Hivi unajua unaweza kutumia akili kidogo tu ukapata pesa nyingi?

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,979
Kila mtu anawaza pesa, kila mtu kichwa chake ina picha ya mafanikio na asilimi 90% ya hawa watu wote wanaowaza pesa na mafanikio na maisha mazuri hufikiri pesa inapatikana kwa kufanya biashara tu, labda auze kitu fulani ndipo apate pesa.

Kuna njia nyingi za kupata pesa kwa wewe ulie na mtaji, hapo ulipo unaweza ukawa na pesa yako ila hujui uifanyie biashara gani au labda muda wa kusimamia hiyo biashara kwako ukawa mdogo hivyo unaogopa na hujui cha kufanya.

Sasa sikia leo nitakupa list ya vitu vya kufanya ujitoe na stress. Kuna watu najua hata tuongee na maturumbeta tupige ila hampo tayari kuacha kazi mnazofanya mjiajiri ila mpo tayari kuanzisha biashra ikafa, mkafungua ingine ikafa mkafungua tena na tena hamchoki ila sio eti mjiajiri najua mpo.

Sasa najua kuna watu mmeshajaribu kufungua biashara nyingi sana na mwsho kwasababu ya usimamizi biashara zote zimekufa, mmechoka na mmekata tamaa hamjui mfanye nini, hamna shida soma nitakavyoviandika leo kisha chomoka na kimoja kakifanyie kazi.

Leo naongelea biashara ya KUKODISHA VITU

Najua unaweza jiuliza utakodisha nini na kinauzwaje na kinakodishwaje,mimi leo ntawapa mfano ya ninavyovijua tu na ambavyo nina uhakika navyo, hivyo kama na wewe utapata idea usiache itoa yako ili namimi niipate nione nafanyaje.

1. VIBANDA VYA TIGO PESA
Nadhani wewe ni shahidi ya Mawakala wangapi unawakuta na miamvuli huko barabarani, nataka kukwambia kitu hao Mawakala sio kwamba wanapenda kukaa na miamvuli na meza tu ila sababu ni kwamba hana pesa ya kutengeneza kibanda,chakufanya wewe tengeneza kibanda kidogo cha wakala wa Tigo Pesa ambacho gharama yake kuanzia mabati, bomba mpaka kinakamilika ni 250,000 kwa kibanda kimoja, ina maana kama una Milioni 1 una uwezo wa kutengeneza vibanda vinne vilivyokamilika imebaki mtu kuchukua kwenda kufanyia kazi.

Kodi ya kukodisha hivi vibanda kimoja kwa mwezi ni 20,000 ina maana kwa vibanda vyako vinne una uhakika wa 80,000 kila mwezi hiyo ni uhakika yaani, sio ya kutafuta au kupigizana kelele na mtu na uchukuaji kodi wa hivi vibanda ni wa mwezi mtu akupe kodi ya mwezi tu kisha apige zake kazi.

2. BANDA LA BIASHARA
Hili banda halina utofauti na hilo banda la tigo pesa hapo juu tofauti yake ni ukubwa, kutegemea na uwezo wako ila kwa banda la ukubwa waupana futi 5 na urefu kwa futi 10 gharama ya ujenzi wa hili banda ni 500,000 hivyo ukiwa zako na 1M utaweza tengeneza mabanda mawili ambayo utayakodisha kwa wanaotaka yakodi bei yake kwa mwezi 30,000 to 50,000 kodi itategemea na wapi unaenda kumuwekea hilo banda, ukienda liweka sehemu nzuri kodi utaweza kumpa hata 60k to 100k na akalipa bila shida maana eneo hilo frem kodi ni 300k kwenda mbele. Assume una mabanda yako mawili ya kodi 50k kwa mwezi utakua unaingiza 100,000 isiyo na maelezo.

3. MASHINE YA KUCHOMELEA
Hizi mashine zipo za aina mbili kuna zile portable za kubeba halafu kuna yale transforma lake limesukwa na nyaya za aluminum, bei ya kuyanunua haya

- Portable: 400,000
- Kusuka: 300,000

Kukodisha haya ma mashine ni kwa masaaa 6 na masaa 12, kuna bei ya 6hrs na bei ya 12 hours, bei yake kwa 6hrs 20,000 na 12hours ni 30,000, ila kwa mashine portable 6hrs ni 30,000 na 12hrs 40,000.

Calculate hapo uone kwa siku utakuwa unaingiza sh ngapi, hii biashara ukijuana na mafundi welding kazi zitakuwa kila siku 5000 elfu kumi vitakuwa havikauki kwenye wallet/ pochi yako kiufupi huwezi kuwa na shida ndogondogo.

4. MUZIKI SPEAKER ZILE ZA KUCHOMEKA FLASH
Hizi speaker nilijaribu kununua kwa ajili ya ki pub changu uchwara fulani hivi sikuwaza kama hizi speaker ni dili basi wateja wale wale wakawa wakija wakisikia muziki wake wananiuliza kama nakodisha nikaanzaga zikodisha kama utani kwnye visherehe vya birthday huko mitaani, bei ni 50,000 kwa event 1 kiukweli hamnaga weekend hizi speaker nakosa simu ya kuombwa watu wakizitaka maana watu n wana sherehe kila leo na miziki yao ya subwoofer haitoshelezi haja zao.

Zitafute hizi speaker zinunue usiogope hela yako itarudi bila wasi wasi, zipo size tofauti ila kwakuwa unataka ya kibiashara nunua ya 600k to 700k hapo utapata heavy weight mziki kwa shughuli za mitaani, mfano ni kama hii Ailipu hapa chini japo kampuni zipo kibao zinazotengeneza hii mispika ya hivi.

st.png

5. KABATI ZA ALUMINIUM
Umeshaenda kununua chips mahali? Umeshaona chipsi zinawekwa kwenye nini? Basi tengeneza yale makabati nakuhakikishia hamna kikwazo kikubwa kwenye biashara ya chipsi kama KABATI Zero IQ ni shahidi muulizeni awambie mtu ataweza jidunduliza anunue kila kitu ila mtihani ukaja kwenye kabati.

Sasa tengeneza makabati yako ya 200,000 tengeneza makabati manne kisha yaweke mahali andika yanakodishwa, humalizi masaa 24 tayari ushapata mteja, haya makabati bei yake kabati per day ni 2000 maana yake kabati 1 kwa mwezi litakupa 60,000 x 4 = 240,000

Unaweza amua tengeneza vikabati vidogo kwa ajili ya mtu kuweka kachumbari na vitu vidogo vidogo ambavyo bei ya kabati kutengeneza ni 150,000 kisha wewe utalikodisha kwa 1000 per day x 30 days = 30,000 x 4(idadi ya makabati) = 120,000 kwa mwezi jumlisha bei ya makabati yako yote uone utakua na kiasi gani.

6. JENERETA
Kwa Tanzania yetu hii ndugu zanguni hii ni biashara nzuri sana, sijui kama utanielewa ila hii ni biashara ambayo ataekufata/ kukupigia simu unamtajia bei huku unakula karanga zako na hawezi kataaa wateja wapo kibao tena wengi tu, vuta picha watu wamekuja kwako kukodisha zile spika plus jenereta yani hela utayoingiza hiyo siku sijui nisemeje.

Kukodi jenereta bei inapatikana kwa aina ya jenereta anachukua kubwa au dogo na linaenda kufanya kazi kwa muda gani ila bei yake kwa dogo ni 30,000 na kubwa ni 50,000 muda ni 12hours.

7. UNA KIWANJA KIPO TU
Unaogopa nini kutangaza kuwa unakodisha eneo la mtu kufuga, au kufanya chochote akipendacho kwenye kiwanja chako kisha ukampa kodi yako kwa mwezi? Huna mpango wa kujenga leo wala kesho ila una likiwanja limekaa huko lipo tu linaoteana majani (ndugu yangu ile ni pesa umeikalia) huwezi itumia wape wengine watumie kisha atakulipa.

Unaona faida gani kusema nina kiwanja changu mahali ila kipo tu hukifanyii kitu? Huo ni uchoyo wa kusaidia wengine na Roho ya kimaskini iliyo ndani yako wape watu wafanye kazi na wewe upate hela (sikulazimishi) ila hii nayo ni fursa, usisubiri kudhani wapangishaji ni wenye nyumba tu utakuwa upo ulimwengu wa Analog.

Siku hizi kuna wababa wenye vibanda, baba wenye viwanja, mama mwenye vyombo, dada mwenye ma dryer, nk nk yaani fursa juu ya fursa ila ni lazima uwe na roho ya kutoa na kusaidia wengine nawe ndipo utafanikiwa kupitia wao.

Biashara ni nyingi sana wakati mwingine huna haja ya kufanya wewe biashara ukijiona huwezi biashara sio mbaya ukawasaidia wengine kisha na wewe ukajipatia kitu kupitia kuwasaidia huko maana mwisho wa siku na wewe unahitaji pesa.

Hizi biashara hazina gharama ukinunua hivyo vifaa gharama ya kuvitunza ni wewe mwenyewe tu, yule anayekutafuta lazima anakujua na yule ndio atakuwa jicho lako huko kifaa chako kinapoenda na kwa hivi vifaa kama makabati, mabanda nk ni vitu unavyoweza vizungukia hata wewe mwenyewe kuona usalama wake upo vipi.

Una pesa unataka kufanya biashara na huoni biashara ya kufanya, Fungua jicho lako angalia pembeni yako utamuona machinga katandaza vitu chini mfuate muulize nataka kukununulia meza uweke vitu juu kwa siku unipe 1000 au 500 upo tayari? akikubali kamtengenezee.

Ukimalizana naye angalia upande huu utamkuta mama ntilie anauza sana ana wateja sana ila wateja wake wanakalia viti vibovu, mfuate mwambie unataka mnunulia viti then atakulipa 2000 per day kwa viti na meza zako, akikubali kamfuatie vitu.

Inawezekana kama ukiamua kuwaza tofauti na wengine, sio lazima wote tuwe wakulima hebu mimi na wewe tuhakikishe yule mkulima analima vizuri tumpelekee maji ya kunywa, leso ajifute jasho, ajisikie anajaliwa halafu tuone kama akivuna atakuacha bure na tuone kama maisha hayatoenda, shida yetu binadamu tuliozaliwa na mwanamke tuna roho za UMIMI tukizikemea na kuzikataa hizi roho tutafanikiwa sana.
 
Kwenye malipo hapo nina wasiwasi kwa jinsi tulivyo wadaiwa kulipa ni mtihani.
Malipo ya kila kitu ni kwa siku hata kama ni 1000 unatafuta kijana wako atafata pesa

wale wa kwenye vibanda kodi ni kwa mwezi na ni mwanzo wa mwezi sio mwisho, Hana unatia kufuli.

hizi buku ni ndogo ndogo sana ila ni kubwa kama utamuachia zikazidi,hizi biashara zimekaa kmtego sana.

Mtu unaweza mwambia nakupa hili kabati kwa siku nataka unipe 500 tu au 1000 tu

yeye akachukulia jero kitu gani (naweza) buku kitu ganii (naweza) hawa watu hawana mahesabu

ya mwisho wa mwezi ntakua nmetumia kiasi gani,kwa mwaka ntakua nmetumia kiasi gani

na sisi kwenye udhaifu wao huo huo wakutopiga hesabu na kudharau jero/buku (tunapita nao)
 
Nawaza hizi mobile vibanda muda wowote kanahamishwa?
kanahamishwa ila sidhani kama wewe utaweza mpa mtu kibanda

kisha ukamuachia halafu usitafute mtu wakukupgia jicho kimya kimya.

umeshawahi pita sehemu mtu kaacha biashara yake barabarani kweupee

ukiangalia huku huoni mtu anaeangalia,ukiangalia kule huoni mtu analinda.

sasa kajaribu kuiiba uone kama utaonwa au hutoonwa.
 
Back
Top Bottom