Mtaani kuna pesa nyingi sana inayotafuta wahitaji

.....unataka kutuambia ni mahindi tu, ndio yenye uwezo wa kumfanya mtu atoboe na asiwaze vidaraja?....hongera, lakini kumbuka kuna watu wanafanya deal nyngne wanapata mafanikio na kufelia pia. So, kama lengo lako ni kutufunza uthubutu umefanikiwa kwa asilimia 90. Lakini kama lengo lako ni kutuaminisha utajiri upo hapo, binafsi najiweka pembeni kama 20percent. Afterall,....fursa hutegemea mahitaji, mazingira, n.k,pengine huko uliko mazingira yamekuleta kwenye neema ya mahindi ya kuchoma.
 
Sasa namuelewa sana JPM !

Jamani mtaani kuna pesa nyingi sana ambayo haina pa kwenda. Inatafuta mwenye uhitaji , ipo nyingi sana.

Ukiwa mbunifu (creative), mjanja na mhangaikaji hukosi pesa , tena nyingi tu. Ukiumiza kichwa ukachapa kazi (bila ubaguzi) unapata pesa tena kiulaini kabisa.

MAHINDI YA KUCHOMA

Hindi moja nimekuwa nikinunua kwa TZS 50 mpaka 100 shambani kulingana na wingi wake.

Nikishalifikisha mjini umbali wa 20 km nikalichoma , naliuza TZS 500 hadi 600.

Nikinunua mahindi 200 nitauza TZS 120, 000.

Matumizi:

Bei ya kununulia ni TZS 20,000 ; Usafiri 3,000 ; nauli yangu 3, 000 ; mkaa TZS 2,000. JUMLA YA MATUMIZI NI TZS 30,000 per day

Faida = 120,000 - 30,000 = 90,000 per day.


Kwa siku 20 = 1,800,000.


Endelea kudai kupandishwa madaraja na nyongeza ya mshahara mpaka Yesu arudi.
Vitu kuviandika ni rahisi sana kama kunywa maji,utekelezaji wake ndio shuguli,kwa maandiko haya kila mtu angekua tajiri
 
Biashara sio kama siasa...kuwa kila unachotaka kinakuwa na kutokea, inahitaji muda, uvumilivu na subira kutengeneza wateja na faida
# achana na kasumba za waajiriwa wanaowahimiza mjiajiri wakati wao wameajiriwa...ukiamua kupambana na kujiajiri ingia ukijua sio lelemama na sio kila siku faida itatokea asee.
Nawatakieni jioni njema
 
Utakuwa uko frustrated na kadigrii wewe kachape kazi pesa ipo, jifunze uthubutu.
siwezi Kuwa frustrated na kadegree haka kwa kuwa nimekulia mtaani na kazi ngumu nazimudu ndo zinaniweka mjini,kadegree kapo kwenye begi mkuu nasubiri foleni isogee
 
Acha kuleta elimu yako ya CBE au TIA virtual na real ni vitu tofauti sana .
 
Hizo ni hesabu za kwenye makaratasi hazina tofauti na hesabu za kilimo cha tikiti ila ukija kwenye uhalisia hamna kiti
 
Mara nyingi biashara ndogondogo huwa zinalipa lakini biashara hizi hazipo constant kwamba Kama leo umepata Tsh ..... na kesho au siku zijazo utapata kiasi hichohicho.

Biashara inapima uvumilivu hususani pale unapoanza kuna
i/ kutokujulikana
ii/ changamoto za usafirishaji wa mahindi (kuna changamoto hasa wakati wa Asubuhi mjasiliamali kupanda kwenye daladala na kipeto/kiroba wakati kondakta anataka abiria wajae.;;;;;;;; ukisikia kupambana kupo hapa)
iii/ mahindi kubaki
iv/ kupata mahindi ambayo ni mateta sana au yameanza kukauka

Si kwamba napinga jamaa alichokisema, inategea Sana yupo kwa muda gani katika Game, yupo site ipi pia customer care kwa wateja
 
Za kwenye makaratasi zinafika maana huwa hazina emmergency wala hakuna kupotea....

Kiuhalisia wao ndio wanaojua zaidi.,
Sawa mkuu

Sema kinachonishangaza waandishi wa zile tarakimu za kwenye makaratasi huwa hawaendi kufanya yale wanayoyahubiri.
 
Back
Top Bottom