Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

Mtaa wa kwa Kindande Temeke visa vyake

Profesa ntare nkobe

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2018
Posts
6,955
Reaction score
8,144
Ukifika Temeke kuna mtaa unaitwa Mji mpya ndani yake kuna kamtaa korofi kanaitwa KINDANDE.

Kindande kuna maskani maarufu inaitwa Lebanon.

Huu mtaa kwa kindande ni mtaa ambao unaogopeka kupita bila taadhari kwa saa 24..Mambo yote maovu yapo hapo kuanzia wizi kukaba mchana umalaya uvutaji bangi ulio kubuhu.

Katika maisha yangu yote sijawai kuona wanawake wanavuta bangi kupita wanaume ni mewaona kwa Kindande.

Mabinti wa kwa Kindande wanatabia ya kukaa nje wakikuomba hela ukakataa kutoa hayo matusi yake ni balaaha.

Mabinti wa kwa Kindande wanaongoza kucheza vigodoro wakiwa uchi sometimes wanakodishwa kwenda kusasambua kwenye vigodoro vya majirani zao Mtongani,Tandika,Wailes, na Mbagala.

Hawa mabinti wana tabia ya kukodi boda boda usiku mishale ya saa 7 usiku na kuendelea wana tegesha sehemu za starehe ukijiroga ukampakia mkifika tu kwa Kindande kuna makaburi mitaa hiyo litakuja kundi litakupiga piki piki inaondoka.

Kwa Kindande ukimpenda demu ukichepuka kazi unayo utapigwa na kundi lake plus matusi juu hila yeye kuchepuka ruksa.

Wana maskani yao inaitwa Lebanon hiyo na polisi ni kufukuzana kila siku hapo unawapata madogo wa miaka 12 waliopinda wapiga bangi hatari.

Huku unakuta dogo naye ni baba vibinti vidogo navyo ni single mother.

Huu mtaa unaongoza kwa matusi kwa lika zote hakuna heshima kwa mkubwa wala mdogo.

Hiki kimtaa kimepakana na Tandika Kwa Aziz Ally Temeke mwisho na Mtoni mtongani.

Kama sio mtu wa vulugu usipange mtaa huu...
 
Back
Top Bottom