwe
aliongoza hadi bustanini,
akifuatiwa na mwenzake Hanga.
Nyuma yao, kama upepo, wale
askari wa Makattani walielea na
kuwatangulia vijana wale,
wakiizingira ile chemchemi ya
uhai wao. “Haraka sana irukie ile
hirizi mtini, na uizungushe
hewani mara nyingi!” Kibwe
alimwambia Hanga, aliyekuwa
hodari kwa kuruka. Bila kupoteza
muda, kijana yule akainua miguu
yake mirefu na kuchukua hatua
mbili kabla ya kujirusha na
kuning’inia mtini, akizuka na ile
hirizi kubwa ya
kimazingaombwe! Wakati ule
wale majini waliojitahidi kuelea
kama upepo ili kumzuia Hanga,
walikwisha chelewa kwa
sekunde! Walipohisi hatari
iliyokuwa mbele yao, wakaanza
kurudi nyuma, wakijiweka mbali
na Hanga, kabla hawajatahamaki
na kumuona kijana yule
akiizungusha ile hirizi! Hamadi,
mara ukazuka upepo mkali mno
uiliowakumba wale majini na
kuwamwaga upande mmoja!
Kibwe naye aliruka na kujaribu
kukiwahi kile kibatali
kilichokuwa kikielea kwenye
chemchemi! Mmoja kati ya majini
aliyeangukia karibu na Kibwe,
alimshika mguu wake! Hanga
alipoona vile, haraka
akaizungusha ile hirizi mara
nyingi sana, na tena kwa nguvu
zake zote! Afana aleik! Kwa mara
hii, upepo mkali zaidi ulitokea na
kuwazowazowa wale majini,
ukawabwaga upande mmoja,
walibaki wakielea sehemu moja,
wakikosa uwezo wa kwenda
popote!
Wakati huo, mfalme Makattani
alianza kuamka pale mahali
alipokuwa amelala fo fo fo kwa
kipindi cha miaka mingi iliyopita,
bila kuamka! Kadiri alivyokuwa
akitwangwa na wale mabinti,
ndivyo alivyozidi kulala! Siku ile
alipoanza kuamka, wale mabinti
wote wakasituka na kushangaa
sana. Mara wakamuona mfalme
yule wa majini akianza
kubadilika kutoka kwenye umbo
la joka kubwa la ajabu, na kuwa
kiumbe mmoja mwenye umbo la
ajabu sana! Alionekana akiwa na
kichwa kirefu na kipana sana,
chenye uso wenye macho manne
makubwa, yaliyofunikwa na
sehemu ya nyusi iliyokuwa kama
nundu kubwa mbili! Kiumbe
huyo alikuwa na mikono mine
mirefu kupita kiasi, miwili kila
upande,iliyokuwa haina mifupa,
kwani ilikuwa na uwezo wa
kujinyonga nyonga kama nyoka!
Kila mkono uilikuwa na vidole
sita, vilivyoning’inia mithili ya
mikia ya pweza! Na miguu yake
minne, miwili kila upande, nayo
ilikuwa na uwezo wa kutambaa
kama nyoka, na pia kukamata
kitu chochote kwa nguvu za
ajabu. Ama kwa hakika, umbo
lake zima baada ya kubadilika,
lilifanana na umbo la buibui,
lakini katika mwili mkubwa mno
kuliko buibui!
Kwa kutumia mdomo wake
ulioonekana kama wa sokwe mtu,
Mfalme wa majinni, Makattani
alipiga ukelele uliorindima hadi
matumboni mwa kila
mwanaadamu aliyeusikia, na
kisha kwa mlio wa hasira wa
kukoroma uliotingisha miti yote
na kudondosha matunda
yaliyokuwa kwenye bustani yake,
jinni huyo akanena. “Ni nani
huyo anayethubutu kuniamsha
mimi Makattani wa Samsuri!”
Wale mabinti wote waliokuwa
wakimkanda Makattani bin
Samsuri, walianguka na kuzirai!
Jinni hilo katika umbo lake la
ajabu, likainuka kitandani na
kujitingisha, na kisha likaiongoza
miguu yake mirefu iliyokuwa
kama nyoka wanne, na miguu
hiyo kama nyoka, ikaanza
kutambaa na kumfanya
Makattani taratibu atoke kule
ndani, akielekea kwenye bustani,
huku mikono yake nayo
ikikamata nguzo na vikuta, ili
kujirahisishia mwendo!
Alipotokea kwenye bustani katika
umbo hilo na mwendo wa
kustaajabisha, Hanga aliyeanza
kumuona, akashikilia mdomo
wake kwa mastaajabu! Wakati
huo hakukumbuka kuwa alikuwa
ameshikilia hirizi ambayo ndiyo
iliyokuwa ikiwanusuru na vitimbi
vya majini! Bila kuelewa,
akaiachia hirizi ile ya miujiza,
iliyoanguka chini karibu ya
miguu yake. Kwa tukio hilo, wale
majini i ambao ni askari wa
Makattani, wakaanza kukusanya
nguvu, na taratibu wakamfuata
Kibwe, aliyekuwa akifuata kile
kibatali kieleacho kwenye
chemchemi, kwa nia ya kukizima.
“Moshi wa hicho kibatali baada
ya kuzimika, utawazingira majini
wote, ambao nao watageuka
kuwa moshi, na kuchanganyika
na moshi wa kibatali kabla ya
kuyeyukia angani!” Kibwe
aliambiwa na Mzee wa Busara
hapo awali. Alikumbuka pia
kuwa mzee huyo alimwambia
Hanga atahadhari kwa vyovyote
vile, asithubutu kudondosha ile
hirizi, na kwamba akifanya hivyo,
majini watapata nguvu upya, na
hivyo kumshambulia Kibwe
atakayeonekana kuwa anatishia
maisha yao!
Masikini Kibwe alikwisha kuwa
mikononi mwa yale majini ambao
ni askari maalum wa Makattani!
Wakati huohuo jini Makattani
naye alikuwa akijitoa sebuleni
kwake na kuwasili kwenye ile
bustani. Alijiburuza na kutambaa
mithili ya buibui, na kisha akatoa
ukelele mwingine wa aina yake,
kama vile mtu anaye kuna nazi
kubwa sana kwenye mbuzi
kubwa!
“Kirrrrrrraaah! Kirrrrrrrraah!
Kirrrrrrraaah!” Jini makattani
lilikoroma hivyo, na huku
likimaka kwa hasira likisema;
“Mleteni hapa kwangu huyo
kijana mkorofi!” Aliwaamuru
askari wake. Wakati huo, Hanga
alizinduka kutokana na lile
butwaa alilolipata baada ya
kumuona jini Makattani katika
umbile lake la kustaajabisha! Na
hapohapo, Kibwe naye akapiga
kelele za kumzindua Hanga,
wakati wale askari wa kijini
walipokuwa wakimpeleka kwa
mfalme wao kama
walivyoamrishwa. “Hangaaaa!
Hangaaa! Acha kushangaa!
Haraka sana okota hiyo hirizi!”
Hanga akagutuka na kwa wepesi
usio kuwa wa kawaida, akadiriki
kuiokota hirizi ile wakati ambapo
mmoja kati ya askari wa kijini
aliwasili akielea hewani kama
samaki baharini, pale mahali
alipokuwepo Hanga, ili
kumuwahi. Lakini wapi!
Alikwisha chelewa! Baada ya yule
kijana kuidhibiti ile hirizi, alianza
kuisukasuka na kuitingisha kwa
nguvu zake zote, zaidi ya vile
alivyoelekezwa na Mzee wa
Busara, Kakakuona! Alizidisha
nguvu na kuisukasuka ile hirizi
mara chungu nzima! Halafu wee!
Kasi ya upepo uliotokea kwa
mara ile ya tatu, ilikiuka ile kasi
ya awali, na badala yake, upepo
huo ukachanganyika na tufani
kubwa, iliyotingisha ardhi na
kuipasua, na wakati huohuo
kusababisha mafuriko makubwa
ya maji!
Wakati yakitokea hayo
yaliyosababishwa na Hanga,
majini wengi walizolewa na
upepo mkali, na wakati huohuo,
baada ya Kibwe kuachiwa huru,
akawahi kukifikia kile kibatali
kilichokuwa kwenye chemchemi
na kukizima! Lo! Moshi uliotoka
kwenye kibatali hicho kidogo,
ulianza kufunga na kutanda
katika bustani, na kuwafunika
wale majinni, waliogeuka moshi
uliojiunga na ule uliotoka kwenye
kibatali! Kibwe na Hanga
wakauona moshi ule ukiyoyoma
angani na kupotelea huko! Hata
hivyo, hali hiyo iliyotokea
haikumdhuru mfalme wa majini
asilani. Wakati Kibwe alipotaka
kuwahi kwenda kwa Hanga na
upanga wake ili kusaidia kuikata
kata ile hirizi, Makattani ghafla
aligeuka ndege aliyeruka moja
kwa moja hadi kwa Hanga,
akikusudia kumpokonya ile hirizi.
“Irushie kwangu upesi!” Kibwe
alimwambia Hanga, ambaye
haraka alifanya hivyo. Bila
kupoteza muda, Kibwe alitoa
upanga wake kiunoni, na
kuuzungusha hewani, na wakati
hirizi ile bado iko hewani,
akaiwahi kabla haijatuwa, na
hivyo kuikata katika mapande
mawili!
“Aaaaaaaaaagh! Aaaaaaaaaggh!
Jini Makattani aliugulia huku
akigaagaa chini mithili ya buibui
anaposhambuliwa! Baada ya robo
saa, jini yule akayeyuka kama
kwamba hakuwepo pale kabisa!
Katika saa moja iliyofuatia, kila
kitu katika jumba lile la mfalme
wa majini kikawa kimya na
shwari, wakati wale mabinti
waliokuwa wakifanya kazi ya
kumkanda mfalme yule,
wakizinduka baada ya kuzirai!
“Jamani, kimetokea nini hapa?”
Waliulizana kwa mshangao,
kwani kulikuwepo uharibifu
mkubwa wa vitu na mazingira.
Hali ile ilipotulia na wale mabinti
Sultani wote sita walipotoka nje
kwenye bustani, Kibwe na Hanga
waliduwaa,kuona jinsi mabinti
wale walivyoshindana kwa uzuri!
Dada yao Jasmin aliligundua hilo
mara moja, akaelewa kuwa wale
vijana walibabaishwa na wadogo
zake, kama walivyobabaika mara
baada ya kumuona yeye!
“Hawa watano ni wadogo zangu,
na majina yao ni Sabrina, Samiya,
Samira, Shamshir, na Shabnam.”
Binti yule aliwatambulisha
nduguze. CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vijana wale walishangaa kusikia
majina yale mazuri, na
yaliyoanzia na herufi ‘S.’ Ila
walitaka kujua kwanini majina ya
Jasmnin na Bhaduri yalitengwa
na yale ya wenzao watano.
“Kwa sababu wazazi wetu
walitaka majina ya mabinti wao
wa katikati yafanane, na kuwepo
tofauti baina ya binti zao wa
kwanza na kitinda mimba.”
Alijibu Jasmin.
Wakati mabinti wale wakiendelea
na utambulisho, masikini
hawakuwa hata na fununu
kuhusu mambo yaliyokuwa
yanatendeka kule nchi kavu
kwenye majabali, alikobaki
mdogo wao Bhaduri!
Binti Sultani ambaye ni kitinda
mimba, alisubiri kwa muda
mrefu sana pale alipoachwa na
Kibwe na Hanga. Hatimae
akatokea mchungaji mmoja na
mifugo yake, waliokuwa
malishoni, na wakati ule, aliileta
mifugo hiyo pale mtoni ili
kuinywesha maji, kwani alivizia
wakati ule maalum, akitarajia
kuwa tayari yule binti Sultani
atakuwa amekwisha chukuliwa
na lile joka kuu! Mchungaji yule
aliyeshikilia fimbo mkono mmoja
na mkuki mkono wa pili,
alishtuka sana alipoona mwili wa
lile joka liliokuwa likihofiwa nchi
nzima, eti umelala kwenye
majabali bila uhai! Mara,
akagundua kwamba yule binti
Sultani ambaye angetolewa
kafara, hakuchukuliwa kama
walivyochukuliwa wenzake wa
awali! Bahati ilioje kwake!
Lazima ajifanye kuwa yeye ndiye
aliyeliua lile joka ! Palepale
akachukua mkuki na kuanza
kuuchoma choma ule mwili wa
lile joka , huku akipiga kelele
kuita watu washuhudie kazi
aliyoifanya!
“Jamani eeh! Jamani!
Nimekwisha muua yule nduli
aliyekuwa akisumbua jamii yetu
kwa miaka kadha wa kadha! Leo
nimemuua jamani! Njooni
mshuhudie!” Yule mchungaji
alichacharika kama punguani,
akilalama bila kuwaza kuwa
huenda yule aliyeifanya ile kazi
yuko jirani na pale. Vilevile bila
kuwaza kuwa huenda Bhaduri
akasema ukweli kuhusu hali
halisi ya mambo yalivyotokea,
mtu yule mnafiki aliendelea
kujitangaza kwa kelelele!
Alichokifikiria yeye ni kwamba
mara tu, Sultani Bashar
atakaposikia kuwa yeye ndiye
aliyemuua yule nduli, bila shaka
atamuoza yule binti Sultani, na
kumfanya awe tajiri! Ajabu ni
kwamba, Bhaduri naye,
alinyamaza kimya, akimwangalia
mchungaji huyo aliyekuwa
akilalama na kujigamba!Yule
mchungaji akaukusanya ule
mwili wa lile joka, akauweka
kwenye gari lake la ng’ombe na
kuondoka nao hadi kwa Sultani,
ambako alipokewa kwa shangwe
na hoihoi! Haya, wapi na wapi!
Kazi afanye mwingine, sifa apewe
mwingine. Lakini kwa wakati ule,
hivyo ndivyo ilivyokuwa!
Sultani alituma watumishi wake
na gari la farasi kumfuata binti
yake kule mtoni! Furaha
aliyokuwa nayo haikuwa na
mfano, kwanza kwa kumpata
mwanae, na pili kwamba raia
wake hawatasumbuliwa tena na
lile joka, na watachota maji kwa
amani!
“Wee Nokora! Haraka sana piga
mbiu ya mgambo uwatangazie
raia wangu habari hii njema! Na
pia uwaambie kuwa kutakuwa na
sherehe kubwa ya kumuoza
mwanagu kitinda mimba kwa
shujaa aliyetuokoa na tatizo lile la
kudumu!” Sultani alimwamuru
mtumishi wake.
Shamrashamra zikaanza, nchi
nzima ikachangamka, na raia
wote wakasherehekea habari zile
nzuri kwa furaha. Bhaduri binti
Sultani akaweka mkono wake
shavuni, bila kuamini jinsi
wanaadamu wanavyoweza
kukosa haya, na wakaweza
kudhulumu jasho la wenzao
kimacho macho! Alinyamaza tu,
ili aone mwisho wake!
Kibwe na kundi la wasichana
waliochukuliwa na majini na
kutumikishwa kwa mfalme
Makatta, Jasmin na wadogo zake
pamoja na Hanga, walipotoka
kwenye mji wa majini chini ya
mto, hawakumkuta Bhaduri pale
walipomuacha!
“Bila shaka alichoka kusubiri
akaamua kurudi nyumbani.”
Jasmin aliwaambia wenzake, na
akashauri kuwa na wao lazima
warudi haraka
wakawafahaimishe wazazi wao
kuwa wako hai, waweze
kuwatambulisha kwa baba yao
wale wasichana wengine
waliochukuliwa na majini kutoka
sehemu mbalimbali za dunia bila
ridhaa yao, ili wafanyiwe mpango
wa kurudishwa kwa wazazi wao.
Wakati binti yule akiyasema
hayo, Hanga alikuwa akiangaza
kila sehemu, akijaribu kuelewa
kuwa je, ule mwili wa lile joka la
kutisha ulipelekwa wapi? “Hivi
Kibwe ulibeba vichwa tu vya yule
nyoka Maimuni, au uliubeba na
mwili wake wote? Mbona siuoni
mahali popote?” Kibwe alicheka
sana kwa mas-khara hayo ya
Hanga.
“Ningetembea nao vipi mwili ule,
na hapohapo niweze kufanya
yote tuliyoyafanya huko
tulikotoka? Mwili kama ule
unahitaji kubebwa kwa gari la
farasi au gari la ng’ombe! Na bila
shaka aliyeuondoa hapa
aliuondoa kwa kutumia kitu
kama hicho!” Kibwe alimjibu
Hanga, ambaye kama kawaida
alidodosa kutaka kujua je, Kibwe
anafikiri kuwa ni nani
aliyeuondoa huo mwili?
“Tusubiri tu, na bila shaka
tutafahamu baada ya muda si
mrefu,” alijibiwa na Kibwe, na
kisha, wote wakaondoka kule
mtoni kuelekea kwenye jumba la
Sultani Bashar, ambako
hawakujua kuwa kulikuwa na
sherehe kubwa kupita kiasi!
Kila walikopita, Kibwe na
wenzake walikuta shamrashamra
mitaani. Kila mtu alionekana
kuwa mwenye furaha kubwa, na
kwa mara ya kwanza baada ya
miaka mingi, mji ya Majabali
katika nchi ya Shamsi,
ulichangamka kupita kiasi.
Jasmin binti Sultani na nduguze
waliwaambia Hanga na Kibwe
kuwa awali, hali ya mji wao
haikuwa ya kawaida hata kidogo.
“Bila shaka kuna hafla ya aina
fulani,” alinena Sabrina binti
Sultani, na Samiya na Samira
nao, waliomfuatia Sabrina kwa
kuzaliwa, wakashangaa kusikia
neno hafla, ambalo katika muda
wote wa utoto wao, hawakuwahi
kulisikia, kwani mji wao
umekuwa kwenye hali ya misiba
kila mwaka!
“Au tuseme baba ameandaa hafla
maalum ya kumpokea Bhaduri?”
aliuliza Samiya.
“Kama hivyo ndivyo, subirini
muone jinsi sherehe hizo
zitakavyozidi, mara baba
atakapotuona tukiwasili
nyumbani!” Sabrina naye
akawaambia wadogo zake kuwa
wajiandae kuona jinsi wazazi
wao watakavyosituka na
kushangaa kwa kuona sura za
mabinti zao waliodhaniwa kuwa
wameitoka dunia kwa miaka
mingi sasa! Mara tu baada ya
maneno hayo ya Sabrina binti
Sultani, ukasikika mdundo wa
goma kubwa likiwazindua raia
kusogea karibu kupokea taarifa
za Sulitani wao. Waliyoyasikia
kina Sabrina hayakuwa ya
kawaida!
“La mgambooo! La mgambooo!
Likilia lina jamboo! La
mgambooo! Leo jamani asiye
mwana aeleke jiwe! (abebe jiwe)
Raia wote wa mji huu wa
majabali nchini Shamsi,
mnaalikwa kwenye viwanja vya
tamasha katika kasri la Sultani,
kusherehekea ndoa ya mwanae
kitinda mimba, aliyenusurika
kuchukuliwa na lile joka kuu!
Wote msikose kuhudhuria!”
Waliposikia tangazo hilo, Jasmin
na wadogo zake wakaupata
ukweli wa mambo. Lakini sasa,
anayemuoa mdogo wao ni nani?
Shabnam, binti Sultani
aliyemuachia ziwa Bhadura,
yaani bibi harusi mtarajiwa,
akavunja ukimya uliotawala
wakati wote walipokuwa
wanajaribu kuelewa ni nini hasa
kiini cha lile ‘lamgambo’.
“Nadhani hii ndoa ya haraka
haraka hivi, mara tu baada ya
Bhaduri kurejea nyumbani, ina
walakini kabisa!” Samiya na
Shamshir hawakumuunga mkono
kwa kutia neno lolote, bali wote
wawili wakaitikia kwa vichwa na
mguno wa pamoja;
“Mmmmhuuuu!” Na kisha Hanga
aliyenyamaza kwa muda mrefu
pamoja na mwenzake Kibwe,
akasema kuwa kwa kuwa hali ile
inaelekea kuwa ni ya kutatanisha,
hususan kwa kuzingatia kupotea
kwa mwili wa lile joka, ni
muhimu sana waharakishe kufika
kwenye hilo jumba la Sultani.
Kibwe naye, huku akilipapasa
fuko lake mgongoni, alitabasamu
tu, alipotafakari kuhusu wingi wa
busara za Kakakuona!
Bhaduri binti Sultani kwa mara
nyingine, alipambwa kama
alivyopambwa awali ili kutolewa
kafara kwa joka kuu la mtoni,
kwa faida ya raia wa mji wao wa
Majabali, katika nchi ya Shamsi.
Mara hii tena, baada ya
kunusurika na nduli wa mtoni,
binti yule alikuwa akitayarishwa
kama vile kwa kutolewa tena
kafara, kwa mtu aliyedai kumuua
huyo nduli ambaye angemchukua
kule mtoni kama kafara! Kwa
Bhaduri hali zote mbili zilikuwa
zikimkandamiza tu. Bahati
mbaya, kitinda mimba yule
hakuweza kusema lolote, kwani
hakuwa na ushahidi wowote wa
hoja yoyote atakayoitowa kuhusu
mtu aliyefanya kazi kubwa ya
kumuua yule nduli. Tatizo ni
kwamba, yule kijana na
mwenzake, wote walipotelea
chini ya mto! “Nitaelezea vipi
habari zao kwa kadamnasi hii ya
watu, wakati ambapo sina
uhakika wowote wa uhai wao,
kwani sijui kama wazima au
wameuawa na majoka ya huko
baharini.” Binti Sultani yule
alizidi kutafakari, na hatimae
kuamua kukaa kimya tu, liwalo
na liwe!
Katika jukwaa maalum, yule
bwana harusi aliketi akisubiri
ndoa ifungwe. Kwenye uwanja
wa matamasha, raia walifurika
kushuhudia shujaa wao
aliyewaokoa na msukosuko wa
kupata maji, akimuoa binti
mrembo wa Sultani wao! Nyimbo
na ngoma mbalimbali zilitawala
eneo lile, pamoja na mashairi na
tenzi bila kusahau vicheko na
furaha. Walichokua
hawakukifahamu ni kwamba
punde, hali ile yote ingebadilika,
kama kupepesa kwa macho!
CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe na wale mabinti sita wa
Sultani pamoja na mabinti
wengine waliochukuliwa bila
ridhaa zao na kutumikishwa na
majini, waliwasili kwenye ile
hafla maalum ya ndoa ya
Bhaduri, katika wakati muafaka
kabisa! Walipowasili, Sultani
alikuwa akimsifu shujaa
aliyemuua nyoka, aliyeisumbua
jamii ya mji wa Majabali nchini
Shamsi, wakati mtu yule aliyedai
kuwa ndiye aliyefanya kazi ile
ngumu, akiwa amesimamishwa
kadamnasi, juu kabisa ya
membari, ili watu wote
wamuone!
“Bila ushujaa wake, licha ya raia
wote kuendelea kusumbuka
kutafuta maji, lakini pia
ningempoteza binti yangu mmoja
aliyebaki, baada ya kuwapoteza
wanangu sita katika kipindi cha
miaka sita!” Sultani aliwaambia
raia wake, kabla ya ndoa
kufungwa. Wakati hayo
yakisemwa, msururu wa takriban
mabinti ishirini na sita, uliingia
mahali pale, wakifuatiwa na
vijana wawili. Watu wote
wakasahau kwa muda, kuhusu
hafla maalum iliyoandaliwa kwa
heshima ya shujaa wao, na
macho yote yaliwageukia hao
walioongozana wakiingia kwenye
uwanja wa sherehe, kama
kwamba ile sherehe iliandaliwa
kwa ajili yao! Baada ya hapo,
kukawa kimya! Kilikuwa ni kimya
kizito mno, kiasi kwamba hata
pumzi ya watu wakipumua
iliweza kusikika! Sultani alipigwa
butwaa lisiloelezeka! Bwana
harusi mtarajiwa naye,
akatahayari kuwaona mabinti
sultani sita miongoni mwa kundi
la wale mabinti walioingia pale!
“Sijui wale vijana wawili ni kina
nani?” alijiuliza yule mfugaji,
huku akianza kugwaya kwa hofu
na tahayuri!
“Naam, Maulana, Mheshimiwa
Sultani! Tuwie radhi sana kwa
kuivamia hafla hii bila taarifa,”
Kibwe alianza kujieleza, alipoona
kaumu nzima iliyokuwepo pale
ikiwashangaa! Na pia alipoona
kuwa kila mtu aliyehudhuria
mahali pale, ghafla hakuelewa
kilichokuwa kikiendelea! Sultani
alifungua mdomo kusema, lakini
hakuna maneno yaliyotoka.
Malkia akashuka kwenye kiti cha
enzi na moja kwa moja
akakimbilia kule walikokuwa
wale wasichana, na alipofika
karibu yao, hakujua amkumbatie
nani! “Aah! Ama kweli Mwenyezi
Mungu ni mkubwa! Hivi hawa ni
wanangu kweli?” Mke huyo wa
Sultani alihamanika na
kubabaika, akiwaita majina
wanawe mmoja mmoja, huku
akikagua na kuzingira sura ya
kila mmoja kwa viganja vya
mikono yake miwili, kila
alipomtaja jina lake. “Ah!
Mwanangu Samira….! Mwanangu
Sabrina…! Jamani Samiya wangu
wee! Nawe ni Shabnam kipenzi
changu! Shamshir nawe
hujabadilika kabisa! Ooooh!
Mama huyoo! Jasmin mashavu
wangu! Umewalinda wadogo
zako wote na kuwalea vema hadi
mkarejea na afya nzuri kabisa!
Kisha akawageukia Hanga na
Kibwe na kuwaambia, “Sidhani
kama kuna haja ya kuuliza kuwa
mabinti zetu waliwezaje
kunusurika na kurejea salama
nyumbani! Kabla hamjajieleza
zaidi, natoa shukurani zangu za
dhati kwa kunirejeshea
wanangu!” Vijana Kibwe na
Hanga wakanyamaza kimya,
wakipata faraja kubwa kuona
jinsi mzazi yule alivyofurahi!
Wakati huo, Sultani naye
akazinduka kutoka kwenye
msituko alioupata baada ya
kuwaona mabinti zake. Alihisi
kuwa kutokana na hali ile
iliyojitokeza, yalikuwepo maelezo
ya kina ambayo kila mmoja
alistahili kuyasikia! Muda wote
wa yale matukio pamoja na
taharuki ya Malkia, watu wote
walikuwa kimya. Baada ya Malkia
kuwashukuru kibwe na Hanga na
kwenda kuchukua nafasi yake
katika kiti cha enzi ubavuni mwa
Sultani, minong’ono ikaanza!
“Jamani, haya ni maajabu
makubwa! Mabinti hawa sio wale
walioliwa na nduli wa mtoni?
Sasa leo hii wametoka wapi
tena?” Mmoja alimuuliza
mwenzake, ambaye alimkatisha
asiendelee na maneno yale,
akihofia wasije wakaeleweka
vibaya na jamii ya Sultani.
“Nahisi mwenzangu wewe
hujipendi kabisa! Aliyekwambia
kuwa mabinti wale waliliwa na
nduli ni nani? Achana na uvumi
utakaokutosa mahali pabaya
ndugu yangu wee!”
“Eeeh! Kwani nani amenisikia
jamani na nilikuwa
nakunong’oneza wewe tu? Haya!
nimenyamaza!” Wengine
walinong’ona kuhusu lile kundi
la wasichana wasiowajua! “Aisee!
Hivi wale vimwana ndo kina
nani? Nao ni wana wa masultani,
nini? Maana wanarusha roho
kwelikweli! Laiti kama…”
Mwenzake akamzuia kuendelea
na maneno yale, na kumwambia,
“Ndiyo! Kama kawaida yako!
Laiti kama ungepata fursa ya
kuongea na mmoja …..na hivi na
hivi! Siku moja utaponzeka nawe!
Hebu achana na mambo hayo, na
tusikilize hatima ya matukio ya
leo!” Mara, kijumbe mtangazaji
wa taarifa za jumba la Sultani
akaanza kupiga goma lake, ili
kupata usikivu wa raia wote!
“Haya, haya! Mabibi na
mabwana! Tunyamaze na tutulie
ili kumpa nafasi Mheshimiwa
Maulana Sultani aongee. Kama
mlivyoona, kumekuwa na
mabadiliko ya matukio, tofauti na
mpangilio wa awali. Baada ya
muda si mrefu, kila mmoja wenu
atapata majibu ya maswali yake.
Karibu Mukufu Waziri Mkuu
umkaribishe mtukufu Sultani
aendelee.” Sultani alipoanza
kuongea, kwanza kabisa
aliwataka Kibwe na Hanga
wajieleze na kuweka wazi
kitendawili kilichojitokeza mahali
pale.
“Ningependa kujua kuwa ninyi ni
kina nani, na mmewapata wapi
hawa mabinti zangu waliopotea
miaka mingi iliyopita.”
Minong’ono ikarudia palepale!
“Eeheee! Hilo neno jamani!
Lazima tupate maelezo hayo!”
walisema baadhi ya watu, na
wengine wakawa wanagunaguna
na kutingisha vichwa. “Hebu
tusikilizane! Hamtayasikia
mnayotaka kuyasikia kama
mtaendelea hivyo! Tusikilizane
jamani!” Alisema kijumbe wa
Sultani. Baada ya muda, Kibwe
akaanza kujieleza.
“Mtukufu Sultani wa nchi hii ya
Shamsi, jina langu ni Kibwe
mwana wa Ilunga Mbuyu wa
Kala, na mwenzangu ni Hanga
mwana wa Hazari Basari Nkulu.
Tulikutana tulipokuwa katika
harakati zetu za kutafuta hali ya
maendeleo ya kijamii, na tangu
wakati huo, tumekuwa
tukitembea pamoja,” Kibwe
alieleza pia kuwa yeye na
mwenzake Hanga walikutana na
wale mabinti zake kwenye nchi
ya majini, ambako walikuwa ni
watumwa! Maneno hayo
hayakuaminiwa kabisa na kaumu
iliyohudhuria mahali pale.
“Bwana mdogo, heshimu mahali
hapa, maana ni mahali pa
heshima na utukufu mkubwa.
Acha maskhara na tueleze
yaliyojiri huko utokako. Mbona
uyasemayo ni kama simulizi za
paukwa pakawa?”aliuliza waziri
wa Sultani, akimshangaa yule
kijana kwa kuanzisha porojo zile.
Hanga alicheka kusikia maneno
ya waziri, na kisha, kama vile
kuongezea mafuta ya taa kwenye
moto uliokwisha washwa,
akasema; “Kwa hiyo mheshimiwa
waziri, ukiambiwa kuwa huyo
kijana mwenye maskhara na
simulizi za kale, ndiye aliyemuua
yule nduli kule mtoni, na wala si
huyo bwana harusi wenu
mtarajiwa, utasema nini?”
Kimya!
Katika watu waliohudhuria hafla
ile, hakuna hata mmoja
aliyesema kitu! Kila mtu alizama
kwenye dimbwi la mawazo
mazito!
“Kijana, hebu sogea hapa mara
moja!” Waziri wa Sultani
alimwita Hanga aende karibu
yake.
“Wewe unao ushahidi gani wa
maneno uliyoyasema hivi sasa?
Tuonesheni ushahidi kwamba
huyo kijana ndiye aliyemuua yule
nyoka, maana mwenzenu
ametuletea ushahidi wa nyoka
mzima. Ninyi mnasemaje kwa
hilo?” Waziri alitoa rai zake.
Wakati ule, Kibwe naye
akajisogeza kwa waziri, akapanda
kwenye membari alikokuwa yule
aliyedai kuwa ndiye aliyemuua
nyoka maimuni, na kisha
akasema kwa sauti ya juu ili kila
mtu asikie. “Nasema kwa
ushahidi kwamba mimi ndiye
niliyemuua yule nyoka. Na kama
mheshimiwa waziri na baraza
lako mliamini kuwa mwenzangu
huyu ndiye aliyeifanya kazi hiyo,
tafadhali naomba mmwambie
awaoneshe na vichwa vya huyo
nyoka mwenye mwili aliouleta
kwenu kuwa ni ushahidi!”
Kimya tena.
Watu wote wakaduwaa, hususan
Sultani ambaye awali, hakufikiria
kuulizia jambo kama hilo . Lo!
Yule laghai aliyechangamkia ile
nafasi ya Kibwe, kijana aliyefanya
kazi yote ya kupambana na joka
la ajabu, akatamani mno ardhi
ipasuke ili ajifiche humo, kwa
jinsi alivyofedheheka, pia kwa
jinsi alivyohofu hatima ya uongo
wake!
Wakati huo, waziri naye
akazinduka, baada ya kuipata
habari ambayo hakutarajia kuwa
itatoka kwa wale vijana wa
kawaida, na ili kuwabana,
alimuuliza Kibwe, “je, unaweza
kuvionesha vichwa vya joka hilo?
Palepale Kibwe akashusha lile
fuko lake kubwa alilolibeba
mgongoni, akalifungua na kisha
kumwaga chini vichwa saba vya
lile joka! Kwa hakika mahali pale
hapakukalika! Watu wote
walitimka kila mmoja akitafuta
njia ya kupitia, kwani vichwa vile
vilionekana kama vina uhai!
Kichwa cha saba kilizidi
kuwachanganya raia wote, jinsi
kilivyong’ara kama bati la shaba!
Ilikuwa ni pata shika na nguo
kuchanika. Ama kwa hakika
penye kweli uongo hujitenga, na
njia ya muongo, siku zote ni fupi
mno!
Ukweli ulipofichuka, Sultani
alitoa hukumu kali sana kwa yule
mnafiki aliyedai kuwa alikuwa
mkombozi wa raia wa Shamsi, na
wale mabinti waliochukuliwa na
majini kutoka sehemu
mbalimbali za dunia,
wakapelekwa nchini kwao kwa
wazazi wao. “Kwa hakika, pamoja
na kuwashukuru ninyi vijana
wawili shujaa, nawapa fursa hii,
ya kila mmoja kujichagulia mke
ampendaye miongoni mwa
mabinti zangu ili nimuozeshe,
tuweze kuunda udugu wa
kudumu!” CHANZO: https://
deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kibwe alitabasamu, halafu
akasema, “Nafikiri
tutakapokamilisha kazi yetu na
tutakaporejea huku, tutawaachia
wao mabinti zako wachague yule
wampendaye kati yetu, ndipo
tuweze kufunga ndoa nao!”
Sultani, mkewe na mabinti zake
walicheka sana, wakikubaliana na
wazo la Kibwe, wakati Hanga
akigugumia kwa kutoridhika na
uamuzi ule wa Kibwe. Yeye
alimpenda sana Sabrina! Wakati
vijana wale walipokuwa
wakifurahi na kucheka pamoja
na mabinti Sultani, mambo kule
kusini magharibi ya mbali ya
dunia, katika eneo lililokuwa
sanjari na sehemu ya machweo ya
jua, Malkia Sharara alipungukiwa
na kichwa cha mtu mmoja, ili
kukamilisha ujenzi wa jumba
lake la ajabu la matofali ya
vichwa vya watu!
Kibwe na mwenzake wakaagana
na Sultani wa nchini Shamsi na
familia yake, na baada ya hapo
wakaanza safari yao, wakielekea
kusini, kutoka pale Kaskazini ya
mbali katika mji wa Majabali.
MWISHO

Story nzuri sana.... Safi sana....

Chapter Closed...


Cc: mahondaw
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom