TANZIA Mtangazaji Fred Fidelis ''Fredwaa'' afariki dunia kwa ajali ya gari

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
885
1,000
Mtangazaji Fred Fidelis maarufu kwa jina la Fredwaa amefariki dunia leo tarehe 12 Juni, 2021 baada ya kupata ajali eneo la Kawe.

Kwa wale wakongwe, utamkumbuka Fredwaa kwa lipi?

fredwaa-data.jpg

====

Dar es Salaam. Mwandishi wa habari Fred Fidelis maarufu Fredwaa amefariki katika ajali ya gari iliyotokea leo Jumamosi Juni 12, 2021 saa 8 mchana Kawe mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai amesema chanzo cha ajali hiyo ni ulevi na kwamba wanamshikilia dereva wa gari hilo.

“Inaonekana dereva alikuwa amelewa wakati akiendesha gari liliacha njia na kuingia mtaroni eneo la Tanganyika Packers karibu na sehemu ambayo Mchungaji Boniphace Mwamposa huwa anatoa neno, mtangazaji (Fredwaa) alifariki ila dereva tunamshikilia,” amesema Kingai.

Amesema kwa mujibu wa taarifa hata Fredwaa hakuumia ila inaonekana alipata mshituko kwani dereva hajaumia.

Fredwaa amewahi kufanya kazi Times FM Dar es salaam, Radio Free Africa Mwanza pamoja na Clouds FM Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
5,296
2,000

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom