Mswaki: Ni baada ya muda gani niutupe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mswaki: Ni baada ya muda gani niutupe?

Discussion in 'JF Doctor' started by Abdulhalim, Mar 4, 2010.

 1. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Linaeza kuwa swali la kijinga, lakini kiukweli linanitatiza. na ni muhimu kwangu na watoto wangu, na huenda hata baadhi yenu.

  Naomba majibu mujarabu ya kitaalamu,

  Je ni muda gani optimum wa kutumia mswaki?

  Madhara ya kuzidisha huo muda ni yepi (kaa yapo)?

  Mswaki unaotumika currently kiafya unatakiwa utunzwe wapi na kivipi?
  Kimshazari, wima, au chali, kichwa chini?

  NB: Tafwadhaal nipo chini ya miguu yako, kaa huna input ione sred hii kaa kituo cha polisi.
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mweee umekuwa mkali kweli leo.
  anyway back to the topic: unashauriwa mswaki utumie ndani ya miezi 3 tuu ikishapita tupa nunua mwingine. Kuhusu madhara ya kuzidisha ni wamba unavyoupigia zaidi ya muda huo wa miezi mitatu nguvu yake inakuwa imekwisha ya kusugua meno na kutakatisha. inakuwa overused na matokeo inakuwa kama unajipakaza uchafu tena.

  Kiafya mswaki should be kept in an open space where kuna hewa nyingi inapita na i suppose unapaswa usimamishwe kichwa juu hata ukiangalia vyombo vya kuekea mswaki kwa kidhungu Toothbrush Holder vina design ya kueka hivo.

  Punguza ukali basi kidogo kaka au vipi..........
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Shukran kwa maelezo yako. Siko mkali ni kawaida yangu tu ktk kujaribu kutumia muda vizuri, usinielewe vibaya. Sikujua mambo ya miezi 3, itabidi kesho nikanunue mswaki mpya..ishakuwa soo tena. Mi nilikua nachukulia miezi 6. Mambo ya toothbrush holder bado kidogo ..
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ingawa hujasema unazungumzia mswaki gani, lakini hakuna muda specific unaopendekezwa kitaalam kuwa unafaa kutumia mswaki kabla hujautupa, muda wa matumizi unategemea aina na uimara wa mswaki. kumbuka kuna miswaki ya vidole, mpira, uzi (au nyuzi), miti, na plastiki (brashi za plastiki) ambayo ni ya kisasa zaidi.

  kwa miswaki ya brashi za plastiki, unashauriwa kutumia mswaki hadi utakapoona nyuzi zake (zile za plastiki) zinachomoka au kupinda. ikifikia hapo unashauriwa kununua mwingine bila kujali muda gani umetumia hata kama ni siku moja kwani ikiwa imepinda haiwezi kupenya hadi kwenye mbavu za meno yako (sehemu za kati ya jino na jino) na fizi (gums) kwa ajili ya usafi muafaka wa meno na kinywa chako.

  kwaa miswaki ya miti unatakiwa kuutafuna mara kwa mara (angalau kila baada ya siku tatu) ili kwezesha kusafisha hadi ehemu za katikati ya meno ako na usiutafune sana hadi ukarainika kupita kiasi.

  miswaki ya nyuzi ni maalum kwa kusafishia kati ya jino na jino na kuondoa mabaki ya chakila na uchafu wa muda mrefu usiofikiwa kirahisi na miswaki mingine. huu unatakiwa kutumika hadi utakapodhoofika n akukatika.

  miswaki mingine haishauriwi kutumika kitaalamu kutokana na uduni wake

  utunzaji wake pia utehemea aina ya mswaki, lakini unashauriwa kuutunza kwa namna mabayo utabaki msafi na mkavu kwa ajili ya matumizi yanayofuata
   
 5. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 5,094
  Likes Received: 1,530
  Trophy Points: 280
  kwa ujumla wangu pia umepotea leo na ndio nikapata wazo ninunue mwingine,kuhusu muda nilioutumia mmh hata sikumbuki,anyway sasa nimeelewa ni ndani ya miezi mitatu tu,thanx JS
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nway, haya bana nimekuelewa.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ehh ?ati? Umepotea? Sasa ulikua unafanyajefanyaje?

  Duh, kaaz kwelikweli, naona somo linasaidia..
   
 8. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,878
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
 9. K

  Kekuye Senior Member

  #9
  Mar 5, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyongeza: Pia ukiugua magonjwa ambayo yanasababisha bakteria kunywani mfono vidonda kweye koo/sore throat au influenza wataalamu wanashauri ubadilishe mswaki mara baada ya kupona.
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mi sred mingine inaudhi sana! kwani we huoni kama jimswaki lako limeisha ukachonge jingine porini au ukanunue dukani?
   
 11. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 526
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Huwa baada ya miezi sita. Choose flexi tooth brush na tunza kwenye toothbrush holder. Inabidi uwe makini ambapo mnakaa watu wengi kwa sababu kuna tendency ya kutumia mswaki ambao sio wa kwako. Kwa hiyo ni vizuri chioce za mswaki ziwe rangi tofauti .

  Pia muhimu kumwona dentist mara mbili kwa mwaka.
   
 12. T

  Tall JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kila uamkapo asubuhi, na wakati mwingine ukigundua meno yako ni machafo
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,301
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Usitunze mswaki ambao ni disposable!
   
 14. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #14
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,359
  Likes Received: 1,084
  Trophy Points: 280
  Mbona Abdulhalim katoa angalizo zuri sana kama inavyoonekana hapa chini


  "NB: Tafwadhaal nipo chini ya miguu yako, kaa huna input ione sred hii kaa kituo cha polisi.
  "
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ahh..sikuiona hii post ya Pepe..Oh nimekumbuka, kumbe yumo kwenye ignore list ..he he he he..
   
 16. k

  kany Member

  #16
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 20, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  M'ngu unatakiwa kila jioni baada ya chakula na kabla ya kulala upige mswaki. Hii ni kwa sababu ya kuondoa mabaki ya chakula na hivyo kuondoa uwezekano wa bacteria kufanya kazi yao pale na kuharibu meno yako!!!! Nadhani umenipata mdau
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...