Mtanisamehe kwa hili

Sasa usiwanange wasio na magari, ilitakiwa uikoromee serikali yako inakuaje nchi yenye utajiri wa kila kitu wananchi wake wanahangaika na usafiri tena kwenye jiji kubwa haswa la kibiashara kama Daslama. Hio mwendo kasi tatizo ni nini?? Wangeshusha mabasi ya kutosha mwendo kasi na kuifanya public transport kua ya uhakika, hivi unafikiri watu wangehangaika kununua magari?? kwa mfano kila baada ya dakika 15 basi hilo hapo, na daladala /bodaboda na bajaji marufuku kuingia mjini kati. Afrika matatizo makubwa tunayo kichwani na ubinafsi uliokithiri. Fika hapo tu nchi za kaskazini Morocco, Algeria na Tunisia, wale jamaa usafiri si ishu, public transport zipo poa kabisa. Africa kusini mwa sahara kwa watu weusi tulilaaniwa.
 
Watu wana magari lakini bei ya mafuta ni kubwa kiasi ambacho huwezi kuwa na pesa ya kununua mafuta kila siku, hivyo kuna siku unalazimika kupaki gari na kupanda daladala ni hivyo tu yaani, kumiliki gari sio tatizo, kulimaintain ndio changamoto.
 
Actually haijalishi jinsia ukisha fika 35 and above wewe sio wa kuonewa huruma. Kabisa. Unajua huwa wanaona soo sana na huwa wanajistukia ila ndo ivyo hamna jinsi
 
Na hiyo laana unaanza kichwani. Sio kwingineko
 
Watu wana magari lakini bei ya mafuta ni kubwa kiasi ambacho huwezi kuwa na pesa ya kununua mafuta kila siku, hivyo kuna siku unalazimika kupaki gari na kupanda daladala ni hivyo tu yaani, kumiliki gari sio tatizo, kulimaintain ndio changamoto.
Sawa nimekuelewa na hoja yako. Ila bado haiondoi wimbi la hawa ninao wazungumzia
 
"nasikitika tu moyoni najiuliza hata 6M mtu anashindwa kweli kudunduiza akipata? Dah"

Dogo,
de Gunner i think siku utakayokua... Kiakili &kiumri...

Utakapotoka Kwa shemeji yako na kuanza kujitegemea, ukapata na familia inayokutegemea...ukiwa kama baba(kichwa cha familia)...

iko siku Utayakana haya maneno yako wewe mwenyewe!, ama utajutia maandiko haya kuwa huenda ndiyo chanzo cha tatizo!

Maandiko yanaishi!
 
Karma is not real mkuu.
Nilikuwa naiamsha jamii iliyo lala tu.

Sikuwa na nia mbaya ni watu tu na hasira zao
 
Sawa nimekuelewa na hoja yako. Ila bado haiondoi wimbi la hawa ninao wazungumzia
Wengine wanafamilia kubwa na majukumu pia mishahara midogo, lakini pia wamewekeza maeneno mengine sio kwenye magari, kuna watu ukiwashauri wanunue magari hawawezi kukuelewa kabisa, wengine madeni mengi yanawaathiri, amekopa amejenga nyumba kabla ya kumaliza mkopo linakuja hitaji lingine anafanya top up, kwa hiyo kuna top up juu ya top up bado taasisi nyingine za fedha, bado kwa mangi, bado viccoba, bado vyama vya kishikaji! watu wana balaa mbaya, toka nett ya 2.2m mtu anaweza kubaki na 400k, nyingine imeishia kwenye madeni. Nina mfano wa ndugu yangu wa karibu.
 
Nimekuelewa mkuu una point.
 
Lazima tukuelewesha hata kwa bakora
Nimeelewa perspective hiyo sio nyie mnaokuja na maelezo yasio na mbele wala nyuma.

Na kingine isiwe ndo kisingizio cha application kwa kila mtu kuna watu wajinga wamejikatia tamaa na hawana majukumu mengi
 
Collola chafu aitoe wapi japo sijaisoma yote ila umemsikia anataja mjomba, si ajabu anaishi kwa mjomba wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…