Mtangazaji wa Clouds tv 360 awataka Wasomi wadaiwa HESLB wakauze Ice Cream walipe deni

Mawazo ya kuwadhihaki Watu huwa siyo mawazo ya Tija na acha kutetea Upumbavu. Huwezi kutumia platform kubwa kama ya kuwa katika Kipindi kinachoheshimiwa cha 360 Clouds tv halafu ukatokwa na comment ya Kifedhuli kabisa kama aliyoisema huyo Mtangazaji Hassan Ngoma. Na kibaya zaidi basi bora angekuwa kasema hayo maneno Kiutani tungemwelewa ila kayasema akimaanisha kabisa na kuonyesha kuwa alidhamiria kutuonyesha dharau na nyodo zake aliyarudia tena mara mbili tatu na kusisitiza kuwa Wasomi Wadaiwa sugu wote wa HESLB wafanye hima watembeze madeli ya Ice Cream wauze ili wapate Mamilioni ya Bodi ya Mikopo.

Hii ni dharau isiyovumilika na tunamtaka huyu Mtangazaji Hassan Ngoma wa Clouds tv upesi na haraka sana awaombe radhi hao wote aliowadhihaki. Kuna Watu hadi sasa wana maumivu makubwa ya kukosa Ajira huku wengine wakiwa wameshaathirika Kisaikolojia baada ya kujua wanadaiwa na HESLB na kimsingi tulidhani Mtu kama yeye mwenye Heshima yake Kijamii angekuwa na kauli nzuri na za kuwatia matumaini Wadaiwa na badala yake sasa anawadhihaki na kuwadharau.

Amenisikitisha mno.
Mr Hassan Ngoma ni nani?
 
hivi ninyi ndugu yangu bado mnaangalia clouds!? Hayo mmejitakia wenyewe!

Sasa bila ya sisi kuangalia Clouds tv huu ' upuuzi ' tungeujuaje na tungeumaliza vipi? Kuna Watu huwa mnanilazimisha wenyewe ' niwadharau '. Hivi kwa mfano zile ' Kashfa ' za Ufisadi kama zisingeonekana na Wachache wenye uchungu na nchi hii halafu ' wakaziibua ' bungeni na Wahusika wakawajibishwa leo hii tungejua kama Watanzania tulikuwa tunaibiwa?
 
Mr Hassan Ngoma ni nani?

Msanii na Mjanja Mjanja mmoja wa mjini mwenye Chuo chake cha Uandishi wa Habari Mbezi Kimara ambacho kina usajili ' tata ' wa NACTE na sasa kinaelekea kumshinda huku akijipendekeza sasa kwa CCM na Serikali yake ili apate ' Madaraka ' wakati ni yeye huyu huyu tokea mwezi wa Saba ( July ) mwaka jana hadi mwisho wa Kampeni alikuwa ni mmoja wa Strategists wa Lowassa na kwa mtakaokumbuka ni huyu huyu ndiyo alikuwa ' akiiponda ' sana CCM katika kila analysis zake katika Tv stations mbalimbali lakini kwa mshangao mkubwa kabisa leo hii ndiyo Mtu ambaye anaongoza kuisifia na kuishauri Serikali iliyo chini ya CCM huku mara kwa mara akiwabeza ' Wapinzani ' akina UKAWA na hasa hasa Chama cha CHADEMA huku akisikia tu taarifa yoyote inayomuhusu Mzee Lowassa ' ataishadadia ' kwa nguvu zote za kumkashifu japo ' Kidiplomasia '. Sijui nimuweke katika Kundi gani huyu Mtu.

Mkuu hivyo ndivyo binafsi ninavyomjua Mtangazaji Hassan Ngoma na naomba niwaachie na wengine wanaomjua zaidi ili na Wao ' watiririke ' kuliko Mimi.
 
Weka CV yake please ndio tumjadili

Kasoma Vidudu Zimbabwe, Msingi South Africa, Upili Canada, Chuo Kikuu Degree Havard Marekani, Chuo Kikuu Masters Oxford Uingereza, Ajira Mikocheni ( Dar es Salaam, Tanzania ) na Makazi yake Sinza vumbini ( Dar es Salaam, Tanzania ). Sijui una swali jingine tena Mkuu!
 
Kasoma Vidudu Zimbabwe, Msingi South Africa, Upili Canada, Chuo Kikuu Degree Havard Marekani, Chuo Kikuu Masters Oxford Uingereza, Ajira Mikocheni ( Dar es Salaam, Tanzania ) na Makazi yake Sinza vumbini ( Dar es Salaam, Tanzania ). Sijui una swali jingine tena Mkuu!
Certified CV please
 
Anawaonea gere walionufaika,pia anajionyesha kwa Ngosha ili amkumbuke kwenye himaya yake ila tz hatuna waandishi wa habari wengi ni vilaz.a
 
katika watu waliofukuza watazamaji was clouds 360 ni huyu bwana. anaweka hisia zake wazi bila kujali matakwa ya kipindi.
kwa kipindi kama clouds 360 kinahitaji mtu aliye vizuri kichwani anayejua vitu vingi asiye mropokaji lakini jamaa hana sifa anaharibu kipindi siku hizi watu hawaangalii, tunaomba uongozi ulifuatilie hili
 
Katika hali ya kuonyesha kuwa ni mwenye dharau na asiye na huruma na Watanzania wasomi ambao kila uchao wanahangaika kutafuta Ajira kutokana na mfumo mbovu na mazingira yaliyopo na bado mpaka leo hawajafanikiwa Mtangazaji wa Clouds tv 360 Hassan Ngoma akizungumza tena bila aibu na akiwa mkavu kabisa na akili timamu amewataka wale Wasomi wote wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo nchini Tanzania ( HESLB ) kuanza kutembea popote katika miji yao walipo wauze Ice Cream katika Ofisi mbalimbali ili waweze kupata Pesa ya kulipia madeni yao wanayodaiwa.

Niwe wa kwanza kutaka kumwomba huyu Mtangazaji Hassan Ngoma awaombe radhi haraka sana Wadaiwa wa HESLB kwani nina uhakika kuwa hata alivyokuwa anayasema haya maneno hakuwa akitania bali alikuwa anamaanisha kitendo ambacho hadi Watangazaji wenzake Babie Kabae na Sam Sasali wakawa wanamshangaa.

Kuna wale vimbelembele ambao hudhani kuwa huwa nakurupuka tu kuwasema Watu humu hivyo kwa mnaotaka kujionea alichokisema bahati nzuri Clouds tv 360 Vipindi vyao huwa vipo Youtube hivyo kitafuteni Kipindi cha leo ili mjionee hizo dharau za wazi wazi alizozifanya Mtangazaji Hassan Ngoma kwa Wadaiwa sugu wa HESLB.

Kuwaambia Watu tena Wasomi ambao wanahangaika kutwa kutafuta ajira kuwa Watembeze Ice Cream ili waweze kulipia Madeni yao HESLB ni dharau kubwa, kali na isiyovumilika na ambayo imetolewa na Mtu ambaye tulidhani ndiyo angekuwa mfano mwema katika Jamii yetu kumbe ndiyo Kiongozi wa kuwadhihaki Wasomi Wadaiwa wa Bodi ya Mikopo.
Tumia akili wewe kwani alichosema ni kosa ulitaka aseme nini? Huwezi mfundisha mtangazaji cha kuongea
 
Back
Top Bottom