Mtanisamehe kwa hili

Mtanisamehe kwa hili

Better life Kwa shemeji,ni kukwepa majukumu yanayokuhusu , Wewe Mwenyewe!
I have my reasons to live there,
Sina mindset ya kimatumbi na hata nikitaka nje siwezi kuishi kimatumbi. Naona watu mmetumia hicho kigezo kuni attack badala ya kuchakata hoja iliyopo mezani. What a pitty society
 
Enyi wamatumbi mnao taka kuwahi magari ya daladala. Naombeni mnisamehe kwa bandiko hili ila naomba mjitafalari kidogo.

Hivi huwa mnajisikiaje ndani ya nyoyo zenu? Yaani unakuta mtu wa miaka kuanzia 35 na kuendelea eti na yeye anakaa kupambana na vijana wa miaka 20 kwenye daladala.

Wth is wrong with you guys? Hivi ni kwamba mmekata tamaa ya maisha Liwalo na liwe tu? Mimi sema kweli juzi gari la shem lilikua bovu so tu kasema instead of ubering gari ngoja nikapande gari za daladala just for fun maana ni muda mrefu sana.

So katika kufikia pale kituoni kulikuwa na abiria wengi sana, Ila cha kushangaza ni kuwa kulikuwa na watu wazima kabisa.. Yaani nikawa nawacheki wale watu nasikitika tu moyoni najiuliza hata 6M mtu anashindwa kweli kudunduiza akipata? Dah aisee alafu ukiangalia hata mindset za hawa watu, bado kabisa they are man child. Bado hawajakuwa kifikra, basi unaishia kusononeka tu.

Jamani hiki kitu so kizuri hasa kwa watu wazima. Imagine baba wa familia huna usafiri wako, inaitwa mzee wa Kaya. Hapo kuna watoto nyuma yako.. How does that feel?

Hivi wewe kweli una hisia? Kweli kabisa uko sawa kuona wenzako wanaishi maisha na wewe una survive? Kweli kabisa huna uchungu ndani yako wa kujifanya upambane not just for you, ila kwa ajili ya watu walio nyuma yako?

Atleast hata uwe example nzuri kwa wanao kuangalia? Ndugu zangu fanyeni kama kujihurumia. Angalieni mustakabli wa maisha yenu. Angalieni kuwa tayari umri umesha sogea na regrets za mtu mzima ni mbaya zaid ya kijana aliye kuja kubadilika na kutoboa.

Haya, kuna watu huwa wana nongwa. Wewe mwenye nongwa endelea kuona uko sawa mpaka siku utakapo kuja kidharauliwa na vitoto vya elfu mbili ndo utajua na maanisha nini.

Asubuhi njema. Na eny wamatumbi wahini kazin mkaendelee kufanya jambo lile lile kwa miaka 50 straight.

Nimemaliza.
Siyo kila mtu kipaombele chake ni kumiliki gari ...mbona watu wanapanda ndege na siyo ndege zao ..siyo kila mtu anayo afya ya kuendesha gari .. wengine uwezo wao wa kuona umefifia hivyo umuhimu wa kuwa na gari umepotea vinginevyo wawe na dereva (usumbufu na gharama zisizo na msingi ) usafiri wa daladala ukiboreshwa na kuwa standard ni bora mara 100 ya gari binafsi ...
 
Nilipokuwa early 20's nilikuwa nawashangaa watu ambao hawajafanikiwa. Yani inawezekanaje ufike 30's na huna ramani au hata nyumba ya mbavu za mbwa.

Ahhh life limenihambo sanaaa. Nikaelewa tu sometimes maisha ni mchakato wa kila siku so, ukimuona mtu anajilisha na kuwalisha wengine. Anasimama wanasoma na kukaa vizuri..

Hata ukimkuta sehemu muache
Sawa mkuu. Umejibu kiutu uzima and I respect that...
 
Toka hapo kwa shemeji yako ukatafute gari lako, uone kazi hata tu ile ya kutafuta tu chakula itakushinda. Yaani upo kwa shemeji yako unaanza kuzodoa watu,yaani shemeji yako akifika upo na dada yako sebureni anaambiwa nimeimisi tangulia site kweli dada yako anatangulia chumbani akaliwe wewe unabaki unang'ata ng'ata kucha. Pumbavu sana
Halafu anachukulia maisha rahisi kwa vile amewekewa masofa ya bure na TV ya bure sebuleni hajui vilitafutwa kwa njia gani.
 
Seran mbona kama wasukuma mnatuzoea vibaya humu ndani🙆‍♂️🙆‍♂️
sio wote🥹
0C8913D4-C4E7-4764-8936-3BFFED76A05E.jpeg
 
Vijana tunakosea sana kuyachukulia maisha kiwepesi.

Kwanza kabisa napinga vikali hoja ya kwamba kuajiriwa ni utumwa. Kuajiriwa ni fursa. Haiwezekani kila mtu ajiajiri, sio kila mtu anayataka mateso ya kujiajiri. Waajiriwa pia ni wazalishaji, kuna taasisi inaweza kusimama bila waajiriwa? Ni vibaya kutaka maisha ya kawaida?

Elewa kwamba maisha ya mtu ni mjumuiko wa hali mbalimbali anazopitia toka utotoni. Mtu kazaliwa kaya masikini, hajasoma na hana ajira ya kudumu, unadhani atamiliki gari kirahisi? Unamlazimisha ajiwekee kipaumbele cha kumiliki gari badala ya vitu vingine vya msingi?

Tukikuzodoa kwanini huna ndege ya $60m kama Elon Musk ambaye baba yake alimiliki migodi utaona ni sawa?

"Meritocracy" ni kipande tu cha ukweli kuhusu maisha. Maisha yana mengi mno.
 
Gari ya shemeji
Nyumba ya shemeji
Kula kwa shemeji
Sabuni ya kufua na kuogea ya shemeji
Nguo unanunuliwa na shemeji
Halafu eti unawaponda wenzio hawana magari!!
Wewe na wao kuna tofauti gani?
Really
Kwani Unaumia ukiwa wapi?
 
Back
Top Bottom