Mtangazaji aogopa kutamka 'Serunkuma'

Bosi wangu mjapani alikuwa kumamoto! Kasheshe ilikuwa wakati wakiitana...kawaida huwa wanaitana majina nusu halafu wanamalizia na neno 'san'...mfano mie wangeita kitesan!! Pata picha hapo...tulikuwa tunaingia chini ya viti kucheka!!!
 
itakua shega tu lazima hao wachezaji watafute majina rahisi lol
 
Tatizo Wanahabari na watanzania(hasa wa BARA, afadhali WAZENJI) kwa ujumla hatufundishwi jinsi ya kutamka maneno kwa kiufasaha ,mfano Magharibi tunaitamka isivyo sahihi. Wanahabari wetu hasa wa michezo wajifunze jinsi gani watangazaji wa mpira ulaya wanavyotamka majina ya wachezaji kulingana na yanavyotakiwa kutamkwa ktk lugha za asili za wachezaji.Mfano Thierry Henry,(Henry) linatamkwa Kifaransa( Aanre) sio kienglish ,vile vile Robert Pires (Robert)linatamkwa kifaransa (Robee ) ingawaje lipo hata kwa kienglish. Kesho ukiangalia mpira au International news zingatia majina yanavyotamkwa. Kurudi katika hili jina huyo mtangaji atakuwa alidhani jina linatamkwa kwa Kiswahili badala ya lugha asili ya mwenye jina. Anyway ndiyo weakness moja ya lugha yetu kubwa ya Kiswahili matamshi yake yapo katika staili moja.Vile vile watanzania tuna ujinga wa kutozingatia jinsi neno linavyotakiwa kutamkwa bali ili mradi limekaribia na jinsi linavyotamkwa.
 

kuna mtangazaj wa magic fm hutangaza morning magic hawez kutamka magharibi hutamka mangaribi
 

Ni matatizo yake binafsi tu, kama aliweza kutamka 'Libolo laichomekea Simba kimoja Dar', anashindwa nini kutamka Sserunkuma? Mbona anatamka 'Msukuma' bila shida yoyote? Asituzingue huyo mtangazaji, kama kashindwa kazi alipwe chake asepe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…