Mtaani jamani pagumu!

Haki ya Mungu kusema ukweli ni mpenzi wa Mungu, mtaani kugumu mbaya. Yani kama upo kazini usijaribu kuchezea kazi, ni kugumu sanaa!

Waajiri wamefunga milango, ilhali vigezo tunavyo ila ndo hivyo jamani mtaani mpaka mtu unatamani uuze mwili.
Uuze mwili? Wewe ni mwanamke au?
 
Uuze mwili? Wewe ni mwanamke au?
hahaa!

Mkuu huyu kapitiwa tu, ujue maisha yakikuchanganya unaweza kujikuta unafanya mambo low sana.

Mimi mwenyewe niko mtaani mwaka sasa bila ajira lakini sijakata tamaa..

sasa sifi leo anasema auze mwili, basi tuanze kumsaka kabisa kabla hajapata bwawa. lol
 
Mtaani pagumu pagumu kweli, oohhoo sio masihara!! Ukitaka kujua kweli pagumu simama sehemu bila dira kisha mwenye dira akuone umesimama mbele ya dira yake Kama hujaitwa mwizi sijui.
 
Acha nikasafishe mabanda ya kitimoto..mkuu pole sana
 
Pole sana. Kupata nafasi ya kazi inayoendana na usomi na uwezo wako ni haki ya msingi.

Basi tu mambo ya uchumi hayalazimishiki.
 
Hii ndiyo JF ya maGreatThinker bwana...jinsi utakavyokuja na mada yako ndivyo utakavyojibiwa
Ungekuja na maswali kama haya
1. Nimemaliza masomo yangu na sasa natafuta kazi lakini sijapata huu mwaka wakadha na kadha, naombeni msaada.
2. Nimeajiliwa lakini nataka Kuacha kazi, naomba mnisaidie nini cha kufanya nikiwa mtaani.
Hayo na mengine mengi yanaweza kukupa wazo jipya kichwani mwako kuhusu kukabiliana na changamoto za maisha nje ya mfumo rasmi wa ajira.
 
Mimi mwenyewe najuta kusoma sana. Unajua ukiwa na elimuya wastani ni rahisi sana kujichanganya kila kona. Ila ukiwa na hii mivyeti yani ni full kukunyanyapaa. Unakuta bosi ana elimu ndogo kuliko wewe kwa hiyo anaogopa kukuajiri. Mara muajiri anaogopa kukulipa mshahara n.k. So ukiwa na elimu shida, ukiwa pia huna elimu ni shida.
 
Kusanya hata vitoto uanze katuition hutalala njaa alimradi uhakikishe una deliver
 
Wakuu acheni kabisa ukiona mtu hadi anasema hivyo ujuwe ashajaribu jitihada nyingi ila una kwama mambo ya kuchagua kazi yalipitwa na wakati ila hata hizo za kawaida kabisa nazo zimekuwa na ugumu wake wewe kama unayo kazi sshivi iheshimu sana huku mtaani hali sio kabisa
 
Mkuu naombako namimi kazi yoyote coz unaonekana una moyo wa huruma na upendo.
 
Kuna mzee kastaafu juzi kazi ya upolisi,, kakaa mtaani kaona ugumu wke kaamua kuomba tena apewe kazi huko huko polisi,,

Kwa kweli mtaani sasa tight si mchezo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…