Naona sasa hivi huu uzi inataka kufungwa, nishahisi dalili maana kila nikiandika inagoma kutuma na wakati nina zaidi ya MB 50 sijajua kama ujumbe huu utafika, nahisi ONYO tayari washapewa wanaomiliki JF.
Jambazi, ungetutupia walau kipengele kimoja kilichosainiwa alipokuja kiongozi wao hao wachina; kile chenye utata plz kama hautajali.
Miss Chaga, sijui upo nje ya nchi ama, nahofia tu usije ukasumbuliwa, ila binafsi nakushukuru sana kwa kunielewesha mambo fulani fulani hapo juu, Mungu, akulinde tu, sema Amina!
Mshana Jr, usalama wako sijui utakuwaje, maana umeleta habari nyeti sana, tena hadi kuwatambua wachina wanaotoka maeneo korofi na wale wa kawaida, nahisi utafatiliwa na tutakukosa humu ukitupa mawazo ya michango yako iliyo makinika, nawe Mungu, aliye juu na akulinde, sema Amina!
Jamani siyo uwoga, ila najikuta tu nikihofia usalama wa hao tajwa juu hapo, hasa lile la baunsa kumiminiwa risasi 12 na haikusikika hata, sasa wale viongozi WAADILIFU wakilisikia hili, watataka lifuatiliwe, kaka mkubwa Mshana Jr, sijui utakuwa wapi. Nawaza tu kwa sauti ya ndani.
Ahsante!