Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 82,146
- 159,061
Kabla haujaniquote na kuandika gazeti angalau hata ungeelewa, tatizo sio kuuza icecream hata kidogo. Tatizo ni uropokaji wake,na sio katika hili tu ni mropokaji mzuri tu.Wewe unaona anaropoka wenzako wanatumia ushauri wake wanasonga mbele...Mtaani kwangu kuna mtu ni msomi wa degree ya medicine lakini anauza mkaa na ana store yake kubwa tu ya mkaa,magunia yanaondoka na anapiga pesa mbaya,mwingine ana masters ya education na anauza pumba kwa ajili ya chakula cha kuku nyie mnashangaa kuuza icecream?!
Tatizo la wasomi wa Tanzania mnataka kiyoyozi na kwenda mabega juu,mtaani fursa kibao nyie mnasubiri ofisi huku mnakufa njaa,kaulizeni mabilionea wa leo kina bakhresa,Mengi nk walianzaje kama hamjabaki midomo wazi.
Hakuna sehemu yeyote iliyoandikwa kwamba msomi hatakiwi kuuza Icecream,kama nyie mnaona aibu endeleeni na ubishoo wenu,vaeni tai sana,pigeni polish viatu ving'ae zaidi na muendelee kutafuta kazi za viyoyozi huku mkiendelea kudaiwa na HESLB na wakati mwingine utakuta huyo anayejidai msomi na hataki kuuza ice cream anakwenda kukopa hela ya kula kwa muuza icecream.
UKITAKA KUTAFUTA PESA USIONE AIBU,ukiuza nyanya,ukiuza mchicha,ukiuza mkaa,ukiuza pumba,ukiuza icecream utapata pesa.
Uliangalia kipindi au umeandika gazeti tu!! The way alivyoongea ndio tatizo, hakuongea kama ushauri, hapa suala sio kudharau kazi,anauza ice cream hadi maandazi Bakhresa itakuwa msomi!!!