Yanajirudia yale ya Salim Ahmed Salim kutuhumiwa kumuua Karume. Uchaguzi unaibuka na mambo mengi sana.
Tunapokaribia kuadhimisha miaka 31 tangu kilipotokea kifo kilichojaa utata cha aliyekuwa Waziri Mkuu Ndg.Edward Moringe Sokoine,ni wakati mwafaka sasa kumhoji Mh.Cleopa Msuya juu ya tuhuma za kuhusishwa na kifo cha Mh. Sokoine;kwa sababu Mh. Msuya kwa siku za karibuni amejitokeza kukemea maovu mbalimbali yanayofanywa na viongozi wa CCM bila shaka pia atakuwa na ujasiri wa kujitokeza na kutolea ufafanuzi wa tuhuma hizi.
Ndugu yangu Mleta mada angalia tena vyanzo vyako vya habari kuhusu Kifo cha Marehemu Sokoine,Hizi taarifa unaloleta humu zinasababisha usumbufu kwa baadhi ya ndugu na jamaa wa Marehemu na sisi wengine ambao tunawafahamu hao Wazee wote na utumishi wao Serikalini.Jioni ile ya Jumatano,April 12/1984 pale Wami-Dakawa katika wilaya ya Mvomero,Mzee Sokoine alikufa katika ajali ya kawaida kabisa ya gari? Nasema hivi kwa sababu tulikuwa katika msafara ule.Kulikuwa na makosa yaliyofanywa na gari lililokuwa linakuja upande wa pili,ambalo lilikuwa linaendeshwa na Mkimbizi Dumisani Dube.Gari hilo liliserereka na kugonga gari la Waziri Mkuu,Upande aliokuwa amekaa Sokoine,na wakati huo inasadikiwa Marehemu alikuwa amelala.Mara tu baada ya ajali ile Mkimbizi yule alishikiliwa na vyombo vya usalama.Marehemu Sokoine aliiingizwa kwenye gari Jingine na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa,Morogoro mjini.Hakuna aliyeweza kusema pale kwenye ajali ambayo ilitokea saa 10 jioni kama Waziri Mkuu alikuwa Hai au Amekufa.Habari za kifo zilithibitishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na maelezo yake yalisema Waziri Mkuu alifariki kwenye ajali.
Hizi habari unazoziandika hapa kwamba Mzee Msuya anahusika kwa namna moja ama nyingine hazina ukweli wowote.Marehemu Sokoine alifariki katika ajali ya barabarani.Kuandika habari kama hii unaleta sintofahamu,umemuhusisha Mzee Msuya na tukio jingine la kupotea kwa secretary wake karibu miaka 30 iliyopita,siwezi kulisemea hilo kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kulisikia.Lakini naomba usielekeze tuhuma hizi nzito kwa sababu tu ya misimamo tofauti ya Kiitikadi.Mzee Msuya kama wewe anaweza kusema lolote kuhusu hizi harakati za baadhi ya Watanzania kuwania nafasi ya Urais, hana upendeleo wowote kwenye mchakato huu,mwisho wa siku ana kura yake moja tu.Nipo wazi kukosolewa lakini nimeamua kuandika hili kwa makusudi ili tusiifanye forum kama kijiwe cha kuchafua Watanzania wenzetu!
mi nadhan hustahil kujibiwa ila kwa faida ya watanzania ni kwamba sokoine alikufa kwa ajali ya gari wakat akitoka dom kwenda dar gari lake liligongana na gar ilokuwa ikiendeshwa na mkimbizi kutoka south akiitwa DUBE kuhusiana na kumzika sekretari mzee msuya hajawah kufanya kaz idara ya mazishi kwenye halmashauri yoyote nchini
Umekariri tu vya kuambiwa pasipo kuchanganya na Akili yako, Sokoine hakufa kwa Ajali bali ni mpango ulikuwa umesukwa ile Ajali ilikuwa ni Feki tu kama ilivyokuwa Ajali ya Chacha wangwe, kubali ukatae Sokoine alipigwa Risasi wakati amesinzia kisha Gari zikagonganishwa kuwazuga watu, hata Chacha wangwe ilikuwa hivyo hivyo lakini tofauti ni kwamba wauaji watumia Kijiko ( Greda) kuiponda Gari kisha kuibinua kwenda pembeni baada ya kuwa wamempiga Risasi kupitia Mdomoni Wakati akiwa amesinzia wanaondoka haraka na kumwacha Deus Mallya akizuga kuwa ni Ajali. R. I . P chacha wangwe na Sokoine.
Ni aibu sana kulete uzushi ambao hauna vielelezo.Sijawahi kusikia kama ipo ripoti yoyote kwenye mihimili yote 3 inayoonyesha kuwa msuya alihusika.kama ipo ripoti wekeni hapa JF.EL anaweza kutuongoza sisi kama nchi,kaweza JK bwana?tatizo anatoa hela kila kona.sasa tunamkataa kwasababu hizo na tuhuma za ufisadi.Msuya anaweza kujibu kama mnaweka hapa vielelezo.ila hivi hawezi kujibu bali mtaleta ubishani.kwanza ccm hatuitaki hata mgombane kiasi gani.
Haya ya Chacha Wangwe nayo ndio yapo hivyo??
Mtu ambaye anahusishwa na vifo vya utata ili aendelee katika utawala kimsingi hana mshipa wa kushauri chochote.mi nadhan hustahil kujibiwa ila kwa faida ya watanzania ni kwamba sokoine alikufa kwa ajali ya gari wakat akitoka dom kwenda dar gari lake liligongana na gar ilokuwa ikiendeshwa na mkimbizi kutoka south akiitwa DUBE kuhusiana na kumzika sekretari mzee msuya hajawah kufanya kaz idara ya mazishi kwenye halmashauri yoyote nchini
Msimpe ujasiri mtu asiyestahili.tunajua hayo ila ujasir wa mze msuya kukemea ufisadi ndio uliofumua hili kwa sabab yey hakuwa msafi tangu mwanzo hasa mambo haya ya ufisadi mpaka akahusishwa na kifo cha sokoine ndio mana watu wanamtaka aje na ufafanuz wa aliko sokoine mana yey ni fisadi mkubwa wa wakati ule akijulikana kwa jina mhujumu uchumi. sasa leo anawezaje kutoa kibanzi kwenye jicho mwenzake wakati yey ana boriti kweny jicho lake? katoe kwanza boriti kweny jicho lako ndipo uweze kutoa kibanz kweny jicho la mwenzako
sio tu msemaji bali hata sasa niko siting room kwake tunajianda kwa chakula cha jioni na ananipatia historia nzur ya mapinduzi ya zenj. akimaliza nitapost kwa faida yenu mnaopotosha historia kwa faida ya fisadi wenu
Uzalendo uko chini sana nchini .. Ni Aibu. Inawezekana .. classified info .. kuanza kusambaa hovyo .. kwa sababu za kibinafsi tu
Haya ya Chacha Wangwe nayo ndio yapo hivyo??
Kwani chacha wangwe aliuwawa kwa kuficha nini
tunajua hayo ila ujasir wa mze msuya kukemea ufisadi ndio uliofumua hili kwa sabab yey hakuwa msafi tangu mwanzo hasa mambo haya ya ufisadi mpaka akahusishwa na kifo cha sokoine ndio mana watu wanamtaka aje na ufafanuz wa aliko sokoine mana yey ni fisadi mkubwa wa wakati ule akijulikana kwa jina mhujumu uchumi. sasa leo anawezaje kutoa kibanzi kwenye jicho mwenzake wakati yey ana boriti kweny jicho lake? katoe kwanza boriti kweny jicho lako ndipo uweze kutoa kibanz kweny jicho la mwenzako
Ni aibu sana kulete uzushi ambao hauna vielelezo.Sijawahi kusikia kama ipo ripoti yoyote kwenye mihimili yote 3 inayoonyesha kuwa msuya alihusika.kama ipo ripoti wekeni hapa JF.EL anaweza kutuongoza sisi kama nchi,kaweza JK bwana?tatizo anatoa hela kila kona.sasa tunamkataa kwasababu hizo na tuhuma za ufisadi.Msuya anaweza kujibu kama mnaweka hapa vielelezo.ila hivi hawezi kujibu bali mtaleta ubishani.kwanza ccm hatuitaki hata mgombane kiasi gani.
Ukiambiwa uthibitishe kuwa mwili ulikuwa na matundu ya....utakubali!!? Au wewe ndiye ulihusika kwenye Postmortem. Halafu Je mlikuwa wapi kumuuliza Julius maana ndiye alikuwa Mkulu kabisa. Je ni nani alikuwa IGP, Intelligence chief , Home Affair minister nk.
Nasema mna imani za kichawi kwa kuwa kati ya hoja zenu eti kwavile alikuwa anapata mauzauza.!!! Sasa hii inahusika vip.!!!? NDIO MAANA NASEMA TOKENI HUKO kwenye fikra za ajabu ajabu.
Otherwise mpo hapa KISIASA ZAIDI. but be very careful unapoamua kumchafua mtu huwa inarudi na wewe ipo siku utahusishwa na kifo cha mtu hata kama hujahusika. ACHENI SIASA MAJI TAKA
Hallucinations ni uchawi? Mambo mengine yanahitaji jitihada binafsi kuelewa siy lazima yawe kwenye syllabus ya shule bwana.
Naomba usiweweseke. Ukitulia inaleta sense kuliko unavyotaka ku punic. Kwani wewe unajihami nini? Vifo vingapi vya watu duniani vinachunguzwagwa baada ya miaka mingi kupita? Tunapoulizana yahusuyo kifo cha sokoine wewe hutaki yaongelewe, kwa sababu gani?
Sasa nani anachafuliwa hapa na nani anamchafua? Nimekuambia nani alimuua sokoine ama umenisikia nimesema alikufa kifo cha namna gani?
Acha watu wajadiliane. Hakuna ubaya katika hilo. Lakini ukweli utasemwa siku zote kwamba Sokoine hakupimwa morogoro hospital kujua kama alifika pale ameshakufa ama alikuwa hai!.
Hili ninalijua. Maswali mengine bwana. Unataka nisemeje? Wenye ufahamu wameshaelewa. Unajuaje kama sikuwepo Morogoro wakati Dr. Materu anaambiwa hana sababu ya kupima?
Jifunze kuwa msikivu kuliko kubisha masual usiyoyajua!.
Kamuulize Deus Mallya