Mgito
Senior Member
- Aug 1, 2016
- 163
- 69
Kule kwao wanakimbia ile sheria ya kunyongwa, kwahiyo tujiandae kupokea makundi ya wachinaNmeshaanza kuona dalili ya kuwapo genge la mafia wa kichina almaarufu triads hapa tanzania
Kule kwao wanakimbia ile sheria ya kunyongwa, kwahiyo tujiandae kupokea makundi ya wachinaNmeshaanza kuona dalili ya kuwapo genge la mafia wa kichina almaarufu triads hapa tanzania
View attachment 424873
Wageni huja na mengi mazuri na mabaya! Tuna historia ya muda mrefu ya mahusiano mazuri na wachina lakini kuna mambo hayako sawa na viongozi wetu wa sasa ni butu mbele ya hawa raia.
Ukiachana na wale wauza pembe za ndovu mbao nk kuna huu uhalifu wa utekaji utesaji na kuua unaofanywa na hao watu
Mabinti wengi huchukuliwa huko china kwa ahadi ya kuja kufanya kazi nzuri lakini wakifika nchini hupelekwa mitaa ya mikocheni masaki nk kwenye magorofa na kufungiwa huko huku wakipokonywa hati zao za kusafiria
Baada ya hapo huuzwa kutoa huduma ya ngono kwa wachina wenzao na mataifa mengine kwa uchache na gharama ikiwa si chini ya dola 100 short time na si chini ya dola 300 usiku mzima
Hawa mabinti hupigishwa kazi mchana mzima na usiku wanachoka hasa
Sasa hutokea ugomvi kati ya wanaume ama wamiliki wa hao mabinti au wamiliki na mabinti
Binti yeyote anayeleta ukorofi na kutaka kurudi kwao huuliwa na kutupwa. ..kwa nyakati tofauti wameokotwa mabinti walioteswa na kuuawa mitaa ya ufukweni mapori ya chuo kikuu kibaha mkoani pwani na mkuranga
Inawezekana kabisa kuna wengine wameuawa na kuzikwa ndani ya majumba waliyopanga wachina
Kisa cha wiki hii kuhusiana na binti wa El grand casino kutekwa kuteswa sana kisa picha zake kutumwa kupitia mtandao wa wechat huko kwao watesaji wakitaka walipwe dola 19000 ndio wamwachie ni kielelezo kingine cha u mafia mpya
Yanayofanywa na wachina hapa nchini huku yakifumbiwa macho na viongozi wetu so hapa kuna magenge ya kusafirisha watu
Kuna magenge ya kusafirisha pesa vituo vinne vikubwa vinahusika hapa
Kariakoo
Palm beach casino
Chinese supermarket karibu na ubalozi wa kenya
Hotel ya wachina Kinondoni
View attachment 424875
Kuna mengi mabaya machafu yanayifanywa na wachina hapa nchini naomba kukatisha hii mada
Umenipa mwanga Juu ya mile nilichokuwa nahisi. Kuna mchina mmoja yeye gari lolote LA maana likipata ajali basis huwa anapewa taarifa na kufika police kulikaguwa Kwa ajili ya kulitengeneza au kulinunua. Na huyu ukienda karibu garage zote za spring city atapigiwa simu kama ndio bosi upatane nae Kwa matengenezo. Ame link mpaka na kampuni zote za insurance za Magari. Watu wako very corrupt na syndicated wanajenga network hata uhamiaji,dawasco,Tanesco sababu wanajua kukata kitu kidogo.
Kampuni moja ya kichina ya ujenzi sasa imekuwa kubwa walikuja hapa tz hata mtaji hawana lakini walinetwork na vibopa flank wenye mamlaka zao wakakopa na mtaji hata collateral waliitolea hapahapa.
Duh ndo naisikia hii, mbona haikuangaliwa kwa upana wake na kuwadhibiti hao wachina? Huyo aliyekodisha mabaunsa ndio angekuwa chachu ya kupatikana kwa hao wengine.SERIKALI IWE MAKINI NA WACHINA WA FU JIAN
sio wachina wote ni wabaya kivile, lakini wachina wa FU JIAN nwengineatukio sana ndio maana baadhi ya mataifa wakiangalia mchina husika anatoka huko hawampi visa sisi huku hatujastuka...lakini ndio hawa wengi wanaofanya biashara za kamari hapa nchini
Kisa hiki cha mwaka jana
Kuna mchina alitafuta mabaunsa wa kumlinda (huyu mchina alikuwa na ugomvi na wenzake, wote ni wamiliki wa madanguro, hivyo wakapokonyana wateja)
akapata vijana watatu mabaunsa toka gym moja mwananyamala akawa anatembea nao popote aendapo
Siku moja akiwa na mabaunsa wake akakutana na wale wachina wengine zikapigwa kung fu za kufa mtu lakini wale walipozidiwa walimpiga risasi binti wa huyu mchina mwenye walinzi
Baunsa mmoja kuona vile akataka kumvamia yule mchina mwenye silaha ili ampokonye, aliishia kulishwa risasi 12 mwilini
Hii kesi haikufika popote na Baunsa alizikwa kwao bagamoyo kwa msaada mkubwa wa mchina
Kuna mengi ya wachina jamani
Nakubaliana nawe Mshana jr, serikali hasa vyombo vya usalama waliangalie hili kwa jicho la tatu vinginevyo hali itakuwa mbaya sana baadae. Maisha ya wawekezaji na shuguri wanazofanya nje uwekezaji vichunguzwe.mshana jr ,
nimesoma sehemu kwamba,wachina na wajapan wanapohamia ktk mataifa mageni na kuwa wengi kiasi cha kumiliki njia za muhimu za uchumi na biashara kubwa kubwa,huwa wanaanzisha matawi ya siri ya taasisi zao zinazo jihusisha na masuala ya kimafioso.
mfano mafioso wa triad na yakuza mob wametapakaa sana USA ktk miji ambayo idadi yao ni kubwa.
moja ya biashara yao kubwa ni umiliki wa mabinti na kuwatumia ktk biashara ya ukahaba,biashara yao nyingine ni uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.
kwa maana hiyo basi,sishangai kusikia kuna wachina tz wanajihusisha na deal haramu zinazo fanana na hizo nilizotaja hapo juu.
yawezekana tayari kuna matawi ya triad nchini.nasikia hawa jamaa ni very powerful,matawi yao yametapakaa ktk kila nchi ambayo wachina wameingia kwa mgongo wa uwekezaji.
Rushwa haitaisha kwa hali hii, na wanajua kuhonga hawa pale uhamiaji acha tu.Uhamihaji watakuwa wanahusika sana nahawa watu, unapewaje permit kama huna shughuli inayoeleweka?
Huwa wanachoma moto hawa jamaa, ukishakuwa majivu ndo basi tena, hakuna ushahidi.Hili unaloliongea inaelekea lina ukweli kabisa...hawa watu wanaoua..
Kuna baba mmoja wa Kiarabu alikuwa na ugomvi na mchina miaka kama 3 iliyopita....alikuwa na kiwanda cha kusaga chupa...Ikawa siku kama leo ijumaa wamegombana na wachina wanadaiana hela..Siku ya juma mosi huyo baba kama kawaida yake kutembelea sehemu mbali mbali za starehe kwaajili ya kupumzisha akili, kwani alikuwa hana ndugu hapa zaidi ya kazi yake na wafanya kazi wake ndio walikuwa ndugu zake....Siku hiyo ya juma mosi hakurudi, msichana wake wa kazi akasubiri akachoka akaondoka, kesho yake msichana wa kazi akaja asubuhi (Juma pili) mzee hajarudi...Akakaa hadi juma tatu alipoona hajarudi ikabidi aende kazini kwake Keko -kiwandani kuulizia...kule nako aliambulia patupu, huku pia wafanyakazi wake wakijihoji boss hawamuoni...
Kwa ufupi hadi hivi leo yule baba hajulikani alipopotelea, maiti haikuonekana....Wafanyakazi walitoa taarifa ubalozi wao wa EGYPT, taarifa zikafika kwa familia yake huko EGYIPT, na polisi Keko taarifa zilitolewa bila kuambulia kitu...hakuna aliyemuona hadi leo....Kiwanda kilifungwa, na wafanyakazi kujichukulia kila kile mtu anachoweza...
Kwa hakika inaelekea hawa wachina huenda walimuua pengine wakamzika huko majumbani mwao....
Na tanzania hii hivi hatuna utaratibu wa kutafuta kwa kina..ndio watamaliza wengi....
Inatakiwa wapekuliwe hawa watu majumbani mwao...
hhahagaa wawekezaji wa sirikaliUFUKUZE WAWEKEZAJI WA CCM
View attachment 424881 View attachment 424882 View attachment 424883
Hapo wameshikwa wakitengeneza maji ya kilimanjaro wanatumia maji ya bomba.
swissme
hhahagaa wawekezaji wa sirikali
Ndetimakete kwa masikitiko makubwa nimelazimika kusitisha hii simulizi na wala usiniulize kwanini
Naomba radhi sana[emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144] [emoji144]
Au sio bora mlimuadabishaKuna mchina Maaruf wanamwita Ngosha yupo gereji ya pale SAYANSI kuelekea rose garden kuna siku alimfanyia unyanyasaji mkubwa kijana mmoja yupo pale kama fundi eti akazoe mavi kwa mikono ambayo walijinyea wachina baada ya kulewa usiku kucha..baada ya dogo wa kitaa kukataa alimpa kibano na kumfukuza kibarua kama mwizi.
Dogo ni wa kitaani baada ya kutupa stori tukaona hakuna haja ya kwenda polisi wala wapi maana kesi za aina hiyo zikienda jamaa wanakata mipunga kibao unageuziwa wewe..Tulimuwekaea mazingira Mchina Ngosha akaingia line kilichompata(sisemi) siku ya pili kampigia dogo arudi kazini na anamuheshimu kama Mao tse Tung..!!!
Nakubaliana nawe japo Tanzania ni tofauti kidogomshana jr ,
nimesoma sehemu kwamba,wachina na wajapan wanapohamia ktk mataifa mageni na kuwa wengi kiasi cha kumiliki njia za muhimu za uchumi na biashara kubwa kubwa,huwa wanaanzisha matawi ya siri ya taasisi zao zinazo jihusisha na masuala ya kimafioso.
mfano mafioso wa triad na yakuza mob wametapakaa sana USA ktk miji ambayo idadi yao ni kubwa.
moja ya biashara yao kubwa ni umiliki wa mabinti na kuwatumia ktk biashara ya ukahaba,biashara yao nyingine ni uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya.
kwa maana hiyo basi,sishangai kusikia kuna wachina tz wanajihusisha na deal haramu zinazo fanana na hizo nilizotaja hapo juu.
yawezekana tayari kuna matawi ya triad nchini.nasikia hawa jamaa ni very powerful,matawi yao yametapakaa ktk kila nchi ambayo wachina wameingia kwa mgongo wa uwekezaji.
Niko mbali na Tanzania napata mtandao kwa wifi nitarejea ila kwa masikitiko makubwa sitaweza kuendelea na hiyo simulizi kwa sasa na in the near futureKaka mkubwa Mshana Jr na wadau humu, habari ya leo? Wazima bila shaka.
Nini kimekupata kaka Mshana Jr, mbona unakatisha simulizi yako nzuri hii, na hata wewe naamini sasa unajionea namna wadau kama hawa; mookiesbad98, kadoda11, na emie emie, walivyofunguka baada tu ya wewe kuuanzisha uzi huu? Nikiamini wapo wengine watakaofunguka zaidi wanasubiria tu uzi uchangamke.
Unatuaminisha nini mkubwa, tayari ushapigwa Pin na watetezi wa uhalifu huu kwa kisingizio cha nchi kuwa salama? Usalama upi wakati.....daah hadi hasira yaani.
Kwa kuangalia tu post za watu humu, huoni namna watu wanavyofaidika na simulizi hii aisee, na zaidi utawafanya Watanzania haswa Vijana, kuwa makini na hao wadudu
(wachina wahalifu).
Binafsi siwezi kukulazimisha uendelee ama la, ila nasikitika sana kuona umeishia hapo. Basi sawa, tujiandae kwa maumivu zaidi, tena ndani ya nchi yetu.
Ahsante!