GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Katika hali ya kuonyesha kuwa ni mwenye dharau na asiye na huruma na Watanzania wasomi ambao kila uchao wanahangaika kutafuta Ajira kutokana na mfumo mbovu na mazingira yaliyopo na bado mpaka leo hawajafanikiwa Mtangazaji wa Clouds tv 360 Hassan Ngoma akizungumza tena bila aibu na akiwa mkavu kabisa na akili timamu amewataka wale Wasomi wote wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo nchini Tanzania ( HESLB ) kuanza kutembea popote katika miji yao walipo wauze Ice Cream katika Ofisi mbalimbali ili waweze kupata Pesa ya kulipia madeni yao wanayodaiwa.
Niwe wa kwanza kutaka kumwomba huyu Mtangazaji Hassan Ngoma awaombe radhi haraka sana Wadaiwa wa HESLB kwani nina uhakika kuwa hata alivyokuwa anayasema haya maneno hakuwa akitania bali alikuwa anamaanisha kitendo ambacho hadi Watangazaji wenzake Babie Kabae na Sam Sasali wakawa wanamshangaa.
Kuna wale vimbelembele ambao hudhani kuwa huwa nakurupuka tu kuwasema Watu humu hivyo kwa mnaotaka kujionea alichokisema bahati nzuri Clouds tv 360 Vipindi vyao huwa vipo Youtube hivyo kitafuteni Kipindi cha leo ili mjionee hizo dharau za wazi wazi alizozifanya Mtangazaji Hassan Ngoma kwa Wadaiwa sugu wa HESLB.
Kuwaambia Watu tena Wasomi ambao wanahangaika kutwa kutafuta ajira kuwa Watembeze Ice Cream ili waweze kulipia Madeni yao HESLB ni dharau kubwa, kali na isiyovumilika na ambayo imetolewa na Mtu ambaye tulidhani ndiyo angekuwa mfano mwema katika Jamii yetu kumbe ndiyo Kiongozi wa kuwadhihaki Wasomi Wadaiwa wa Bodi ya Mikopo.