NOW YOU KNOW: Tottenham ndiyo majogoo wa jiji na siyo Liverpool kama mnavyofikiria

Mjumbe Wa Buza

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,292
2,000
Jumatano ya Oktoba 30, kipindi cha dira ya dunia cha BBC - Swahili, kwenye habari za michezo kulikuwa na habari ya mechi ya Liverpool na Arsenal...na kuandika MAJOGOO.

KUZUIA BUNDUKI?

Haya ni makosa makubwa sana kwa BBC chombo kinachotangaza katika nchi ambayo timu hizo zinapatikana.

Liverpool siyo majogoo na wala hawajawahi kuwa. Na hakuna sehemu yoyote kwenye nyaraka zao ambapo pameandikwa neno JOGOO likihusishwa na klabu hiyo.

Jogoo ni jina la utani la Tottenham Hotspur, timu ya kutoka London yalipo makao makuu ya BBC.Hata nembo ya klabu hiyo ya Kaskazini mwa London ina picha ya jogoo aliyesimama juu ya mpira.LIVERPOOL FC

Liverpool wao wanatumia ndege wa kufikirika anayeitwa Liver Bird ambaye ndio nembo ya asili ya mji huo.

Kupitia tovuti yao rasmi, Liverpool wanasema matumizi ya ndege huyo kwenye nembo yao yalianza tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo 1892.

Ndege huyo ni nembo ya mji wa Liverpool tangu 1352 ilipotengezwa nembo hiyo.

Historia ya sasa ya Liverpool inaanzia 1207 pale mfalme John wa Uingereza aliporidhia eneo la Liverpool liwe mji. Mrithi wa John, Henry wa pili akauruhusu mji huo kuwa na nembo yake rasmi mwaka 1229.

Nembo hiyo ikapotea na mwaka 1352 ikatengenezwa mpya ndiyo iliyokuwa na huyo ndege.

Kwa hiyo Liverpool FC ilipoanzishwa 1892 na kutumia jina la mji ikarithi hadi yule ndege.

Lakini hata hivyo kuna ugomvi kati ya Liverpool FC na Everton FC kuhusu nani anayestahili kumtumia ndege huyo baina yao.

Everton wanasema walianza kumtumia ndege huyo 1891, hata kabla Liverpool FC haijaanzishwa.

Itakumbukwa kwamba Liverpool FC ilianzishwa na watu waliojitenga kutoka Everton FC.Lakini mwaka mmoja kabla ya kujitenga, Everton walishinda ubingwa wa England.

Wakati huo hakukuwa na medali kwa mabingwa kutoka kwa FA, hivyo Everton wakajitengenezea medali zao na kuweka ndege yule.TOTTENHAM HOTSPUR

Hawa ndio majogoo halisi. Majina yao ya utani ni Spurs au Cockerel.

Timu hii ilianzishwa 1882 na kuporwa jina la mtu anayehesabika kuwa shujaa wa eneo ambalo inatokatoka.

Mtu huyo ni Harry Percy ambaye alifahamika zaidi kama Harry Hotspur. Mtu huyo anatoka kwenye familia ambayo ndio ilikuwa ikimiliki eneo lote la Northumberland, inakotokea Tottenham Hotspur.

Huyo alikuwa shujaa wa vita akiisaidia Uingereza kushinda vita kadhaa. Alikuwa akitumia farasi kupigana vita. Farasi huendeshwa kwa kamba inayoitwa SPURS kwa Kiingereza, au HATAMU kwa Kiswahili.

Alikuwa akiishika kamba, anaivuta hadi inakuwa ya moto ili farasi akimbie zaidi... kuwa ya moto ndiko kulikozaa jina la Hot Spur yaani “Hatamu ya Moto”.

Mtu huyu alikuwa akifurahia sana ugomvi wa majogoo na ndio maana pia akaitwa Cockerel (Jogoo).

Kwa hiyo klabu hii iliporithi jina la Hotspur ikarithi na jina la Cockerel yaani Jogoo na hata kwenye nembo yao jogoo anaonekana.ALAUMIWE NDUGU MTANGAZAJI

Dira ya Dunia wametumia neno Jogoo kwa Liverpool wakikumbwa na upepo ulioanzia Mikocheni, Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Kulikuwa na mtangazaji mmoja wa redio wa kipindi cha michezo aliyekuwa akipenda kuwaita Liverpool ‘Majogoo wa Jiji’ na kusababisha jina hilo kuwa maarufu sana Tanzania.

Mtangazaji huyo alifanya makosa mengi ambayo hadi leo bado yanaiathiri Tanzania.

Yeye ndiye aliyekuwa akiita Barcelona ‘Baka’ badala ya ‘Basa’, wakati akitaka kutumia jina lao la BARCA. Na ndiye aliyekuwa akimuita ‘Kluveti’ badala ya ‘Klaivet’, mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.
Hadi leo asilimia kubwa ya Watanzania timu ya Barcelona wanaiita BAKA badala ya BASA.Ni huyu huyu ndugu mtangazaji.

Sasa makosa yake ya Liverpool na majogoo yamevuka mipaka hadi hukohuko wanakotoka wenye majina yao, nao wanajikuta wanaingia mkenge.

Liverpool siyo jogoo na wala hajawahi kuwa. Jogoo ni Tottenham Hotspur.
 
Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,933
2,000
Nimefika mkuu nimependa andiko lako

Ndo maana bwana Muhammad said huwa analalamika sana kuhusu history ya uhuru wa tanganyika na wapigania uhuru kuwa kuna watu walipotosha kwa manufaa yao maana kuna wapigania uhuru hawajatajwa kabisa na wanao pewa sifa siyo wenyewe

Sasa ndo nafikiria huku mtaan shabiki wa barca umwambie kuwa siyo baka ila ni basa, aisee sijui atakutupia mawe

Yaan Barcelona ni basa!

Asante sana kwa ilimu hii
 
Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
11,058

Jamaa umeandika pumba kwa muda mrefu mnoo

Wow... We have time for so much crapppp
 
Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,107
2,000
Nimefika mkuu nimependa andiko lako

Ndo maana bwana Muhammad said huwa analalamika sana kuhusu history ya uhuru wa tanganyika na wapigania uhuru kuwa kuna watu walipotosha kwa manufaa yao maana kuna wapigania uhuru hawajatajwa kabisa na wanao pewa sifa siyo wenyewe

Sasa ndo nafikiria huku mtaan shabiki wa barca umwambie kuwa siyo baka ila ni basa, aisee sijui atakutupia mawe

Yaan Barcelona ni basa!

Asante sana kwa ilimu hii
Mbona hilo la Basa linafahamika mana hata ukisikiliza nyimbo zao utasikia Basa. Ila hapo Kwenye majogoo ndo mwandishi kanifungua macho.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom