MTALINGOLO hebu fatilia tukio .... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MTALINGOLO hebu fatilia tukio ....

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Judgement, Feb 19, 2012.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mh. Mtalingolo ,
  Rejea jana nyakati za adhuhuri, tulikua katika sharerin' za kawaida hapa Jamvini.
  Kama nilikunukuu vizuri ulisema uko Iringa, nami nikakupa pole kua muda ule nilikua naangalia habari via ITV nikaona panahabarishwa mvua kunyesha kandokando mwa msitu wa Saohill.
  Mvua iliyoacha athari ya mabonge ya Theluji , ambayo pia ITV walifanikiwa kuchukua picha ya baadhi ya Theluji hiyo , na kutuonesha.
  Tabu yangu hapa kwetu East Africa tangu mimi nimekua sijawahi kusikia acha kuona kiwango cha Theluji ile niliyoiona.
  Nachokuomba kama wasaa au fursa itakuruhusu na kama itakua ni kuna uwepesi wa wewe kuwaona wataalamu wa Metreology ukawadodosa nini sababu ya Theluji nyingi kiasi kile kudondoka katika maeneo ambayo geographically hayana tabia hizo! Je ? Ni uharibifu wa mazingira tunaoufanya sisi au ni nini ?
  Usiku wa Jana pia imeripotiwa Nchi za Uropa Romania, Bulgaria na majirani zao, kudondoka Theluji mapande mengine yakiwa na mita 6 na uzito wa kg 500- 600 ! Mabonge ambayo yaliwaangukia baadhi ya wakazi na kuwaua.
  Je ? Na sie tupo njiani kwa kuanzia Iringa ?
  Mie mwenzenu nalichukulia tukio hili kwa macho mawili .
   
 2. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Inshallah mkuu ntajitahdi kulifuatilia kwa undani na kuwahabarisha bt kwa sasa nipo msibani shemeji yake na baba yangu(mjomba)amefariki...
   
 3. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  pole sana kwa msiba
   
 4. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Pole na msiba my fellow Jf Member !
  "KILA KILICHOPO DUNIANI NI CHA MWENYEZIMUNGU NA HAKIKA KWAKE TUTAREJEA"
  R I P
   
 5. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,023
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  sijaisikia hii au ndo mambo ya ulaya haya!
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hiyo ipo ! Source TBC , ITV, STARTV N.K fatilia habari za jana, au magazeti ya leo.
   
 7. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nimefanikiwa kuzungumza na mzee mmoja ambae yeye aliwah kufanya kazi katika msitu ule kwa zaidi ya miaka 20 nae alinidokeza baadhi ya mambo kadhaa..

  "Hali kama iliyotokea wiki moja iliyopita na weza kusema imetushangaza wengi kwa sababu kwa kipindi cha miaka ishirini nilioishi katika maeneo yale haijawah kutokea hali kama ile. Lakin kwa mieneo ya Mufindi, Mafinga na Njombe ambako kuna mashamba makubwa ya miti aina mbalimbali na Kilimo cha chai kwa wingi hali yake huwa tete kidogo, kwa miezi kama Desember, January na february ilikuwa ni kawaida sana kukuta nguo ulioianika jana usiku ikiwa imeganda kwa baridi na hata kuona particles za barafu katika matawi ya miti lakin sio kama haya ya sasa yaliyotokea, pia kwa miezi ya June, July na August hali huwa ni tete sana kwa maeneo tajwa hapo juu, ambapo hufikia hatua hata yakuchemsha maji na kunywa yakiwa yavuguvugu. Na pia kukuta theruji ktk nyumba za nyasi na matawi ya miti ilikuwa ni kawaida sana kwa miaka ya nyuma, lakini miaka ya leo kutokana na uvunwaji wa miti kwa wingi hali hyo haipo tena, sasa tukio la hv juzi ni lakushangaza kidogo"

  Na kuhusu uharibifu wa mazingira kuchangia hali hiyo anasema" Uharibifu wa mazingira, kama ukatwaji wa miti hovyo haiwezi kuwa sababu kwani kupungua kwa miti kungesababisha kiwango cha baridi kupungua katika maeneo husika na kutoruhusu hali kama ile kutokea"

  Mkuu Judgement nimepata hayo maelezo kidogo kutoka kwa mstaafu wa eneo husika...
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nashukuru kwa hilo , hata hivyo umejitahidi.
  Katika vitu ambavyo ni vema tukawa tunaviwekea umanani ni pamoja na mabadiliko ya kimazingira yatuzungukayo.
  Nina imani wahusika na Metreology baadae watalielelezea kiupana.
  Nashukuru kwa hatua hiyo.
   
Loading...