Mtaje Mnyama au Mdudu unayemuogopa

Mtaje Mnyama au Mdudu unayemuogopa

mie sio jasiri sana lakini napenda kuiga ujasiri,
Kuna rafiki yangu nilimuona akishika chura, toka hapo mimi chura nadaba kama panzi na kutupa nje. 😁😁😂😂😂

natafuta rafk mshika nyoka
Chura kuna wale wa kwenye maji na wa nchi kavu, wa kwenye maji hata mimi nawadaka, ila wa nchi kavu yamekaaga kijeda sana😄
 
Eti kuna wengine wanakaogopaga haka kadudu washawasha cjui
 

Attachments

  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    11.9 KB · Views: 13
Hata

yule mwenye jumba lake nacheza naye kabisa nakamata naweka mfukoni😄.

Ila wife akimuona yule konokono wa jumba lake anaweza piga kelele hadi balozi aje

Yupo konokono kule maji chumvi anaitwa tondo ukila siku ya kwanza uwezi kuacha kula tena
Tondo mtamu kama firigisi za kuku
 
Snake in the monkey shadow.
Nyoka anaheshima yake, hasa yule anayesimama na kutanuka kichwa kama ungo.
 
Yupo konokono kule maji chumvi anaitwa tondo ukila siku ya kwanza uwezi kuacha kula tena
Tondo mtamu kama firigisi za kuku
Mhh, watu wa Pwani mpo vizuri, huyo mm naweza mla kama sijui au sijamuona, ila nkishamuona tuu basi siwez
 
Mimi na nyoka nahusi tunaogopana, sio mnyonge kiivyo kwa hao viumbe.
Mimi nyoka sijawahi kumuua, ila kwa bahati nzuri nakuwaga nawaona mapema, ila kubwa zaidi ni Mungu ananilindaga dhidi yao, maana mazingira mengine niliepuka sio kwa ujanja wangu.
Mfano, kipindi nipo std.3-4, kijijin kwetu hapakuwaga na umeme enzi hizo, tukiwa mezani kwenye nyumba kubwa tunataka kuanza kula nikaagizwa kitu jikoni (nyumba nyingine), nje kuna giza ila tushazoeaga mazingira, asa hyo siku nataka kutoka nimeshafika mlangoni nimeufungua, ila nafsi ikasita kabisa, nikarudi kuchukua tochi 🔦, ile naiwasha tuu namulika pale chini mlangoni nichukue viatu namuona nyoka mweusi unene wa kidole gumba amelalia tambara ya kudekia, kajisokota katulia tulii, inamaana pale ningetoka na giza ningemkanyaga na asingeniacha salama. Basi nikawajulisha wakamuua, ila sijawahi kushiriki kuuaga nyoka. Na sio tukio hilo tuu, yapo mengine ila sikuepuka kwa ujanja wangu.
 
Hili suala sijawahi kujua linatokana na nini, wataalamu watatuambia..

Pale inapotokea unamuogopa tuu mnyama (wanyama wadogo) au mdudu. Yaan ukiulizwa sababu za kumuogopa hata huna jibu lakueleweka bali unamuogopa tuu, hata kama uwe baunsa ila utashangaa unaogopa kajongoo😄

Sasa bana kila mtu atutajie mnyama au mdudu anayemuogopa na sababu za kumuogopa, huenda tukajifunza kitu.

Binafsi namuogopa sana PANYA, sio kwamba namuogopa kwamba ataning'ata, hapana... Namuogopa tuu bila sababu.
Kadhalika, sijawahi kuweza kumuua panya, hata umfunge kamba hlafu unipe fimbo au jiwe nimpige afe, siwezi kabisa, maana mikono ni kama inapata ganzi na kukosa nguvu na sitaki awepo/apite karibu yangu.

Nikifika sehemu hlafu nijue kuna panya, hapo sitokuwa na amani kamwe.
Na hata nimkute amekufa hlafu uniambie nimshike, utakuwa umenipa adhabu kubwa sana nisoiweza.

Karibuni kwenye mada.
CCM mtandao ndiye mdudu hatari sana na anasumu mbaya sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom