Mtaje Mnyama au Mdudu unayemuogopa

Mtaje Mnyama au Mdudu unayemuogopa

Kuna huyu kiumbe anaitwa popo sijui ni ndege wa wapi huyu ananyonyesha, anatisha kinoma
Popo bana kuna mahala nlifikaga alitusaidia sana maana palikuwa pana mbu balaa na hatuna neti, na madirisha yapo wazi (hakuna finishing), ebana yule popo alikuwa anasubiri tuumwe na mbuu then anakuja anazururazurura tuu mule anatoka zake, nkamuuliza mwenzangu huyu popo vipi katumwa nini, akaniambia anakuja kula mbu. Na ni kweli, alikuwa akija akipiga round zake kadhaa mule akitoka husikii mbu hta mmoja, had baada ya muda wakiingia tena. Popo naskia anakula mbu kama hana akili😄
 
Kinyonga na tandu...hawa wadudu wana utisho wa pekee aisee...hebu vuta picha eshtuka usiku kitandani unashangaa kinyonga Upo nae ndani ya shuka,au unashtuka unakuta tandu limekomaa mpk limekuwa jeusi linakutambaa miguuni ghafla ukarusha miguu na likarukia Kwenye manguo Afu lipotee usilione.....,unaweza ukahama hicho chumba
 
Konokono ni chakula mkuu
Niliona Jose mla vichwa anayala huko YouTube lakn Ile video yake sikuweza kuitazama kbs kbs yaan

Nadhani tukubali kuna vitu vingine si kwa ajili ya kila mtu vingine vya wachache hao wadudu kipindi cha mvua kwangu nazungishia chumvi no entry kbs
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom