Kizibo
JF-Expert Member
- Jul 3, 2018
- 3,871
- 8,381
Heshima kwenu wakuu.
Mimi ni mfanyabiashara mdogo wa duka, Ukerewe . Kuanzia mwezi wa 6 kurudi nyuma, nilikuwa mtu wa kuhemea mzigo kwenye maduka ya jumla hapa hapa Nansio kwa pesa taslim laki 4 na kushuka. Yaani uwezo wangu ulikuwa wa kununua mzigo wa bidhaa kwa laki 2, laki 2.5, laki 3-4 basi.
Kuanzia mwezi wa 6+ mambo yakaanza kubadilika tena kwa kasi ya ajabu. Kutoka mwezi huo wa 6 hadi sasa mtaji umekuwa ukikua na sasa nimefikia uwezo wa kuingiza dukani mzigo wa milioni 2+.
SASA NATAKA NIANZE KUWA NANUNUA BIDHAA MWANZA KWENYE MADUKA AU MACHIMBO AMBAYO HAWA WAFANYA BIASHARA WANAOTUUZIA JUMLA JUMLA HUKU UKEREWE WANAPONUNUA LAKINI SASA SIJUI YALIPO HAYO MADUKA AU MACHIMBO.
Je, wanaonunua mizigo yao yote pamoja?? Yaani anaponunua ngano hapo hapo anaenunua sukari, mafuta ya kula, vinywaji baridi, lotion na mafuta mgando au wananunua kila category ya bidhaa kivyake??
Naomba kwa anaejua maduka au machimbo wanaponunua hawa wafanya biashara wa jumla kwa mkoa wa MWANZA anielekeze.
Je, kuna kiwango ambacho lazima ufikie ili mtu aweze kununua huko??
Kwa mkoa wa Mwanza wapi nipate ngano?
Wapi nipate vinywaji baridi?
Wapi nipate sukari?
Wapi nipate mafuta ya kula
Vyote kwa bei ambayo na mimi naweza kuja kuuza kwa jumla ??
Pia NATAFUTA WAUZA NAFAKA KWA BEI YA JUMLA WA JIJINI MWANZA.
Karibuni