Mtaa wa Mkwepu ni kwa heshima ya Rashid Sisso

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,902
30,235
MTAA WA MKWEPU NI MTAA KWA HESHIMA YA RASHID ''SISSO'' MOHAMED MKWEPU

Mtoto wa Rashid Sisso kaniandikia leo akaniuliza swali, ''Unajua asili ya Mkwepu Street kule Posta?''

Nikamjibu sijui.

Akaniuliza swali lingine.

''Jina la Rashid Mohamed Sisso je? Hilo ''Sisso'' ni la utani.
Jina halisi ni Rashid Mohamed Mkwepu.''

Nikajibu, ''Mzee Rashid Sisso ni mtu maarufu sana katika waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Namfahamu toka udogo wangu.''
''Na mimi ndiyo baba yangu.''

''Una maana ule mtaa wa Mkwepu ni kwa heshima ya baba?''

''...hati ya nyumba yetu iliandikwa hivyo na mdhamini wa nyumba yetu alikuwa Rashid Kawawa.''

''Nimefurahi sana kupata taarifa hii."

''Unayo picha ya baba ningependa kuandika kitu kuhusu yeye na urafiki wake na Mwalimu Nyerere.

Nimefurahi sana kupata taarifa hii.''
Hakuwa na kumbukumbu yoyote ya baba yake hana picha hata moja.

''Unaweza kuniandikia yale ambayo unayajua kuhusu baba?
Nami nitaongeza yangu tupate kitu cha maana kumuadhimisha mzee wetu?''

Hakuwa anajua chochote katika historia ya baba yake kwani alifariki yeye akiwa mdogo.

Alinambia kuwa Rashid Sisso ni Mmatumbi kutoka Kilwa Masoko kijiji cha Kisangi, Mkoa wa Lindi.

Alikuja Dar es Salaam na baba yake Mzee Mohamed Mkwepu akiwa mtoto mdogo wakaishi Karikaoo.

Nikamwambia kuwa hiyo ni bahati mbaya sana.
Mkwepu Street wakati wa ukoloni ulikuwa ukiitwa Windsor Street.

Nani huyu Rashid Mohamed Mkwepu?
In Shaa Allah nitakuja kumueleza.

Katika hiyo picha hapo chini kushoto ni Hastings Kamuzu Banda wa Nyasaland, Julius Kambarage Nyerere, Rashid ''Sisso'' Mohamed Mkwepu na Kaluta Amri Abeid wakiwa Uwanja wa Ndege Dar es Salaam katika miaka ya 1950 wakati wa kupigania uhuru wa Afrika.

Kaluta Amri Abeid na yeye amepewa mtaa unaitwa Kaluta.
Mtaa huu uko mbele ya Mkwepu.

Majina ya mitaa hii laiti ingeitwa Rashid Sisso na Amri Abeid au Kaluta Amri Abeid ingesaidia sana kwa watu kuwatambua wazalendo wapigania uhuru hawa waliokusudiwa kuadhimishwa.

Picha ya Mtaa wa Mkwepu ukianzia hapo Mtaa wa Jamuhuri ukitembea kama dakika tano kwa mwendo wa kawaida utafika mzunguko wa Mtaa wa Makunganya na kushoto kwako kuna mgahawa Cosy Cafe uliokuwa maarufu katika miaka ya 1950.

Wakati wa ukoloni Mtaa wa Jamhuri ulikuwa ukifahamika kama Ring Street.

Julius Nyerere Rais wa TANU na Katibu wa TANU Zuberi walikuwa wakikutana hapo Cosy Cafe kunywa chai na kupanga kazi za kufanya kwa siku ile.

Huu mtaa wa Makunganya ilipo Cosy Cafe umepewa jina hili kutokana na Hassan bin Omar Makunganya aliyepambana sana na Wajerumani kwa silaha na mwishowe alikamatwa na kunyongwa.

Katika picha ya mwisho kulia ni Hassan bin Omari Makunganya, Omari Muenda na Jumbe.

View attachment 2217614

1652069411210.png
 
Cosy Cafe ilikuwepo hadi miaka ya 2000 baadaye ilichukuliwa na Wasomali wa iliyowahi kuwa Hotel Paradise,Bagamoyo. Na sasa ni Wamiliki wa City Mall. Sijapita siku nyingi hapo lakini jengo bado lipo
 
View attachment 2217613
Tunyweni bia jamani
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom