Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,775
Sabalkheri wapendwa, wengine poleni na mfungo wa Kwaresima.
Leo nina ki story cha shost Jacquieline lakini nitamkatisha Jacq katika story hii maana mpaka nimalize kuandika jina lote itakuwa shughuli kidogo.
Jacq akiwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDSM alialikwa kwenye sherehe ya harusi, classmate wake alikuwa anaolewa, katika meza aliyokaa Jacq alikaa mkaka mmoja mtulivu tu, wale makaka wa heshima zao, basi katika kusalimiana walianza kutoleana maneno ya utani na mwisho walicheza wote mziki na vicheko vingi.
Mpaka mwisho wa sherehe Jacq alifahamu mkaka anaitwa Clement na alioffer kumpa Jacq lift kwenda kokote anakokwenda. Ilikuwa bahati sana kwani Clement aliishi Boko na Jacq alikua anaishi Mwenge ukizingatia sherehe ilikua maeneo ya katikati ya mji.
Jacq aliposhushwa nyumbani walishabadilishana namba za simu na Clement, walishapanga kukutana tena weekend inayofuatia.
Jacq alikuja kufahamu Clement ni mkaka wa 35+ na amerudi Tanzania si muda mrefu aliishi ughaibuni kwa miaka mingi akiwa masomoni na kutafuta maisha. Jacq alikua na miaka 27, lakini alivutiwa sana na Clement, kuanzia maongezi, mavazi, utanashati, jokes na vingi vingine.
Urafiki wao uliendelea na Jacq alikuwa mgeni mzoefu nyumbani kwa Clement. Clement alimsaidia Jacq kulipa kodi ya mwaka mzima mpaka atakapomaliza shule. Mipango ya baadae ilikuwa ni ndoa mara Jacq atakapomaliza shule. Kuishi Mwenge ilikuwa rahisi kwa Jacq kuwahi lectures na alikuwa na uwezo wa kukaa library kwa muda mrefu bila kuwaza kero ya usafiri.
Kulitokea tatizo mkoani katika ofisi ya Clement, boss wake alimtuma yeye aende kuliangalia limekaaje. Clement alimuaga Jacq kuwa hajui atarudi lini kwani haelewi tatizo liko vipi, inawezekana ikamchuka wiki nzima au hata wiki mbili. Kwa masikitiko Jacq alipokea muago ule.
Jacq alikuwa na boyfriend wake wa kwanza ambaye walimaliza wote form six anaitwa James, wote walikuwa chuo, James akiwa anasoma BA Hons Education Jack alisomea sheria. Walishaachana long time lakini walibaki marafiki.
Siku hiyo Jacq alipenda kula samaki lakini muda wa kupata samaki fresh ulikuwa mdogo akitoka asubuhi anarudi nyumbani saa nne/tano usiku akitokea library baada ya lectures. alimuomba jirani yake amnunulie samaki, jirani aliahidi kumkaangia pia samaki wale. Lakini jirani apomaliza ku marinate samaki wale kwa limao chumvi na pilipili alipata udhuru, aliwaweka samaki kwenye fridge.
Jacq alirudi saa nne usiku akiwa na James, baada ya maongezi ya mchana waliamua kukumbushia. Alipofika nyumbani alikabidhiwa samaki wake, jirani akimtaka radhi. Jacq alitoa jiko nje akaanza kukaanga wale samaki, kule ndani James akiwa ndani ya shorts alikuwa anaburidika na upepo wa feni huku akiwa anaangalia taarifa ya habari ya saa nne.
Kumbe bwana Clement alipigiwa simu anahitajika ofisini kwao Dar na asitishe safari yake, aliingia Dar saa kumi jioni lakini hakutaka kumsumbua Jack wakati alifahamu ratiba yake, hivyo aliamua kwenda nyumbani kwake lakini aliamua kumfanyia surprise saa nne usiku.
Alipofika alimkuta Jacq anakaanga samaki nje lakini unajua ile ghafla mtu anakuona na furaha kumwishia, Clement hakuelewa, walisalimiana na akamwambia mumii ninaona umechoka ngoja nikusubiri ndani. Amefika ndani anamkuta James ameenea kitandani na shorts yake.
Clement alikuwa muungwana sana, alimuuliza yeye ni nani kwa Jacq, bila kufahamu Clement alimueleza kuwa walianza kudate long time ago lakini anaona alifanya mistake kumwacha Jacq na yeye anahisi kama Jacq pia anahisi hivyo hivyo mpaka amemwalika pale, anaamua kurudisha majeshi.
Clement akiwa anatetemeka alisikiliza vizuri na kwa umakini, James alitaka kufahamu Clement ni nani, Clement alimwambia yeye ni mtoto wa shangazi yake Jacq na alikuwa na salamu kutoka nyumbani, hivyo hakutaka zichelewe ndiyo maana alikuja usiku ule, alimkaribisha James kwenye familia na akaondoka, nje alimuaga Jacq vizuri na kuondoka.
Jacq alijua kosa alilolifanya, asubuhi aliwahi ofisini kwa Clement, Clement alishamfahamisha secretary wake kuwa akija Jacq amfahamishe kuwa yuko busy, Jacq kufahamishwa Clement yuko busy alisema atamsubiri, alishinda na secretary mpaka alipochoka aliondoka. James alipogundua Clement ni nani yeye pia alipata hasira na kumuacha Jacq.