Mtangazaji wa Clouds tv 360 awataka Wasomi wadaiwa HESLB wakauze Ice Cream walipe deni

Elimu yake please..... mwenye nayo atuletee hapa.... pia siku moja ruge alisema ana miaka 3 hajawai kusoma CV ya mtu pale clouds means ni connection yako tu na ujanja wako mdomo ndo maana mpaka mtu alikua muuza magazeti now mtangazaji na ndo wanaoleta shida mfn ata mwanza pale jamaa wa futuhi nae anatangaza sasa redioni akina gig money
 
Japo kuuza hivyo vitu sio jambo baya lakini huyo kijana ni mbwabwajaji na msema hovyo..

Na mara nyingi huwa anajionaga anazungumza vitu vya msingi kumbe pumba tupu..
 
Na mwisho wa siku hawatapigiwa simu za pongezi wala kadi za sikukuu. Kimsingi hachombezi kwenye hoja fikirishi na jenzi. Jana alikuwepo prof Mkumbo akipresent yanayoitesa nchi, badala ya kuuliza maswali ya hoja tangulizi yeye anajamtoa kwenye hoja ya msingi. Nilichoka kabisa.
Japo kuuza hivyo vitu sio jambo baya lakini huyo kijana ni mbwabwajaji na msema hovyo..

Na mara nyingi huwa anajionaga anazungumza vitu vya msingi kumbe pumba tupu..
 
Kuna wakati, rais mmoja aliwahi kusema , hawa waandishi wa habari ni sawa na , mwanamke kukaa upande wa kulia wa Mme wake
 
Mimi nadhani tungejua CV yake kwanza labda ingeweza kutusaidia kujua ni MTU wa aina gani .Anaweza kuwa Division 5
 
Katika hali ya kuonyesha kuwa ni mwenye dharau na asiye na huruma na Watanzania wasomi ambao kila uchao wanahangaika kutafuta Ajira kutokana na mfumo mbovu na mazingira yaliyopo na bado mpaka leo hawajafanikiwa Mtangazaji wa Clouds tv 360 Hassan Ngoma akizungumza tena bila aibu na akiwa mkavu kabisa na akili timamu amewataka wale Wasomi wote wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo nchini Tanzania ( HESLB ) kuanza kutembea popote katika miji yao walipo wauze Ice Cream katika Ofisi mbalimbali ili waweze kupata Pesa ya kulipia madeni yao wanayodaiwa.

Niwe wa kwanza kutaka kumwomba huyu Mtangazaji Hassan Ngoma awaombe radhi haraka sana Wadaiwa wa HESLB kwani nina uhakika kuwa hata alivyokuwa anayasema haya maneno hakuwa akitania bali alikuwa anamaanisha kitendo ambacho hadi Watangazaji wenzake Babie Kabae na Sam Sasali wakawa wanamshangaa.

Kuna wale vimbelembele ambao hudhani kuwa huwa nakurupuka tu kuwasema Watu humu hivyo kwa mnaotaka kujionea alichokisema bahati nzuri Clouds tv 360 Vipindi vyao huwa vipo Youtube hivyo kitafuteni Kipindi cha leo ili mjionee hizo dharau za wazi wazi alizozifanya Mtangazaji Hassan Ngoma kwa Wadaiwa sugu wa HESLB.

Kuwaambia Watu tena Wasomi ambao wanahangaika kutwa kutafuta ajira kuwa Watembeze Ice Cream ili waweze kulipia Madeni yao HESLB ni dharau kubwa, kali na isiyovumilika na ambayo imetolewa na Mtu ambaye tulidhani ndiyo angekuwa mfano mwema katika Jamii yetu kumbe ndiyo Kiongozi wa kuwadhihaki Wasomi Wadaiwa wa Bodi ya Mikopo.
Sidhani Kama ice cream inalipa.

Kwanini hamtaki kulipa mikopo yenu, si mlijua ni mikopo na siyo grant.
 
Je, sidhani kama ni sahihi kuanza kunikata mkopo kwa asilimia 15 wakati Mimi na wao tuliingia mkataba wa kukatwa asilimia 8. Hii haivumiliki, kwa kweli. Sheria hii ya 15% ilitakiwa itumike wakati gani? Nadhani hapa kuna changamoto, tunaomba wanasheria mtusaidie
Wanasheria watusaidie ufafanuzi wa matumizi ya Sheria hii, ni wapi hii 15% inapaswa kuanza kutumika, ni kwa wale walio tayari na contract ya 8%, au wanaoingia mkataba mpya na Bodi ya mkopo.
 
Ni ukweli usiopingika Kuwa dawa ya deni ni kulipa. Huyo mtu alikuwa analipa 8% ya mshahara wake HESLB. na kiasi kilichobaki kwenye mshahara wake alikopa ili aweza kufanya maendeleo mengine. Sasa unapomwambia alipe 15% ya mshahara wake serikali inatakiwa kujiuliza huyo mtu inamlipa mshahara Sh. ngapi?. Na wanao shabikia hii 15% ni eidha wamesomeshwa na wazazi au walezi wao waliokuwa na uwezo lakini wenzangu ambao mkopo uligeuka kuwa msaada kwa familia tunajua shida tunayoipata, tuwahurumie wenzetu, tuache ushabiki wa kuwakomoa wanaodaiwa. Tuishauri serikali vizuri na tuache kujipendekeza.
 
Naona huu msemo wa "Strengthening the week by weakening the stronger" unabadilika, na sasa kinachofanyika ni "Strengthening the weak(HESLB) by weakening the weak( Wanufaika wa Mkopo).
 
Mkuu,huyu jamaa ni shida. Anaongea mipasho kama muimba taarabu.
MIE NIKAJUA NI MTU MWENYE AKILI ZAKE KUMBE ANA AKILI MGANDO SANA ALIDHANI ALIVYOKOPESHWA MKOPO NANI AMLIPIE,NILIDHANI ATALETA MBINU MPYA KWA WANACHUO WENZIE NAMNA YA KUREJESHA MKOPO BADALA YAKE ANAANDIKA MIPASHO
 
Tafadhali ungana na lile jibu ' murua ' na ' mujarab ' kabisa nililowapa Wapumbavu wenzako kadhaa hapo juu na nachoka sasa kulirudia kila mara kwani nilijua baada ya kuwajibu wale basi Wapuuzi waliisha kumbe na Wewe ulibaki!
Mpuuzi wewe unaedhani ni msomi kumbe kichwa maji tu..!! Usomi wako una kiwango gani duniani hapa kiasi cha kudharau kazi?? Sina tusi zuri linalokufaa lakini lolote utakalo tukana ni saizi yako utakuwa umeniwakilisha kukutusi. ?#%&#%@!7: zako.
 
Shukhrani ya Punda mateke.
Mtangazaji ustaadh Hassan nakupa 100,deni lilipwe,mlipewa mkasema msipangiwe matumizi,kulipa nako msipangiwe?ebo?
Tena nasema,kuanzia mwakani kama hujaanza kulipa hakuna kuoa!
 
Yaani huyu mtu sijui walimtoa wapi, anaropokaga tu.
Wewe unaona anaropoka wenzako wanatumia ushauri wake wanasonga mbele...Mtaani kwangu kuna mtu ni msomi wa degree ya medicine lakini anauza mkaa na ana store yake kubwa tu ya mkaa,magunia yanaondoka na anapiga pesa mbaya,mwingine ana masters ya education na anauza pumba kwa ajili ya chakula cha kuku nyie mnashangaa kuuza icecream?!
Tatizo la wasomi wa Tanzania mnataka kiyoyozi na kwenda mabega juu,mtaani fursa kibao nyie mnasubiri ofisi huku mnakufa njaa,kaulizeni mabilionea wa leo kina bakhresa,Mengi nk walianzaje kama hamjabaki midomo wazi.
Hakuna sehemu yeyote iliyoandikwa kwamba msomi hatakiwi kuuza Icecream,kama nyie mnaona aibu endeleeni na ubishoo wenu,vaeni tai sana,pigeni polish viatu ving'ae zaidi na muendelee kutafuta kazi za viyoyozi huku mkiendelea kudaiwa na HESLB na wakati mwingine utakuta huyo anayejidai msomi na hataki kuuza ice cream anakwenda kukopa hela ya kula kwa muuza icecream.
UKITAKA KUTAFUTA PESA USIONE AIBU,ukiuza nyanya,ukiuza mchicha,ukiuza mkaa,ukiuza pumba,ukiuza icecream utapata pesa.
 
Back
Top Bottom