Mtandao gani wenye bundles za internet bora?

Mtandao gani wenye bundles za internet bora?

kama upo nje ya dar cheki na smart kwanza kama wapo eneo lako wana unlimited ya siku kwa 1000 na mwezi 20,000 na ni unlimited ya kweli haishuki speed,

kama upo dar angalia vifurushi vya usiku cheki mtandao utakaokupa speed nzuri usiku kati ya halotel na airtel, na kiasi fulani tigo.
-halotel utapata gb 18 usiku mmoja kwa shilingi 1500
-Airtel utapata gb 10 kwa shilingi 600
-tigo gb 4 kwa sh 1500 ila ni usiku miwili

tumia kwanza airtel na halotel halafu angalia unamaliza gb ngapi kama ni chini ya 4 kwa siku moja then 4g ya tigo gb4 zinaisha kwa siku.

pia airtel wana vocha za chuo ambazo hata kama mtu sio mwanachuo anaweza nunua utapata gb 1.2 kwa sh 600 tu nenda cbe zipo kibao.

halotel/voda/tigo unaweza pia kupata vifurushi vya chuo ila itabidi usajili line.

pia angalia tigo kwenye menu yao ya offer maalum kunakuwa na vifurushi vizuri sana kutegemea na eneo ulipo.
Shukran kwa maelezo mazuri je vipi issue ya 4G haiwezi kupunguza gharama ? au haihusiki kwa namna yeyote ?
 
Nenda halotel mkuu, wako vizuri saana sajili university pack yao utaenjoy saana.

Wafanyakazi wa serikali wanapata GB 3 bure.
Mkuu mbona halo wapo hovyo au labda cjui namna ya kupata hivo vifurush maana nna line ya chuo ila napewa mb 800 kwa wiki akat voda wanatoa gb 2 moja mchana nyingine usiku
 
Hivi hii airtel mbona kwangu ina speed ya konokono.
Ipo slow sana lakini watu mnaisifia.
Kwanini mimi ni tofauti?.... hadi nimeiacha kutumia.
Airtel siku hiz magumashi
Nimehamia Ttcl ,soon nitaongeza na halotel
 
Shukran kwa maelezo mazuri je vipi issue ya 4G haiwezi kupunguza gharama ? au haihusiki kwa namna yeyote ?
Kupunguza gharama compare na 3g? Mi naona vifurushi vinashuka sana gharama, atleast vile ambavyo sio rasmi, kila mtandao unajitahidi kuwa na vifurushi vya pembeni vizuri.
 
Hivi bundles za tigo zikoje ? Maana kuna kipindi nilikuwa napiga *147*00# na kupata 2GB weekly lakini sasa siwapati
Hivi ni vifurushi maalum, vinakuja na kupotea. Mimi napata 10gb na dakika 1000 kwa 10,000 kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom