Ni mtandao gani una kifurushi kizuri?

creedfx

Member
Jun 24, 2022
86
37
Salam salam

No wazi hali ni ngumu alafu kila siku bro za vifurushi zimekua zinapanda bei mfano halotel kwangu mimi ndio nikiwa ona ni mtandao wenye gharama nafuu kwa miezi fulani hapo nyuma nilikua najiunga kifurushi cha 10 000 unapewa GB 4.4 kwa mwezi hii kidogo inapunguza gharama kwa matumizi ya kawaida ila now unaenda kwenye kile kifurushi cha royal kujiunga kwa mwezi unakutana na gb 3.8 kitu ambacho ni dhahiri itakulazimu kuongeza pesa ili upate Gb za ziada

Binafsi lengo la kuja huku ni kutaka msaada na ushauri kuhusu mtandao gani unakifurushi kizuri ambacho ukipiga Avarage ya pesa unayolipia kifurushi na kiasi cha data utazopewa basi inakua ni msaada mkubwa kwa kiasi fulani

Kwa sababu nafahamu kuna ma great thinkers na kuna watu ambao wanauzoefu na ufahamu mkubwa kuhusu mitandao ya simu na gharama zake kiujumla natumai nitapata msaada mzuri na kwa wakati na kama basi umefanikiwa kupata Uzi huu na sio mtaalam basi naomba umtag yeyote mwenye unafahamu anaweza tusaidia

Mpaka kuandika Uzi huu na kuomba msaada nimeshapitia Uzi kadhaa zilizopostiwa humu kuanzia 2020 mkapa 2022 kwa kusearch ROUTER na nyingi nimeona kipengele cha Tigo kile kifurushi cha kutumia bando ndo ulipe kinapigiwa debe mno

Kama kuna kingine basi naombeni msaada
 
Tigo kwa mwez 10k unapata GB 4.4
Msg kwa mwez elf 1 tu unapata msg Zaid ya elf10
Dakika kwa wiki elf 1 unapata dkk300+

Kwa mwez vocha kiumla ni elf15 kwa Mimi nisiekua na social network nyingi
 
Bado ni haohao halotel gharama zao zipo chini, tofauti ni kwamba walikua chini zaidi kuliko wengine ila kwa sasa wanawakaribia wengine kwa tofauti ndogo
 
Back
Top Bottom