Mtandao upi una vifurushi nafuu Tanzania

Mtandao upi una vifurushi nafuu Tanzania

Airtel ndo wako cheap ila utakubali kwenye speed, konokono akasome.
Airtel na Voda mimi ndiyo nawakubari, napiga kifurushi changu cha week au mwezi week gb5 kwa 5000 na mwezi inaanzia 20,000 speed yao inaridhisha nilipo sometimes donwload speed inafika mpaka mb 15 kwa sekunde
 
Kwa upande wa airtel kwangu mambo yapo hivi.
Screenshot_20200807-071747_Phone.jpg
 
Mabadiliko hufanyika ili kuendana na mabadiliko ya kibiashara,tafadhali piga *148*30# ili kujiunga na vifurushi vilivyopo kwa sasa.
Jibu gani hili? hivyo vifurushi vyenu bebeni msepe kama hamtaki kusikiliza wateja...sasa laini yenu nimeikanyaga nikapiga nyundo nikaitia sumu nikaitupa akala panya alaf panya akaliwa na paka then paka naye akafa nikaenda fungua chemba nikamtupa kwenye shimo la choo afe na laini yenu....
 
Jaribu Vodacom, GB 1, 1000 ila kuanzia GB 30 kwenda juu.

Mimi natumia kifurushi cha GB 38 kwa TZS 35,000 kwa mwezi ama GB 60 kwa TZS 50,000 kwa mwezi.


Voda wana dabo bando yao safi sana

20k unapata 40GB kwa week

Netflix kiroho safi kabisa
 
Sijutii kutumia mtandao wa vodacom, halotel ni wazuri ila MB zao zinakimbia kama upepo
 
Jibu gani hili? hivyo vifurushi vyenu bebeni msepe kama hamtaki kusikiliza wateja...sasa laini yenu nimeikanyaga nikapiga nyundo nikaitia sumu nikaitupa akala panya alaf panya akaliwa na paka then paka naye akafa nikaenda fungua chemba nikamtupa kwenye shimo la choo afe na laini yenu....

Mweeh umejua kunivunja mbavu mchana huu 🤣 🤣 🤣 🤣🤣🤣
 
Jaribu Vodacom, GB 1, 1000 ila kuanzia GB 30 kwenda juu.

Mimi natumia kifurushi cha GB 38 kwa TZS 35,000 kwa mwezi ama GB 60 kwa TZS 50,000 kwa mwezi.
Wewe ni mkurugenzi wa kampuni fulani ya madini.Kiasi hicho cha fedha kuna watu wanaitafuta kwa mwezi wala hawaioni,sembuse kwenye simu!!

Kweli duniani hakuna fair,ila kwa Mungu hakuna cha Bill Gates au yule wa Mchomolo-Tunduru.Haki sawa kwa wote!!!

Hahahahaaaa,tusipotoshane!!!
 
Back
Top Bottom