Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,741
- 861,138
Wageni huja na mengi mazuri na mabaya! Tuna historia ya muda mrefu ya mahusiano mazuri na wachina lakini kuna mambo hayako sawa na viongozi wetu wa sasa ni butu mbele ya hawa raia.
Ukiachana na wale wauza pembe za ndovu mbao nk kuna huu uhalifu wa utekaji utesaji na kuua unaofanywa na hao watu
Mabinti wengi huchukuliwa huko china kwa ahadi ya kuja kufanya kazi nzuri lakini wakifika nchini hupelekwa mitaa ya mikocheni masaki nk kwenye magorofa na kufungiwa huko huku wakipokonywa hati zao za kusafiria
Baada ya hapo huuzwa kutoa huduma ya ngono kwa wachina wenzao na mataifa mengine kwa uchache na gharama ikiwa si chini ya dola 100 short time na si chini ya dola 300 usiku mzima
Hawa mabinti hupigishwa kazi mchana mzima na usiku wanachoka hasa
Sasa hutokea ugomvi kati ya wanaume ama wamiliki wa hao mabinti au wamiliki na mabinti
Binti yeyote anayeleta ukorofi na kutaka kurudi kwao huuliwa na kutupwa. ..kwa nyakati tofauti wameokotwa mabinti walioteswa na kuuawa mitaa ya ufukweni mapori ya chuo kikuu kibaha mkoani pwani na mkuranga
Inawezekana kabisa kuna wengine wameuawa na kuzikwa ndani ya majumba waliyopanga wachina
Kisa cha wiki hii kuhusiana na binti wa El grand casino kutekwa kuteswa sana kisa picha zake kutumwa kupitia mtandao wa wechat huko kwao watesaji wakitaka walipwe dola 19000 ndio wamwachie ni kielelezo kingine cha u mafia mpya
Yanayofanywa na wachina hapa nchini huku yakifumbiwa macho na viongozi wetu so hapa kuna magenge ya kusafirisha watu
Kuna magenge ya kusafirisha pesa vituo vinne vikubwa vinahusika hapa
Kariakoo
Palm beach casino
Chinese supermarket karibu na ubalozi wa kenya
Hotel ya wachina Kinondoni
Kuna mengi mabaya machafu yanayifanywa na wachina hapa nchini naomba kukatisha hii mada
Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.
Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.